KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, September 9, 2009

Idadi ya wanafunzi wa kike wanaoacha shule kwa sababu ya mimba isiotarajiwa inazidi kupanda.


Kimasomaso
Idadi ya wanafunzi wa kike wanaoacha shule kwa sababu ya mimba isiotarajiwa inazidi kupanda.
IDADI ya wasichana wanaokatisha masomo yao na kuacha shule wilayani Kericho, kwa sababu ya kupachikwa mimba wasiotarajia imewashangaza maafisa wa Elimu na wadau wengine.
Katika kisa ambacho kimezua mjadala mkubwa juu ya Elimu na mimba miongoni mwa wanafunzi wa kike, imeibuka kuwa toka kwa idadi ya wasichana 25 waliojiunga katika kidato cha kwanza katika shule moja katika eneo hilo, 24 waliacha shule baada ya kutwikwa mimba.

Katika makala ya wiki hii tunahoji nini kinachopelekea hali kama hii ya mimba za mapema miongoni mwa wanafunzi???? Mwalimu mkuu alizungumzia umbali wa shule kuoka kwa makao ya wanafunzi ambao wanalazimika kupitia katika misitu ya chai jambo amabalo linawaweka katika hatari ya mahusiano ya kimapenzi na hata ubakaji.


Sikiliza Kipindi

Mwalimu huyo mkuu alisema ni jambo la kushangaza sana. Aliongezea kuwa idadi ya waichana katika shule hio sasa ni ishirini pekee. Wengi wa wasichana waliokuwa wakifanya vyema katika masomo wameacha shule baada ya wanafunzi wenzao na baadhi ya wafanyakazi katika mashamba ya chai kuwatwika mimba.

Elimu ya watoto wa kike inaendelea kuwa ndoto isioweza kutimika katika eneo hili la Afrika. Wasichana wengi wanadanganywa na wanaume na kujitosa katika tabia na mahusiano ya kingono yanayopelekea mimba isiotarajiwa. Jambo ambalo huwafanya wasichana hawa kuacha shule na kuanza maisha ya uzazi wakiwa wao wenyewe bado wachanga.

Wengine wanakumbwa na vizingiti vya kitamaduni kama vile tohara ya wanawake, ndoa za mapema, kazi za nyumbani, magonjwa na umasikini. Kumekuwa na mjadala iwapo kuratibishwa kwa masomo ya afya ya uzazi katika silabasi za shule kutaksaidia kudhibiti mimba isiotarajiwa na magonjwa ya zinaa miongoni mwa wanafunzi.

Inchini Tanzania serikali, kwa mara ya kwanza, imewaruhusu wale waliopata mimba wakiwa shuleni kufanya mitihani. Hapo awali wanafunzi waja wazito walikuwa wakikatazwa kufanya hivyo.

Je, nini mchango wako kuhusu yote haya??????

Tuma maoni au maswali yako kupitia kimasomaso@bbc.co.uk, au tuma text message kwa namba hii + 44 77 86 202 005, au tuandikie barua kwa kutumia sanduku la barua 58621, Nairobi.

No comments:

Post a Comment