KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Sunday, June 28, 2009
Tandja kukatalia madarakani Niger
Rais wa Niger Mamadou Tandja amejiongezea mamlaka ya kukiuka katiba
Rais wa Niger Mamadou Tandja anasema atachukua mamlaka ya dharura yasiyozingatia katiba kuongoza nchi , baada mahakama kukataa mpango wake wa kuongeza muda wa uongozi kwa miaka mitatu.
Tandja mwenye umri wa miaka 71 alitoa tangazo hilo baada ya mahakama kuu ya Niger kutoa uamuzi wa kupinga kura ya maoni ambayo ingemuongezea muda wa miaka mitatu zaidi uongozini.
Bwana Tandja ametawala taifa hilo la Afrika magharibi tangu mwaka wa 1999 , ambayo ni mihula miwili.
Mpango wake wa kukatalia madarakani umeibua malalamiko makubwa nchini Niger na umeshtumiwa na wafadhili wa kimataifa.
Lakini wafuasi wa Bwana Tandja wanasema ameleta ukuaji wa uchumi na anastahiki kugombea tena uongozi.
Kwenye hotuba kupitia Televisheni, rais huyo amesema anachukua mamlaka ya kuzidi , '' kwa sababu uhuru wa nchi unatishiwa''.
Hotuba yake ilitolewa saa kadhaa baada ya mahakama ya kikatiba kukatalia mbali ombi lake la kuitaka ibadilishe uamuzi wa hapo awali uliosema kura ya maoni ni kinyume cha sheria.
Bwana Tandja alitangaza mpango wake wa kuitisha kura ya maoni mwezi Mei. Lakini pingamizi kubwa zilifuatia kutoka kwa upinzani na vyama vya wafanyakazi , ambavyo vilikwenda mahakamani .
Rais huyo baadaye alivunja bunge na kuamua kuchukua madaraka ya kuzidi, yasiyozingatia katiba.
Wakati huo huo, tume ya uchaguzi nchini Niger imepanga uchaguzi wa bunge ufanyike tarehe 20 mwezi Agosti , wiki mbili baada ya tarehe iliyopendekezwa ya kura ya maoni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment