KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, September 12, 2009

HADITHI YA KWA NINI NAMCHUKIA MAMA MZAZI !?



MAMA NI CHIMBUKO LA MAISHA YANGU, NAAMINI NA NTAZIDI KUAMINI KWAMBA SINA MAMA MWINGINE MAISHANI MWANGU, ISIPOKUWA NNAKIWANDA CHA MATESO NA CHENYE MSINGI WA PICHA YA MZAZI ASIYEKUWA NA HURUMA.
MIEZI TISA TUMBONI MWAKO, ILIKUWA NI JAMBO LA KUJIFUNZA MENGI KUHUSU UMUHIMU, HASARA, FAIDA …..N.K., KUHUSU ULICHOKIBEBA TUMBONI MWAKO.

NI NINI MAANA YA UPENDO, KUMBE HUJAJUWA MAANA YA KUITWA MLEZI AU MZAZI.

NILIVYOANZA KUPATA UFAHAMU NA KUANZA KUISHI MAISHA YENYE MAHITAJI YA KITOTO NILIJIKUTA KATIKA UTATA NA UHASAMA WA MAISHA YA TAABU NA KUSIMANGWA.

ADHABU, KIPIGO, NA MATESO YA KUCHOMWA MOTO KATIKA BAADHI YA VIUNGO VYA MWILI WANGU, VILIKUWA ALAMA ZA KUDUMU MAISHANI MWANGU KISA MTOTO KAJIKOJOLEA AU KAMWAGA CHUMVI.

MAMA MZAZI HAKUNITENDEA HAKI KATIKA MSINGI WA MALEZI YA MZAZI NA MWANAE.
UKWELI NI KWAMBA BABA MZAZI ALIKUWA KAMA TAMBIKO MAISHANI MWANGU. SIJAWAHI KUBEMBELEZWA NA KUFURAHIA MAISHA KAMA WATOTO WENGINE.
TOFAUTI ZA UHUSIANO WA BABA NA MAMA ZILINIFANYA NIWEZE KUWA KAMA MTOTO ALIYECHANGANYIKIWA, KWA SABABU MAPAMBANO YA BABA NA MAMA, USHINDI WAO WA HASIRA ULIKUWA NI MSIBA AU MSHAHARA MAISHANI MWANGU.
KUTOKANA NA TABIA NGUMU YA MAMA MZAZI NA BABA, HALI HIYO ILIWAFANYA BABA NA MAMA MZAZI KUACHANA NA KILA MMOJA KUCHUKUWA CHA KWAKE. KWAKWELI NILIKUWA MTOTO MDOGO SANA MWENYE UMRI WA MIAKA MINNE (4 YEARS), KATIKA UMRI HUO, KILA MTOTO HUWA ANAHITAJI UPENDO NA MSAADA WA MAELEKEZO YENYE MSINGI WA KUTAMBUWA MAISHA NA KUPEWA UHAKIKA WA KUISHI KATIKA UTULIVU, AMANI NA UPENDO.

BAADA YA KUTENGANA KWA MAMA NA BABA, NILICHUKULIWA NA BABA MZAZI. NA KUMBUKA BABA MZAZI ALIKU AMEOA MWANAMKE MWINGINE. NILIPELEKWA KWA MAMA WA KAMBO, NA AKAWEZA KUNILEA NA KUNIPA MAPENZI NA UPENDO AMBAO SIJAWAHI KUYAPATA KWA MAMA MZAZI.

MAMA WA KAMBO ALIKUWA AKITUMIA MANENO SANA KATIKA MUONGOZO WAKE NA KUCHAPA MIGUUNI NILIPOKUWA NIMEZIDI KATIKA KUKOSA. LAKINI MAMA MZAZI ALIKUWA AKITUMIA SANA BAKOLA, NGUMI, MATEKE NA MARANYIMGINE KUINGIZA KISU KATIKA MOTO NA KUNICHOMA MWILINI MWANGU. MATUSI NA MANENO YENYE MFUMO WA HASIRA NA CHUKI JUU YANGU VILIKUWA KAMA WIMBO WA TAIFA MAISHANI MWANGU.

