UNAFIKI NI NINI ?
UNAFIKI NI KIFAA AMBACHO KINATUMIWA NA NAFSI YA MTU FULANI KATIKA HARAKATI ZA KUKUBALI MANENO NA KUTOTENDA MAKUBALIANO YA MANENO HUSIKA AU KUTENDA JAMBO FULANI, NA KUKANUSHA KATIKA MANENO KUHUSU KITENDO HUSIKA.
MTU MNAFIKI HANA SURA MAALUMU YENYE KUONESHA KAMA NI MUONGO KATIKA MANENO AU VITENDO VYAKE, BALI MTU MNAFIKI DALILI ZAKE ZINATAMBULIKA KUTOKANA NA KAULI YA NAFSI YAKE NA MATENDO YA NAFSI YAKE. NDIO MAANA TUNAANGALIA MISINGI YA KUMTAMBUA MTU MNAFIKI KWA DALILI ZAKE.
DALILI ZA MTU MNAFIKI ZINA MISINGI MITATU.
DALILI HIZO NI :
AKIZUNGUMZA , HUONGEA MANENO YA UONGO.
AKITOA AHADI, HATEKEKELEZI ALICHO KIAHIDI.
ANAPOAMINIWA, HAAMINIKI KATIKA JAMBO HUSIKA.
AKIZUNGUMZA , HUONGEA MANENO YA UONGO.
BINAADAMU WAMEUMBWA, ILI WAWEZE KUSHIRIKIANA KATIKA MANENO NA VITENDO VYA KWELI. KUNA BAADHI YA
BINAADAMU,AMBAO WANA ASILI YA UNAFIKI NDANI YA NYOYO ZAO, NA KUWATAMBUA SIYO RAHISI MPAKA WAZUNGUMZE MANENO YASIYOTEKELEZEKA. UNAFIKI HAUNA UMRI WALA RANGI AU UKOO AU URAFIKI. WATU WENGI WANAKUMBWA NA UNAFIKI WA MANENO KUTOKA KWA MME,MKE, MTOTO,RAFIKI,NDUGU, JAMAA AU MUAJIRI. AHADI NYINGI ZITATOLEWA, NA ZENYE KULETA MATUMAINI JUU YA MUAHIDIWA LAKINI MWISHO WASIKU HAKUNA UKWELI UTAKAOKUEPO AU KUONEKANA KATIKA MANENO AU MAZUNGUMZO YA YULE MUAHIDI JUU YA MUAHIDIWA.
AKITOA AHADI, HATEKEKELEZI ALICHO KIAHIDI.
MTU MNAFIKI,ANAPOTOA AHADI HATEKELEZI KILE ALICHO KIAHIDI, KUTOKANA NA MANENO YAKE KUWA NA MSINGI WA UONGO NAFSINI MWAKE.
MARANYINGI AHADI INATOKA KWA YULE MTU ALIOKO KARIBU ( RAFIKI, NDUGU, JAMAA, MUAJIRI, MTAWALA, MPENZI, MME, MKE,BABA, MAMA…..N.K. ).
SIRAHISI NAFSI YA MUAHIDIWA KUAMINI KWAMBA AHADI HUSIKA INA MFUMO WA UONGO KATIKA UTEKELEZAJI. AHADI NI MSINGI WA MATUMAINI JUU YA NAFSI ILIOAHIDIWA NA HUJENGA NDANI ( YA MUAHIDIWA ) UTULIVU WA NAFSI.
AHADI YA UONGO SIKU ZOTE HUPUNGUZA HESHIMA YA MUAHIDI ( MTU ALIYE AHIDI ) NA KUJENGA CHUKI JUU YAKE. MTU MWENYE MATUMAINI YA AHADI ANAMPENDA SANA YULE ALIYEMUAHIDI, KWASABABU ALIMPA MATUMAINI YA KUTUWA MZINGO WA WASIWASI JUU YA TATIZO LAKE. UKOSEFU WA UTEKELEZAJI WA AHADI UTAMFANYA YULE MUAHIDIWA KUANZA UPYA KUTAFUTA NJIA YA KUFANIKISHA KUTATUWA TATIZO AU MATATIZO YAKE NA INAWEZA KUWA NGUMU ZAIDI YA MWANZO.
UGUMU WA KUTATUA AHADI YA UONGO UTAMFANYA MUAHIDIWA KUMCHUKIA YULE MTU ALIYE WEZA KUMPA MATUMAINI YENYE MSINGI WA UONGO, NA CHUKI YA SABABU HIYO ( YA AHADI YA UONGO ) INAWEZA KUPUNGUZA AU KUONDOA MISINGI YA URAFIKI, UNDUGU, UTIIFU BORA, UAMINIFU, UJAMAA…..NA KUJENGA MISINGI YA CHUKI NDANI YA NAFSI MBILI ZINAZO HUSIKA.
MANENO YALIOPAMBWA YA MNAFIKI NDIO SILAHA YAKE KUBWA YA KUMPA ANACHOKIHITAJI NA HUA NI MZITO KUTEKELEZA MISINGI NA NGUZO ZA JAMBO HUSIKA KATIKA AHADI. UZITO WA UTEKELEZAJI WA NAFSI YA MNAFIKI UNATOKANA NA MSINGI WA MANENO NA AHADI ZA UONGO.
MTU MNAFIKI ANAPOAMINIWA NA ASIWEZE KUAMINIKA KATIKA JAMBO HUSIKA, ATAJIKUTA AKITENGENEZA UKOSEFUA WA UADILIFU, HURUMA, TABIA NZURI, HESHIMA ,UPENDO , BARAKA ZA MANENO NA VITENDO……...NA MWISHO WAKE HUJIJENGEA CHUKI KATIKA JAMII NA KUSHUSHA AU KUONDOA HADHI YA USTARABU BAINA YAKE NA YULE AU WALE WALIOKO KATIKA KUNDI LA KUAMINIANA.
ANAPOAMINIWA, HAAMINIKI KATIKA JAMBO HUSIKA.
NAFSI YENYE MSINGI WA UNAFIKI HUWA HAINA UAMINIFU NDANI YAKE KWASABABU HUWA NIYENYE UPUNGUFU AU UKOSEFU WA KURIDHIA AU KURIDHIKA KATIKA JAMBO MOJA.
MTU MNAFIKI TABIA YAKE KATIKA MATENDO HUWA NI NDOGO KUTOKANA NA KUELEKEZA NGUVU YAKE KUBWA KATIKA KUPAMBA MANENO YA KUONGEA. MTU MNAFIKI ANAKUWA NA MANENO YENYE NGUVU YA LADHA KATIKA UPANGAJI WA MANENO.
UHATARI WA MTU MNAFIKI
UHATARI WA MTU MNAFIKI NI KWAMBA SI RAHISI KUMTAMBUA, NA UNAPOMTAMBUA ANAKUWA AMEISHAANGAMIZA MALENGO YAKO MENGI. KWASABABU UNAPOKUWA NARAFIKI MNAFIKI, HUWEZI KUFANIKIWA KUTOKANA NA MVUJO WA SIRI ZAKO. MTU MNAFIKI ANAKUWA NAMARAFIKI WA PANDE MBILI ( UPANDE WAKO NA UPANDE WA ADUI ZAKO ) ZENYE MATATIZO.
YEYE ( MTU MNAFIKI ) ANATEGEMEA MAPATO YAKE KATIKA KUONGEA NA KUTENDA KATIKA MFUMO WA KURIDHISHA KILA UPANDE WENYE MATATIZO, NA KILA UPANDE WENYE MATATIZO HUMPOKEA JAMAA HUU MNAFIKI KAMA MKOMBOZI WA KULETA TAARIFA NA KUTOA USHAURI.
LAKINI JAMBO LA KUSHANGAZA MTU MNAFIKI, HUWA NI MWENYE KUWASHA MOTO KATIKA KILA UPANDE ILI MLO WAKE UDUMU. KWA MTAZAMO WA NJIA HII YA MTU MNAFIKI HUBEBA SIRI NYINGI ZA KILA UPANDE NA HUWA NA MBINU ZA KUTENGENEZA MANENO NA MATENDO YA UONGO KUTOKANA NA UWEZO WAKE WA KUCHAMBUA UDHAIFU WA KILA UPANDE HUSIKA KATIKA MGONGANO WA MANENO NA VITENDO.
