KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, September 5, 2009

Wafuasi wa upinzani nchini Gabon wamezusha machafuko kwenye mitaa ya mji mkuu


Wafuasi wa upinzani nchini Gabon wamezusha machafuko kwenye mitaa ya mji mkuu Libreville kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais ambayo yamehakikisha Ali Bongo anarithi madaraka kutoka kwa babake hayati Omar Bongo.
Kwa saa kadha polisi walipambana na waandamanaji ambao walilalamika kwamba matokeo ya uchaguzi hayakuwa halali.

Waandamanaji hao walivamia ofisi za ubalozi wa Ufaransa katika mji wa Port Gentil ambako pia walishambulia gereza moja na kuwaachilia huru wafungwa.


Ahadi ya Rais
Nitawahudumia wote bila ubaguzi


Ali Ben Bongo

Wengi wao wanailaumu Ufaransa kwa kuunga mkono utawala wa rais wa zamani Omar Bongo ambaye alitawala Gabon kwa zaidi ya miaka 40.

Machafuko zaidi

Ufaransa tayari imetoa taarifa ya kuwahimiza raia wake wanaoishi Gabon kutotoka nje.

Hofu kubwa imetanda kwenye mji mkuu Libreville kwamba huenda machafuko zaidi yakazuka.

Kwa mujibu wa maafisa waliosimamia uchaguzi huo, Bwana Ali Ben Bongo alinyakua asilimia 42 ya kura zilizopigwa.

Omar Bongo alitawala kwa zaidi ya miaka 40

Pindi tu baada ya kutangazwa mshindi, Ali Bongo aliahidi kudumisha utangamano nchini.

"Kulingana na mtazamo wangu, nitawahudumia watu wote kama rais wa Gabon."

"Nitawahudumia wote bila ubaguzi," alisema rais mpya wa Gabon, nchi yenye utajiri mkubwa wa mafuta.

No comments:

Post a Comment