KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, June 27, 2009

KILA NAFSI ITAONJA MAUTI, KIFO CHA MICHAEL JACKSON NI UJUMBE TOSHA KUHUSU MWISHO WA UHAI WA NAFSI.







KIFO CHA MFALME WA POP DUNIANI MICHAEL JACKSON ALIEAGA DUNIA GHAFLA USIKU WA KUAMKIA LEO KATIKA HOSPITALI YA UCLA MJINI LOS ANGELES. TAARIFA ZA AWALI TOKA KATIKA CHANZO KIMOJA KWENYE HOSPITAL ALIOFIA YA UCLA ZIMEDAI KUWA HUENDA KIFO CHAKE KIMETOKANA NA KUTUMIA KWAKE DOZI ILIYOPITILIZA YA DAWA ZA KUONDOA MAUMIVU. CHANZO KATIKA CHUMBA CHA DHARURA CHA HOSPITALI HIYO YA UCLA KIMEDAI WASAIDIZI WA JACKSON WALIMUAMBIA DOKTA KUWA ALIANGUKA BAADA YA KUDUNGWA SINDANO YA KUTULIZA MAUMIVU YA DEMOL - AMBAYO NI SAWA NA MORPHINE.





CHANZO NYUMBANI KWA JACKSONI KIMESEMA : “MUDA MFUPI BAADA YA KUPATA SINDANO YA DEMOROL ALIANZA KUPUMUA KWA SHIDA.

“ KUPUMUA KWAKE KUKAZIDI KUPUNGUA NA KUPUNGUA NA HATIMAYE KUKASIMAMA.

“ WAFANYAKAZI WAKE WAKAANZA KUHAHA NA KUITA GARI LA WAGONJWA AMBALO LILIFIKA BAADA YA DAKIKA NANE.

“LAKINI WAKAMKUTA AMEZIMIKA KABISA, HAPUMUI NA MAPIGO YAKE YA MOYO YAMESIMAMA. WAKAANZA KUMHUDUMIA NA KUMKIMBIZIA HOSPITALI.


“ ALIPOFIKA HOSPITALI …..WAKAMWEKEA MIPIRA YA KUMSAIDIA KUPUMUA NA PIA KUCHUKUA HATUA NYINGINE KADHAA ZA KUJARIBU KUOKOA MAISHA YAKE.

“HAKUWEZA KUREJEWA NA FAHAMU. FAMILIA IKAAMBIWA BAADAYE KUWA AMESHA FARIKI DUNIA.”

MASHABIKI NA FAMILIA WAPAGAWA KABISA

KADRI HABARI ZA KIFO CHA M.JACKSON ZILIVYOSAMBAA, MAELFU YA MASHABIKI WAKE WAKAPAGAWA NA KULAZIMIKA KUFURIKA KWA WINGI KWENYE VIUNGA VYA HOSPITALI YA UCLA.

WENGI WAO WALIONEKANA WAKIWA NA MAVAZI YENYE ALAMA ZA KIBIASHARA ZA MWIMBAJI HUYO NA WENGINE WAKAWA WAKIREJEA MAPIGO YA BAADHI YA NYIMBO ZAKE.



FAMILIA YA M.J ILIJAWA NA KIHORO ,HUKU IKISEMA KUWA MPENDWA WAO HUYO ALIKUWA AMEZIMIA KATIKA JUMBA LAKE LA KUKODI LA LOS ANGELES WAKATI KAKA YAKE RANDY AKIWEPO.

MAMA YAKE KATHERINE ALIKIMBILIA HARAKA HOSPITALINI, HUKU BABA YAKE JOE AKIFANYA HIVYO AKITOKEA LAS VEGAS. DADA YAKE ELIZABETH TYLOR PIA ALIKIMBILIA HOSPITALI KUMUAGA.




MWISHOWE, FAMILIA ILIPAGAWA ZAIDI WAKATI DOKTA ALIPOWAAMBIA KUWA JITIHADA ZOTE ZA KUWEZESHA MOYO WAKE KUPIGA TENA ZIMESHINDWA NA KWAMBA AMESHAFARIKI DUNIA.

DADA YAKE LA TOYA ALIONEKANA AKIKIMBIA HOVYO HOSPITALINI HUKU NA HUKO WAKATI ALIPATA TAARIFA ZA KIFO HICHO CHA KAKA YAKE.




M. JACKSON ALIKUWA AKIKAA KWENYE JUMBA HILO LA LOS ANGELES WAKATI AKIENDELEA KUJIFUA KWA AJILI YA ONYESHO KUBWA LA ZIARA YA KUTAMBULISHA MAREJEO YAKE YA MWEZI UJAO.



ZAIDI YA TIKETI 750,000 ZILISHAUZWA KWA AJILI YA MAONYESHO YA ZIARA HIYO YA MATAMASHA YA KUREJEA KWA MFALME WA POP MWEZI UJAO.

“ALIKUWA NA AFYA NJEMA.
ALIKUWA AKIFANYA MAZOEZI,AKICHEZA,AKIJIANDAA NA MAONYESHO YAKE YA UINGEREZA NA KWAKWELI NIMESTUSHWA NA KIFO CHAKE, HILO NDILO NINALOWEZA KUSEMA,”
ALISEMA NDUGU YAKE MMOJA.

HISTORIA YA MACHAEL JACKSON KWA KIFUPI



M.J. NI ALIKUWA MTOTO WA SABA KATIKA WATOTO TISA.
M.J. ALIZALIWA MAWAKA WA OGOSTI 29 – 1958,
HUKO GARY,INDIANA, AMEFARIKI SAA 6:26 TAREHE 26 JUNE MWAKA 2009.

M.J. AMEFARIKI DUNI AKIWA NA UMRI WA MIAKA 50

M.J. ALIINGIA KWENYE ULIMWENGU WA MZIKI AKIWA NA UMRI WA MIAKA 11.
M.J.ALIITIKISA DUNIA KWA STAIRI ZAKE ZA MASHAIRI,KUCHEZA,MAVAZI…………NK.




MFALME HUYO WA POP,AMBAYE VIBAO VYAKE VILIVYOTIKISA NI PAMOJA NA ‘THRILLER’ NA
‘ BILLIE JEAN’,ANAONDOKA AKIACHA NYUMA MZIGO WA MADENI NA MLOLONGO WA MAONYESHO YASIYOTIMIZWA YA KURUDI TENA KWAKE JUKWANI YALIOKUWA YAMEPANGWA KUFANYIKA LONDON MWEZI UJAO.


WATU WENGI WALIKUWA NA MATUMAINI KWAMBA MAONYESHO HAYO YATAINGIZA MAMILION NA KUMALIZA MATATIZO YAKE YA KIFEDHA.

LAKINI MUDA WA NAFSI YA BINAADAMU MAISHANI MWAKE NI SIRI YA MWENYEZI MUNGU. PANGA KILA JAMBO LAKINI USISAHAU KUSEMA INSHALLAH
( MWENYEZI MUNGU AKIPENDA )








REKODI NYA JACKSON KATIKA MAUZO

JUMLA YA REKODI AMBAZO AMEUZA KATIKA MAISHA YAKE ZILIKUWA ZIKIAMINIKA KUWA TAKRIBANI MILIONI 750, NA AKIWA MTU ALIYE SHINDA TUZO 13 ZA GRAMMY NA MAUZO MAKUBWA YA VIDEO ZA MUZIKI DHAHIRI ALIKUWA NI MMOJA KATI YA WABURUDISHAJI WALIOFANIKIWA ZAIDI DUNIANI.








M.J. ALITOA ALBAMU YAKE YA KWANZA MWAKA 1972, NA ALITOA “THRILLER” MWAKA 1982, AMBAYO ILITIKISA MASHABIKI WENGI DUNIANI NA KUTOA NYIMBO SABA KATIKA KUMI BORA DUNIANI.

ALBAMU HIYO ILIUZA NAKALA MILIONI 21 NCHINI MAREKANI NA TAKRIBAN MILION 27 SEHEMU MBALIMBALI DUNIANI.


MAISHA YA NDOA YA MICHAEL JACKSON

MWAKA 1994,M.J. ALIMUOA MTOTO PEKE WA MWANAMUZIKI NYOTA MAREHEMU ELVIS PRESLEY, LISA MARIE, LAKINI NDOA HIYOILIHITIMISHWA KWA TALAKA MWAKA 1996.

M.JACKSON ALIMUOA DEBBIE ROWE MWAKA 1996 NA NA WALIPATA WATOTO WA WILI,KABLA YA KUACHANA MWAKA 1999, NA BAADAYE ALIPATA MTOTO MWINGINE KWA MWANAMKE MMOJA AMBAYE HAJATAMBULIKA.





M.J. ALIOA WANAWAKE WAWILI NA WOTE WAMEBAKI KATIKA HALI AU MAISHA YA UJANE.

M.J. AMEACHA KIHORO KWA WATOTO WAKE WATATU AMBAO NI MICHAEL JOSEPH JACKSON, JR,PARIS NA PRINCE “BLANKET” MICHAEL JACKSON II.


KUTAMBULIKA KWA VIPAJI VYA JACKSON NA NDUGU ZAKE

WATOTO WA TANO WA FAMILIA YA JACKSON AMBAO NI JACKIE,TITO,JERMAINE, MARLON NA MICHAEL - WALIFANYA KWANZA ONYESHO LA PAMOJA LA KUDHIHIRISHA VIPAJI VYAO WAKATI MICHAEL AKIWA NA UMRI WA MIAKA 6.


WALIIBUKA NA ZAWADI YA USHINDI NA KUJA KUWA KUNDI LILILOUZIKA SANA LA THE JACKSON FIVE, NA KASHA THE JACKSONS.

WATOTO WA KIKE NI REBBIE, LA TOYA NA JANET HUKU MWINGINE WA KIUME NI RANDY.

LAKINI MICHEL JACKSONI ALIWEZA KUTOA ALBAMU YAKE YA KWANZA KIVYAKE MWAKA 1972, NA ALITOA “THRELLER” MWAKA 1982,AMBAYO ILITIKISA NYOYO ZA WASHABIKI WENGI WA MZIKI DUNIANI.

No comments:

Post a Comment