KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, August 25, 2009

Viongozi wakutana Addis Ababa


Hii itakuwa ni mara ya kwanza viongozi wa Afrika kukutana kwa ajili ya kuzungumzia maswala yanayohusiana na madadiliko ya hali ya anga, na kutaka kuyazungumzia kwa sauti moja.
Mkutano huu unaodhaminiwa na Umoja wa Afrika, unakusudiwa kusaidia nchi za Afrika kuwasilisha msimamo moja katika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa kujadili mabadiliko ya hali ya anga utakaofanyika huko copenhangen, Denmark mwezi December mwaka huu.

Kufikia sasa, nchi mbalimbali barani Afrika zimewasilisha misimamo tofauti tofauti jambo ambalo wengi wanakusudia limechangia kutotiliwa maanani msimano wao.

Akizungumza na BBC, Daktari Alice Kaudia ambaye ni katibu katika wizara ya mazingira nchni Kenya alisema kwamba ilikuwa ni muhimu kwa nchi za Afrika kushirikiana katika jitihada za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya anga.

Dk Kaudia alisisitiza kwamba matatizo yanayotokana na mabadiliko ya anga hayawezi kutatuliwa na nchi moja.

Mkutano huu unaoongozwa na mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Muammar Gaddafi, unatarajiwa kujadili maswala mbali mbali yakiwemo pendekezo kwa nchi zilizoendelea kupunguza uchafuzi wa hewa kwa asilimia 40.

No comments:

Post a Comment