KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Friday, September 25, 2009

HAKUNA MAISHA BILA MAZOWEZI MAISHANI


ASALAMU ALYKUM MAISHANI CLUBU?

KULIA NI BROTHER NEMES POWER CHIWALALA NA KUSHOTO
NI ISMAIL A.K ISMADO. ISMADO NA NEMES NI MARAFIKI NA HUFANYA KAZI ZAO KWA USHIRIKIANO MZURI KABISA.
KWA UPANDE WA POWER CHIWALALA, ANAAMINI KWAMBA HAKUNA MAISHA BILA MAZOWEZI MAISHANI MWAKE. NEMES NI MTU MWENYE UWEZO WA NGUVU YA MWILI NA NI MJUZI WA MBINU NYINGI ZA KIMAZOWEZI. WATU WENGI NAFIKIRI WANAMFAHAMU HUYU JAMAA (POWER CHIWALALA) KUTOKANA NA UMUHIMU WAKE WA KUSAIDIA JAMII, KATIKA KUJENGA AFYA ZAO NA KUSAIDIA WANAMICHEZO, ZIKIWEMO TIMU MAARUFU KAMA YANGA NA SIMBA. POWER CHIWALALA VILELE NI MOJAWAPO WA WATU WALIONGOZA SAFARI YA KUTEMBEA KWA MIGUU, KUANZIA DAR ES ALAAM HADI DODOMA, KATIKA KUMBUKUMBU YA BABA WA TAIFA MWALIMU J.K NYERERE. POWER CHIWALALA AMESHIRIKI KATIKA HARAKATI YA KUANDAA NA WALEMAVU KITAIFA NA KUFANIKIWA KUWAONGOZA WALEMAVU WA TANZANIA NCHINI WINGEREZA MWAKA WA 2002 NA AUSTRARIA MWAKA WA 2006. HII NI HATUWA MUHIMU NA YENYE KUHITAJI KUPEWA SIFA NA VIONGOZI NA WANACHI WOTE WA TANZANIA NA AFRICA. SIRAHISI MTU AANZISHE WAZO NA KULITETEA NA KULIFANYIA KAZI NA KULIFANIKISHA KIMATAIFA AKOSE SIFA AU MSAADA WA VIFAA NA NISHATI YENYE KUMTIA NGUVU YA KUENDELEZA VIPAJI NA MICHEZO KATIKA NCHI YETU NA AFRICA, KUSIFIWA KATIKA HARAKATI YA POWER CHIWALALA, KWA KUHAKIKISHA NCHI YAKE(TANZANIA) NA EAST AFRICA NA AFRICA ZIKIFANIKIWA KATIKA KUJENGA AFYA ZAO NA MAZOWEZI.
POWER CHIWALALA NI MPEZI SANA NA NIMWALIMU WA WANYANYUWAJI WA VYUMA VYENYE UZITO WA HALI YA JUU KITAIFA. VILE VILE NEMES AU POWER CHIWALALA ANAJULIKANA KWA JINA LA SON OF AFRICA. JINA HILI LILIANDALIWA NA WALEMAVU AMBAO ALIKUWA AKIWAFUNDISHA NA KUFANIKISHA SAFARI YAO YA KWANZA KUELEKEA KWENYE OLIMPIC NCHINI WINGEREZA NA CHINA.
POWER CHIWALALA ANA UWEZO WA KUVUTA MAASKARI HAMSINI 50 NA KWA MONO WAKE MMOJA NA KUZIWIA GARI KUONDOKA NA KUZUIA PIKIPIKI TATU (CC 250, MOJA KICHWANI, MKONO WA KULIA NYINGINE NA WAKUSHOTO NYINGINE) KWA MPIGO. POWA CHIWALALA ANAO UWEZO WA KIMWILI, GARI LINAWEZA KUPITA JUU YA MKONO WAKE NA ASIATHIRIKE. VILE VILE POWER CHIWALALA ANAWEZA KUNYANYUWA AU KUMBEBA MTU MWENYE UZITO WA KILO TISINI AU MIA KWA MENO………………………………………………………………..N.K.

TANZANIA IMEBEBA WATU WENYE UWEZO MKUBWA WA MATENDO NA MANENO LAKINI UWEZO WAKUFIKISHA VITU VYAO VYENYE MAFUNDISHO NA AFYA KWA JAMII, NDIO NJIA AMBAYO AMEKUWA NI YENYE MSINGI WA MABONDE NA MILIMA NA KUJENGEWA KUTA ZA LAWAMA NA FITINA NATIKA MSAADA WA UTEKELEZAJI.
NAAMINI POWER CHIWALALA ANGEWEZESHWA NA NCHI (WANANCHI, SERIKALI AU MASHIRIKA BINAFSI) ANGEWEZA KUFANYA MAMBO MENGI NA YENYE KUMBUKUMBU YA KUDUMU KATIKA TAIFA LETU NA EAST AFRICA NA AFRICA KWA UJUMLA. LAKINI JAMBO HILI LA KUWASAIDIA WATU WENYE VIPAJI AU KAZI ZINAZOONEKANA KATIKA JAMII, LIMEKUMBWA NA MSINGI WA KILA MTU KUANGALIA MASLAHI YAKE NA SIO YA TAIFA LAKE NA JAMII. LILIKUWA FUNDISHO TOSHA KWA KILA MPENDA MICHEZO KUANGALIA UWEZO WA MTU HUYU, NA KUJITUMA KWAKE KATIKA KUWASAIDIA WALEMAVU NA KUFANIKISHA SAFARI YAO YA KUELEKEA KATIKA NCHI KUBWA (WINGEREZA 2002 NA AUSRRARIA 2006 NA NCHINA 2008) NA MASHINDANO MAKUBWA DUNIANI.
HUU ULIKUWA NI MFANO WENYE KUONEKANA KATIKA MANENO NA MATENDO YA POWER CHIWALALA AU SON OF AFRICA.
NEMESI NI MTU MWENYE UWEZO WA KUISHI SEHEMU YEYOTE NA KUISHI NA WATU WA KILA AINA BILA KUJALI RANGI, KABILA, KOO AU LUGHA.
NI MTU MWENYE KUTUMIA BAADHI YA MDA WAKE AKIFANYA SHUGHURI ZAKE NA MARANYINGINE AKIPANGA MDA WA MAZOWEZI NA UTANI.
POWE CHIWALALA, ALIWEZA KUTEMBELEA NA KUONESHA MAANJUMATI YAKE KATIKA NCHI YA RWANDA, UGANDA, TANZANIA, AUSTRARIA, WINGEREZA NA KOMORO. KOTE HAPO, ALIPEPERUSHA BENDERA YA TAIFA LA NCHI YAKE NA KUITAMBUWA KWAMBA TANZANIA INA WATU WENYE UWEZO WA MANENO NA MATENDO KATIKA MSINGI WA PICHA YA SURA YA POWER CHIWALALA.
TUNAMENGI YA KUMZUNGUMZIA SON OF AFRICA LAKINI MDA HAUTOSHI. UKITAKA KUMJUWAV SON OF AFRICA NA MAANJUMATI YAKE, ANGALIA MATANGAZO YA KIPINDI CHA MICHEZO YA EAST AFRICA TV. UTAMSHUHUDIA KIJANA HUYO SHABABI.
MUNGU AKUBALIKI NA AKULINDE NA AZIDI KUKUPA MOYO WA KUPENDA JAMII NA NCHI YAKO POWER CHIWALALA.

KWA UPANDE WA ISMADO, POWER CHIWALALA ANASEMA “ MIMI NILIPOMUONA ISMADO, NILIFANIKIWA KUONA MTU MWENYE MANENO YENYE UTATA NA UTANI MWINGI SANA, LAKINI KADIRI NILIVYOZIDI KUZUNGUMZA NAE, NILIMUONA KAMA MTU MWENYE KUNIFAA MAISHANI MWANGU. NILIWEZA KUMSHAWISHI ISMADO KUWA MSHAURI WANGU KATIKA MSINGI WA AFYA NA MAZOWEZI NA AKAKUBALI OFA YANGU NIKAJISIKIA KUWA NA FARAJA NA FURAHA MOYONI MWANGU. ISMADO NI MTU MWENYE MTAZAMO WA MBALI KATIKA KUJALI HISIA YA MTU MUONGEAJI NA MTENDAJI. ISMADO NI MTU MWENYE KUKUPA MOYO NA KUJARIBU KUKUPA NJIA NA KUKUONESHA MFUMO WA UNAWEZA. YAANI MAANA YAKE UNACHOKIWAZA KINAWEZEKANA LAKINI KWANZA NIA IWEPO. NAKUMBUKA NENO AMBALO ISMADO ALINIAMBIA, NAMII NIKAINAMA KISHA NIKAMTAZAMA, UDOGO WAKE NA MANENO YAKE YA BUSARA NIKASEMA HIVI, ISMADO UKWELI NDIO HUU NAMI NTAUFUATA KABISA NA ASANTE KWA MUONGOZO WA HEKIMA.
ISMADO ALINIAMBIA HIVI “ BROTHE NEMES USIJALI, UTAFANIKISHA JITIHADA YAKO, LAKINI KUMBUKA BROTHER NEMES, HUWEZI KUPATA JAMBO LOLOTE BILA KUUMIA (NO PAIN NO GAIN ).
KWA KWELI NILIVUTA HISIA NA NIKAONA KWAMBA NIWAJIBU WANGU WAKUONGEZA BIDII NA MAUMIVU ILI NIWEZE KUFANIKISHA KUWAPELEKA WALEMAVU KATIKA MASHINDANO YA KIMATAIFA NA KWELI NILIFANIKIWA”
KILA JAMBO LINAWEZEKANA MAISHANI MWETU. ISMADO NA KUPENDA NA NTAZIDI KUKUPENDA NTAKAPOKUWA HAI. MUNGU ATUJALIE AFYA NJEMA AMIN.
TUNAWATAKIA RAMADHANI NJEMA NA SIKU KUU YA EID.

No comments:

Post a Comment