KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Sunday, June 28, 2009

Michael Jackson 'hakufanyiwa hila'

Michael alihama kutoka makazi yake ya Neverland na alienda kuishi Dubai. Sherehe yake ya kutimiza miaka 50 ilifanyika Las Vegas. Amekuwa akionekana kuwa na afya dhaifu, ingawa alikuwa akijiandaa kufanya mfululizo wa matamasha jijini London.



Mwaka 2003 kibali kilitolewa kukamatwa kwa Michael akikabiliwa na mashtaka ya kunajisi mtoto mwenye umri wa miaka 14. Baada ya kesi iliyoungura kwa miezi mitano na kumalizika 2005, mwanamuziki huyo hakupatikana na hatia yoyote.

Katika maisha yake Michael alizongwa na utata kila alikoenda. Mwaka 1994 alimwoa Lisa Marie Presley baada ya kuwa wamekutana kwa mara ya kwanza mwaka 1975. Walitalikiana chini ya miaka miwili baadaye.



Michael Jackson

Hizi ni baadhi tu ya picha zinazotukumbusha maisha ya mwanamuziki Michael Jackson aliyeaga dunia akiwa na umri wa miaka 50.


Michael aliipua "Bad" mwaka 1987 na baada ya hapo kufanya ziara ya matamasha ya kwanza duniani, nchini Uingereza tiketi katika uwanja wa Wembley ziliuzwa zote alipofanya matamasha saba na kuweka rekodi ya mashabiki.


Baada ya hapo Michael alijitenga na kaka zake kisha akapakua kibao "Off the Wall" mwaka 1978, lakini Thriller iliyotolewa miaka minne baadaye ndiyo ilifanya muziki wa pop kupata umaarufu mpya, ilifanikiwa kuuza nakala milioni 65.




Michael Jackson alianza shughuli za muziki akiwa na kaka zake wakiunda kundi la Jackson 5, na kundi hilo lilipofyatua kibao chao cha kwanza "I Want You Back" mwaka 1969, kiligonga namba moja kwa umaarufu - wakati Michael alikuwa na umri wa miaka 11 tu.







Mara ya mwisho imebadilishwa: 27 Juni, 2009 - Imetolewa 09:46 GMT




Mtumie rafiki barua pepe Chapisha

Michael Jackson 'hakufanyiwa hila'

Imeandikwa na Mwandishi wa BBC








Madaktari waliochunguza kifo cha mwanamuziki maarufu wa mtindo wa Pop, Michael Jackson, aliyefariki dunia Alhamisi, wamesema matokeo ya awali hayajaonyesha hila yoyote.
Lakini vipimo vingine vikiwemo vya sumu vimechukuliwa ambapo uchunguzi wake unaweza kuchukua majuma kadhaa, ofisi ya mchunguzi wa vifo vya Los Angeles ilieleza.

Maafisa wamesharuhusu ndugu kuuchukua mwili wa Jackson, lakini bado hakujawa na taarifa zozote kuhusu mazishi yake.

Waombolezaji wakiwemo wasanii wenzake, viongozi wa mataifa mbali mbali na mashabiki wamekuwa wakitoa rambi rambi zao kwa mwanamuziki huyo.

Jackson aliyekufa akiwa na umri wa miaka 50, siku ya kifo chake alikimbizwa hospitalini huko Los Angeles, Marekani, baada ya kupata matatizo yanayodhaniwa kuwa ya moyo.


Picha za maisha ya Michael Jackson

Taarifa za awali zilieleza kuwa mwanamuziki huyo alikuwa hapumui wakati madaktari wa huduma ya kwanza walipofika kumsaidia nyumbani kwake maeneo ya Bel Air yapata saa sita na nusu majira ya huko. Lakini mwishowe maafisa wakathibitisha kifo chake.

Utata mkubwa uligubika hali ya afya ya mwanamuziki huyo aliyewahi kutamba na albamu mbali mbali kama Thriller.


Maoni ya kifo cha Michael Jackson

Wavuti ya TMZ ambayo huandika taarifa za watu mashuhuri katika maswala ya burudani ilikuwa ya kwanza kuandika kuwa Michael Jackson mwenye umri wa miaka 50 alikuwa ameaga dunia.

Vile vile, gazeti maarufu la Los Angeles Times liliandika katika wavuti yake kuwa Michael Jackson amefariki. Lakini vyombo vingine vya habari vilikuwa vikisema alikuwa bado yu hai, ingawa alikuwa mahututi.


Picha za maisha ya Michael Jackson

Madaktari wa huduma ya kwanza walijaribu kuuzindua moyo wa Jackson wakati gari ya wagonjwa ilipokuwa ikimkimbiza katika hospitali ya UCLA, maafisa wameeleza.

Jackson alikuwa akitarajiwa kuanza matamasha mbali mbali ya kufufua kipaji chake kwenye ukumbi wa O2 jijini London ifikapo tarehe 13 Julai.

Imeelezwa alikuwa na historia ya matatizo ya kiafya na hajawahi kukamilisha ziara ya matamasha kwa kipindi cha miaka 12 iliyopita.

Maoni
Utakumbuka kitu gani kuhusu maisha ya mwanamuziki Michael Jackson? Tuandikie nasi tutayachapisha maoni yako katika wavuti hii.

No comments:

Post a Comment