KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Saturday, September 12, 2009
ASALAMU ALAYKUM MAISHANI CLUB?
ASALAMU ALAYKUM MAISHANI CLUB?
KATIKA MAISHA KILA JAMBO LINAWEZEKANA, LAKINI KUTOKA KATIKA MSINGI WA NIA, JITIHADA, NA MATUMAINI YENYE UJASIRI. PICHANI KULIA NI MODESTUS KISHA KUSHOTO YUKO FIDES. WATU HAWA NI MARAFIKI NA NIWADAU WA MAISHANI CLUB. SIKU ZOTE TUNAPOSEMA, MAISHANI CLUB, TUNAMAANISHA MFUMO WA MAISHA, MAANA YAKE MFUMO WA KUJIPA RAHA KATIKA TAMADUNI TOFAUTI, MILA TOFAUTI, DINI TOFAUTI, KOO TOFAUTI NA RANGI TOFAUTI. CLUB YETU YA MAISHANI INAMPA KILA MTU KUWA NA MSINGI WA UHURU WA MAONI NA UKUTA WA AMANI NA UTULIVU.
UKIANGALIA KWA MAKINI, NYUMA YA MODE NA FIDES, KUNA PICHA YA SIMBA MWENYE HISTORIA MBAYA KWA BINAADAMU. SIMBA YULE ALICHUKIWA NA BINAADAMU WA MLOKA (TANZANIA), HADI KULA NYAMA YAKE NA KUMJENGEA KABURI LENYE MFUMO WA KUMBUKUMBU YA VIFO VYA WATU AROBAINI ( WATU 40)
(WERE KILLED 40 PEOPLE) NA KUJERUHI SABA (KUJERUHI 7)
(AND WOUNDED SEVEN PEOPLE). HILI NIJAMBO LA KUSIKITISHA VILE VILE NILAZIMA KWETU SISI KAMA BINAADAMU, WALIOJALIWA AKILI TIMAMU NA MWENYEZI MUNGU TUJIULIZE SWALI KAMA :
KWANINI YULE SIMBA ALIWEZA KUWASHABULIA WANA KIJIJI NA KUWAUWA BAADHI NA KUWAJERUHI BAADHI?
BAADA YA KUJIULIZA, KATIKA MCHAKATO WA KUPATA JIBU NA KUTOWA HOJA, TUNAAMINI KUNA UWEZEKANO WA KUGUNDUWA JAMBO FULANI, AMBALO LINAWEZA KUTUFANYA KUWA WACHA MUNGU ZAIDI AU KUREKEBISHA TABIA ZETU AU KUPATA KINGA YA KUJIEPUSHA NA MADHARA MAPEMA.
MODESTUS NA FIDES, WAMEWEZA KUFIKA ENEO LA TUKIO NA KUWEZA KUWASIKILIZA WANA KIJIJI, USHUHUDA WAO. MODESTUS NA FIDES, KAMA TUNAVYOWAONA, UTAONA KENYE PICHA WAKIWA NA POZI LA UJASIRI. POZI HILO LINAASHIRIA USHUJA WAO MAISHANI. NAFIKIRI MISTA SIMBA ANGEFUFUKA WASINGEWEZA KUPIGA POZI KAMA HILO!!!!!!!!!??
LAKINI KAMA TUNAVYOJUWA MAISHANI, UTULIVU HUJENGA AMANI NDANI YA NYOYO HUSIKA. NA NDIO MAANA MODESTUS NA FIDES WAMETULIA NA KUPIGA POZI LA UTULIVU KWASABABU WANAAMINI KWAMBA KWA SASA MLOKA KUNA AMANI. SIMBA MLA WATU ALIISHA KUFA ZAMANI.
TUNAWATAKIA RAMADHANI NJEMA WA DAU WOTE WA MAISHANI.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment