KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Wednesday, June 10, 2009
28 wafariki katika mlipuko Iraq
Mlipuko mkubwa umetokea katika soko moja ambalo lilikuwa limejaa pomoni katika mji wa kusini wa Bathaa nchini Iraq, na kulingana na maafisa wa serikali, kusababisha vifo vya watu wasiopungua 28.
Wengine wengi walijeruhiwa katika mlipuko huo uliotokea saa za asubuhi.
Eneo hilo limeshuhudia vita vikali hivi karibuni kati ya makundi mbalimbali ya Ki-shia.
Shambulio hilo limefanyika wiki chache kabla ya wanajeshi wa Marekani kuanza kuondoka kutoka miji ya Iraq.
Kufuatia mlipuko huo, sasa kuna wasiwasi kuhusiana na suala la usalama nchini Iraq, kwani inaelekea visa vya ghasia vinaendelea kuzidi.
Maafisa wa polisi wameelezea kwamba gari ambalo lilikuwa na bomu hilo lilikuwa limeegeshwa katika mji wa Bathaa, katika jimbo la Dhiqa, kilomita 320 kusini-mashariki mwa mji wa Baghdad.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment