KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Wednesday, June 10, 2009
Maharamia wateka meli ya Marekani
Meli ya kampuni ya Maersk.
Taarifa zinaeleza kuwa meli sita zimetekwa nyara katika siku za karibuni na maharamia wa kisomali.
Maharamia wa kisomali wameteka meli moja iliyokuwa imebeba chakula cha msaada ikiwa na mabaharia wa kimarekani wapatao 20 ndani yake. Duru zimeeleza kuwa maharamia hao walichukuwa udhibiti wa meli hiyo iliyokuwa ikisafiri kupitia bahari ya Hindi.
Meli hiyo ya kubebea makontena yenye jina Maersk Alabama, inayoendeshwa na kampuni ya Marekani, ilitekwa katika bahari ya Hindi takriban kilometa 645 mashariki mwa mji mkuu, Mogadishu.
Wafanyakazi katika meli hiyo inayomilikiwa na kampuni ya Denmark, inaaminika wako salama, kwa mujibu wa shirika la kusimamia usalama wa usafiri wa majini.
Hiyo ni meli ni ya sita kuteka katika siku za karibuni, nyingine ni kutoka Uingereza na Taiwan. Taarifa zinaeleza kuwa meli hiyo yenye uwezo wa kubeba tani 17,000 ilikuwa imebeba chakula cha msaada kinachopelekwa Somalia na Uganda.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment