KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Friday, September 11, 2009
Kiongozi mwandamizi wa LRA akamatwa
Serikali ya Uganda imetangaza imemkamata kiongozi mmoja mwandamizi wa kikundi cha waasi cha Lord's Resistance Army (LRA) kinachoendesha mampano na majeshi ya serikali.
Msemaji wa jeshi la Uganda amesema Okot Atiak alikamatwa wiki mbili zilizopita katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Hata hivyo hakutoa maelezo zaidi.
Okot Atiak anatuhumiwa kuongoza wapiganaji wa kundi hilo la waasi waliowauwa raia zaidi ya 200 katika kijiji kimoja kaskazini mwa Uganda mwaka 1995.
Hata hivyo msemaji wa LRA amekanusha madai hayo ya jeshi la Uganda.
LRA imekuwa ikiendesha mapambano kwa miaka 20 iliyopita, hali iliyopindukia hadi nje ya mipaka ya nchi hiyo, wakiwa na nia ya kuiangusha serikali ya Uganda na kuunda taifa litakalofuata sheria za Biblia.
Waasi hao katika vita vyao wamekuwa wakiendesha vitendo vya ukatili, ikiwemo kuwakata watu viungo, utekaji nyara na ubakaji wa wasichana na wanawake.
Maelfu ya watu wamekufa na wengine wengi wamezikimbia nyumba zao wakati waasi hao wa LRA wakiendesha ukatili wao eneo la Afrika ya Kati.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment