KWANINI NABII IBRAHIMU ALIPEWA CHEO CHA IMANI ?
NA KWA NINI WA ISRAELI NA WARABU BABA YAO NI MMOJA AMBAE NI IBRAHIMU ?
NABII IBRAHIMU ALIZALIWA IRAQ KATIKA MJI WA UR ZAIDI YA MIAKA ELF 8
( MORE THAN 8,OOO YEARS AGO ) ILIYOOPITA. TUKIZINGATIA KUWA NABII NUHU NA NABII SALEH NA WENGINEO, WALITUMWA KULETA UJUMBE KWA WATU MAALUM, NABII IBRAHIMU ANABAKI KUWA MTUME WA KWANZA KUTANGAZA UJUMBE WA MWENYEZI MUNGU ( ALLAH ) KWA WALIMWENGU WOTE BAADA YA NABII NUHU ( A.S). ALIZALIWA KATIKA KIPINDI CHA HISTORIA AMBAPO UJAHILI NA SHIRKI NDIVYO VILIVYOTAWALA MAISHA YA WATU KIASI KWAMBA HAKUWEPO ALIYEMJUA MUNGU WA KWELI, WACHILIAMBALI KUMUABUDU. TAIFA ALIMOZALIWA NABII IBRAHIMU, NDIO WAKATI HUO LILILOKUWA MBELE KWA MAENDELEO YA SANAA. WALIZAMA KATIKA IBADA YA MASANAMU NA NYOTA. UNAJIMU, UCHAWI, RAMLI NA TIBA ZAKE VIKAWA MAARUFU KATIKA JAMII.
KISIASA NA KIJAMII
KISIASA NA KIJAMII WATU WALIGAWANYIKA KATIKA MATABAKA MATATU. WALIKUWEPO MAKASISI WALIOCHUNGA MAHEKALU NA KUONGOZA IBADA ZA MATAMBIKO ZILIZO FANYWA NA WATIIFU. WALISIMAMIA MAZISHI, NDOA NA KUCHEZA MICHEZO INAYOENDANA NA MILA YAO YA IBAADA YA MASANAMU, ILIKUWA NI NJIA MOJAWAPO YA KUONDOA AU KUELEZA WAFUASI WAO MAMBO YA GHAIBU.
TABAKA LA PILI LILIKUWA LA WAKUU WA SERIKALI. HAWA NAO WALIWANYONYA RAIA KWA MSAADA WA MAKASISI WALIPANDIKIZA DHANA KATIKA AKILI ZA WATU KUWA WAKUU WA SERIKALI NI MIUNGU WA DUNIA, HIVYO SHERIA ZAO NILAZIMA ZITIIWE.
TABAKA LA TATU NI RAIA WA KAWAIDA AMBAO WALINYONYWA NA MAKUNDI YOTE MAWILI TULIYOTANGULIA KUYATAJA. UTAGUNDUA KWAMBA KUNA MAMBO MAWILI YANAYOJITOKEZA KATIKA MFUMO HUU WA KISHIRIKINA; MOJA NI DINI KUTUMIKA KAMA CHOMBO CHA KUNYONYEA NA KUWAPUMBAZA WATU.
PILI NI USHIRIKIANO UNAOJITOKEZA BAINA YA VIONGOZI WA SERIKALI ZA KITWAGHUTI NA VIONGOZI WA DINI KATIKA KUWAKANDAMIZA NA KUWANYONYA RAIA.
UKOO WA NABII IBRAHIMU
UKOO ALIMO ZALIWA NABII IBRAHIMU ULIKUWA WA MAKASISI NA BABA YAKE ALIKUWA NDIYE MKUU WA MAKUHANI. KWAHIYO NABII IBRAHIMU ( BABA WA IMANI ) ALIKULIA NA KUPATA ELIMU YAKE KATIKA MAZINGIRA YA UKUHANI. AIDHA CHEO CHA UKUHANI MKUU KILIKUWA KINAMSUBIRI AKIRITHI
TABIA YA NABII IBRAHIMU.
TUMEONA KUWA NABII IBRAHIMU ALIZALIWA NA KULELEWA KATIKA JAMII AMBAYO ILIKUWA INAONGOZWA NA ITIKADI YA USHIRIKA. HATA HIVYO NABII IBRAHIMU ALIPOFIKIA UMRI WAKUWEZA KUTUMIA BUSARA, ALIANZA KUTAFAKARI ANAJIULIZA MASWALI KAMA :
VIPI SAYARI KAMA NYOTA NA MWEZI VYAWEZA KUWA MIUNGU ?
VIPI JUA LAWEZA KUWA MUNGU ?
VITU AMBAVYO VYAPATIKANA NA KUTOWEKA. YAWEZEKANA VIPI MASANAMU AMBAYO HAYASEMI WALA KUSIKIA KUWA MUNGU. TANGU HAPO MASANAMU YENYEWE YAMECHONGWA NA WATU. VIPI MWANADAMU APEWE SIFA YA UUNGU WAKATI ANA UDHAIFU MKUBWA ? BAADA YA KUTAFAKARI MASWALI KAMA HAYA NABII IBRAHIMU ALIFIKIA UAMUZI KUWA HATAABUDU MIUNGU INAYOABUDIWA NA JAMII YAKE AKATANGAZA MSIMAMO WAKE HUO MBELE YA WATU.
AKASEMA :
QURAN : “MIMI NIKO HURU NA HIVYO MNAVYOMSHIRIKISHA NAVYO MWENYEZI MUNGU ( ALLAH ). MIMI NIMEUELEZA USO WANGU KWA YULE ALIYEUMBA MBINGU NA ARDHI. MIMI SI MIONGONI MWA WASHIRIKINA.
(6:78,79)
HUU NDIO USHUJA WA NABII IBRAHIMU, WAKUWEZA KUKATAA SERA ZA JAMII YAKE KUTOKANA NA MTAZAMO WAKE.
MAFUNDISHO YA NABII IBRAHIMU
NABII IBRAHIMU ALIKUWA MHUBIRI MKUU WA UJUMBE WA MWENYEZI MUNGU ( ALLAH ). ALIKUWA MUAMRISHAJI MEMA NA MKATAZAJI MABAYA .
KAZI HII ALIANZIA NYUMBANI KWAKE; AKAIFANYA NDANI YA IRAQ, KISHA AKASAFIRI SEHEMU NYINGINE KAMA SYRIA, PALESTINA,EGYPT NA ARABIA. BAADAYE ALIWEKA WAJUMBE ( WAWAKILISHI ) KATIKA KILA KITUO CHA HARAKATI ZAKE. ALIMWEKA RUT-MPWAE ; JORDAN, IS-HAKA ( MTOTO WAKE ), SYRIA NA PALESTINA, ISMAIL MTOTO WAKE MKUBWA AKAMUWEKA HIJAZ.
NABII IBRAHIMU ALIZALIWA KATIKA NCHI YA IRAQ. NABII IBRAHIMU ALIZALIWA NA WAZAZI WENYE KUABUDU SANAMU ( WENYE KUMSHIRIKISHA MUNGU NA MIUNGU AU MASANAMU).
NABII IBRAHIMU ALIPOKUWA MTOTO MDOGO ALIWEZA
KUKAA NA KUFIKIRI KUWEPO KWA MWENYEZI MUNGU. ALIMTAFUTA MWENYEZI MUNGU KATIKA NJIA NYINGI SANA MOJA WAPO NI KUANZA KUANGALIA AU KUKAGUA KWAMBA JUA AU MWEZI VINAWEZA KUWA MUNGU, LAKINI ALISHINDWA KWASABABU JUA LINAANZA KUWAKA NA KUONDOKA NA MWEZI UNAANZA KUNG’ARA NA KUONDOKA ALFAJIRI. YOTE HAYO NABII IBRAHIMU ALIWEZA KUYAJARIBU KATIKA HARAKATI ZA KUMTAFUTA MWENYEZI MUNGU.
LICHA YA NABII IBRAHIMU KUZALIWA NA WAZAZI WENYE KUABUDU SANAMU, LAKINI KWA IMANI YAKE YA KUHISI KWAMBA KINYAGO AMBACHO KIMECHONGWA AU KUCHORWA HAKIWEZI KUWA MUNGU.
IBRAHIMU ALIWEZA KUTUKANA MASANAMU BILA GHOFU,NA WATU WAKIMSHANGAA JUU KAULI YAKE,KWASABABU BABA WA IBRAHIMU ALIKUWA KUHANI KATIKA HEKALU YA MASANAMU NA ALIKUWA NA NGUVU KATIKA IMANI YA SANAMU.
NABII IBRAHIMU SIKU MOJA ALIWEZA KUVUNJA SANAMU HEKALUNI, NA AKAPEWA ADHABU YA KUCHOMWA MOTO.
NABII IBRAHIMU ALIKUBALI KUCHOMWA MOTO LAKINI HAJAACHA KUMWOMBA YULE MWENYEZI MUNGU AMBAE YEYE ANAAMINI NI WA KWELI.