JAMBO AMBALO SIJAPATA, MDA WA KULIULIZA MAMA MZAZI NI HILI, “ HIVI MAMA ULIZALIWA NA MZAZI KAMA ULIVYO NIZAA MIMI? AU ULINIZAA KWA BAHATI MBAYA ?”

MIMI BAADA YA KUWA NA UMRI WA MIAKA SABA BILA KUMWONA MAMA MZAZI,
NILIONA NI JAMBO LA KAWAIDA NA MAPENZI YA MOYO WANGU YALIZIDI JUU YA MAMA WA KAMBO NA BABA MZAZI KUTOKANA NA UPOLE NA MAELEKEZO YA HURUMA WALIKUWA NAYO, JUU YA MAISHA YANGU.

SIKU MOJA KOSA LIKAJIRUDIA

MAMA MZAZI ALIOMBA KUNIONA NA BABA MZAZI AKAKUBALI KUNIPELEKA KUMSALIMIA MAMA MZAZI.
NILIFIKA NIKAMWONA, LAKINI MOYO WANGU HAUJAWA NA FURAHA JUU YAKE, NILIMWONA KAMA MTU WA KAWAIDA. NIKAKAA NAYE KWA MDA WA SIKU TATU, SIKU YA NNE NILIVUNJA KIKOMBE KWA BAHATI MBAYA, KAMA KAWAIDA YAKE MATUSI, FIMBO, MIKWINO VIKAWA CHAKULA CHANGU, HADI NGOZI YA MWILI IKACHUNIKA KWA MIKWIDO. MOYONI MWANGU NIKATAMANI KUKUMBIA NYUMBA LAKINI NIKASHINDWA. SIKU INAYOFUATA, NILIJISAHAU NIKAKOJOA KITANDANI, KWA KWELI NILICHOMWA MOTO MGONGONI NA NIKAHISI MAUMIVU MAKALI NA YENYE KUJIRUDIA MARA KWA MARA.

NILIVYOONDOKA KATIKA NYUMBA HIYO, NILIMSHUKURU MUNGU KUNIONDOA MIKONONI MWA MAMA AMBAYE HANA HURUMA JUU YA MWANAE.

ROHO INAUMA NNAPOSIKIYA WATOTO WENZANGU WAKITAJA NENO MAMA NA BABA AU NNAPOWAONA WAZAZI WA KIZUNGUMZA NA WATOTO WAO NA KUWAPA MWELEKEO WA MAWAZO( FANYA NA USIFANYE) MAISHANI MWAO.

KILA NNAPOKA NAKUFIKIRI NAJIULIZA, KWA NINI MIMI NIMEKUWA CHAGUO LA MZAZI KATILI ASIYEJUWA THAMANI YA MAPENZI YA MTOTO JUU YA WAZAZI WAKE.
JE! MLEZI HUYU(MAMA WA KAMBO) AMBAYE NIMEKUTANA NAYE, KATIKA UHUSIANO WAKE NA BABA MZAZI, MBONE ANANIPENDA SANA WALA HAJAWAHI KUNICHOMA MOTO WA LA MIKWIDO YA KUNKOA NGOZI HANA HAZINA YAKE.

KWAMARA NYINGINE NAFIKIRIA, KAMA MAMA MZAZI ANAMATATIZO YA AKILI LAKINI JIBU NASHINDWA KULIPATA, KUTOKANA NA KUONA KWAMBA NI MTU MZIMA NA MWENYE AKILI YAKE.
UGOMVI WA BABA NA MAMA UMEKUJA KUWA KIKWAZO CHA MAISHA YANGU BORA KATIKA MSINGI WA THAMANI YA KUISHI NA WAZAZI WANGU WA WILI.
MARA YA KWANZA NILIJUWA KWAMBA MAMA MZAZI ALIKOSEA NA AKAJUTIA ADHABU ZAKE ZA MATESO JUU YANGU, LAKINI MWISHO WASIKU(BAADA YA MIAKA MIWILI) AKAWADHIHIRISHIA NDUGU ZAKE NA BABA NA MKE MWENZA UBAYA WA ROHO YAKE.
WALINISHANGAA SANA NILIPORUDI NYUMBANI NA MAKOVU YA MIKWIDO NA DONDA LAKUCHOMWA MOTO, KWA MDA WA WIKI MOJA TU!!!!!.
WALISHANGAA SANA, NA WALIPONIULIZA NILIWAHADITHIA KILA JAMBO KUHUSU TABIA ZA MAMA MZAZI, NA KILA MMOJA ALILANI TABIA HIYO NA BAADHI YAO WA KAWEZA KUSEMA HIVI
“KAMA ZINGELIKUWEPO AU KUNA LESENI YA MTU KUWA AU KUITWAZAZI, BASIMAMA YAKO MZAZI, LESENI YAKE INGELIFUTWA NA AKAPEWA ADHABU YA KIFUNGO CHA MAJUTO MAISHANI MWAKE.
INAKUWAJE MWANAMKE AKUBALI KUZAA AKOSE HURUMA JUU YA MWANAE.

MAMA, WEWE NI MZAZI WANGU, LAKINI IMANI JUU YAKO BADO INANIPA MASHAKA. NAJILAZIMISHA KUKUPENDA LAKINI MOYO WANGU UKIKUMBUKA MATESO ULIONIPA NA FIKIRA ZAKO ZENYE UHABA WA MAPENZI SITAMANI KUKUONA HATA KAMA NTAAMBIWA KWAMBA UNAUMWA. KWASABABU UKIUMWA MAMA UTAPATA MAUMIVU, KAMA YALE AMBAYO ULIYAFANYA STAREHE YA NAFSI YA YANGU, KWA MAANA HIYO SIDHANI KWAMBA KUNA JAMBO LA KUNITISHA JUU YA MAISHA YAKO. LABDA KIFO CHAKO NDICHO KITAKACHOWEZA KUNIFANYA NIJE KUZIKA KIWANDA CHA MAUMIVU YA MWILI WANGU.

NA WATHAMINI WANAWAKE WENGINE ZAIDI YAKO MAMA, KWASABABU WENGI WANANIONEA HURUMA NA WANATUMIA NJIA ZA BUSARA KATIKA KUNIELEKEZA AU KUNIPA MUONGOZO MAISHANI MWANGU.
THAMANI YAKO MAMA MZAZI JUU YANGU NI MOJA, NAYO NI KUZALIWA AU KUWA NA MAMA MKATILI MWENYE UKOSEFU WA MALEZI YENYE MSINGI WA ELIMU.
MAMA UNGELIKUWA NA ELIMU YA KUJUWA NI NINI MAANA YA FAIDA, HASARA, UMUHIMU NA THAMANI YA MZAZI KATIKA JAMII, BASI UNGEAMUA KUPOKEA MIMBA YA BABA AU KUACHA KUIPOKEA, ILI USIJE UKAJIJENGEA NJIA YA CHUKI KUTOKA KWA MWANAO.

KUMBUKA MAMA , MOYO WA BINAADAMU UNAPENDA YULE ANAYEUPENDA MAMA WALA SIKOSA LANGU BALI MATENDO YAKO, ULISHINDWA KUNIPA MAPENZI YAKO NAMI NIMESHINDWA KUKUPA MAPENZI YANGU.
NDIO MAANA NAKUCHUKIA MAMA .

@ BY ISMAIL MUSA A.K ISMADO @

No comments:

Post a Comment