MTU MNAFIKI ANAO UWEZO WA KUONGEA NA KUTOA AHADI ZENYE KULETA MGONGANO WA MAWAZO NA KUSABABISHA UGOMVI BAINA YA NDUGU,MME NA MKE, NDUGU, JAMAA, MARAFINI, TAWALA, MARAFIKI, KUVUNJA NDOA, MAUWAJI, …..N.K.
NILAZIMA KILA MTU KUJIEPUSHA NA KUWA KARIBU NA MTU YEYOTE MWENYE DALILI HIZI ZA UNAFIKI MAPEMA KABLA HAJAKUMBWA NA MAJUTO YA KUMFAHAMU SWAHIBA MNAFIKI. KUMBUKA DALILI HIZO NI :
AKIZUNGUMZA , HUONGEA MANENO YA UONGO.
AKITOA AHADI, HATEKEKELEZI ALICHO KIAHIDI.
ANAPOAMINIWA, HAAMINIKI KATIKA JAMBO HUSIKA.
DALILI HIZI ZINAPATIKANA :
MAJUMBANI, MAOFISINI, SHULENI, ………………..N.K.
UNAFIKI NI MSINGI WA KUPUNGUZA AU KUONDOA MAENDELEO KATIKA JAMII.
UNAFIKI NI KIWANDA CHA KUPOTEZA MDA BAINA YA WATU WALIOKO KATIKA KUNDI LAKE.
UNAFIKI UNAONGEZA CHUKI NA KUONDOA UAMINIFU, UTULIVU NA UPENDO.
UNAFIKI UNAONDOA FURAHA NA MISAADA BAINA YA MARAFIKI, NDUGU, JAMAA, MKE, MME, MTAWALA………..N.K.
KWA USHAHIDI ZAIDI JUU YA UNAFIKI SOMA KATIKA QURAN NA BIBLIA KUHUSU MTU MNAFIKI NA MADHARA YAKE.
BIBLIA
YESU “AKAWAAMBIA KATIKA MAFUNDISHO YAKE, JIHADHALINI NA WAANDISHI, WAPENDAO KUTEMBEA WAMEVAA MAVAZI MAREFU, NA HUSALIMIWA MASOKONI. NA KUKETI MBELE KATIKA MASINAGOGI, NA VITI VYA MBELE KATIKA KALAMU. AMBAO HULA NYUMBA ZA WAJANE, NA KWA UNAFIKI HUSALI SALA NDEFU,HAWA WATAPATA HUKUMU ILIYOKUBWA.
( MARKO 12 : 38,39,40 )
KWA MTAZAMO WA AYA HIZI, MNAFIKI NI MTU MWENYE TABIA YA KUBADILIKA NA KUJIFANYA MTUZI WA MAANDIKO NA MTU MWEMA KATIKA SALA NDEFU NA HUTUMIA NJIA YA KIPATO CHAKE CHA MLO KATIKA NYUMBA ZA WAJANE. MNAFIKI NI MTU MWENYE KUPEWA KIPAO MBELE KATIKA SHEREHE, NA AKIPEWA KITI CHA MBELE. MNAFIKI HUJIJENGEA MBINU ZA KUONYESHA WATU KWAMBA NI MTU MWEMA NA NDIOMAANA HUSALIMIWA KATIKA SOKO. HESHIMA YA MNAFIKI INATOKANA NA UBUNIFU WA MANENO NA MATENDO YA UONGO, NDIO MAANA HUJIFANYA KUWA YUKO KARIBU NA MUNGU AKITUMIA MBINU YA KUSALI SALA NDEFU NA MBINU NYINGINE YA MNAFIKI NI KUANDIKA VITABU AMBAVYO VINATETEA SERA YAKE YA UONGO ILI APATE KUWARUBUNI WATU KATIKA JINA LA MUNGU. YOTE HAYO YESU ( NABII ISA ) ALIWEZA KUYAONA NA KUTOA TAHADHARI KWA WATU WAKE WENYE AKILI YA KUCHAMBUA MBINU ZA WANAFIKI.
QURAN
MWENYEZI MUNGU ANASEMA “WANAUME WANAFIKI NA WANAWAKE WANAFIKI, WOTE NI HALI MOJA, HUAMRISHA YALIO MABAYA NA HUYAKATAZA YALIO MAZURI, NA KUZUILIA MIKONO YAO ( HAWASAIDII MAMBO YA KHERI ), WAMEMSAHAU MWENYEZI MUNGU ( WAMEPUUZA AMRI ZAKE ), NA YEYE PIA AMEWASAHAU ( AMWAPUUZA ). HAKIKA WANAFIKI NDIO WAVUNJAO AMRI.
( 9 : 67,73,80,84 )
KWA MUJIBU WA QURAN, UNAFIKI HAUNA JINSIA. MWANAMKE AU MWANAUME WOTE WANAWEZA KUWA WANAFIKI. KAWAIDA YA NAFSI (MTU) INAMPENDA YULE MWENYE KUIPENDA. MTU KUMPENDA ADUI WAKE HUWA NI JAMBO AMBALO SIO RAHISI, NA AKIWEZA KUJITAHIDI KATIKA KUMPENDA ATAJIKUTA AKIKWAZWA NA BAADHI YA MANENO NA MATENDO MABAYA YA YULE ADUI WAKE.
JAMBO HILO LINAWEZA KUWA RAHISI KWA WALE WATU WENYE UCHA MUNGU WA KUTOSHA NAFSINIMWAO NAO NI WACHACHE SANA. MTU MBEA ANAPENDA KUSHIRIKIANA NA MBEA MWENZAKE AU MTU MWENYE KUPENDA MUZIKI ANAPENDA MPENDA MUZIKI MWENZAKE ILI WAWEZE KUSHIRIKIANA KATIKA KUPATA TAARIFA ZA MIZIKI BORA AU ILIOKO KWENYE CHATI.
MTU MBAYA HUWA NI MWENYE KUMKIAMBIA AU KUMCHUKIA MTU MWENYE TABIA NZURI.
UJUMBE WAKUZINGATIWA NI KWAMBA WANAFIKI NI MARAFIKI, KUTOKANA NA KUWA NA MTANDAO BORA NA WENYE MARIDHIANO YA UNAFIKI WAO. MWANAMME NA MWANAMKE WENYE KUTAFAUTIANA TABIA ( MMOJA MNAFIKI NA MWINGINE MKWELI ) MAISHA YAO YATAKUWA NIYENYE MZOZO WA MAWAZO NA KUGOMBAMBA AU KUACHANA KWA UBAYA ) LAKINI MWANAMKE MNAFIKI NA MWANAMME MNAFIKI WANAWEZA KUISHI MDA MREFU KUTOKANA NA NDOA YAO KULINDWA NA MSINGI WA UNAFIKI, NA MWISHO WAKE HUWA NI MWENYE MADHARA NA KUJENGA MSINGI WA UADUI.
NYUMBA YA MKE NA MME WANAOSEMA KWELI, HUTAWALIWA NA MAPENZI NA UTULIVU NA KUONGOZWA NA AMANI KATIKA KILA NYANJA MAISHANI MWAO. MWISHO WA WATU WAZURI KITABIA ( VITENDO NA MANENO ) HUWA NI MZURI DUNIANI NA AKHERA WANAPATA NAFASI NZURI YENYE UTULIVU. UTULIVU WA MWISHO WA MAISHA ( BAADA YA KIFO ) UNAJENGEWA DUNIANI. KUMBUKA YA KWAMBA KILA NAFSI ITABEBA MZIGO WAKE. MZIGO WA WEMA HUPITA NJIA NJEMA NA MZIGO WA MABAYA HUPITA NJIA MBAYA.
KAZI KWETU.
ndo mana mtt azliwapo huwa analia sana coz anajua anaigia kwenye uwanja wa vita
ReplyDelete