KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, September 25, 2009

Maharamia washambulia meli Mogadishu


Maharamia kutoka Somalia wamepanda meli iliyokuwa ikielekea katika bandari ya Mogadishu na kumwuua kwa kumpiga risasi nahodha wa chombo hicho ambaye ni raia wa Syria.
Maafisa wamesema nahodha wa meli hiyo alikataa kutii matakwa ya maharamia hao iliyomtaka asielekee kwenye bandari hiyo.

Inaaminiwa hili ni shambulio la kwanza la aina yake kutokea karibu na mji mkuu wa Somalia.

Maharamia wana desturi ya kufanya mashambulio yao maeneo ya kaskazini, hasa karibu na Eyl.

Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika na majeshi ya usalama ya Somalia walivamia na kuweza kuokoa meli hiyo yenye bendera ya Panama.

Hata hivyo, mabaharia watatu nao wameripotiwa kujeruhiwa katika shambulio hilo

No comments:

Post a Comment