KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Sunday, September 6, 2009
Mzozo wazuka tena Gabon
Waziri wa mambo ya ndani wa Gabon anasema bunge litaombwa kuidhinisha amri ya kutangazwa kwa hali ya hatari katika mji wa Port Gentil ikiwa ghasia zitaendelea zaidi katika mji huo.
Waziri huyo ametoa taarifa hiyo akiwa ziarani kwenye mji huo wenye viwanda kufuatia maandamano yenye ghasia ya kupinga kuchaguliwa kwa Ali Bongo kuwa rais, kuchukua nafasi ya baba yake marehemu Omar Bongo.
Mamia ya raia wameripotiwa kuutoroka mji huo wa Port Gentil . Mkazi mmoja ameambia BBC kwamba watu wengi wameonekana wakilekea katika mji mkuu wa Librevile , na wengine wakitorokea kwenye vijiji vya karibu pamoja na misitu.
Watu kadhaa wameripotiwa kuuwawa kwenye ghasia zilizofuatia uchaguzi mkuu.
Siku ya jumamosi Bwana Bongo alitoa wito wa kuwepo utulivu na akawasihi wapinzani wake kupeleka malalamiko yao mahakamani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment