KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, August 15, 2009

MAPENZI NI KITU GANI ?


PART 1.




MAPENZI NI KIFAA KINACHOHIFADHI UPENDO, NDANI YA NAFSI YA
BINADAMU.
ILI NAFSI IWEZE KUPENDA MTU AU KITU FULANI, LAZIMA KUWEPO CHANZO CHA UPENDO HUSIKA NDANI YAMOYO WA NAFSI HUSIKA.

KUNA ALAMA MBILI KUU ZINAZOONESHA MSINGI BORA WA UPENDO AU CHUKI JUU YA NAFSI FULANI.
ALAMA HIZO NI :

MANENO:
MANENO YANATOKANA, NA MSIMAMO WA NAFSI HUSIKA, KUMBUKA KWAMBA MANENO MAZURI YANATOKANA NA UPENDO WA MAOYO WA NAFSI HUSIKA. MANENO YENYE UKALI AU MSIMAMO WA UONGO AU KUPINDA PINDA KATIKA NJIA YA UTAMKAJI AU MAZUNGUMZO, TAYARI HUWA NA MASHAKA NDANI YAKE. MASHAKA YA NAFSI YANATOKANA NA KUTOAMINI NAFSI NYINGINE KATIKA MAZUNGUMZO HUSIKA. UAMINIFU UNATOKANA NA UTULIVU WA NAFSI FULANI JUU YA NAFSI NYINGINE. UKIWA NA RAFIKI AMBAYE ANAPOZUNGUMZA NA WEWE, HUPINDAPINDA MANENO AU HUTUMIA MANENO YENYE UKALI, LAZIMA KUANGALIA FAIDA, UMUHIMU, NA HASARA JUU YA MPANGO WA MANENO AU MAZUNGUMZO HUSIKA KWA HARAKA, ILI ASIJE AKAKUPOTEZEA MDA, KATIKA UTENDAJI.



MAPENZI YAKWELI KATIKA MANENO, HUONGOZWA NA MATAMSHI YENYE MSINGI WA FAHAMU(ELIMU), KATIKA MUONGOZO WA MAZUNGUMZO. IKIWA HUNA UJUZI JUU YA MANENO AU MAZUNGUMZO HUSIKA USIONGEENENO LOLOTE BALI JITAHIDI KUULIZA, ILI UPATE KUFAHAMU, UMUHIMU, FAIDA NA HASARA YA MAZUNGUMZO HUSIKA, KISHA POKEA AU TOA USHAURI WENYE MSINGI WA AMANI NA UTULIVU( MAAMUZI YENYE UKOSEFU WA MAUMIVU JUU YA KILA UPANDE).
KILA MTU ANAPENDA NENO NAKUPENDA NA ANACHUKIA NENO NA KUCHUKIA. NDIOMAANA TUNATAKIWA KUISHI KATIKA MSINGI WENYE MATUMIZI YA MANENO YA UPENDO, ILI TUNUSURU UPENDO WETU MAISHANI MWETU.
MATENDO:
MATENDO YANAFSI YANATOKANA NA UTEKELEZAJI WA AHADI YAKE, YENYE MFUMO WA MATAMSHI. NAFSI HUTOA AHADI KATIKA MAZUNGUMZO, NA HUTEKELEZA AHADI KATIKA MATENDO. MATENDO NI USHAHIDI WA MANENO YA NAFSI. UKIWA MWEPESI KUONGEA, USIOWEZA KUYATEKELEZA, UTAKUWA UNAJISHUSHIA THAMANI YA NAFSI YAKO BILA KUJIJUWA. UTAKUWA NA UPUNGUFU WA UAMINIFU NA MARAFIKI.
MABADILIKO MENGI YATAJITOKEZA KATIKA MANENO NA MATENDO KUTOKA KWA MARAFIKI ZAKO. NA MARANYINGINE UNAWEZA KUHISI KWAMBA MUNGU ANAKUONEA AU UMEROGWA KUMBE MAZUNGUMZO NA MATENDO YAKO NDIVYO VIKWAZO VYA MAISHA YAKO KUWA MABAYA AU KUSHINDWA KUELEWANA NA WATU WENGINE. UKIWA NA BIASHARA INAZOROTA AU KUFA KABISA MATOKEO YAKE UTAKUWA NI MWENYE KUILAUMU NAFSI YAKO, KATIKA MSINGI WA NINGELIJUWA.

NINGELIJUWA SIO DAWA BALI DAWA NI KUBALISHA TABIA YAKO, NA KUINGIA KATIKA MFUMO WA MAZUNGUMZO BORA (UKWELI ) NA MATENDO BORA(HAKI KATIKA MATENDO. IKIWA NI MIZANI, MTIMIZIE MTU KIPIMO CHAKE NA IKIWA NI AJIRA MPE MFANYAKAZI WAKO HAKI YENYE UNAFU MAISHANI MWAKE, ILI AWEZE KUWA NA BIDII KATIKA UTENDAJI WA KAZI ZAKO NA KUZILINDA KATIKA MFUMO BORA WA MATUNZO).

JIULIZE ?

WATU WANGAPI WALIOKUAHIDI AU UMEWAAHIDI NA UMESHINDWA KUTEKELEZA AHADI ZAO?
JE! UNAWAFIKIRIAJE?
AU
UNAHISI WAO WANAKUFIKIRIAJE?
IKIWA HUWEZI KUANZA MAISHA YENYE MFUMO WA KIBIASHARA BILA MTAJI, UNAZO AHADI NGAPI ZAKUTOA AU KUPEWA MTAJI ILI UANZE AU AANZE MTU BIASHARA YAKE?
NA KWANINI USITOWE AU USIPEWE?
NI WATU WANGAPI KATIKA JAMII AU FAMILIA WENYE UWEZO KUKUKUSAIDIA KIELIMU, LAKINI AHADI ZAO ZIMEISHIA KATIKA MANENO NA UKOSEFU WA UTEKELEZAJI?

WANGAPI WANAOWATEMBELEA WATOTO WA YATIMA VITUONI NA KUWAPA FARAJA? AU KUWACHUKUWA MAJUMBANI MWAO? AU KUCHUKUWA JUKUMU LA KUWASOMESHA?

WANAWAKE WANGAPI AMBAO WANAPEWA TALAKA NA WAUME ZAO BILA HATIA?
WATOTO WANGAPI AMBAO HAWANA MALEZI BORA MAJUMBANI MWA BABA ZAO, WAKITESWA NA MAMA WA KAMBO?

NDUGU WANGAPI WENYE MOYO WA KUHURUMIAYANA NA KUPENDANA, KATIKA MFUMO WA UYATIMA? AU KATIKA MFUMO WA MAMA MMOJA? AU MAMA NA BABA MMOJA?

KWANINI MAJIRANI KWASASA NI WENYE KUCHUKIANA ZAIDI?

YOTE HAYO YANATOKANA NA UPUNGUFU AU UKOSEFU WA UAMINIFU NA MSINGI WA UPENDO NA UKUTA WA WIVU WA MAENDELEO MAISHANI MWETU.

MWILI WA BINADAMU UNAVYAZO ZAIDI YA SITA VYA MAPENZI, NAVYO NI :

1) MACHO

2) MASIKIO

3) PUA

4) ULIMI

5) MDOMO

6) HISIA

1) MACHO


MCHO : MACHO NI KIFAA AMBACHO KINAWEZESHA NAFSI KUPENDA PICHA ( SURA, RANGI, UMBILE, MWENDO, CHEKO, ……..N.K) KWA NJIA HII TUNAONA KWAMBA MACHO YANA UWEZO WA MWANGA WA PICHA NDANI YA MWILI WA BINADAMU. HUWEZI KUPENDA SURA YA MTU FULANI, BILA NAFSI KUMTAMBUWA KISURA. MAPENZI YA SURA, RANGI, UMBILE, KIMA…..N.K, YANATOKANA NA VIGEZO VYA AKILI JUU YA PICHA (SURA, RANGI….N.K) HUSIKA. MWANAMKE ANAWEZA KUMPENDA MWANAUME KUTOKANA NA SURA YAKE LAKINI MWANAUME, ALIYEPENDWA NA MWANAMKE HUYO, AKAWA HAJAPENDEZWA NA SURA YA HUYO MWANAMKE. NJIA HII INATUONESHA KWAMBA, KILA NAFSI INACHAGUO LAKE LA MAPENZI YA SURA, RANGI, UMBILE………..NA KILA NAFSI INAPOCHAGUA MPENZI MWANAMKE INATUMIA NJIA YAKE YA MACHO ILI KUKAGUWA SURA, RANGI, AU UMBILE LA MTU( MTU NA MCHUMBA). KAZI YA MACHO NI KUINGIZA TASWIRA YA PICHA ( MTU AU KITU ) NDANI YA KILA NAFSI YENYE MACHO MAZIMA.

KUNA BAADHI YA BINADAMU AMBAO WAO NI WALALAMIKAJI JUU YA MATENDO YA WACHUMA AU WAUME AU WAKE ZAO. MALALAMIKO HAYO YANATOKANA NA CHANZO CHA MAPENZI YA MOYO WAKE JUU YA MTU ( MWANAUME, MWANAMKE AU MME NA MKE) HUSIKA. ULICHOKIPENDA MARA YA KWANZA NI SURA SIO TABIA. SURA NA TABIA NI VITU VIWILI TOFAUTI.

SURA NI ALAMA YA UMBILE NA TABIA NI MATENDO YA UMBILE. UKIPENDA ALAMA UTAWEZA KUSTAHAMILI MATENDO YAKE?

NDIO MAANA WATU WALIOWENGI WANAOINGIA KATIKA MAPENZI YA MACHO, HUWA NI WALALAMIKAJI NA WENYE KUVURUGIANA MAISHA KILA KUKICHA.
KAMA NI KUMPENDA MTU , KWANZA KILA UPANDE URIDHIKE NA SURA ZAO NA PILI KUWENI WATU WENYE KUHURUMIANA.




KWA MFANO :

UKIMCHAGUWA MWANAMKE AU MWANAUME KUTOKANA NA UZURI WA SURA, RANGI, UMBILE…….. YAKE, KUMBUKA YA KWAMBA KUNA BAADHI YA BINADAMU AMBAO UTAKUMBANA NAO NA WENYE VIGEZO KAMA VILE ULIVYOVICHAGUWA MARA YA KWANZA.HAKUNA MTU MWENYE KUPENDA KITU KIBAYA, KILA MWANAMKE ANAPENDA KUISHI MAISHANI MWAKE NA MWANAMUME MWENYE SURA, UMBILE, RANGI…...NA KILA MWANAUME ANAHITAJI KUISHI NA MWANAMKE MWENYE SURA, RANGI, UMBILE…,VIZURI. UZURI WA SURA, RANGI, UMBILE……..MSINGI WAKE AU NJIA YA MAPENZI YA SURA, UMBILE, RANGI…...INATOKANA NA MTAZAMO WANAFSI HUSIKA JUU YA MTU ( MKE AU MME) HUSIKA.

USAFI NA MAPAMBO VYA MWANAMKE, NDIO MSINGI WAKE WA KUMVUTIA MWANAUME AU WANAUME. WANAUME WENGI WANAWAPENDA WANAWAKE WASAFI NA WENYE KUJILEMBA NA KUPENDEZA. JAMBO HILO WANAWAKE WANALIFAHAMU, NA NDIO MAANA WANACHUKUWA MDA MREFU KWA KUJIKAGUWA KWENYE KIO, SALUNI WAKITENGENEZA KUCHA, NYWELE……..N.K.

ASILIMIA KUBWA YA MAPATO YA MWANAMKE YANAINGIZWA KWENYE MAVAZI NA MAPAMBO, JAMBO HILO NI JAMBO AMBALO LINACHUKUWA ASILIMIA KUBWA YA UCHUMI WA MWANAMKE.


MWANAMKE MWENYE KUJIPODOA SANA NA KUONESHA VIUNGO VYAKE VYENYE MVUTO KAMA MATITI, MAPAJA, KITOVU…...N.K, ANAJITENGENEZEA NJIA KUBWA YA KUWAITA WANAUME. SIKU ZOTE WANAUME WENYE SIFA YA KUBADILISHA WANAWAKE, WANAPENDA KUCHAGUWA WANAWAKE WENYE KUJIPAMBA NA KUONESHA VIUNGO
( MAKALIO, MAPAJA, KITOVU, MIGUU, MATITI…...N.K)VYAO KATIKA NJIA YA KIMVUTO.



MWILI WA MWANAMKE UNAMVUTO WA KUTISHA JUU YA MWANAUME, NA NDIO MAANA BAADHI YA WANAUME WANASHINDWA KUVUMILIA KATIKA HALI HUSIKA, NA KUJIKUTA WAKIMALIZA HAJA ZAO KATIKA MAVAZI YAO AU MARANYINGINE WA KIWASUMBUWA WANAWAKE HUSIKA, KATIKA NJIA YA KUTONGOZWA NA MARANYINGINE WANAUME WENYE UDHAIVU WA UVUMILIVU, HUJIKUTA KATIKA HALINGUMU YAKUTAMANI KATIKA MSINGI MGUMU WAKUPATA MAHITAJI YAO YA NGONO JUU YA MWANAMKE HUSIKA, NA UDHAIFU HUO UNAWEZA AU UNAMPA FURSA YA KUBAKA. KUBAKA NI KOSA LA KULAZIMISHA MTU KUFANYA MAPENZI BILA RIDHA YAKE, NA MBAKAJI ANAHUKUMIWA NA SHERIA YA UBAKAJI. CHANZO CHA MATATIZO HAYO YOTE NI UTATA WA MAPAMBO NA USAFI WA MWANAMKE.

MWANAMUME MWENYE MWANAMKE MWENYE KUJIPAMBA NAKUACHA VIUNGO VYAKE WAZI, ANAWEZA KUJIKUTA KATIKA UTATA WA MAPENZI JUU YA MKE AU MCHUMBA WAKE, KUTOKANA NA CHANGAMOTO AMBAZO HUYO MWANAMKE ANKUTANA NAZO NJIANI. CHANGAMOTO ZINATOKANA NA USUMBUFU AMBAO MWANAMKE ANUPATA KUTOKA KWA WATONGOZAJI. MWANAMKE MZURI NA MWENYE KUJIPAMBA ANA UWEZO WA KUTONGOZWA ZAIDI YA MARA KUMI KWA SIKU.


MARANYINGI WANAWAKE WANAOTEMBEA KWA MIGUU, WANA USUMBUFU WA KUTONGOZWA ZAIDI YA WALE WENYE KUTUMIA USAFIRI BINAFSI. MWANAMKE MWENYE KUTEMBEA KWA MIGUU, ANATEMBEA KATIKA NJIA ZENYE MCHANGANYIKO WA WANAUME WENYE TABIA NZURI (WENYE KUJIHESHIMU NA KUHESHIMU UHURU WA NJIA) NA WENGINE WENYE MFUMO WA MATAMANIO ( WANAPENDA KUZINI NA KILA MWANAMKE MZURI AU MWENYE VIUNGO VIZURI BILA MPAKA)YA NGONO.



HAPO NDIPO KULIKO NA UTATA, NA PANAHITAJI UVUMILIVU WA KUTOSHA.KUMBUKA YA KWAMBA, NDOA NYINGI ZINAVUNJWA NA WIVU WA MAPENZI. KINACHOHITAJIKA NI UVUMILIVU BAINA YA WAPENZI, KUMBUKA MWILI UNACHOKA (UNAPUNGUKIWA NA NGUVU) LAKINI MOYO WAKE HUWA BADO UNAPENDA VITU VIZURI.
NAWE USIMWONE MKEO AU MMEO KACHOKA, SURA YAKE IMEANZA KUZEEKA NA UANZE KUTAFUTA SURA NYINGINE MPYA, SIO USTARABU MAISHANI. IKIWA ULIMPENDA MKEO AU WAKE ZAKO, KATIKA HALI YA UJANA, LAZIMA UKUBALI KUISHI KATIKA MABADILIKO YA MAUMBILE NDANI YA MSINGI WA MAPENZI. UKIMWACHA MUMEO AU MKEO KWA SABABU YA ILE SURA, RANGI, UMBILE…...ULIVYOVICHAGUWA KATIKA MDA MUAFAKA WA UJANA WAKO, UTAONEKANA KAMA MTU MWENYE UPUNGUFU WA UJASIRI WA MAPENZI MAISHANI MWAKO. UVUMILIVU KATIKA MATENDO NI MUHIMU NA NIMSINGI WA USHUJAA.



2) MASIKIO

MASIKIO : MASIKIO NI VIFAA AMBAVYO KAZI YAKE NI KUNASA SAUTI NA MANENO, KUTOKA NJE YA MWILI NA KUVIINGIZA NDANI YA MWILI, KITENDO HICHO CHA MASIKIO KUSAFIRISHA SAUTI NA MANENO KINAITWA U.N ( USIKIVU WA NAFSI ). USIKIVU WANAFSI UNATOKANA NA VINASA SAUTI ( MASIKIO) VYA NAFSI KUINGIZA MANENO NA SAUTI NDANI YAKE NA KWA MDA MUAFAKA. NAFSI HAINA MLANGO WA KUZUIA SAUTI KUINGI, LABDA IKIWA (NAFSI )USINGIZINI. USINGIZI UNAFANYA KILA JAMBO LA NAFSI LIWEZE KUPUMZIKA NA NDIO MAANA MARANYINGI MTU MWENYE UCHOVU SI RAHISI, KUSIKIA, KUONA……….N.K, ANAPOKUWA USINGIZINI. USINGIZI NI NUSU YA KIFO.


3) PUA

PUA : PUA NI KIFAA AMBACHO KINAVUTA NA KUTOA HEWA, KUVUTA HARUFU……..N.K. ILI NAFSI IWEZE KUPUMUA AU KUHISI HARUFU YA KITU FULANI, INAHITAJI MSAADA WA PUA. NAFSI INATUMIA PUA LAKE KAMA MLANGO WA MAISHA KATIKA MSINGI WA UHAI (KUPUMUA), VILE VILE NAFSI INAWEZA KUPENDA AU CHUKIA HARUFU FULANI, KUTOKANA NA UBORA WAKE( KIKIWA NI KITU CHENYE HARUFU NZURI(MANUKATO), MOYO WA NAFSI HUSIKA UTAIPENDA (HARUFU) NA KIKIWA KITU ( MNUKO ) CHENYE HARUFU MBAYA MOYO UTAKICHUKIA. KILA NAFSI INA UHURU WA KUPENDA AU KUCHUKIA HARUFU FULANI, KUTOKANA NA VIGEZO VYAKE(NAFSI).



MANUKATO NI NJIA MOJA WAPO YA MVUTO WA MAPENZI. KUNA BAADHI YA WANAWAKE AU WANAUME WENYE KUWAPENDA WATU (MKE AU MME) AMBAO WANANUKIA. KWA NJIA HII, MTU MWENYE KUPENDA MANUKATO ANAPENDA KUISHI NA VITU VINAVYONUKIA. NA SIKU ZOTE NAFSI HAIWEZI KUZIBA AU KUZUIA PUA LAKE KUPOKEA KITU CHENYE KUNUKIA VIZURI LA BALI HUKIWEKA KARIBU NA KUKUPENDA ZAIDI.

KWA MFANO :

MANUKATO NI KITU CHENYE KULETA HARU NZURI NA KUIPENDEZESHA NAFSI. UNAONAJE UKISAFIRI NA MTU MWENYE KUNUKIA MANUKATO ?
AU
UNAONAJE UKILALA NA MTU AMBAYE HAJAOGA ANANUKA KIKWAPA NA MMEJIFUNIKA SHUKA MOJA?

YOTE HAYA TUNAYASHUHUDIA, PALE TUNAPOKARIBIA AU KUFIKA KWENYE ENEO LA MAAKULI (CHAKULA), PUA LIKIVUTA HARUFU YA CHAKULA, NAFSI YAKE INATAMBUA AINA
(SAMBUSA, CHAPATI, MAHARAGE, PILAU, CHAI, JUICE……...N.K) YA CHAKULA HUSIKA. YOTE HAYA NI MAPENZI YANAYOTOKANA NA NAFSI JUU YA HARUFU FULANI. HARUFU YA MWILI INAWEZA KUONGEZA AU KUPUNGUZA MAPENZI BAINA YA WAPENZI. KUTOKANA NA NAFSI KURIDHIKA KATIKA MFUMO WA KUZOWEA HARUFU YA CHUMBA AU RAFIKI AU MKE AU MME, INAPOKOSA ILE HARUFU KUTOKA KWA MTU (MCHUMBA AU MKE AU MME AU RAFIKI) WAKE WA KARIBU, HUJISIKIA VIBAYA NA MARANYINGINE MATENDO NA MANENO YA SIKU HIYO VINAWEZA KUWA NA KASORO KUTOKANA NA KASORO YA MANUKATO AU HARUFU MBAYA.

KILA JAMBO MAISHANI LINAHITAJI UVUMILIVU NA ELIMU YA KUTOSHA JUU YA MAISHA YAKO. KUMBUKA YA KWAMBA MTOTO MCHANGA ANAMTAMBUWA MAMA YAKE KUPITIA NJIA YA HARUFU. VILE VILE PUA KATIKA WANYAMA WENYE KULA MAJANI( TWIGA, ZEBRA, MBOGO…….N.K) NI SILAHA NZURI YA KUWAPA TAARIFA (KWA MNUSO ) YA KWAMBA ADUI(SIMBA, HUI, FISI…...N.K) YUKO KARIBU.




4) ULIMI

ULIMI NI KIFAA KINACHOWEZESHA NAFSI KUTNGENEZA MANENO AU KUZUNGUMZA NA VILE VILE ULIMU ANAWEZESHA NAFSI KUHISI LADHA YA CHAKULA NA KINYWAJI. NAFSI INATUMIA ULIMI KUTENGEZA MANENO YENYE MSINGI WA HUSIA ZAKE ZA MANENO. ULIMU UNAWEZA KUSABABISHIA NAFSI YAKE KUWA NA UTULIVU AU UCHUNGU WA MWILI. UVUMILIVU NA UCHUNGU UNATOKANA NA KAULI YA NAFSI HUSIKA.




5) MDOMO


MAPENZI HAYAPATIKANI ISIPOKUWA KWA NJIA MBILI, NAZO NI

MANENO MAZURI NA VITENDO VIZURI. MDOMO NI NJIA MOJAWAPO YENYE KUKUZA, KUPUNGUZA AU KUONDOA MAPENZI BAINA YA NAFSI MBILI AU ZAIDI ZINAZO PENDANA.

6) HISIA

HISIA NI KIFAA CHA KUHIFADHI NA KUTOA TAARIFA, ZA UTULIVU NA AMANI AU KUTOA TAARIFA YA HATARI MWILINI MWA BINADAMU. KUNA AINA NYINGINE YA HISIA YENYE MSINGI WA UPUNGUFU WA ELIMU. MARANYINGI MTU ANAPOHISI KITU FULANI, NJE YA MWILI WAKE, ANAJIKUTA AKIPATIA (HISIA ZAKE ZIKIWA ZA KWELI) AU AKIKOSEA KATIKA HISIA
( DHANA YAKE IKIWA DHAIFU YENYE UKOSEFU WA UKWELI).


KWA MFANO :

UNAWEZA KUHISI KWAMBA UNA UGONJWA FULANI, LAKINI HUNA UHAKIKA. HII NI DHANA YENYE MFUMO DHAIFU WA HISIA. NA KATIKA MAPENZI NDIVYO ILIVYO, UNAWEZA KUHISI KWAMBA MTU (MWANAMKE AU MWANAMME) FULANI, ANAKUPENDA KUMBE NI KINYUME CHAKE. HAKUPENDI AU ANAKUPENDA KWASABABU YAKITU FULANI, SIO KWASABABU YA HISIA ZAKO.

UGONJWA UNAHAKIKISHWA NA DAKITARI KWA VIPIMO NA MANENO YENYE UHAKIKA WA VIPIMO. NA MAPENZI YANAPATIKANA KATIKA VIPIMO VYA MANENO NA MATENDO. AKUPENDAYE UTAMTAMBUWA KWA ISHARA ZA MATENDO YA MWILI WAKE JUU YAKO NA MATAMSHI YAKE (MPENZI WAKO) JUU YAKO.

UKIONA KUNA TOFAUTI KATIKA MANENO NAVITENDO, JUWA KWAMBA HAMWEZI KUJENGA UPENDO WENYE MSINGI WA UTULIVU NA AMANI.


UPENDO AU MAPENZI HAYAPATIKANE KULIKO TAFAUTI ZA NAFSI NA MSINGI WA CHUKI ZA MOYO. JAMBO LA MUHIMU NA LENYE ULINZI KATIKA UJENZI WA MAPENZI NI KILA UPANDE KURIDHIA PICHA SURA, UMBILE, RANGI……..N.K, BAINA YA WAPENZI. UVUMILIVU NI MUHIMU JUU YAKILA MTU ALIYOKO KWENYE MUUNGANO WA MAPENZI.

KILA MOYO UNAJENGA MAPENZI PALE PENYE CHEMCHEM ZA MAPENZI. HATA PAKA NDANI YA NYUMBA HUWA NA MTU AMBAYE NI MPENZI WAKE ZAIDI.
ONGEA MANENE MAZURI NA FANYA MATENDO MAZURI YENYE MSINGI WA UPENDO NA UKUTA WAKWELI UTAPENDWA NA WENGI KATIKA MSINGI WA MAPENZI.

No comments:

Post a Comment