KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Sunday, September 6, 2009
SPLM waungana na chama kutoka kaskazini
Chama kikuu cha upinzani katika Sudan ya kusini kimeingia mkataba na mojawapo ya vyama vikuu vya upinzani kutoka Sudan kaskazini kuunda muungano kabla ya uchaguzi mkuu wa mwezi Aprili mwakani.
Makubaliano hayo kati ya chama cha waasi wa zamani cha Sudan People's Liberation Movement au SPLM, na kile cha UMMA kutoka kaskazini yalitiwa sahihi mjini Juba.
Msemaji wa SPLM amesema muungano huo utahakikisha kuwepo uchaguzi huru na wa haki , na pia utekelezwaji wa kura ya maoni mwaka 2011 , kuhusu uhuru wa Sudan kusini kujitawala.
Mkataba ulitiwa sahihi kufuatia mazungumzo yaliyodumu muda wa siku tatu tangu siku ya Alhamisi mjini Juba.
Kufuatia mwaliko wa mwenyekiti wa chama cha SPLM Salvar Kiir , ujumbe wa chama cha UMMA ukiongozwa na mwenyekiti Sadiq El Mahdi uliwasili Juba siku ya Alhamisi.
Katibu mkuu wa SPLM Pagan Amum aliambia waandishi wa habari kwamba vyama hivyo viwili vimeungana ili kushirikiana mawazo ya kuindoa Sudan kutoka lindi la matatizo.
Viongozi hao wamesema mkataba huo unajumuisha mipango ya kuzingatiwa endapo watu wa Sudan kusini watachagua kuwa nchi huria , kuhakikisha kwamba pande zote mbili zinaishi kwa uelewano na ujirani mwema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment