KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Sunday, September 6, 2009

Familia nzima yamalizwa Mogadishu


Watu watano kutoka familia moja wameuwawa katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, wakati kombora liliporushwa kwenye nyumba yao siku ya jumaamosi.
Walikuwa wamekusanyika kufuturu baada ya kufunga kutwa nzima.

Shambulizi hilo lilitokea muda mfupi tu baada ya waziri wa mambo ya nje wa Somalia Ali Ahmed Jama kutangaza kwamba serikali ya mpito ya Somalia inafanya mashauriano na wapiganaji wa kiislamu.

Bwana Jama alisema amefanikiwa kuwashawishi baadhi ya wanamgambo kujiunga na utawala.

Kwa mujibu wa mwandishi wa BBC Mohammed Olad Hassan, watu wengine kadhaa walijeruhiwa vibaya kwenye nyumba iliyoshambuliwa.

Wakati huo huo , raia wasiopungua 19 walijeruhiwa kwenye mapigano mjini Mogadishu .

Mmoja alifariki baadaye akipelekwa hospitalini.

No comments:

Post a Comment