ALIINGIZWA KWENYE KUNI NA UMATI WA WASHIRIKINA AU MAKAFIRI MOJAWAPO AKIWEMO BABA YAKE. BAADA YA KUMWEKA KATIKA KUNI NA KUWASHA MOTO NABII IBRAHIMU
ALITAMUKA AU ALIFANYA MAOMBI HIVI
“ EWE MWENYEZI MUNGU NAKUOMBA NA NINAAMINI UPO NA UNANISIKIA NAOMBA UNIOKOE NA MOTO HUU”
MWENYEZI MUNGU ALIYASIKIA MAOMBI YA NABII IBRAHIMU , AKAMTUMA MALAIKA JIBRILI AU GABRIELI, ILI AOKOE MAISHA YA NABII IBRAHIMU KUTOKA KWENYE MOTO WA MAKAFIRI WA IRAQ.
ALIPOMFIKIA IBRAHIMU KATIKA MOTO , NABII IBRAHUMU ALIWEZA KUKATAA MSAADA WA MALAIKA GABRIELI ( JIBRILI ) , KWASABABU ALIONA MALAIKA SURA YAKE NI YABINAADAMU KAMA YEYE.
ILIBIDI MALAIKA ARUDI KUTOA UJUMBE KWA MWENYEZI MUNGU,KWAMBA MJA WAKE NABII IBRAHIMU, AMEKATAA MSAADA WAKE BALI ANAHITAJI MSAADA WA MWENYEZI MUNGU PEKE YAKE, NA SABABU KUBWA NABII IBRAHIMU ALISHINDWA KUMTAMBUWA MALAIKA JIBRILI AU GABRIELI, KWASABABU ALIKUWA HANA DALILI ZA MOJA KWA MOJA KWAMBA HUYU NI MALAIKA NA AMETUMWA NA MWENYEZI MUNGU.
MWENYEZI MUNGU AKATOA AMRI JUU MOTO AKASEMA “ EWE MOTO KUWA WA BARIDI NA SALAMA KWA IBRAHIMU, NA MOTO UKAWA WABARIDI NA SALAMA JUU YA NAFSI YA NABII IBRAHIMU.
HII ILIKUWA JITIHADA YA KWANZA YA NABII IBRAHAMU, YAKUWA NA IMANI YAKUWEPO MUNGU NA KUAMINI KWAMBA MUNGU YUPO NA NI MWENYE UWEZO JUU YA KILA JAMBO.
BAADA YA CHUKI HIYO WA MAKAFIRI AKIWEMO BABAYAKE, NABII IBRAHIMU ALIPEWA AMRI NA MUNGU YA KUHAMA NA KWENDA MBALI YA ENEO HILO AKIFUNDISHA NENO LA MUNGU.
KATIKA HARAKATI ZA NABII IBRAHIMU ZA KUFUNDISHA WATU KUACHA KUABUDU,JUA,MWEZI,PICHA NA SANAMU ZA AINA MBALI MBALI, ALIWEZA KUFUNGA NDOA NA SARA ( MKE WA KWANZA WA NABII IBRAHIMU).
BAADAE NABII IBRAHIMU ALIWEZA KWENDA NA KUINGIA AFRIKA KATIKA INCHI YA MISRI. ALIPOINGIA KATIKA CHI YA MISRI, ALIKUWEPO MFALME MWENYE TAMAA YA WANAWAKE WAZURI. SARA (MKE WA IBRAHIMU ALIKUWA NI MKE MWENYE UMBO ZURI NA SURA NZURI YA KUVUTIA. MFALME ALIPEWA TAARIFA YA KWAMBA KUNA MWANAMKE MZURI ALIYE INGIA NDANI YA NCHI YAKE NA NI MZURI NA ANASIFA ZA KUCHUKULIWA NA MFALME. MFALME ALIKUJA HARAKA KUANGALIA MREMBO HUYO NA KISHA AKAMUULIZA NABII IBRAHIMU KUHUSU UHUSIANO WAKE NA MWANAMKE HUYO, NABII IBRAHIMU KWA UPEO WA FAHAMU ALIOJALIWA NA MUNGU ALIWEZA KUELEWA NIA YA MFALME YULE NA AKATUMIA NJIA YA UONGO ILI AEPUKE SHARI YAKE.
NABII IBRAHIMU ALIMWAMBIA KWAMBA SARAH NI DADA YAKE, KISHA MFALME AKAMCHUKUA NA KWENDA NAYE NYUMBANI KWAKE.MFALME ALITAKA KUFANYA MAPENZI AU KUMBAKA SARAH, LAKINI KUTOKANA NA ULIZI WA MWENYEZI MUNGU JUU YA NABII IBRAHIMU NA MKEWE SARAH,MFALME ALIPOOZA MWILI WAKE, NA AKAWEZA KUTAMBUWA KWAMBA MWANAMKE HUYO SI WAKAWAIDA NA ANA ULINZI WA MWENYEZI MUNGU.
MFALME ALIHITAJI TIBA KUTOKA KWA SARAH,AKASEMA IKIWA UTAMWOMBA MUNGU WAKO ANIRUDISHE KATIKA HALI YANGU YA KAWAIDA NTAKUPA MALI NA KIJAKA VITAKUWA MALI YAKO.
SARAH AKAMWOMBA MWENYEZI MUNGU, ILI AMUONDOLEE MFALME ADHABU HUSIKA. MFALME KAMA ALIVYOMUAHIDI SARAH AKAMPA MALI NA KIJAKAZI KUTOKA AFRIKA NAYE KIJAKAZI HUYO NI HAJIRI.
NABII IBRAHIMU ALIMWAMBIA KWAMBA SARAH NI DADA YAKE, KISHA MFALME AKAMCHUKUA NA KWENDA NAYE NYUMBANI KWAKE.MFALME ALITAKA KUFANYA MAPENZI AU KUMBAKA SARAH, LAKINI KUTOKANA NA ULIZI WA MWENYEZI MUNGU JUU YA NABII IBRAHIMU NA MKEWE SARAH,MFALME ALIPOOZA MWILI WAKE, NA AKAWEZA KUTAMBUWA KWAMBA MWANAMKE HUYO SI WAKAWAIDA NA ANA ULINZI WA MWENYEZI MUNGU.
MFALME ALIHITAJI TIBA KUTOKA KWA SARAH,AKASEMA IKIWA UTAMWOMBA MUNGU WAKO ANIRUDISHE KATIKA HALI YANGU YA KAWAIDA NTAKUPA MALI NA KIJAKA VITAKUWA MALI YAKO.
SARAH AKAMWOMBA MWENYEZI MUNGU, ILI AMUONDOLEE MFALME ADHABU HUSIKA. MFALME KAMA ALIVYOMUAHIDI SARAH AKAMPA MALI NA KIJAKAZI KUTOKA AFRIKA NAYE KIJAKAZI HUYO NI HAJIRI.
NABII IBRAHIMU AKAONDOKA NA MKE WAKE NA KIJAKAZI WAO PAMOJA NA MALI ZAO NA KUELEKEA KATIKA NCHI YA KANANI ( NCHI YAKANANI AU SHAMU NI ENEO LA MASHARIKI YA KATI AU ENEO LA KATIKATI YA DUNIA ).
IBRAHIMU ALIKUWA LIPEZI CHA WATOTO LAKINI ALIFIKIA UMRI WA MIAKA ZAIDI YA SABINI BILA KUWA NA MTOTO. KILICHOTOKEA NI KWAMBA SARAH ALITAMBUWA KWAMBA MME WAKE NABII IBRAHIMU ANAHAJA YA MTOTO LAKINI YEYE NI TASA HAWEZI KUPATA MIMBA. SARAH ALICHOKIFANYA ALIONGEA NA MME WAKE AKAMWELEZA YA KWAMBA KAMA ANAWEZA AU KAMA YUKO TAYARI, ANAWEZA KUMCHUKUWA HAJIRI NA AKAMFANYA MKE WAKE WA PILI, WENDA MWENYEZI MUNGU ANAWEZA KUWAPA MTOTO.
KUMBUKA YA KWAMBA KIJAKAZI HUYO ALIKUWA MALI YA SARAH ALIOPEWA NA MFALME KAMA SHUKURANI. SARAH ALICHUKUA MAMUZI YA KUCHUKUWA MALI YAKE ( KIJAKAZI WAKE HAJIRI ) NA AKAMTOA KWA MME WAKE NABII IBRAHIMU NA AKABARIKI ( SARAH AKARIDHIA JUU YA USHIRIKIANO HUO WA IBRAHIMU NA HAJIRI ) KUISHI KATIKA NDOA BAINA YA HAJIRI NA IBRAHIMU, NAYE SARAH AKIWA KAMA SHAHIDI WA NDOA HUSIKA.
HAKUNA UHARAMU WA MAISHA YA NABII IBRAHIMU NA HAJIRI KATIKA KUISHI KAMA MKE NA MUME KWASABABU NI JAMBO AU KITENDO KILICHOBARIKIWA NA MKE WAKE WA KWANZA ( SARAH ).
IBRAHIMU ALIWEZA KUMTIA MIMBA HAJIRI ( YULE MWANAMKE KUTOKA AFRIKA NDANI YA CHI YA MISRI ) NA WAKAPATA MTOTO WAO WA KWANZA JINA LAKE ISMAIL.
ISMAIL ALIKUWA MTOTO WA KWANZA WA NABII IBRAHIMU AU BABA WA IMANI,NA AKAWA NA NASABA AU AKAWA NI KIUNGANISHI KITUKUFU KILICHOUNGANISHA BARA LA AFRKA NA MARA LA MASHARIKI YA KATI. ISMAIL MAMA YAKE ALIKUWA NI MWAFRIKA NA BABA YAKE AKIWA NI MTU WA BARA LA MASHARIKI YA KATI.
KUNA BAADHI YA WATU WANAODAI YA KWAMBA ISMAIL NI MTOTO HARAMU WA NABII IBRAHIMU. LAKINI IKUINGALIA HISTORIA YA MAISHA YA NABII IBRAHIMU ALIPEWA CHEO KIKUBWA CHA KUITWA BABA WA IMANI. IKIWA ALIWEZA KUZAA MTOTO WA HARAMU CHO HICHO KINA MANA GANI ?
NA KWANINI WATU WASEME KWAMBA HAJIRI ALIKUWA MKE HARAMU WA IBRAHIMU AU KWASABABU ALIKUWA NI KIJAKAZI NA MTU KUTOKA KATIKA BARA ( LA AFRIKA ) AMBALO BAADHI YA WATU, WANAAMINI KWAMBA AFRIKA HAINA WATU WENYE UPEO AU UWEZO WAKUFIKIRI NA KUFANYA MAAMUZI SAHIHI.
INAKUWAJE SARAH AMKUBALIE AU ATOE USHAURI WA KUTENGENEZA NDOA YA UASHERATI NA KUJENGA MISINGI YA KUPATA MTOTO HARAMU KWA MME WAKE ? UKWELI WA MAMBO NI KWAMBA HUO NI UBAGUZI WA RANGI AMBAO VINYWA VYA WATU VILIJARIBU AU VINAENDELEA KUTAMKA NA KUTENDA BILA KUJALI MADHARA YA KUMSINGIZIA NABII IBRAHIMU KWAMBA ALIFANYA UASHERATI NA HAJIRI NA WAKAPATA MTOTO WA KAMWITA ISMAIL. HUU NI UONGO DHAHIRI.
USHAHIDI WA SIFA YA IBRAHAMU UNAPATIKANA KATIKA BIBLIA UKISEMA HIVI :
BASI, TUSEMEJE KWA IBRAHIMU,BABA YETU KWA JINSI YA MWILI ? KWA MAANA IKIWA IBRAHIMU ALIHESABIWA HAKI KWA AJILI YA MATENDO YAKE.
( WARUMI 4:12 )
NABII IBRAHIMU KUWA TENGANISHA WAKE ZAKE
BAADA YA KUZALIWA ISMAIL ZILIPITA SIKU KADHA NABII IBRAHIMU AKAPEWA AMRI NA MWENYEZI MUNGU YA KUMHAMISHA HAJIRI NA KUMPELEKA KATIKA NCHI YA SAUDIA.
BAADA YA SAFARI HIYO MUNGU ALIMPA AMRI NABII IBRAHIMU YA KUMWACHA MKE WAKE NA MTOTO WAKE JANGWANI, KATIKA JANGWA HILO PALIKUWA HAKUNA MAJI WALA MTI AU CHAKULA CHOCHOTE. IBRAHIMU ALIKUWA NA IMANI KUBWA SANA JUU YA MUUMBA WAKE NA AKAVUMILIA KUMWACHA MKE WAKE NA MTOTO WAKE JANGANI SEHEMU AMBAYO KUNA KILA DALILI YA HATARI( WANYAMA WAKALI,NJAA,KIU,HAKUNA NYUMBA WALA MSAADA WOWOTE.
NABII IBRAHIMU ALIWEZA KUINUWA MIKONO YAKE NA AKAMUOMBA MWENYEZI MUNGU ULINZI WA FAMILIA YAKE NA KUOMBA CHAKULA NA MAJI JUU YA FAMILIA YAKE. BAADA YA HAPO NABII IBRAHIMU ALIRUDI AU ALIONDOKA AKAENDA KWA MKE WAKE AU MAKAZI YAKE YA ZAMANI.
SARAH,ALIKUWA MWANAMKE MWENYE KUMHESHIMU MWENYEZI MUNGU NA MUME WAKE. SARAH ALIKUBALI KUBAKI KATIKA MTIHANI MKUBWA LAKINI MWISHOWE MTOTO AKAWA ANAHITAJI CHAKULA NA MAJI. SARAH ALIHANGAIKA SANA AKITEMBEA HAPA ( SAFA )NA PALE ( MARUA ) AKITAFUTA MAJI SAFARI HII ILIKUWA NA TIRIPU SABA.
SARAH ALIPORUDI KUANGALIA HALI YA MTOTO WAKE ( ISMAIL ) ALIKUTA KUNA CHEMCHEM YA MAJI ILIOANZA KUJITOKEZA CHINI YA MIGUU YA MWANAE ( ISMAIL ), AKAMNYANYUA AKAMNYWESHA ISMAILI (MWANAYE) MAJI NAYE SARAH AKANYWA. MAJI HAYO YALIOTOKANA NA KILIO,KUHANGAIKA KWA SARAH NA SAFARI YA IBRAHIMU, YANAITWA MAJI YA ZAMZAM. MAJI YA ZAMZAM YANAPATIKANA KATIKA NCHI YA SAUDIA KATIKA MJI WA MAKKA.
MTOTO MWENYE MCHANGANYIKO WA BARA LA AFRIKA NA BARA LA MASHARIKI YA KATI AKAJENGA UKUTA WA HISTORIA NA MAMA YAKE HAJIRI AKAWA NDIO MSINGI WA HISTORIA NA SARAH MKE WA KWANZA WA NABII IBRAHIMU AKAWA NI MWEZESHAJI WA HISTORIA NA NABII IBRAHIMU AKAWA MWENDESHAJI MKUU WA HISTORIA NA MWENYEZI MUNGU AKAWA NDIE MPANGAJI BORA WA KILA JAMBO KATIKA HISTORIA HUSIKA.
BIBLIA
BASI, YEYE AWAPAYE ROHO NA KUFANYA MIUJIZA KATI YENU, JE! AFANYA HAYO KWA MATENDO YA SHERIA, AU KWA KUSIKIA KUTOKANA NA IMANI ?
KAMA VILE IBRAHIMU ALIVYOMWAMINI MUNGU AKAHESABIWA HAKI.
( WAGALATIA 3:5, 6 )
BIBLIA
FAHAMUNI BASI, YA KUWA WALE WALIO WA IMANI, HAO NDIO WANA WA IBRAHIMU. NA ANDIKO, KWA VILE LILIVYOONA TANGU ZAMANI KWAMBA MUNGU ATAWAHESABIA HAKI MATAIFA KWA IMANI, LILIMHUBIRI IBRAHIMU KWA HABARI NJEMA ZAMANI, KUSEMA,KATIKA WEWE MATAIFA YOTE WATABARIKIWA. BASI HAO WALIO WA IMANI HUBARIKIWA PAMOJA NA IBRAHIMU ALIYE KUWA MWENYE IMANI.
( WAGALATIA 3: 7……..9 )
KILA JAMBO MAISHANI LINA MFUMO WAKE NA MPANGAJI MKUBWA NI MWENYEZI MUNGU. MWENYEZI MUNGU ALIANZISHA MAISHA YA NABII IBRAHIMU KATIKA FAMILIA YA WASHIRIKINA NA AKAMWEZESHA KUWA MBORA WA IMANI ZAIDI YA WATU WOTE BAADA YA MAISHA YAKE.
YESU “ NAJUA YA KUWA NINYI NI UZAO WA IBRAHIMU, LAKINI MNATAFUTA KUNIUA KWA SABABU NENO LANGU HALIMO NDANI YENU.
( YOHANA MTAKATIFU 8 : 37 )
YESU ( ISA ) ALITOA MFANO HUO KWA WANA WA ISRAEL, KWASABABU WALIKUWA WAKITENGENEZA HILA ( UBAYA ) YA KUMUONDOA DUNIANI.
WANA WA ISRAELI WANAAMINI KWAMBA NABII IBRAHIMU NI BABA YAO, NA HILO YESU ALIKUWA ANALITAMBUA LAKINI KILICHOMSHANGAZA YESU NI KWAMBA LICHA YA WANA WA ISRAELI KUAMINI NABII IBRAHIMU KAMA BABA YAO KATIKA MWILI NA IMANI, MATENDO YAO YALIKIUWA TOFAUTI NA TABIA YA MANENO NA VITENDO VYA NABII IBRAHIMU.
WANA WA ISRAELI WALIJENGA MISINGI YA KWENDA KINYUME NA UTARATIBU WA DINI ( NJIA YA IBRAHIMU ) YA BABA YAO IBRAHIMU NA ISAKA NA YAKOBO, WAKAANZA KUFUATA MATAMANIO YAO YA MAISHA YA DUNIA BILA KUJALI AMRI NA SHERIA ZA MWENYEZI MUNGU NA KANUNI NA UTARATIBU WA IMANI YA NABII IBRAHIMU.NDIO MAANA YESU AKAWAAMBIA WANA WA ISRAELI AU WAYAHUDI HIVI “
BIBLIA
KAMA MNGEKUWA WATOTO WA IBRAHIMU, MNGEZITENDA KAZI ZAKE IBRAHIMU.
( YOHANA MTAKATIFU 8 : 39 )
QURAN :
MWENYEZI MUNGU ANASEMA “ NA BILA SHAKA TULIMPELEKA NUHU NA IBRAHIMU, NA TUKAUWEKA KATIKA KIZAZI CHAO UNABII NA KITABU, LAKINI WENGINE KATIKA WAO WALIKUWA WAONGOFU NA WENGINE KATIKA WAO WALIKUWA WAASI.
( 57 : 26 )
MAJARIBIO YA NABII IBRAHIMU YA KUMCHINJA MWANAE ISMAIL
BAADA YA NABII IBRAHIMU KUMPATA MTOTO WA PEKE AMBAYE NI ISMAIL, MWENYEZI MUNGU ALITOA MAJARIBU MENGINE KWA NABII IBRAHIMU NA MWANAE ISMAIL. JARIBIO HILO LA IMANI LILIKUWA NI AMRI KUTOKA KWA MUNGU KWENDA KWA NABII IBRAHIMU. MUNGU ALIMPA ABRAHAMU AMRI YA KUMCHINJA MWANAE WAPEKE, NAKIPINDI HICHO SARAH ALIKUWA HAJAPATA MTOTO.
BIBLIA INAELEZA SIFA ZA NABII IBRAHI, YAKWAMBA ALIHESABIWA HAKI KWA AJILI YA MATENDO YAKE. NABII IBRAHIMU ANGELIKUWA AMEZINI AU AMEFANYA UASHERATI NA HAJIRI, ANGEWEZAJE KUPATA HAKI KWA AJILI YA MATENDO YAKE?
KWA KWELI SI JAMBO LA BUSARA KUZUNGUMZA KWAMBA HAJIRI NI MWANAMKE MALAYA NA ISMAIL KUWA NI MTOTO WA HARAMU. HUU NI UKOSEFU WA HESHIMA NA TAHADHIMA JUU YA NABII IBRAHIMU ,HAJIRI NA MTOTO WAO ISMAIL.
ALICHOKIFANYA NABII IBRAHIMU ALIKUBALI, KUTEKELEZA AMRI YA MWENYEZI MUNGU AKAWEZA KUMFUATA MWANAE KATIKA NCHI YA SAUDIA KATIKA MJI WAKE MKUU WA MAKKA. AKAMCHUKUWA MWANAE ISMAIL, AKAMPELEKA MPAKA SEHEMU AMBAYO MUNGU ALIMPANGIA. NABII IBRAHAMU ALIWEZA KUMUELEZA MWANAE ISMAIL, KUHUSU AMRI ILIOTOKA KWA MWENYEZI MUNGU. ISMAIL ALIWEZA KUPOKEA AMRI HUSIKA NA AKWEZA KUMTIA MOYO BABA YAKE AKASEMA “ BABA UNOE KISU CHAKO KIWE NA UKALI WA HALI YA JUU, ILI UKINICHINJA NISIWE MWENYE KUHISI MAUMIVU MAKALI, NA UNIFUNIKE AU UFUNGE KITAMBA MACHONI MWANGU, ILI USINIONEE HURUMA UKASHINDWA KUTEKELEZA AMRI YA MWENYEZI MUNGU”
MANENO HAYO YALITAMKWA NA ISMAIL, AKIONYESHA KUKOMAA KWA IMANI KAMA BABA YAKE ( NABII IBRAHIMU).
NABII IBRAHIMU ALIJARIBU KUMCHINJA MARA TATU KISU KIKASHINDWA KUKATA SHINGO LA ISMAIL.
BAADA YA HAPO MWENYEZI MUNGU ALITAMBUA YA KWAMBA NABII IBRAHIMU, ALIKUWA NA NIA YA KUTEKELEZA AMRI YAKE, NDIPO MWENYEZI MUNGU KAMTUMA MALAIKA JIBRILI ( GABRIELI ) AKAJA NA KONDO, AKAWA NDIO SADAKA YAKE ( NABII IBRAHIMU NA KUOKOA MAISHA YA MWANAE ISMAIL).
BAADA YA MDA MWENYEZI MUNGU ALIMPA NABII IBRAHIMU AMRI YA KUJENGA NYUMBA YAKE KATIKA MJI WA MAKKA. NABII IBRAHIMU ALIWEZA KUIJENGA KA’ABA KATIKA MJI WA MAKAA NDANI YA NCHI YA SAUDIA.
JENGO LA KA’ABA NI JENGO AMBALO NI KONGWE NA LENYE UIMARA WA HALI YA JUU. KATIKA RAMANI YA JENGO HILI, MBELE KIDOGO KUNA JIWE ( BLACK STONE ) LILILO TOKA MBINGUNI KAMA ALAMA YA SEHEMU YA UJENZI WA JENGO LA MWENYEZI MUNGU.
MIUJIZA YA JENGO LA KA’ABA
JENGO LA KA’ABA KWANZA LINA VIPIMO VILIVYO SAHIHI KATIKA RAMANI YAKE.
JENGO LA KA’ABA LIPO KATIKATI YA DUNIA PIMA MASHARIKI,MAGHARIBI,KUSINI NA KASKAZINI,UTAKUTA KILA KIPIMO KINA FANANA NA KINGINE BILA KUPUNGUA HATA CHEMBE.
MWENYEZI MUNGU ANASEMA “
QURAN :
NA ( KUMBUKA ) TULIPOMKALISHA IBRAHIMU MAHALI PENYE ILE NYUMBA ( TAKATIFU NA TUKAMWAMBIA ): “USINISHIRIKISHE NA CHOCHOTE NA ISAFISHE NYUMBA YANGU KWA AJILI YA WAIZUNGUKAO NA WANAOKAA HAPO ( KUFANYA IBADA YAO) NA WANAO RUKUU NA KUSUJUDU,( WANAOSALI).”
(22:26)
MWENYEZI MUNGU ALIMPA ONYO NABII IBRAHIMU ,KATIKA UJENZI WA NYUMBA YA KA’ABA ,YA KWAMBA ASIMSHIRIKISHE NA KITU
( SANAMU YA AINA YOYOTE ) NA AISAFISHE NYUMBA YAKE YA KA’ABA ILI WATU WAWE WANAIZUNGUUKA KATIKA IBAADA , KWA WAKAZI WA NCHI HIYO PAMOJA NA WAGENI.
NDIO MAANA KILA MWAKA WAISLAMU WANATOKA KATIKA NCHI MBALIMBALI DUNIANI NA KUELEKEA NCHINI SAUDIA KUTEKELEZA IBADA YA HIJA, KATIKA JENGO LILILO JENGWA NA NABII IBRAHIMU NA MWANAE ISMAIL.
WAISLAMU HUSUJUDU NA KURUKUU KATIKA IBADA YAO, NA NI ISHARA KUBWA YA IBADA. HAKUNA ANAE RUHUSA YA KUSUJUDIWA ISIPOKUWA MWENYEZI MUNGU PEKE YAKE. LABDA IPATIKANE AMRI KUTOKA KWA MWENYEZI MUNGU, KAMA ALIVYOAMURU MALAIKA WOTE KUMSUJUDIA ADAMU KAMA ISHARA YA UTUKUFU WA BINAADAMU.
QURAN
“ ILI WASHUHUDIE MANUFAA YAO NA (ILI WAKITHIRISHE) KULITAJA JINA LA MWENYEZI MUNGU KATIKA SIKU ZINAZO JULIKANA (FADHILA ZAKE) JUU YA YALE ALIYOWARUZUKU, NAO NI WANYAMA WENYE MIGUU MINNE. NA KULENI KATIKA WANYAMA HAO NA MLISHENI MWENYE SHIDA ALIYE FAKIRI.
(22:29)
MWENYEZI MUNGU ALIWEKA MFUMO WA HIJA, ILI WATU WAWEZE KUJUA MFUMO MZIMA NA MZURI WA KUFANYA IBADA, NAKUONDOA MASHAKA KATIKA IMANI YA WACHA MUNGU.
NA MWENYEZI MUNGU ANATOA AMRI JUU YA MATAJIRI ( WATU WENYE UWEZO ) KUCHINJA WANYAMA NA KUWAPA NYAMA MASIKINI. KUNA WATU MASIKINI AMBAO HAWANA UWEZO WA KUNUNUWA NYAMA AU KUMCHINJA MNYAMA, NDIO MAANA MWENYEZI MUNGU KAELEKEZA MAHITAJI YAO YA NYAMA JUU YA MATAJIRI WENYE UWEZO WA KUCHINJA MNYAMA AU WANYAMA.
NABII IBRAHIMU HANA MPINZANI KATIKA IMANI NA KILA KIZAZI CHENYE IMANI JUU YA MWENYEZI MUNGU WA KWELI INATOKANA NA MUONGOZO SAHIHI WA MATENDO NA MANENO YAKE.
FAMILIA YA NABII IBRAHIMU
NABII IBRAHIMU ALIKUWA NA WANAWAKE WA WILI AMBAO NI :
SARAH : KUTOKA KATIKA NCHI YA SHAMU, BARA LA MASHARIKI YA KATI.
MTOTO WA SARA NI ISAKA. KIZAZI CHAKE NI WANA ISRAELI.
2) HAJIRI : KUTOKA KATIKA NCHI YA MISRI, BARA LA AFRICA.
MTOTO WA HAJIRI NI ISMAIL. KIZAZI CHAKE WAARABU.
No comments:
Post a Comment