KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Saturday, September 5, 2009
Serikali Cameroon yatetea matumizi ya rais
Serikali nchini Cameroon imeitetea ziara yenye utata ya mapumziko ya rais wa nchi hiyo Paul Biya katika mji wa La Baule, kusini mwa Ufaransa.
Safari ya rais huyo imekuwa ikizingumziwa sana katika vyombo vya habari nchini Ufaransa na Cameroon, kutokana na kutuhumiwa kutumia kiasi cha dola za kimarekani 40,000 kwa siku kwa vyumba 43 vya hoteli.
Lakini waziri wa mawasiliano wa Cameroon Issa Tchiroma Bakary ameiambia BBC kuwa, rais Biya alikuwa na haki kutumia kiasi cha pesa alichopewa kwa namna yoyote anayvotaka.
Wastani wa kipato cha mwananchi kwa mwaka katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi ni dola za kimarekani 1,000.
Bwana Bakary ameiambia BBC kuwa taarifa hizo zimekuwa na lengo la kutaka kuvuruga amani ya nchi.
"Je hayuko huru kutumia pesa zake anavyotaka?' waziri huyo aliuliza.
"Je anapaswa kutoa taarifa ya jinsi anavyotumia pesa hizi kwa waandishi wa habari nchini Ufaransa au hapa?''
Randy Joe Sa'ah wa BBC mjini Yaunde mji mkuu wa Cameroon anasema, Bwana Biya na mke wake Chantal walianza ziara yao ya mapunziko tarehe 15 Agost baada ya mkutano na rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy.
Ripoti katika vyombo vya habari nchini Ufaransa zinasema rais huyo na mkewe pamoja na ujumbe wao wanakaa katika hoteli ya nyota tano ya L'Hermitage Hotel.
Bwana Biya amekuwa rais wa Cameroon tangu mwaka 1982.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment