KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Friday, September 11, 2009
Boti iliyozama S Leone haikuwa na maboya
Waziri wa Habari wa Sierra Leone, amesema boti iliyozama ikiwa imefurika watu zaidi ya 150, haikuwa na maboya maalum ya kuokolea wakati inapotokea ajali.
Waziri huyo Ibrahim Ben-Kargbo, ameiambia BBC "taratibu hazikufuatwa, boti haikuwa na maboya ya kuokolea maisha na watu wamekufa".
Boti hiyo imeelezwa ilibeba watoto wengi waliokuwa kutoka likizo baada ya shule kufunguliwa.
Kiongozi aliyesimamia kazi ya kuokoaji amesema watu 36 wameokolewa na miili 10 imepatikana.
Naye msemaji wa polisi Ibrahim Samura ameiambia BBC, "wavuvi na vikundi vya watu vilivyojitolea wanajitahidi kutafuta miili ya watu wengine katika eneo ilipotokea ajali na matumaini ya kupata miili zaidi yanaongezeka".
Lakini Bwana Ben-Kargbo amezielezea jitahada za uokoaji kwa sasa ni za kutafuta miili zaidi kutokana na matumaini ya kupata watu walioa hai kufifia.
Boti hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka mji wa Shenge kuelekea kijiji cha Tombo umbali wa kilometa 65 karibu na mji mkuu Freetown.
Ilizama sio mmwendo mrefu tangu ilipong'oa nanga Shenge karibu na kisiwa cha Plantain.
Mwandishi wa BBC katika mji wa Freetown Lansana Fofana amesema boti hiyo hadi sasa haijapatikana na shughuli zote za uvuvi karibu na kijiji cha Tombo zimesimamishwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment