KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Wednesday, June 10, 2009
Kiongozi wa muda achaguliwa Gabon
Rose Francine Rogombe anajaza pengo kwa muda lililoachwa kufuatia kifo cha Bongo
Rose Francine Rogombe
Rose Francine Rogombe anajaza pengo kwa muda lililoachwa kufuatia kifo cha Bongo
Spika wa bunge la Gabon, ameapishwa leo kuwa kiongozi wa muda wa Gabon, kufuatia kifo cha rais wa nchi hiyo, Omar Bongo.
Kulingana na katiba ya Gabon, Rose Francine Rogombe, swahiba wa muda mrefu wa Bw Bongo, lazima aitishe uchaguzi chini ya siku 45.
Siku ya Alhamisi mwili wa Bw Bongo unatazamiwa kusafirishwa kutoka Uhispania alikofariki akiwa anatibiwa, hadi Gabon.
Mawasiliano ya tovuti katika nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa mafuta bado yamekatizwa, lakini angalau mipaka imefunguliwa.
Bi Rogombe aliapishwa katika ukumbi wa International Conference Centre katika mji mkuu wa Libreville, asubuhi ya Jumatano, siku moja tu baada ya katiba ya nchi hiyo kuhalalisha mamlaka yake.
Siku ya Jumanne, mwana wa wa Bw Bongo, Ali-Ben Bongo, ambaye ni waziri wa ulinzi, aliwataka raia wa nchi hiyo kuendelea kuwa watulivu.
Kifo cha rais huyo aliyekuwa na umri wa miaka 73, na akiwa ndiye rais aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi barani Afrika, kilithibitishwa siku ya Jumatatu.
Atazikwa katika mji wa Franceville, katika eneo la Bateke, kusini-mashariki Gabon, Alhamisi wiki ijayo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment