KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Wednesday, September 9, 2009
Mwanamke wa ''suruali'' aachiwa huru Sudan
Mwandishi wa habari mwanamke wa Sudan aliyepatikana na hatia ya kuvaa suruali na kuhukumiwa kifungo cha mwezi mmoja, ameachiwa huru baada ya kukaa jela siku moja tu.
Lubna Ahmed Hussein alipelekwa gerezani baada ya kukataa kulipa faini ya kiasi cha dola 200 za Marekani akisema asingependa ''kuihalalisha hukumu aliyopewa''.
Mohedinne Titawi, wa chama cha waandishi wa habari nchini Sudan, amesema chama hicho kimelipa faini ili mwanamama huyo aachiliwe huru.
Bi Hussein, alikuwa akikabiliwa na hukumu ya kuchapwa viboko hadi 40.
Vikundi vya kimataifa vya kutetea haki za binadamu vilikuwa vikishutumu kesi hiyo tangu ilipoanza, huku Umoja wa Mataifa ukisema siku ya Jumanne kwamba mashtaka dhidi ya mwanamama huyo yalikuwa ni kinyume na sheria za kimataifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment