KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Saturday, September 12, 2009
ISHARA YA MAPENZI BAINA YA WATU MAISHANI IKOJE ?
MAPENZI NI NINI MAISHANI?
MAPENZI NI MFUMO AMBO, UNAMWEZESHA KILA MTU KUWA NA UHURU WA MAONI MAISHANI.
HAKUNA JAMBO AMBALO NI RAHISI NA NIZURI MAISHANI, KAMA KUWA KARIBU NA WATU MAISHANI. WATOTO NI BINAADAMU WENYE KUPENDA YULE MWENYE KUWAVUTIA NA NDIO MAANA UKIANGALIA PICHA HII, UTAONA KWAMBA KUNA WATU WAZIMA WA TATU, LAKINI KUNA WATOTO PIA. UKIANGALIA KWA MAKINI KATIKA PICHA HII, UTAONA KWAMBA KUNA MAKUNDI, LAKINI KUNDI KUBWA LINAASHIRIA MSINGI WA UPENDO JUU YA JAMBO FULANI. UKIANGALIA PICHA HII, WAKWANZA KUSHOTO NI CASTO NA WAPILI NI MODESTUS WA TATU KATIKA WATU WAZIMA NI ISMAIL (ISMADO), AKIWA NA KUNDI KUBWA LA WATOTO. KWA NINI KUNDI KUBWA LA WATOTO LIWE KARIBU NA ISMADO ZAIDI YA MODE NA CASTO ?
JIBU NI KWAMBA KILA MTU ANAKUWA NAKILE ANACHOKIPENDA MAISHANI MWAKE NA KWAMDA MUAFAKA. KWA SASA CASTO, HUU NI MDA WAKE WA KUPOZI LENYE STAIRI YA KUWEKA MIKONO YOTE MKONONI NA HUKU AKIANGALIA KILICHOPO KULIA KWAKE. KUHUSU MODE, YUKO BIZE NA SIMU. KUHUSU ISMAIL, YEYE ANAPIGA STORI NA WATOTO KATIKA MFUMO WA MAPENZI. KILA JAMBO MAISHANI LINAHITAJI MSINGI ILI MAPENZI YAKE YATIMIZWE.
BAADHI YA WATU WANAHISI KWAMBA WATOTO HAWANA MAONI NA UHURU WA KUONESHA HISIA ZAO JUU YA KILE WANACHOKIONA AU KUKISIKIA.
NA MARANYINGINE TUNAJIKUTA TUKIWAKEMEA WATOTO PALE WANAPOTOA MAONI AU KUULIZA SWALI, HII SIO NJIA SAHIHI KWASABABU WATOTO HAWANA MFUMO WA HILA AU CHUKI MAISHANI MAO LABDA WAFUNDISHE NA WAZAZI WAO AU JAMAA ZAO. WATOTO KUISHI NAO KUNAHITAJIKA UMAKINI WENYE MFUMO WA KUJALI HISIA ZAO. TUSICHUKULIE WATOTO KAMA WATU WENYE UJUZI WA KUTAMBUA AU KUCHUJA JAMBO LOLOTE LA HATARI AU LENYE MADHARA KWA HARAKA, NDIO MAANA WANAITWA WATOTO. MAANA YAKE HATA AKILI ZAO NIZA KITOTO.
WATOTO NI WANAFUNZI WAZURI KATIKA MSINGI WAKUNASA SAUTI, MANENO HATA PICHA YA MATENDO. NDIO MAANA UKITAMKA NENO AU UKITENDA JAMBO FULANI NA UKIWA KARIBU NA MTOTO, KWAKO NI RAHISI KUSAHAU ULICHOKIZUNGUMZA AU KUMTENDEA MTOTO HUSIKA, LAKINI MTOTO (MSHUHUDA AU MLENGWA) HUHIFADHI NENO AU KITENDO HUSIKA, KWA MDA MREFU, NA HUWA NI MWENYE KUKUMBUKA TASWIRA YAKO, PINDI ANAPOKUTANA NA YALE MANENO AU KILE KITENDO SEHEMU YEYOTE.
KUNA BAADHI YA WATU WENYE KUJIJENGEA NIDHAMU YA KUWATISHIA WATOTO AU KUKAA MBALI NA HISIA ZAO. MTU KAMA HUYO HUWA NI MWENYE KUOGOPWA NA WATOTO, NA MARANYINGINE ANAWEZA KUSHINDWA KUPATA MAWAZO AU TAHADHARI YENYE MANUFAA KUTOKA KWA MTOTO HUSIKA. LAKINI KUMBUKA YA KWAMBA KUWAPENDA WATOTO, HAKUFUNDISHWI BALI HUTOKANA NA MSINGI WA MAPENZI YA NAFSI YA MTU JUU YA KUWAPENDA WATOTO AU BINAADAMU WENGINE.
UTAKUTA MARANYINGINE KUNA WATU AU MTU AKIFIKA MTAANI KWAKE, UTAKUTA KUNDI LA WATOTO LIKIACHA SHUGHULI ZAO NA KWENDA KUMLAKI SWAHIBA WAO. UNAWEZA KUKUTA FURAHA YENYE MFUMO WA MAPENZI AMBAYO MTOTO ANAONESHA JUU YA MTU FULANI, INAWEZA KUWA KUBWA ZAIDI KULIKO ILE WANAYOONESHA AU KUONESHA PINDI ANAPOMUONA BABA MZAZI. MFUMO HUU UNAJITOKEZA KUTOKANA NA MOYO WA BINAADAMU, MOYO WA BINAADAMU, HUMPENDA ZAIDI YULE MWENYE KUUPENDA ZAIDI.
NA NDIO MAANA KILA KUNDI LA WATU, HUUNDWA NA MAPENZI AU KUAFIKIANA JUU YA JAMBO FULANI KATIKA MSINGI WAKUPENDA KUKAA PAMOJA.
UMOJA BAINA YA BINAADAMU NI RAHISI NA UNAWEZA KUWA IMARA PALE UTAKAPOKOSA KASORO YA CHUKI NA KUJIJENGEA KUTA ZENYE MSINGI WA UVUMILIVU NA UPENDO.
TUNAWATAKIA RAMADHANI NJEMA WOTE WANAOSOMA NA KUPENDA MAISHANI.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment