KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, August 24, 2009

Kadhaa wauawa mapiganoni Somalia


Idadi kubwa ya watu wameuawa katika mapigano zaidi yaliyotokea Mogadishu mji mkuu wa Somalia, kati ya wanamgambo wa al Shabaab na majeshi ya serikali, maafisa wameeleza.

Mgogoro huo umejitokeza licha ya wito wa rais Sheikh Sharif Sheikh Ahmad kutaka kusitishwa mapigano katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Baadhi ya mapigano ya Jumamosi yalijikita zaidi katika barabara muhimu inayounganisha Mogadishu na mji wa Afgoye.

Afisa mmoja wa serikali alieleza kuwa wanamgambo 10 waliuawa. Waziri wa ulinzi wa Somalia, Yusuf Mohamed Siyad, siku ya Jumamosi alieleza kuwa idadi ya wanamgambo waliouawa ilikuwa haijajulikana.

"Waliondoka na kuacha wenzao wamekufa ingawa wengine waliwachukua. Pia waliwachukua wanamgambo wenzao waliojeruhiwa - kwasababu hiyo hatuna idadi yao kamili."

Barabara ya kuelekea Afgoye inatumika kusafirisha shehena kuelekea makambi ambako maelfu ya watu waliokimbia makazi yao wanaishi.

No comments:

Post a Comment