KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, August 25, 2009

Kifo cha Michael Jackson ni dawa kali


Nyaraka za mahakama nchini Marekani zinaonyesha kuwa mwanamuziki Michael Jackson alikuwa akitibiwa ugonjwa wa kusikia mauvimu makali ya mwili na kutokupata usingizi.
Nyaraka za ofisi ya Mchunguzi wa Vifo vinavyotokea katika mazingira ya kutatanisha, zinaonyesha kuwa mwili wa mwanamuziki huyo ulikutwa na kiwango kikubwa cha dawa kali za kutuliza mauvmivu.

Ugunduzi huo unafuatia uchunguzi uliokuwa umefanyika kwa siri na ambao kwa sasa umewekwa bayana kwa jamii mjini Houston.

Mwanamuziki huyo alifariki tarehe 25 mwezi June mwaka huu akiwa na umri wa miaka 50, baada ya kupata mstuko wa moyo akiwa nyumbani kwake mjini Los Angeles.

Daktari wa Michael Jackson, Conrad Murray amekwisha hojiwa mara mbili na polisi lakini hajatamkwa rasmi kama ni mtuhumiwa.

Ofisi za Daktari Murray zilivamiwa na polisi mwezi uliopita ikiwa ni sehemu ya uchunguzi wa polisi juu ya kifo cha mwanamuziki huyo.

Wachunguzi wanajaribu kuangalia iwapo kuna kosa la kuua kwa kukusudia kutokana na uzembe kimatibabu, mwandishi wetu Rajesh Mirchandani aliyeko Los Angeles anasema.

Ofisi ya mchunguzi wa vifo vinavyotokea katika mazingira ya kutatanisha bado hajachapisha rasmi taarifa ya matokeo ya uchunguzi iliyopatikana juu kifo cha mwanamuziki huyo.

Na pia ofisi hiyo imeshindwa kuzungumza kuhusu taarifa kutoka shirika moja la habari kuwa chanzo kimoja kisichotajwa cha polisi kinasema kuwa mchunguzi wa vifo vinavvyotokana na mazingira ya kutatanisha amefikia uamuzi kuwa, kifo cha Michael Jackson ni cha kukusudiwa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ofisi ya Mchunguzi Mkuu wa vifo wa Los Angeles, ''amepitia kwa mara nyingine matokeo ya uchunguzi na taaarifa yake ya awali ni kwamba sababu ya kifo cha Michael Jackson ni matumizi ya kiwango kikubwa cha dawa za kutuliza mauvimu.''

Nyaraka hizo zinaendelea kusema kuwa Dr Murray aliwambia polisi kuwa amekuwa akimpa Michael Jackson dawa kali za kutuliza mauimvu ikiwa ni sehemu ya matibabu kwa ugonjwa wa kusikia mauvimu makali ya mwili na kutokupata usingizi.

Lakini alisema alikuwa na wasiwasi kuwa Michael Jackson alikuwa ameathirika kupenda kutumia dawa hizo kali na pia alikuwa akijitahidi kumzuia kwa kumshauri kutumia dawa mbadala.

Lakini asubuhi ya siku ya kifo cha mwanamuziki huyo, Dr Murray anaripotiwa kuwa alimpa Michael Jackson kiwango kidogo cha dawa hizo kali baada ya kuonekana kuwa dawa alizokuwa akitumia hazikufanya kazi.

Aliondoka na kumwacha mwanamuziki huyo peke yake kwa lengo la kupiga simu kadhaa, na ndipo aliporejea alikuta mwanamuziki huyo hawezi kupumua, gazeti la LA Times linataarifu.

Inafahamika kuwa Dr Murray alijaribu kumrudishia uwezo wa kupumua wakati wakisubiri gari la wagonjwa, lakini mwanamuziki huyo alitangazwa kuwa ameshakufa alipowasili hospitali.

Chupa za dawa kali za kutuliza maumivu zilizokutwa katika nyumba ya Michael Jackson zinaonyesha kuwa zilikuwa zimeidhinishwa na madaktari kadhaa, na si Conrad Murray peke yake, lakini bado anabakia kuwa mtu muhimu katika sula zima la uchunguzi, mwandishi wetu anaongeza.

Mapema mwezi huu, DR Murray aliyekuwa ameajiriwa kama Daktari binafsi wa mwanamuziki huyo kwa ajili ya matamasha kadhaa yaliyokuwa yafanyike jijini London mwezi Julai mwaka huu, ameweka mkanda wa video katika wavuti ya youtube kuwashukuru wanaomuunga mkono.

''Nimesema ukweli na nina imani kuwa ukweli utabakia kama ulivyo,'' alisema katika mkanda huo mfupi wa video wa dakika moja.

No comments:

Post a Comment