KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, August 27, 2009

Muswada haki za wanawake Mali watupwa


Rais wa Mali ametangaza hatatia saini muswada mpya wa sheria inayohusu familia na badala yake ataurejesha tena muswda huo bungeni ili uweze kupitiwa upya.

Makundi ya Kiislamu yamekuwa yakipinga sheria hiyo inayowapa haki kubwa wanawake tangu bunge lilipoupitisha mwanzoni mwa mwezi huu.

Rais Amadou Toumani Toure amesema anaurejesha muswada huo bungeni kwa manufaa ya umoja wa taifa.

Viongozi wa Kiislamu wameielezea sheria hiyo ni kazi ya shetani ni ni kinyume na Uislamu.

Zaidi ya asilimia 90 ya wananchi wa Mali ni Waislamu.

Baadhi ya vipengele ambavyo vimezua utata katika sheria hiyo vinawapa haki zaidi wanawake.

Matahalan chini ya sheria hiyo mpya, wanawake hawatakiwi kuwaheshimu waume wao na badala yake waume na wake wawe wanaheshimiana sawa.

Rais Amadou Toumani Toure amesema amechukua uamuzi huo kuhakikisha kunakuwa na utulivu na jamii yenye amani na halikadhalika aungwe mkono na raia wenzake.

No comments:

Post a Comment