KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, August 14, 2009

NIMPATEJE ! RAFIKI MWENYE UPENDO WA DHATI ?




RAFIKI NI MUUNGANO WA mwili na roho, IKIWA NAFSI MOJA AU ZAIDI YA MOJA. MUUNGANO WA NAFSI,NI KITENDO AMBACHO KINAHITAJI USHIRIKIANO WA VITENDO NA MANENO YENYE URIDHIANO BAINA YA NAFSI HUSIKA.



URIDHIANO WA NAFSI UNAHITAJI MSINGI ILI UWEZE KUWA IMARA. MSINGI WA MARIDHIANO BAINA YA NAFSI ( RAFIKI WA WILI ) NI UVUMILIVU WA KILA NAFSI JUU YA JAMBO HUSIKA.

KWA NINI UVUMILIVU
NI MSINGI WA MUUNGANO WA NAFSI ?





SABABU NI KWAMBA , KILA NAFSI INA AKILI YAKE. AKILI NI KIFA AMBACHO KINAHIFADHI ELIMU, INAYOWEZESHA NAFSI KUTAMBUWA JAMBO FULANI.

NAFSI HUTUMIA AKILI YAKE KATIKA HARAKATI ZA KUTENDA JAMBO FULANI LENYE MANUFAA JUU YAKE.
NAFSI HUINGIZA ELIMU NDANI YA AKILI YAKE NA KUIHIFADHI NDANI YA UBONGO WAKE,KUPITIA
VIFAA MAALUMU.

MOJAWAPO NI :

MACHO: MACHO HUINGIZA PICHA YA VITENDO,RANGI,SURA,UMBILE VYAKITU NDANI YA NAFSI.MTAZAMO WA NAFSI NI MACHO AU TAA LA MWILI NI MACHO.

MASIKIO : MASIKIO NI KIFAA AMBACHO KINAIWEZESHA NAFSI KUPOKEA KILA AINA YA SAUTI NA MANENO.

PUA : PUA HUWEZESHA NAFSI KUPUMUA NA KUONDOA HEWA CHAFU KICHWANI NA VILI VILE KUTAMBUA AINA ZA HARUFU ( ZA KUNUKIA AU KUNUKA )







MDOMO : MDOMO NI KIFAA AMBACHO KINAWEZESHA NAFSI KULA,KUNYWA,KUONGEA AU KUTOA DUKU DUKU ZILIZOMO MOYONI MWAKE. MOYO NI
MOJAWAPO WA KIFAA KINACHOPENDA AU
KUCHUKIA NA VILE VILE HUHIFADHI YA KUMBU KUMBU ZA NAFSI.MDOMO UNAWEZESHA NAFSI KUPATA LADHA ZA AINA MBALI MBALI ZA VYAKULA NA VINYWAJI.

KILA NAFSI YENYE VIFAA HIVYO
( MACHO ,MASIKIO,MDOMO NA PUA ) INAWEZA KUVITUMIA VIZURI KUTOKANA NA UWEZO WAKE WA UTAMBUZI ( ELIMU JUU YA JAMBO HUSIKA ) .
IKIWA KILA NAFSI INA UWEZO WAKE WA MTAZAMO JUU YA JAMBO FULANI.KUNAHITAJIKA UANGALIFU WA KUCHAGUA RAFIKI MWENYE VIGEZO AMBAVYO VINA KARIBIANA KUFANANA.UKARIBU WA TABIA, HUJAZWA NA UVUMILIVU.

No comments:

Post a Comment