KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Friday, September 11, 2009
Ghasia zazidi kutanda mitaa ya Kampala
Mapigano yamezuka huko Kampala mji mkuu wa Uganda, yanayohusisha vikosi vya usalama na wanaomuunga mkono kiongozi wa kijadi mwenye ushawishi mkubwa nchini Uganda mfalme wa Baganda, Ronald Muwenda Mutebi II.
Vijana wenye hasira kutoka kabila la Baganda ambalo ni kubwa nchini humo waliweka vizuizi mitaani na kuchoma moto huku wakiwarushia polisi mawe waliojibu kwa mobomu ya kutoa machozi.
Taarifa za hivi karibuni zinasema kuwa watu saba wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa akiwemo afisa wa polisi.
Vurugu hizo zilianza wakati wa maandamano ya kupinga jaribio la serikali ya Uganda kutaka kuzuia mfalme wa Baganda kutembelea eneo la Uganda linalohofiwa kungalitokea furugu iwapo atalitembelea.
Nguvu ya dola
Kwa mujibu wa katiba ya Uganda mfalme huyo anazuiwa kujihusisha na masuala ya kisiasa ya kitaifa ingawaje ana ushawishi miongoni mwa watu wake.
Mwandishi wa BBC wa Afrika Mashariki anasema kumekuwako na mvutano wa miaka mingi kati ya mfalme huyo na serikali ya Uganda hususani katika mapendekezo ya mabadilko juu ya suala la ardhi.
Wakati huo huo, Redio ya Ufalme wa Buganda, Central Broadcasting Service maarufu kama Chabasa - imefungwa. Hatua hiyo imechukuliwa na baraza la Utangazaji Uganda kuhusiana na machafuko yaliyoanza Alhamsi jioni mjini Kampala.
Ghasia hizo zinasemekana kusambaa hadi maeneo ya nje ya Kampala kama vile Masaka umbali wa kilomita karibu 130 mashariki mwa mji mkuu, Mpigi, takriban kilomita 60 na Mukono, na Mityana. Maeneo haya yote yako katika Buganda.
Usafiri ulitatanika katika baadhi ya mitaa ambapo watu walilazimika kwenda masafa marefu kwa miguu mpaka kwao. Wasiwasi baado ulikuwa umetanda hadi usiku kuingia lakini yaonyesha polisi imedhibiti hali ya mambo.
Ufalme ya Baganda ni moja kati ya falme nne za kijadi nchini Uganda. Falme hiyo ilipigwa marufuku mwaka 1966 na baadaye kurejeshwa tena katika miaka ya 1990.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment