KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, September 25, 2009

CHUKI + SIJUI + SAMAHANI = USIJALI


CHUKI NI KIFAA AMBACHO KINAHIFADHI UADUI NDANI YA NAFSI YA BINADAMU. UADUI SABABU YAKE KUBWA NI NAFSI KUCHUKIZWA NAJAMBO (MATENDO AU MANENO) AU MTU FULANI.
MANENO NDIO MSINGI WA MAWAZO AU MSIMAMO WA NAFSI HUSIKA. MSIMAMO WA MANENO YA NAFSI, UNAONEKANA KATIKA MATENDO YAKE.

SIJUI NI KIFAA AMBACHO KIMEBEBA, UJINGA WA NAFSI JUU YA UJUZI WA KITU( MAPISHI, KUANDIKA, KUSOMA, KUWASHA AU KUENDESHA……N.K)FULANI.
UKOSEFU WA FAHAMU WA NAFSI JUU YA KITU AU MTU FULANI, NDIO MSINGI WAKUJENGA JENGO LA SIJUI MOYONI MWA MTU.
JENGO LA SIJUI NDANI YA MOYO WA NAFSI, LINAHIFADHI MAMBO MENGI, MOJAWAPO NI UJINGA, CHUKI, LAWAMA, HISIA….N.K.
JENGO LA UJINGA NDANI YA NAFSI YA MTU, LINAPOKUWA NA MARADHI YA UJINGA, LAWAMA, CHUKI, HISIA MBAYA……N.K, DAWA YAKE HUWA NI KIFAA KIITWACHO SAMAHANI.

SAMAHANI IMETENGENEZWA KATIKA MATIRIO (MATERIAL) AMBAYO NI MCHANGANYIKO WA WEMA, HURUMA, MSAADA…..N.K.
NENO SAMAHANI LINA THAMANI KUBWA SANA NA NIGHALI KATIKA MAISHA YETU. NDIO MAANA ILI KILA MTU AJUWE KWAMBA THAMANI YA SAMAHANI NI KUBWA, EBU ANGALIA KWA UPANDE WA KILA MTU, KUTOA AU KUPOKEA SAMAHANI!!!!??
KWA UPANDE WAKO UNAJISIKIAJE UNAPOSAMEHEWA AU UNAPOSAMEHE ?
JE UNAJIHISIJE UNAPOSHINDWA KUMSAMEHE AU MTU FULANI KUSHINDWA KUKU SAMEHE?

KAZI KWAKO TAFAKARI, KISHA TOA MAONI YAKO KUPITIA NJIA YA . www.maishani.blogspot.com
SAMAHANI INATOA FURSA YA KUJIELEZA NA NAKUHOJI SWALI. MAELEZO NI NJIA MOJA WAPO YA KUONESHA MTAZAMO AU MSIMAMO WA NAFSI. NA MASWALI NI NJIA MOJAWAPO YA NAFSI KUHITAJI KUJUA JAMBO AU MTU FULANI.MAJIBU YENYE KUJITOSHELEZA NDIO YANAYOTENGENEZA MSINGI WA SAMAHANI. SAMAHANI NI PAMBO LENYE MANUKATO NDANI YA JENGO LAUJINGA LILILOPO NDANI YA NAFSI. DAWA YA HASIRA, CHUKI, LAWAMA, FITNA, MAUMIVU…….NI SAMAHANI.

ISMAIL VS ISMADO = ISMAIL
ISMAIL ALIKUWA NI RAFIKI SANA WA ISMADO. BAADA YA MDA MREFU, MAPENZI YAO YALIINGILIWA NA KASORO YA CHUKI. CHUKI ILISABABISHWA NA KUTAFAUTIA NA KIMANENO NA KIVITENDO BAINA YA ISMAIL NA ISMADO.
ISMAIL ALIMWAHIDI ISMADO KWAMBA, ATAMSAIDIA KUTATUWA TATIZO LAKE LA KIFEDHA. LAKINI ISMAIL ALIPOMUAHIDI ISMADO, ALIKUWA HAJAMWAMBIA, NI LINI ATAKAPOMPA HICHO KIASI CHA FEDHA. SIKU ZILIZIDI KWENDA NA KWENDA.
MOYONI MWA ISMAIL ALIKUWA AKIJITAHIDI KUTAFUTA KILE KIASI CHA FEDHA ILI AWEZE KUTATUWA TATIZO LA SWAHIBA WAKE. LAKINI KWA UPANDE WA ISMAIL ALIKUWA AKIKABILIWA NA TATIZO LA KODI YA NYUMBA KABLA YA AHADI HUSIKA. KAMA KAWAIDA MTU HAWEZI KUISHI NA RAFIKI MMOJA MAISHANI.
KILICHOTOKEA ISMADO ALIKUWA NA SHIDA KUBWA YA MARADHI NA ALIKUWA ANAHITAJI MATIBABU. ISMADO ALIMPATA RAFIKI WA KIKE NA MWENYE FEDHA YA KUTOSHA. ISMADO ALIJARIBU KUMGUSIA ISMAIL, KUHUSU PENZI LAKE NA YULE MWANAMKE. AKAMWELEZA KWAMBA AMEMPATA MWANAMKE MWENYE MAPENZI JUU YAKE, NA AMEMUAHIDI KUMLIPIA MATIBABU NA KUAHIDIANA KUFUNGA NDOA.
ISMAIL ALITOA MAONI YAKE YA MOYO, NA AKASEMA “ SAWA MIMI NAKUBALI KWAMBA UNASHIDA TENA KUBWA KUHUSU AFYA YAKO, LAKINI KWA UPANDE WA KUISHI NA YULE MWANAMKE MIMI SIONE KWAMBA KUNA USTARABU WA KUISHI NA MWANAMKE, AMBAE HUJAMUOA(KUNGA NDOA). NA NILAZIMA KABLA HUJAFUNGA NDOA NA HUYO MWANAMKE, MKAPIME UGONJWA WA UKIMWI, KISHA UJUWE NA HISITORIA YA MAISHA YAKE. KWASABABU HISTORIA YA MAISHA YAKE ITAWEZA KUKUPA NAFASI NZURI YA KUJUWA TABIA YAKE VIZURI. NA KUMBUKA KWAMBA TABIA INAENDANA NA VITU VIKUU VIWILI. NAVYO NI MANENO MAZURI NA MATENDO YANAYOTIMIZA MSEMO”
ISMADO AKASEMA “ HIVI ISMAIL WEWE HUNIAMINI, KWAMBA NINA UWEZO WA KUANGALIA MAMBO HAYO YOTE. MIMI NNA UGONJWA WA KISUKARI, NILIMWELEZA YULE MWANAMKE (Mariana) NA AKAKUBALI KUISHI NA MIMI NA AKAKUBALI KUNISAIDIA MATIBABU. MIMI NAONA KWAMBA HAKUNA BAHATI KAMA HII, AU UNASEMAJE ISMAIL?”
“ISMAIL SAWA, LAKINI KUMBUKA KWAMBA MIMI SINA UWEZO WAKUZUIA HISIA ZAKO, LAKINI NNAWEZA KUTOWA MAONI NA USHAURI KWAKO KAMA RAFIKI YANGU MPENDWA MAISHANI.”
ISMADO AKASEMA “OK. ISMAIL TUENDELEE NA MAZUNGUMZO MENGINE, KUHUSU MASWALA YA HUYU DEMU NTAJUWA LAKUFANYA KESHO.”
ISMAIL ALIPATA SIMU YA MDENI WAKE WA KITAMBO. AKAMWELEZA RAFIKI YAKE KUHUSU, SIMU ILIOPIGWA. ISMAIL AKASEMA “ISMADO NIMEPOKEA SIMU YA MSHIKAJI, ANASEMA KWAMBA NENDE UBUNGO STENDI, AKIFIKA ATANIPA KIASI CHA LAKI 350,00, LAKINI BAADA YA KUNIKABIDHI HICHO KIASI YEYE ANAENDELEA NASAFARI, KUELEKEA MWANZA.”
ISMAIL AKAMWAMBIA JAMAA YAKE (ISMADO), TWENDE TUKIBAHATIKA KUCHUKUWA HICHO KIASI, ITABIDI NIKUPE LAKI MOJA NA NUSU YA MATIBABU YAKO, KISHA KIASI KITAKACHO BAKI NTATOA ADVANCE YA KODI YA NYUMBA”
ISMAIL BAADA YA KUMWELEZA ISMADO WALIKUBALIANA KWENDA PAMOJA HADI UBUNGO. WALIPO KUWA NJIANI YULE MWANAMKE ALIWEZA KUMPIGIA SIMU ISMADO NA KUMUULIZA HIVI : “ ISMADO UKO WAPI NAHITAJI KUKUONA SASA HIVI!”
ISMADO AKASEMA “KWAKWELI MPENZI SIWEZI KUJA KWASABABU NIPONJIANI KUELEKEA UBUNGO.”
YULE MWANAMKE AKASEMA “UKO NA NANI? AU UMEANZA KUNISALITI?”
ISMADO AKASEMA “HAPANA MPENZI NIKOPAMOJA NA RAFIKI YANGU ISMAIL””
YULE MWANAMKE “KWAHIYO UNAMAANISHA KWAMBA ISMAIL NI KIPENZI CHAKO ZAIDI YANGU…….KILA SIKU NIPO NA ISMAIL!? …ISMAIL!? … ISMAIL?!
SASA SIKILIZA UNAKUJA SASA HIVI AU LA? KUNA MAMBO MUHIMU NAHITAJI KUZUNGUMZA NA WEWE NA USIJE NA ISMAIL, KWASABABU YANAHUSU SHIDA YAKO NA NILAZIMA TUMALIZE KILA KITU SASA HIVI. KAMA HUTAKI SHAULI LAKO MIMI SIMO TENA. »
ISMADO
» APANA SIKILIZA ………… ? SIMU IKAKATIKA, BILA KUFIKIA MUAFAKA. »
ISMADO ALITULIA KWA MDA WA DAKIKA 5 AKITAFAKARIIIII.

KISHA SWAHIBA WAKE (ISMAIL) AKAMUULIZA « VIPI MBONA KIMIA, ALAFU UMEBADILIKA KATIKA MFUMO WA CHUKI NA HASIRA.
ISMADO AKASE » ISMAIL NAOMBA USIMAMISHE GARI.”
ISMAIL “ NTASIMAMISHAJE GARI BILA SABABU YA MSINGI. TUNAPOKWENDA BADO HATUJAFIKA ! ISMADO. EBU NIAMBIE ULIKUWA UKIZUNGUMZA NINI NA MARIANA?

ISMADO AKASEMA “UNAJUWA NINI ISMAIL!!!!!!!!!!!!!!?”
KISHA AKATULIA KWAMDA WA DAKIKA KAMA MBILI, KISHA A AKAWAZA MOYONI MWAKE “ PINDI NILIPOONGEA NA MPENZI WANGU ALISEMA KWAMBA ATANISAIDIA KILA JAMBO LEO LEO, NAMI NNAVYOMJUWA ISMAIL, HAWEZI KUNIRUHUSU KUONDOKA BILA KUFIKA UBUNGO.
JE! ISMAIL AKIMKOSA HUYO JAMAA ITAKUWAJE? AU HUYO JAMAA AKIJA NA STORI, NTASAIDIKA VIPI? HUYU MWANAMKE NI MTU WA KUNITOA KATIKA SHIDA NDOGO NDOGO( MSOSI, NGUO, POKETI MANE NA ANAHITAJI KUNISAIDIA MAMBO MENGINE MAKUBWA!!!, SIJUI NIFANYEJE MIMI ISMADO.
LAKINI KUNA JAMBO LA KUFANYA KWA SASA NI KUMCHENJIA ISMAIL KWA KILA NJIA, NA NILAZIMA ATAKASIRIKA NA KISHA ATASIMAMISHA GARI NAMI NTAONDOKA KWENDA KWA MPENZI WANGU KULA BATA”
ISMAIL IKABIDI, KUONA KIMIA KIMEZIDI KWA JAMAA YAKE, IKABIDI ASIMAME, PEMBEZONI MWA BARA BARA. KISHA AKAMUULIZA ISMADO “VIPI ISMADO KUNA TATIZO AU MWANAMKE HUYO AMEKUZINGUWA? ACHANA NAWANAWAKE KIJANA, UTACHANGANYIKIWA, JAMBO MUHIMU KWASASA NI KUTAFUTA FEDHA YA KUMALIZA TATIZO LAKO LA AFYA NA LANGU LA KODI YA NYUMBA TU”
ISMADO “ UMEMALIZA?”
ISMAIL “ KWANI VIPI?”
ISMADO “OK UNAONA KWAMBA UGONJWA WANGU NI KUCHANGANYIKIWA AU SIO?”
ISMAIL “ ACHA UTANI ISMADO, KWANZA NIMESIMAMA SEHEMU MBAYA NGOJA TUWAHI”
ISMADO “ OK. NAONDOKA NA SHIDA YANGU NTAJUWA JINSI GANI YA KUIMALIZA, WALA SIHITAJI MSAADA WAKO WA MASIMANGO!?”
ISMAIL “ OH OH….BASI BWANA YAISHE, IBILISI TAYARI AMEISHA INGIA BAINA YETU”
ISMADO “ UNAMWIDA MPENZI WANGU IBILISI, SASA SIKILIZA IBILISI NI WEWE NA NDUGU ZAKO, NA SITAKI MJADALA MWINGINE”
ISMADO AKAFUNGUWA MLANGO KISHA AKATOKANJE AKAONDOKA BILA HATA KUAGA.
ISMAIL AKAKA KWENYE GARI KWA MDA WA DAKIKA 20, AKIWAZA, KUHUSU UTATA ULIOJITOKEZA BAINA YAKE NA RAFIKI YAKE. KISHA ISMAIL AKAONDOKA, KUELEKEA UBUNGO. ALIPOFIKA UBUNGO ALIWEZA KUMPATA RAFIKI YAKE, WAKAFURAHIA NAFASI YAO YA KUKUTANA TENA MAISHANI, KISHA ISMAIL AKAPEWA MZIGO WAKE WA FEDHA, KIASI CHA LAKI TATU NA NUSU (350,000), KISHA AKAAGANA NA RAFIKI YAKE, WAKATAKIANA KILA LA GHERI MAISHANI MWAO. KISHA KILA MMOJA AKAENDELEA NA SAFARI YAKE.
BAADA YA ISMAIL KUPOKEA KILE KIASI CHA FEDHA, ALIMPIGIA RAFIKI YAKE, ILI AMPE HABARI NJEMA YA KUTATUWA MATAZIZO YAO. SIMU ILIITA KWA MDA MREFU, BILA MAFANIKIO YA KUPOKELEWA.
ISMAIL ALIJARIBU TENA NA TENA……..MWISHO WAKE SIMU ILE ILIZIMWA.
ISMAIL ALIFIKIRI KWAMBA LABDA RAFIKI YAKE(ISMADO) BADO ANAHASIRA NA CHUKI JUU YA YALE MAZUNGUMZO YAO.
ISMAIL ALIAMUA KWENDA NYUMBANI KWAKE,AKAPUMZIKA MPAKA KESHO ASUBUHI.
ISMAIL ALIJARIBU TENA NA TENA KUMPIGIA ISMADO, LAKINI HAKUNA UPOKEAJI WA SIMU NA MWISHO WAKE YULE MWANAMKE ALIPOKEA SIMU NA KUANZA KUMTUSI ISMAIL.

HUU NDIO MWANZO WA GEMU (GAME) BAINA YA ISMAIL NA ISMADO

URAFIKI WA ISMAIL NA ISMADO ULIINGIA DOSARI YENYE MSINGI WA CHUKI. ISMADO ALIENDELEA NA YULE MWANAMKE KATIKA MSINGI WA MAHABA. YULE MWANAMKE ALIWEZA KUTEKELEZEA ISMADO, AHADI YAKE YA MATIBABU NA AKAWEZA KUMFUNGULIA BIASHA YA KUUZA VIFAA VYA MAGARI.
ISMAIL ALIENDELEA KUISHI KATIKA WAKATI MGUMU, AKIFIKIRIA KUHUSU MAISHA YAKE NA MTENGANO BAINA YAKE NA SWAHIBA WAKE.
SIKU MOJA ISMAIL ALIKUWA AKIENDESHA GARI, AKAJIKUTA KATIKA AJALI. ISMAIL ALIPELEKWA HOSPITALI BILA KUJUELEWA, FAHAMU ILIPOMRUDI, ALIJIKUTA AKIWA YUPO KATIKA CHUMBA CHA WAGONJWA NA AKIWA AMEFUNGWA PINGU.
ISMAIL ALIJARIBU KUULIZA, ASIKARI POLICE KUHUSU KUWEPO KWAKE HOSPITALI AKIWA AMEFUNGWA PINGU. ASKARI POLICE ALIMWAMBIA KWAMBA ALIPATA AJARI PINDI, ALIPOKUWA AKIJARIBU KUKIMBIA POLICE. ISMAIL ALIMUULIZA POLISI “ KWANI MIMI NILIKUWA NA HATIA GANI ILI NIFIKIYE HATUWA YA KUKIMBIA POLICE?
ASKARI ALIMJIBU KWAMBA, YEYE NI MTUHUMIWA WA MADAWA YA KULEVYA NA AMEKAMATWA NA KIL KUMI ZA BANGI NDANI YA GARI ALILOKUWA AKIENDESHA.

ISMAIL ALIMJIBU POLICE KWAMBA YEYE ALIKUWA HAJABEBA BANGI WALA YEYE SIO MUUZAJI WA BANGI. ASIKARI ALIMJIBU HIVI “MAELEZO YOTE HAYO YAMEISHA ANDIKWA NA UJIANDAE KWENDA MAHAKAMANI. SISI TUNACHOKIDHIBITI NACHO NI KIASI CHA KILO KUMI CHA BANGI”

ISMAIL ALISHANGAAA SANA NA AKAJIKUTA KATIKA NJIA PANDA. ISMAIL ALIMUOMBA YULE ASIKARI, KUMPIGIA SIMU RAFIKI YAKE ISMADO, LAKINI YULE ASIKARI ALIMWELEZA ISMAIL, KWAMBA HARUHUSIWI KUTUMIA SIMU WALA AINA YOYOTE YA MAWASILIANO.

ISMAIL ALIKUBALI MATOKE, KISHA BAADA YA SIKU YA NNE, AKAPELEKWA MAABUSU. ISMAIL ALIKAA MAABUSU WIKI MOJA, KISHA KESI YAKE IKAPELEKWA MAHAKAMANI. KESI ILIPOFIKA MAHAKAMANI, ILISOMWA NA AKAHUKUMIWA MIAKA KUMI (10 YEARS) MAABUSU.
PINDI ISMAIL ANAPELEKWA MAABUSU, ALIMUONA ISMADO NA YULE MKE WAKE MAHAKAMANI, KISHA YULE MWANAMKE AKAMWAMBIA ISMAIL “ SIKU ZOTE UMBWA HACHEZI MBALI NA MNYUMBANI, NA ANAPOJARIBU KUCHEZEA MBALI NA HOME, ANAPEWA ADHABU KIASI CHAKE. SAFARI NJEMA”

ISMAIL ALISHINDWA KUJUWA NI NANI YULE MWANAMKE WALA LENGO LA YALE MANENO. ILIKUWA MARA YA KWANZA KWA ISMAIL KUMUONA YULE MWANAMKE. LAKINI ISMAIL ALIINGIWA NA GHOFU ALIPOMUONA AKIWA NA ISMADO. ISMAIL ALIHISI KWAMBA YULE NDIE YULE MWANAMKE WA SWAHIBA(ISMADO) WAKE WA ZAMANI.

KWA KWELI ISMAIL ALIHISI MAUMIVU MAKALI NDANI YA NAFSI YAKE, LAKINI MATOKEO YOTE ALIMWACHIA MWENYEZI MUNGU.

ISMAIL ALIPELEKWA MAABUSU, KUTUMIKIA ADHABU YENYE MFUMO WA FITINA NA CHUKI, KUTOKA KWA SWAHIBA WAKE NA BIBI YAKE.
ISMAIL ALITUMIKIA KIFUNGO HADI MIAKA KUMI IKAISHA.

ISMAIL ALIPOTOKA JELA, ALIKUTA MAISHA YA BONGO YAMEBADILIKA SANA. ISMAIL ALIJIKUTA HANA SEHEMU YA KUKIMBILIA.
ISMAIL ALIOMBA MAMA MMOJA AMSAIDIE NAULI, KISHA YULE MAMA ALIMPA SHIRINGI ELF 2,000 KWA KUMHURUMIA.
ISMAIL ALIPANDA GARI LA SEGEREA KARIAKO, KISHA ALIPOTAKA KUTOA NAULI AKAMKUTA ISMAIL NDIE KONDA WA ILE DALADALA.
ISMAIL ALISHANGAA SANA KUMWONA SWAHIBA WAKE KATIKA MAZINGIRA YALE.
ISMAIL KISHA AKAMUULIZA “ HIVI NI WEWE ?!!! SIAMINI MACHO YANGU”
ISMADO AKAANZA KUTOKWA NA MACHOZI, NA ISMAIL ALISHINDWA KUJIZUIA, AKAANZA KILIO KIKUBWA. UKAWA NI MSIBA MKUBWA NDANI YA DALADALA.
WASAFIRI WALISHANGAA NA KUSHINDWA KUELEWA NI NINI KINACHOENDELEA BAINA YA WATU HAO WA WILI.
ISMADO ALIKUWA PAMOJA NA MPIGA DEBE, AMBAE JINA LAKE LILIJULIKA NA KAMA MUSA.
ISMADO AKAMWAMBIA MUSA “TAFADHALI NAKUOMBA UENDELEE NA SAFARI MIMI NNASHUKA KIYUO KINACHO FUATA”
MUSA ALIJARIBU KUMUULIZA ISMADO “MSHIKAJI NI NINI KILICHO KUSIBU?”
ISMADO AKASEMA “MWANANGU NI STORI NDEFU, WEWE ENDELEA KAMA VIPI TUTAONGEA TOMORO (TOMORROW)”

ISMADO AKAMWAMBIA ISMAIL “ISMAIL NAOMBA UJIZUIE NA KILIO KWANI YOTE YALIOKUSIBU MIMI NDIO MSINGI WAKE”
WAKASHUKA KWA PAMOJA KITUONI, WAKIWA KWENYE HALI YA MASIKITIKO.

ISMAIL AKAMWAMBIA SWAHIBA WAKE TUNAELEKEA WAPI? SWAHIBA WAKE AKASEMA TUNAELEKEA SINZA MAKABURINI.

ISMAIL “ MAKABURINI?”
ISMADO “ NDIO”
ISMAIL “ KUNA NINI MAKABURINI”
ISMADO “KUNA BARUA YA UPATANISHO WA MAJUTO.”
ISMAIL “OK”

ISMAIL NA ISMADO, WAKAELEKEA SINZA MAKABURINI.

WALIPOFIKA SINZA MAKABURINI, ISMADO ALIINGIA NDANI YA FENSI YA MAKABURI, KISHA AKASIMAMA PEMBEZONI MWA KABURI MOJA, KISHA AKASEMA “ WEWE KABURI LEO NDIOP SIKU YANGU YA KUTAJA SABABU YAKO YA UBAYA JUU YAKO, BAINA YA NYOTA MBILI ZILIZO PENDANA KISHA UKAZITENGANISHA USIKU WA GIZA KATIKA MSINGIO WA MAHABA NA MSAADA WA MACHOZI NA MACHUNGU YA NAFSI ZOTE MBILI.

ULITUTENGANISHA KATIKA JINA LA WEMA WA MAPENZI, LAKINI NIA YAKO ILIKUWA NI NGUZO YA KUANGAMIZA NAFSI AMBAYO ULIITA MPENZI. SIWEZI KUKU SAHAU WALA KUISHIWA NA MACHUNGU YAKO NDANI YA NAFSI YANGU. ULINIFANYA KUTENDA UBAYA NYUMBANI MWETU, UKAENDELEA KUSAMBAZA CHECHE ZA MOTO NDANI YA YAJIRANI BOARA WA NAFSI YANGU. YOTE HAYA SI KULAUMU WALA SILAUMU MTU YEYOTE BALI UMASIKINI WANGU ULINIFANYA NICHUKUWE MAAMUZI YASIOFAA. NI KAWEZA KUMGEUKA SWAHIBA WANGU KATIKA NJIA YENYE MSINGI WA MSAADA MWEMA . MSAADA WENYE UTULIVU NA AMANI, KISHA NI KAMTAFUTIA SABABU YA KILA AINA ILIMLADI NI HARIBU UHUSIANO WANGU NAYEYE, ILI NIKUPATE WEWE MARIANA.

YOTE HAYA NAILAUMU NAFSI YANGU.

ISMADO AKAENDELEA KULALAMIKA, NA KUMWAMBIA SWAHIBA WAKE HIVI :
ISMAIL KAMA NI HUKUMU NASTAHIKI KIFO NA KAMA UTAAMUA KUISHI NA MIMI KATIKA DUNIA HII, UKINITAZAMA, KWANGU MIMI SITAWEZA KUVUMILIA KUKUONA MBELEANGU KATIKA GHALI HII YA UBAYA NA CHUKI NA FITINA NA MAUMIVU NILIOKUSABABI MAISHANI MWAKO ISMAIL.

ULINIPENDA KWA MANENO NA UKADHIHIRISHA KWA VITENDO. KILA JAMBO ZURI ULINIELEZA NA KILA JAMBO BAYA ULINIPA TAHADHARI. KUTOKANA NA MOYO WANGU KUWA DHAIFU JUU YA MWANAMKE, NILIWEZA KUKUSALITI NA NIKAINGIA KATIKA KUNDI LA KUKUANGAMIZA KWA USHAURI WA MWANAMKE HUYU AMBAE SASA NI MAITI, KATIKA KABURI HILI LA SINZA MAKABURINI.

CHUKU KUBWA YA MWANAMKE HUYU MIMI NDIE MSINGI WAKE.
ISMAIL KAMA UNA KUMBUKA, KUNA KIPINDI AMBACHO NILIKUELEZA KUHUSU UHUSIANO WANGU NA MWANAMKE HUYU, NIKAKUELEZA KUHUSU MTAZAMO WAKE JUU YANGU, ALIKUWA MWENYE NIA NJEMA YAKUNISAIDIA KIMATIBABU NA KUNISHAWISHI KUMUOWA.
YOTE NILIKUELEZA LAKINI KWA UPANDE WAKO, HUKUWA TAYARI JUU YA MAPENZI YANGU NA HUYU MARIANA AMBAYE KWA SASA NI MAITI.
ULINISHAURI KUHUSU AFYA YANGU, UKASEMA KWAMBA NI VUMILIE UKIPATA PESA UTANISAIDIA, KISHA UKASEMA KWAMBA IKIWA NNAMPENDA MARIANA, LAZIMA NIJUE HISTORIA YA MAISHA YAKE KISHA TUPIME AFYA ZETU. YOTE HAYO NILIKUBISHIA KUTOKANA NA TAMAA YA NAFSI YANGU. LAKINI KWASASA NI SEME NINI ISMAIL !!!!!!!!!!!!

YOTE ULIOYAZUNGUMZA NILIYASHUHUDIA.
SAFARI YENYE LENGO LA KUNISAIDIA YA UBUNGO, NILIIVUNJA KWA MAKUSUDI, ILI NIKAPATE MAZIWA KUTOKA KWA MARIAYANA, LAKINI NJIA NILIOTUMIA KUPATA SAFAR HIYO ILIKUWA YENYE MACHUNGU BAINA YANGU MIMI NAWEWE ISMAIL.

KWANI NILIPOACHANA NA WEWE KATIKA NJIA YA MACHUNGU,YENYE UKUTA WA CHUKI NA LAWAMA, NIKAELEKEA KWA MARIANA. NILIPOWASIRI KWA MARIANA, NILIMKUTA AKIWA AMENUNA, NA AKAWA HAWEZI AU HATAKI KUONGEA NA MIMI. MOYONI MWANGU NILITAMBUA KWAMBA HANITAKI TENA NA NIKAHISI KWAMBA AKINIFUKUZA SITAPATA MSAADA WAKE TENA NA KWA UPANDE MWINGINE NIMEISHA KUUDHI WEWE SWAHIBA WANGU. NIKAONA KWAMBA SIWEZI KUPATA MSAADA SEHEMU NYINGINE KWA URAHISI. KWASABABU NDUGU ZANGU WALITENGA, NIKAPATA KIMBILIO KWAKO WEWE ISMAIL. ULIKUWA NI MTU MWENYE UWEZO MDOGO WA KIFEDHA, LAKINI ULIAMUA KUISHI NA MIMI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU NA YENYE KUHITAJI UVUMILIVU. KWA UPANDE WETU MAPENZI YALIKUWA NI JAMBO LA KILA SIKU, TULIPOKUWA TUMEKOSEANA TOFAUTI ZETU TULIKUWA TUKIZIMALIZA KATIKA MFUMO WA MAZUNGUMZO NA MATENDO.
LAKINI ALIPOINGIA MWANAMKE, UHUSIANO WETU ULIANZA KUFIFIA NA KUINGIA CHACHU NDANI YAKE. MWANZO TULIKUWA TUKIZUNGUMZIA KUHUSU MIKAKATI YA MAISHA, LAKINI BAADA YA KUINGIA MWANAMKE BAINA YETU, NILIANZA KUPOTEA NYUMANI, NA NILIPOKUWA NIMERUDI NILIKUWA NI MWENYE MAZUNGUMZO YENYE MSINGI WA KUTOA SIFA ZA MARIANA.

NNAMENGI YA KUELEZA LAKINI ISMAIL, MIMI NAONA HUKUMU YANGU UNAYO WEWE NA MUNGU. KWANI NILIOKUTETENDEA NI CHUKIZO KWA MWENYEZI MUNGU.

NILIPOWASIRI KWA MARIANA NIKAONA HATAKI KUNIELEWA, NIKAMWELEZA KUHUSU LENGO LAKO (ISMAIL) JUU YA MAPENZI YANGU NA MARIANA.

NIKASEMA
« MARIANA MPENZI WANGU, WEWE SIOMTU WAKUNITENGA KAMA ISMAIL, ALIVYONITENGA KWASABABU YA MAPENZI YANGU NA WEWE »

MARIANA ALIKUWA NI MWENYEKUBADILIKA, NA AKATOWA TABASAMU KUBWA KISHA ASEMA « UNAMAANISHA NINI ? »
NIKAMWELEZA KWAMBA ISMAIL, HATAKI WEWE UWE MPENZI WANGU, NA KUNA UWEZEKANO WATABIA ZAKO KUWA SIO NZURI NA KUNA UWEZEKANO WA KUWA UMEATHIRIKA
(UNA UKIMWI). MARIANA ALIONEKANA KUNYWEA, KISHA AKATABASABU.
MARIANA AKASEMA “ ISMADO HAYO NI MAMBO YA BINAADAMU, HUWA NIWENYE WIVU SIKU ZOTE. USIDHANI KWAMBA ISMAIL NI WAKWANZA AU ATAKUWA WA MWISHO KUZUNGUMZA HAYO MANENO YA KIPUMBAVU”

MARIANA, AKAINGIA CHUMBANI AKAKA KWAMDA WA DAKIKA TANO, KISHA AKARUDI AKIWA AMEVAA NGUO YA KULALIA. AKANIAMBIA, MDA WA CHAKULA UMEFIKA, TULE KISHA KUNA JAMBO LA KUNIELEZA NA NDILO LENYE MSINGI KATIKA MAISHA YANGU.
LIKAA MEZANI, KISHA TUKALA, BAADA YA CHAKULA CHA USIKU, MARIANA ALINIPA MAJI YA KUOGA KISHA, NGUO ZANGU AKAZIINGIZA NDANI YA MAJI. NIKABAKI SINA NGUO ZA KUVAA. NILIPOMUELEZA KUHUSU NGUO ALISEMA “ ACHANA NA NGUO ZA MTUMBA VAA KANGA, KESHO ASUBUHI KABLA HUJAAMUKA, UTAANZA KUVAA NGUO ZA ITALI, AMBAZO HAZINA KIKWAPA.

ALINIPELEKA CHUMBANI MWAKE, AKANIONESHA SEHEMU YA KULALA KISHA, AKANIKABIDHI KIASI CHA DOLA $20,000.

NILIZIMIA KWA DAKIKA KADHA, KISHA NILIPORUDISHA FAHAMU, NIKAJIKUTA KATIKA NJIA YA MATENDO YA HUKUMU. NILISHINDWA KUVUMILIA NIKATENDENDA, NA NIKAZOEA KUTENDA BILA KUJALI AJALI YA UKIMWI.


Itaendelea……………………………………..

No comments:

Post a Comment