KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, September 25, 2009

AFYA MAISHANI NI MUHIMU LAKINI ?



ASALAMU ALAYKUMU MAISHANI CLUB ?
MIMI NI MWANAMKE MWENYE UMRI WA MIAKA 39. NILIPOKUWA MDOGO NDOTO ZANGU ZILIKUWA TOFAUTI NA SASA. NILITUMAI NA KUTEGEMEA KWAMBA NIKIFIKISHA UMRI WA MIAKA 25 AU 30 NTAOLEWA NA KUANZA KUISHI VIZURI NA MME WANGU NA WATOTO WA NGU ! LAKINI MWISHO WA SIKUKU, NAJIKUTA KATIKA NJIA PANDA, SINA MME WALA MTOTO. NAJISIKIA VIBAYA KABISA, WALA SINA HAMU YA KUISHI KWA RAHA, KWASABABU MAISHA YANGU YAMEHARIBIWA KATIKA UKUTA WA NDOTO ZA GIZA. NNASHANGAA PALE AMBAPO NAWAONA RAFIKI ZANGU, WANASHI NA WAUME ZAO NA WENGINE WAKISHI NA WATOTO ZAIDI YA MMOJA. KWA UPANDE WANGU SIJUI NIFANYEJE ?
ELIMU NZURI NNAYO, FEDHA ZIPO, NYUMBA NZURI NA USAFIRI VIPO, NAMARANYINGI NIMESIFIWA NA RAFIKI ZANGU KWAMBA MIMI NI MZURI WA SURA !!
JAMANI SIJUI NIFANYE JE ?
KULALA, KULA, KUNYWA, MATEMBEZI, KAZI SINA AMANI KATIKA MFUMO WA YOTE HAYA.
INGELIKUWA RAHISI KAMA MME ANAUZWA AU NNA UWEZO WA KUMNUNUWA, LAKINI NAHISIA NA NI KWELI MAPENZI HAYANA THAMANI, NDIO MAANA HATUWEZI KUNUNUWA MAPENZI. INGELIKUWA MAPENZI YANAUZWA BASI NINGELIKUWA MIONGONI MWA WATEJA WAKE, LAKINI WAPI. HATA UKIMUHONGA MWANAUME KWA HALI NA MALI ILI AKUPENDE, MAPENZI YENU, NIMEGUNDUWA KWAMBA HUWA NI NJIA FINYU NA YENYE MSINGI WA KULAZIMISHA UPENDO KATIKA KUTA ZA MACHUNGU.
YOTE HAYA NIMEYAJARIBU, NILICHOKIPATA AU FAIDA YANGU IMEKUWA NI KUITWA MPUMBAVU, KUPOTEZA MALI NA PESA, KUJIVUNJIA HESHIMA NIKIGOMBANA NA WASICHANA WADOGO, AMBAO WANA NYOTA ZA KUPENDWA NA MARANYINGINE NIKIPEWA VYEO, KIKIWEMO CHEO CHA SHUGA MAMI(MWANAMKE, AMBAE NI MTU MZIMA, MWENYE KUISHI AU KUNUNUWA PENZI KWA WAVULANA WADOGO AU SERENGETI BOYISE KATIKA MSINGI WA VISHAWISHI VYA ZAWADI).
KUHUSU MTOTO, HAMU SINA AU MATEGEMEO YA KUMPATA MTOTO TENA. KWASABABU NILIPOKUWA MDOGO NILIWAZA NA KUTAMANI MTOTO NIKIWA NA UMRI WA MIAKA 30, LAKINI NILIPOFIKIA UMRI WA MIAKA 24 HADI 29 NILIPATA MIMBA ZAIDI YA TATU, NA NIKAZITOA ZOTE. KWA NINI NILITOA MIMBA ZANGU TATU ? KWASABABU NILIKUWA SIJAPANGA KUZAA NIKIWA NA UMRI WA MIAKA 29 BALI NI KIWA KATIKA NJIA YA UMRI WA MIAKA 30. LAKINI MPAKA SASA SINA MOTO WALA MME NIMECHEZEA VYOTE NA VYOTE VIMEPEPERUKA KAMA UPEPO MAISHANI MWANGU. KWELI USICHOKIFAHAMU UNAHITAJI KUKIJUWA.
SIJUWI NI MRUDIE MUUMBA WANGU AU NIBAKI KWASHETANI, WOTE TUSUBIRI HUKUMU YA MWENYEZI MUNGU ?

No comments:

Post a Comment