KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Saturday, September 5, 2009
Maafisa wa Umoja wa Mataifa wamesema mafuriko makubwa ambayo sasa yamewaathiri watu 350,000 maeneo ya Afrika Magharibi
Maafisa wa Umoja wa Mataifa wamesema mafuriko makubwa ambayo sasa yamewaathiri watu 350,000 maeneo ya Afrika Magharibi, yameua watu takriban 30 nchini Ghana na Burkina Faso.
Zaidi ya watu 100,000 nchini Burkina Faso wamelazimika kuzigama nyumba zao zaidi katika mji mkuu Ouagadougou.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema kiwango cha mvua iliyonyesha mji mkuu Ouagadougou kwa siku moja ni sawa na robo ya mvua inayonyesha kwa mwaka mmoja nchini kote.
Nchi jirani nazo zimeathirika zikiwemo Benin, Guinea, Niger na Senegal.
Mapema hospitali kuu ya Burkina Faso iliathirika sana kwa mafuriko na imebidi wagonjwa wahamishwe wengi wakiwa na magonjwa ya kuambukiza.
Takriban watu saba wamearifiwa kufa kutokana na mafuriko hayo nchini Burkina Faso na Rais President Blaise Compaore ameomba jumuia ya kimataifa kuisaidia nchi yake.
Amesema wale ambao wameathirika na mafuriko hayo kwa sasa wamehifadhiwa katika shule na vyuo.
Nchini Burkina Faso lango kuu la kuingizia maji katika bwawa linalozalisha umeme katika mto Volta limefungwa karibu na mpaka wa Ghana ili kuzuia mafuriko zaidi.
Nchini Ghana watu wanaofikia 25 wameripotiwa kufa kutokana matukio yanayohusiana na mafuriko.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment