KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, July 6, 2011

Wahamiaji 197 wazama Sudan



Takriban watu 200 wamefariki dunia katika bahari ya sham wakati boti lilokuwa limebeba wahamiaji haramu kuelekea Saudia Arabia lilipozama katika pwani ya Sudan, shirika la habari la Sudan linasema.


Bahari ya Sham
Kituo cha habari cha Sudan,kinachofahamika kuwa na uhusiano wa karibu na serikali ya nchi hio,kinasema kuwa watu watatu pekee walinusurika.

Boti liliwaka moto,na ndani kulikuwa na watu waliokuwa wanataka kuingia Saudi Arabia kutumia njia haramu, shirika hilo lilisema katika taarifa yake.

Wanasema wahamiaji hao walikuwa wanatoka nchi zinazopakana na Sudan. Haijafahamika pale walipoanzia safari yao.

Mwandishi wa BBC mjini Khartoum James Copnal anasema bahari ya sham ni njia inayofahamika kupitisha wahamiaji haramu wanaokwenda Saudi Arabia na Yemen.











Savic Beki wa pili baada ya Clichy



Klabu ya Manchester city imekamilisha usajili wa beki mwingine Stefan Savic kutoka klabu ya Partizan Belgrade.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 ni beki wa pili kusajiliwa na Man.city baada ya Gael Clichy kutoka Arsenal.

Ikumbukwe kuwa Savic aliwahi kufanya majaribio ya siku kumi kwenye klabu ya Arsenal mwaka jana na badala ya kutia saini na klabu hiyo amesahihisha mkataba wa miaka minne na klabu ya kaskazini mwa England.

Kijana huyo alishiriki mchuano wa Timu yake ya Taifa ya Montenegro katika mchuano dhidi ya England kwenye uwanja wa Wembley mnamo mwezi Oktoba mwaka 2010 katika mechi ya kufuzu kushiriki fainali za Euro 2012.

Vilevile aliwahi kushiriki michuano iliyoshirikisha vilabu vya Ligi ya Premier akiwa na klabu yake ya Partizan ilipochuana na Arsenal katika Ligi ya mabingwa barani Ulaya mwezi Disemba.











Mshukiwa wa ugaidi apelekwa Marekani





Wapiganaji
Raia mmoja wa kisomali amefikishwa mahakama ya kiraia mjini New York, akishtakiwa kushirikiana na al-Qaeda na wapiganaji kutoka kundi la kisomali la al-Shabab.

Ilionekana kuwa Ahmed Abdulkadir Warsame alishikiliwa kwenye meli ya kivita ya Marekani kwa miezi miwili baada ya kukamatwa kwenye ghuba ya Aden.

Maafisa walisema Bw Warsame hakusomewa haki zake za kisheria alipokuwa kizuizini.

Bw Warsame, aliyekana mashtaka, ni mshukiwa wa kwanza kutoka nchi ya kigeni kushtakiwa kwa kosa la ugaidi kupelekwa Marekani ili kesi yake isikilizwe.

Awali washukiwa walikuwa wakipelekwa Guanatanamo Bay huko Cuba, lakini Rais Barack Obama ameahidi kufunga gereza hilo lenye utata.

Mwandishi wa BBC Tom Burridge mjini Washington alisema kesi hiyo ni ishara ya namna ambavyo Bw Obama anadhamiria kuwashughulikia washukiwa walioondolewa Guantanamo.










Gervinho afanya majaribio Gunners




Hatimaye klabu ya Arsenal imefikia tamati ya usajili wa mshambuliaji mpya baada ya mda wa maandishi mengi magazetini, sasa baada ya kukamilisha utaratibu wa kuchunguza afya yake na kufikia makubaliano baina ya klabu yake na Arsenal kwa kitita cha pauni za Uingereza milioni £11.2 Arsenal itamtangaza rasmi Gervinho kuwa mchezaji wake .


Gervais Yao Kuasi


Mchezaji huyo kutoka Ivory Coast atatangazwa kesho baada ya mwezi mzima wa mvutano na mabingwa wa Ufaransa Lille waliobadili msimamo na kutaka waongezewe kitita lakini sasa inasemekana kuwa atajiunga na kikosi tayari kwa ziara ya bara Asia wiki kesho.

Katika juma ambapo mmoja wa wachezaji waliotia fora msimu wa mwaka 2004 amehama, kukiwa na tetesi kuwa Samir Nasri na Cesc Fabregas watamfuata Gael Clichy, kuna habari njema kwa mashabiki wa Arsenal kuwa mmoja wa washambuliaji mahiri katika Ligi za Ulaya anajiunga na klabu yao.

Akizungumza wiki iliyopita, Gervinho alisema kuwa ''Najiunga na Arsenal kwa sababu ni kikosi cha vijana wadogo na nitaweza kushirikiana nao kwa urahisi. Na kuna uwezekano mkubwa wa kipaji changu kukuwa zaidi.

Kivutio kikuu kwa Gervinho kujiunga na Arsenal ilikuwa kushiriki michuano ya Ligi barani Ulaya na hilo siwezi kulikosa nikiwa na Arsenal, alisema Gervinho ambaye jina la kuzaliwa ni ''Gervais Yao Kuasi''.

Gervinho ni mchezaji wa pili kusajiliwa na Arsenal baada ya Carl Jenkinson kutoka klabu ya daraja la chini Charlton na vilevile Timu ya Taifa ya vijana wenye umri ulio chini ya miaka 19 ya Finland.






Kocha Arsene Wenger


Meneja Arsene Wenger anatazamiwa kuwaondoa baadhi ya wachezaji wake wa ziada kama Denilson na Nicklas Bendtner kabla ya msimu mpya.

Habari zilizothibitishwa mapema leo ni kwamba Arsenal imemkosa mcheza kiungo kutoka Argentina, Ricky Alvarez baada ya Inter Milan kukubali kulipa kitita sawa na pauni milioni £10.6 ambazo klabu yake ya Velez Sarsfield ilitaka.

Akijiandalia uwezekano wa kuwapoteza Nasri na Fabregas, Wenger anatarajiwa kusajili ma-beki wa hapa hapa Uingereza ikiwa jicho lake linatizama huko Birmingham kumsajili Scott Dann na huko Bolton kuna tetesi kuhusu Gary Cahill.

Halikadhalika kufuatia habari za kumkosa kiungo Alvarez, Wenger ametegea mchezaji mwingine Thiago Motta kutoka Inter Milan, Kocha huyo anahisi kwamba kuwasili kwa Alvarez huko Inter kutamkosesha raha Motta na huenda akavutiwa na mwito wa kujiunga na Arsenal.

Wakati huo huo, klabu ya Arsenal imesema haitotikiswa na hizo pauni milioni 25 kumuuza mcheza kiungo wake Samir Nassir, hilo likiwa jibu la Arsene Wenger kwa wakuu wa Manchester city waliokuja na pauni milioni 19 kwanza kabla ya Chelsea kutishia kitita kikubwa zaidi ya hicho na Manchester united kutangaza kuwa inamtaka kiungo huyo.











Ukosefu wa chakula Somalia ‘hauelezeki’





Watoto katika kambi ya wakimbizi Daadab, Kenya



Viwango cha utapiamlo kwa watoto wanaokimbia ukame Somalia kinaweza kusababisha ‘janga la kibinadamu ambalo haliwezi kufikirika’ , Mkuu wa shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema.

Watoto wadogo wanakufa njiani au wakti wamefika tu kwenye kambi Ethiopia na Kenya , UNHCR linasema.

Inakadiriwa kuwa robo ya Wasomali ama wamepoteza makazi yao ndani ya nchi au wanaishi nje kama wakimbizi.

Ukame mkali kutokea katika kipindi cha miaka 60 umechangia na pia vita ndani ya Somalia.

"Hailezeki, imepita kiasi," alisema msemaji wa UNHCR katika kitengo cha misaada Melissa Fleming. "wtu wetu wanasema hawajawahi kuona kitu kama kile."

Onyo hilo limekuja wakati mashirika ya misaada ya Uingereza Oxfam, Save the Children, na Msalaba Mwekundu yameanzisha kampeni ya maalum ili kushughulikia janga la njaa ambalo linawaathiri zaidi ya watu milioni 12 katika pembe ya Afrika.

Mashirika hayo kwa ujumla wake yanaomba karibu $150m (£93milioni).

UNHCR linasema mahitaji ya chakula, malazi, huduma za afya na misaada mingine muhimu ya kibinadamu ya dharura na kwa wingi.

Shirika hilo linasema zaidi ya asilimia 50 ya wtoto wa Kisomali wanaoingia Ethiopia wana hali mbaya kiafya kutokana na utapiamlo. Nchini Kenya idadi hiyo sawa na asilimia kati ya 30 na 40.

"Janga kubwa tunalolishuhudia, ni kuwa kuna watoto wanaowasili katika hali dhaifu sana, licha ya huduma ya dharura tunayowapa na matibabu ya chakula cha dharura, wanakufa ndani ya saa 24" Bi Fleming aliwaambia waandishi wa habari mjini Geneva.

"Tunakadiria kuwa robo ya Wasomali 7.5 milioni sasa ama wamepoteza makazi yao ndani yan nchi au wanaishi nje kama wakimbizi," alisema.

UNHCR hivi karibuni lilifungua kambi ya tatu Kusini Mashariki mwa Ethiopia mbayo inafikia uwezo wake wa kuchukua watu 20,000 unafikiwa kwa haraka na sasa ina mpango wa kuongeza kambi zingine.

Ndege ya misaada ya shirika la UNHCR ilielekea Addis Ababa Jumanne na ujumbe wa malori 20 yakiwa yamebeba mahema na misaada mingine ulielekea huko.

Kaskazini Mashariki nchini Kenya, kambi ya Daadab, kiasi cha wakimbizi 1,400 wanaingia kila siku. Mashrika ya misaada yana hofu kuwa idadi inaweza kupanda mpaka nusu milioni.

Badu Katelo, Kamishna wa Mausala ya Wakimbizi Kenya alisema ugawaji wa chakula na maji malzi na mahali, vyote vimewazidi uwezo na haliya usalama inazidi kuwa mbaya.

"Tungependa kuona jumuiya ya kimataifa inachangamka na kujitolea kuingilia kati ," alisema.

Mwansdishi wa BBC Ben Brown aliyeko katika kambi ya Daadab anasema vifo vya watoto wadogo vimepanda mara tatu zaidi huku watoto wengi walio chini ya umri wa miaka mitano wanakufa pindi wakifika tu au siku chahce baada ya kufika

Familia zinatembea siku nyingi bila chakula au maji kufika kambini, ansema mwandishi wa BBC, baadhi wakisema wanaibiwa njiani na kubakwa wakiwa njiani au kuvamiwa na wanyama.











Fifa yajipanga kusikiliza kesi ya Hammam



Kamati ya Fifa ya maadili itakutana tarehe 22 na 23 mwezi huu wa Julai kusikiliza shauri dhidi ya Mohamed bin Hammam, ambaye amesimamishwa kutokana na tuhuma za rushwa.



Mohamed Bin Hammam


Anakabiliwa na tuhuma za rushwa, ikiwemo madai kwamba "alinunua" kura za kuandaa Kombe la dunia mwaka 2022 kwa Qatar, madai ambayo amekanusha.

Uchunguzi umekamilika na ripoti imepelekwa kwa Bin Hammam ambaye ni rais aliyesimamishwa wa Shirikisho la Sola la Asia.

Maafisa wa Umoja wa Soka wa nchi za Carrebean (CFU) Debbie Minguell na Jason Sylvester pia shauri lao litasikilizwa siku hiyo.

Minguell na Sylvester walisimamishwa pamoja na makamu wa Rais wa Fifa Jack Warner, ambaye hachunguzwi tena baada ya kuamua kujiuzulu shughuli zote za soka.

Mashtaka yanahusu mkutano wa vyama 25 vilivyo chini ya CFU mwezi wa Mei, ambapo inatuhumiwa rushwa ya dola 40,000 zililipwa na kwa kila mjumbe ambapo Bin Hammam wakati huo alikuwa katika kampeni za kuwania urais wa Fifa.

"Kamati ya maadili ya Fifa itakutana tarehe 22 na 23 mwezi wa Julai kusikiliza shauri la Mohamed bin Hammam, Debbie Minguell na Jason Sylvester, ambao awali walisimamishwa na kamati hiyo tarehe 29 mwezi wa Mei 2011, wakituhumiwa kukiuka maadili ya Fifa na kanuni za nidhamu za Fifa," taarifa ya Fifa ilieleza.









Libya: 11 wauawa Misrata



Takriban watu 11 wameuawa katika mapigano karibu na mji wa Misrata, waasi wanaokabiliana na majeshi ya Muammar Gaddafi wanasema.





Majengo yalivyoharibiwa Misrata

Waandishi wa habari mjini Misrata wanasema ngome za waasi magharibi mwa Misrata, katika eneo la Dafniya,zimeshambuliwa na wanajeshi wa Kanali Gaddafi.

Wakati huo huo,makamanda wa waasi wameiambia BBC kuwa wameunganisha wanajeshi wao wa upande wa kusini na magharibi mwa Misrata.

Waasi wanasema wanajaribu kutoka Misrata na kuelekea Tripoli sasa.

Tangu maandamano dhidi ya serikali kugeuka na kuwa vita vya kijeshi zaidi ya miezi minne iliopita,pande zote mbili zimekwama, licha ya harakati zinazoongozwa na majeshi ya angani ya Nato kusaidia waasi.








Waasi wanapigana na wanajeshi wa Serikali Misrata

Waasi wanadhibiti eneo la mashariki mwa Libya,pamoja na Misrata na miji mingine katika milima ya Nafusa karibu na mpaka wa Tunisia.


Mwandishi wa BBC Gabriel Gatehouse aliyeko mjini Misrata anasema mapigano ya hivi karibuni yalianza mapema siku ya Jumanne,huku milio ya risasi na mabomu yakiendelea kusikika hadi mchana.

Taarifa za mashirika ya habari zinasema kuwa ngome za waasi katika eneo la Dafniya zilishambuliwa wakati majeshi ya serikali yalipojaribu kusonga mbele.

Mfanyakazi wa hospitali moja mjini Misrata amewaambia waandishi wa shirika la habari la Reuters kuwa wapiganaji 11 wa waasi waliuawa na wengine zaidi ya kumi kujeruhiwa na mpiganaji mmoja wa waasi akawaambia waandishi wa shirika la habari la AFP kuwa watu 11 "wote wakiwa raia" wameuawa.











Liverpool yamkosa Downing wa Aston Villa





Dau walilotoa Liverpool la paundi milioni 15 kwa ajili ya kumchukua Stewart Downing limekataliwa na Aston Villa.

Stewart Downging


Inaaminika Villa wanashikilia walipwe paundi milioni 20 ili wamuachie winga huyo mwenye umri wa miaka 26.

Downing, aliyetokea Middlesbrough mwaka 2009 kwa kitita cha paundi milioni 12, mazungumzo yake ya mkataba yamekwama na meneja Alex McLeish inaonekana yupo tayari kumuachia aondoke.

Mchezaji huyo pia amehusishwa pia kujiunga na klabu ya Arsenal, lakini Liverpool wanaonekana ndio watafanikiwa kumsajili.

Bosi wa Liverpool Kenny Dalglish nia yake kubwa ni kuimarisha kikosi chake kufuatia timu hiyo kushika nafasi ya sita msimu uliopita wa Ligi Kuu ya Soka ya England na tayari amefanikiwa kumchukua kiungo wa Sunderland Jordan Henderson.

Dalglish kwa sasa dira yake ameielekeza kwa Downing, ambaye anaonekana ataongeza kasi na muelekeo kwa Liverpool ambayo ilionekana kukosa ubunifu na mbinu msimu uliopita.

Downing huenda anaamini kwenda kwake Anfield kutamsaidia pia kuwa miongoni mwa wachezaji wa kwanza wa kikosi cha kawaida cha timu ya taifa ya England - lengo ambalo aliliweka hivi karibuni.

Licha ya kucheza mech 27 za timu yake ya taifa, Downing hivi karibuni alikiri: "Ninajiimarisha upya katika nafasi yangu kimataifa. Nimekuwa nikiitwa na kuondolewa katika kikosi cha timu ya taifa tangu nilipoanza kuichezea mara ya kwanza."

Pia aliesema msimu uliopita alipokuwa na Villa ulikuwa si wa kupendeza, walimaliza nafasi ya tisa na ingawa Villa wanaye meneja mpya McLeish, klabu hiyo inaingia katika kupindi cha mpito.

Mashabiki wengi wa Villa walipinga kuingia kwa meneja McLeish aliyetokea Birmingham na iwapo Downing ataondoka Villa Park, kufuatia kuhama kwa Ashley Young aliyejiunga na Manchester United, huenda hali ikawa si shwari.












Strauss-Kahn anakabiliwa na shutuma zingine






Dominique Strauss-Kahn
Mwandishi mmoja raia wa Ufaransa ambaye anadai alishambuliwa na aliyekuwa mkurugenzi wa shirika la fedha duniani, Dominique Strauss-Kahn, miaka tisa iliopita anajiandaa kuwasilisha kesi dhidi yake.Wakili wa mwandishi huyo,Tristane Banon, amesema atawasilisha madai ya kujaribu kubaka dhidi ya Strauss-Kahn.

Saa kadhaa baada ya mwandishi huyo kutangaza azimio lake,Bwana Strauss Kahn alimuagiza wakili wake kumshtaki kwa kile alichokitaja kama kuanzisha madai ya uongo.

Ijumaa iliopita,Bwana Strauss-Kahn aliondolewa masharti aliyokuwa amewekewa baada ya kutoa dhamana huko New York. Hii ni baada ya mwendesha mashtaka katika kesi hiyo kukiri kwamba ana wasiwasi kuhusu uaminifu wa mwanamke mmoja anayedai kuwa Strauss-Kahn alijaribu kumbaka.Amekana madai hayo.

Bado kesi inaendelea,lakini kuna matumaini nchini Ufaransa kuwa kesi hio huenda ikatupiliwa mbali.

Mwezi Mei,mwandishi huyo alisema kwamba kufuatia kesi iliyowasilishwa dhidi ya Bwana Strauss-Kahn huko New York na mfanyakazi wa hoteli moja, hatimaye pia yeye angeweza kuwasilisha kesi pia.


Mwandishi huyo hakutoa taarifa kwa polisi lakini alizungumzia tukio hilo katika kipindi cha mjadala mwaka wa 2007,ingawa jina la Bwana Strauss-Kahn liliondolewa.

Alidai kwamba Bwana Strauss-Kahn alimshambulia wakati alipoenda kumhoji akiwa na umri wa miaka ishirini na miwili na kwamba walikabiliana vikali katika nyumba ya Strauss-Kahn,wakati alipojaribu kumfungua sidiria.

Wakili wake, David Koubbi,alisema siku ya Jumatatu kwamba mashtaka rasmi dhidi ya Bwana Strauss-Kahn yatawasilishwa siku ya Jumanne.

"Haya ni madai yenye uzito mkubwa," Bwana Koubbi alisema alipotangaza azimio la mteja wake nchini Ufaransa.


Alisema kulingana na madai hayo, tukio hilo lilifanyika mwezi wa Februari 2003,wala si 2002 kama ilivyokuwa imeripotiwa.











Fifa kutoka adhabu kali asema Blatter




Rais wa shirikisho la mchezo wa soka duniani Fifa Sepp Blatter, amesema mtu yeyote atakayepatikana na kosa katika kashfa ya kupanga matokeo ya mechi za timu ya taifa ya Zimbabwe atapigwa marufuku ya kutoshiriki katika shughuli zozote za soka maishani mwake.



Rais wa FIFA Sepp Blatter


Wachezaji wa timu ya taifa akiwemo naodha wa timu hiyo, Method Mwanjali waliiambia tume iliyoundwa na shirikisho la mchezo wa soka nchini Zimbabwe, Zifa kuwa walilipwa ili kupoteza mechi zao wakati wa ziara yao barani Asia mwaka wa 2009.

Maafisa wa tume ya kupambana na ufsadi wa Fifa wanatarajiwa kuzuru Zimbabwe hivi karibuni ili kushauriana na maafisa wa Zifa na polisi kabla ya kukamilishi uchunguzi wao kuhusiana na kashfa hiyo.

Blatter aliyasema hayo wakati wa ziara yake fupi nchini Zimbabwe, kutoka kwa mkutano wa Kamati ya kimataifa ya michezo ya olimpiki IOC uliofanyika mjini Durban Afrika Kusini.






Fifa kutoa adhabu kali zaidi

"Hatuwezi kuingilia kati suala hili kwa haraka, ni lazima tupate idhini kutoka kwa mataifa husika na wakati watu watapatikana na hatia, sisi tutawapiga marufuku ya maisha" alisema Blatter.



Mchezaji wa timu ta Taifa ya Zimbabwe Knoledge Musona
"Hatutawaruhusu tena watu hao kujihusisha na usimamizi wa mchezo wa soka, ikiwa wao ni maafisa wa Zifa au wachezaji, wataadhibiwa vikali na kwa mujibu wa sheria" aliongeza Blatter.

Ushahidi uliotolewa na wachezaji kwa tume hiyo iliyoundwa na Zifa, unadai kuwa maafisa wa Zifa walishirikiana na raia mmoja wa Singapore, Raj Perumal, kuwahonga wachezaji hao ili wapoteze mechi zao dhidi ya Syria na Thailand.

Uchunguzi wa pili uliangazia ziara za awali za timu hiyo ya taifa ya Zimbabwe barani Asia, ambako pia walipoteza mechi zao dhidi ya mataifa yanayoorodheshwa ya chini zaidi katika msimamo wa nchi bora duniani.












Ben Ali akutwa na hatia





Bw Ben Ali na mkewe


Rais aliyeondolewa Tunisia Zine al-Abidine Ben Ali amekutwa na hatia kwa makosa ya kuhodhi silaha na dawa za kulevya kinyume cha sheria baada ya kesi yake kusikilizwa kwa siku moja mjini Tunis.

Alihukumiwa kifungo cha miaka 15 jela, licha ya kutokuwepo mahakamani.

Mwezi uliopita Ben Ali na mkewe Leila walihukumiwa kifungo cha miaka 35 jela kwa ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za serikali.

Alikimbilia Saudi Arabia mwezi Januari kufuatia wiki kadhaa za maaandamano- kiongozi wa kwanza kutolewa katika " Ghasia za nchi za kiarabu".

Mpaka sasa Saudi Arabia imeshindwa kumsafirisha Ben Ali, licha ya kuombwa na serikali ya mpito ya Tunisia.

Huko mahakamani, wakili wake, Hosni Beji, alielezea mashtaka ya dawa za kulevya na kuhodhi silaha kama "isiyo na mantiki".









Nataka kuihama Man City-Tevez





Mshambulizi Carlos Tevez anasema anataka kuondoka Manchester City kutokana na sababu za kifamilia.


Carols Tevez akisherekea bao alilofunga


Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Argentina amesaidia Manchester City kumaliza katika nafasi ya tatu msimu uliopita kwenye ligi kuu ya England na kuweza kufuzu kwa ligi ya klabu bingwa barani Ulaya kwa mara ya kwanza.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27,alijiunga na City kutoka kwa wapinzani wao wa mji wa Manchester United mwaka 2009, amesema hawezi kuendelea kuishi kaskazini magharibi,bila binti zake wawili.

Kwa nini ataka kuondoka?

" Nahitaji kuwa karibu nao na kuwa na muda nao," Tevez alisema katika taarifa.

" Kuishi bila watoto wangu Manchester imekuwa changamoto kubwa kwangu.Kila ninachofanya,nafanya kwa ajili ya binti zangu.


Carols Tevez akichezea timu yake ya taifa ya Argentina
" Nataka wawe na furaha kwa kuwa maisha yangu ni kwa ajili yao sasa. Nahitaji kuwa mahali ambapo wao wanaweza kuishi vizuri.

" Natumai kuwa watu wanaelewa mazingira haya magumu ambayo nimekuwa katika miezi 12 iliopita,hasa ukizingatia familia yangu."

Tevez, ambaye alitia saini kandarasi ya miaka mitano na Manchester City kwa kiasi cha pauni za Uingereza milioni £25.5m kutoka Old Trafford,alishukuru uongozi wa timu ya City kwa ushirikiano wao na kuomba mashabiki waelewe masuala yake binafsi kwa sasa.












Urusi na Nato waijadili Libya






Bw Sergei Lavrov akisalimiana na Bw Fogh Rasmussen



Urusi na majeshi ya umoja wa nchi za kujihami za Ulaya Nato wanakutana kwa mazungumzo katika hoteli ya Sochi kusini mwa nchi hiyo, huku kipaumbele kikiwa ni mgogoro wa Libya.

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov alisema Urusi ilitaka kutumia baraza hilo kama "kichocheo cha ushirikiano".

Rais Dmitry Medvedev atakutana na mkuu wa Nato Anders Fogh Rasmussen.

Urusi imekuwa ikikosoa harakati za Nato nchini Libya, huku ikiyapa mazungumzo haya umuhimu wa kipekee.

Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma naye atahudhuria, huku akiendelea kuongoza jitihada za upatanishi baina ya waasi na serikali mjini Tripoli baada ya waasi kukataa juhudi zilizofanywa na Umoja wa Afrika siku ya Jumapili.

Afrika kusini imekuwa mstari wa mbele katika jitihada za kufanya mazungumzo, na Rais Zuma anatarajiwa kukutana na Bw Medvedev, na huenda pia Bw Fogh Rasmussen, katika mkutano huo.

Matumizi ya makombora kama njia ya kujilinda nayo itajadiliwa kwenye mazungumzo hayo.










Rais wa Venezuela ahutubia taifa





Rais Hugo Chavez akiwahutubia wafuasi wake


Rais wa Venezuela Hugo Chavez amehutubia maelfu ya watu mjini Caracas baada ya matibabu nchini Cuba.

Wafuasi wa rais Hugo Chavez walimshabikia wakati alipowaonyesha bendera ya Venezuela kutoka kwa roshani ya kasri yake na kusema kuwa afya yake itaimarika. Rais Chavez amewahutubia maelfu ya wafuasi mjini Caracas baada ya kupata matibabu ya saratani nchini Cuba.

Bwana Chavez,mwenye umri wa 56,amekuwa nchini Cuba tangu Juni 8,alikofanyiwa upasuaji kuondoa uvimbe uliokuwa na saratani.

Nimerudi!

Alisema kuwa hatoweza kushiriki katika sherehe za kuadhimisha miaka 200 ya uhuru wa Venezuela kutoka kwa Uhispania siku ya Jumanne.

Lakini atafuatilia sherehe hizo akiwa kwenye kasri ya rais,alisema.

Akiwa amevaa magwanda yake ya kijeshi na kofia nyekundu,Bwana Chavez kwanza aliongoza umati huo kuimba wimbo wa taifa wa Venezuela.

" Nimerudi," alisema,akishukuru wale wanaomuunga mkono. " Hii ndiyo dawa bora kwa ugonjwa wowote ule."

Hakuna tena uvumi.

Chavez haondoki!


Akisimama bila kusaidiwa,Bwana Chavez alizungumza kwa muda wa dakika 30 bila kuangalia popote.

Maelfu ya wafuasi waliokuwa wamevaa mavazi mekundu,walisema: "Hapana! Chavez haondoki!"

Awali,Bwana Chavez alisema amekuwa "na wakati mgumu" nchini Cuba lakini kwamba sasa anaendelea kupata nafuu.

Bwana Chavez, ambaye ameongoza Venezuela kwa miaka 12 na hata kunusurika jaribio la mapinduzi mwaka 2002,aliambia Televisheni ya taifa kuwa ana utaratibu kamili wa matibabu "anatumia dawa,anatakiwa kupumzika,na kula vyakula maalum".

Kumekuwa na uvumi kuhusu hali ya afya ya Bwana Chavez baada ya kuondoka Venezuela zaidi ya wiki tatu zilizopita kwa kile maafisa walisema ni kufanyiwa upasuaji.







Nataka kuihama Man City-Tevez





Carlos Tevez na wanawe wa kike.

Mshambulizi Carlos Tevez anasema anataka kuondoka Manchester City kutokana na sababu za kifamilia.

Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Argentina amesaidia Manchester City kumaliza katika nafasi ya tatu msimu uliopita kwenye ligi kuu ya England na kuweza kufuzu kwa ligi ya klabu bingwa barani Ulaya kwa mara ya kwanza.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27,alijiunga na City kutoka kwa wapinzani wao wa mji wa Manchester United mwaka 2009, amesema hawezi kuendelea kuishi kaskazini magharibi,bila binti zake wawili.

" Nahitaji kuwa karibu nao na kuwa na muda nao," Tevez alisema katika taarifa.







Carlos Tevez akifanya vitu vyake uwanjani





" Nataka wawe na furaha kwa kuwa maisha yangu ni kwa ajili yao sasa. Nahitaji kuwa mahali ambapo wao wanaweza kuishi vizuri.

Kuishi bila watoto wangu Manchester imekuwa changamoto kubwa kwangu.Kila ninachofanya, nafanya kwa ajili ya binti zangu.
Carlos Tevez
" Natumai kuwa watu wanaelewa mazingira haya magumu ambayo nimekuwa katika miezi 12 iliopita,hasa ukizingatia familia yangu."

Tevez, ambaye alitia saini kandarasi ya miaka mitano na Manchester City kwa kiasi cha pauni za Uingereza milioni £25.5m kutoka Old Trafford,alishukuru uongozi wa timu ya City kwa ushirikiano wao na kuomba mashabiki waelewe masuala yake binafsi kwa sasa.








Yanga yatinga robo fainali



Timu ya Yanga ya Tanzania leo hii imejihakikishia kucheza hatua ya robo fainali ya Michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kagame Cup, baada ya kuisambaratisha timu ya Bunamwaya ya Uganda kwa jumla ya magoli 3 - 2 katika mchezo wa kundi B uliochezwa katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam Tanzania.



Young Africans




Yanga imeingia robo fainali baada kufikisha pointi 7 huku ikifuatiwa na Bunamwaya yenye pointi 6 pamoja na kukubali kipigo hicho nayo inaingia robo fainali ya mashindano hayo.

Al Mereikh yaitwanga Elman
Katika mchezo mwingine uliochezwa katika uwanja huo huo wa Taifa Dar es Salaam Al Mereikh ya Sudan imesambaratisha Elman ya Sudan kwa jumla ya magoli 3 - 0. Japo Al Mereikh imeshinda mechi ya leo lakini itabidi kusubiri hadi mwisho ili kujua kama inaweza kupendekezwa kucheza hatua ya robo fainali kama matokeo yake yatakuwa ni mazuri kuliko timu nyingine zilizokosa kuingia hatua ya robo fainali.

St.George yaichukiza Port
Nako katika uwanja wa Jamuhuri uliopo mkoani Morogoro timu ya St. George ya Ethiopia leo imeinyeshea mvua ya magoli timu Port ya Djibout kwa kuitandika bila huruma magoli 7 - 0 katika mechi ya kundi C na hivyo kuingia moja kwa moja hatua ya Robo fainali ya mashindano ya CECAFA, Kagame Cup.

Ulinzi
Mbali na St.George timu nyingine iliyojihakikishia kuingia hatua ya robo fainali kutoka kundi C ni Ulinzi ya Kenya ambayo leo imecheza na APR na matokeo yalikuwa sare ya 0-0.

Simba kutafuna Red Sea
Siku ya Jumapili kuna mechi mbili za kundi A kumalizia hatua ya makundi ambapo Simba ya Tanzania itacheza na Red Sea ya Eritrea na mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Zanzibar Ocean View na Vital'o ya Burundi.








‘White House’ ya Sudan-Jumba la Kutisha



Jumba la 'white house' kumbukumbu ya mateso Sudan Kusini

Ngazi zilizo wima zinateremka kuelekea chini na katika giza totoro, hewa ni nzito, ina kama moshi hivi na kuna joto katika eneo hili ambalo punde itakuwa Sudan Kusini iliyoo huru.

Kuna pingu zinaning’inia kwenye mhimili wa chuma kwenye dari nyeusi. Kumbukumbu ya ukatili na mateso yaliyowahi kutokea hapa.

Kwa Sudan Kusini, ambyo tayari inajitahidi kumaliza ghasia, eneo hili linatoa onyo kali kwamba siku za usoni hazitakiwi kuwa kama zilizopita.

"Ni Taifa litakalokuwa jumuishi?" aliuliza Jok Madut Jok, Profesa wa taaluma na historia katika Chuo Kikuu cha Loyola Marymount, California, alipozungumza katika mhadhara wa karibuni.

"Au litakuwa halina msimamo kama nchi nyingine zimetumbukia-kwamba unapata uhuru , halafu unaendelea kufanya yale yale uliyoyapinga?" alisema Bw Jok, ambaye pia ni afisa mwandamizi katika

Wizara ya Utamaduni.

Kwa mujibu wa Mwandishi wa BBC Peter Martell, kuna maeneo machache katika mji mkuu wa Sudani Kusini Juba ambayo yanaibua hofu kama jengo lijulikanalo kama "White House".

Wakati wa vita ya Sudan 1983-2005 lilipata umaarufu kama eneo kuu la Kusini la kutesea na kunyongea la serikali ya Khartoum, kwa wale iliyoamini kuwa ni vikosi vya waasi.

Kuta zenye grisi na masizi pamoja na maganda ya risasi yenye kutu yalitapakaa sakafuni.

Balbu yenye mwanga hafifu ikitoa mwanga mdogo kwenye kona za giza kwenye chumba hicho.

"Nina wasiwasi kama waandishi wengine wamewahi kufika hapa," afisa usalama wa serikali alisema kwa kunong’ona.

"Kama waliwahi, basi hawakutoka wakiwa hai," mwenzake aliitikia.

Inakadiriwa kuwa watu 1.5 milioni walikufa katika vita, mgogoro uliotokana na imani, ukabila, udini, maliasili na mafuta.

Waasi wa Sudan Kusini walipigana dhidi ya kile walichokiita kutengwa na kujilundikia madaraka kwa serikali iliyojaa wasomi ya Kaskazini.

'Kuongezeka kwa ukatili'

Sasa wapiganaji hao wamekuwa jeshi rasmi la Kusini, ambayo itakuwa Taifa lililojitenga Julai 9, likiigawa katika mataifa mawili nchi yenye eneo kubwa kuliko yote Afrika.



Wananchi Sudan Kusini kuelekea uhuru kamili
Lakini jengo kama ‘White House’ halibebi kumbukumbu mbaya za Sudan iliyopita iliyokuwa imejaa damu.

Watu wanasema wanatoa ujumbe wa siku zijazo. Kwamba utawala uliotumia mateso dhidi ya watu wake wenyewe katika Sudan iliyokuwa moja ni lazima iwe historia na kwa namna yoyote isibebwe katika Sudan Kusini mpya iliyojitenga.

"Eneo hilo lilikuwa ni jinamizi kwetu-ukisikia mtu amepelekwa huko, utakuwa tayari umeshaagana nao, hawakuwa wanarudi," alisema mwanafunzi wa chuo Mabil William.

“Ingefaa paitwe 'Red House' kwa sababu ya damu na sio “White House” alisema askari wa SPLA.

Baba yake hakuonekana tena baada ya kukamatwa vitani, inaaminika kuwa alikufa huko ‘White House’

"Tulipopiga kura kwa ajili ya kujitenga, kusema kwa heri kwa Khartoum, maeneo kama hayo tunayapungia mkono wa kwa heri."

Lakini wakati matumaini ya mabadiliko ni makubwa, changamoto ni nyingi.

Chama cha Kusini cha Sudan People's Liberation Army (SPLA) hakijawa na rekodi kamili.

Kuhama kutoka chama cha waasi na kuingia kuwa jeshi la kawaida kumezusha tuhuma za mauaji na ubakaji, kwa mujibu wa makundi ya kutetea haki za binadamu

"Taarifa za uporaji, unyanyasaji kwa raia na hata mauaji vimesababisha kuwa na wasiwasi mkubwa" sehemu ya taarifa ya pamoja ya makundi ya Kimataifa na ya Sudan kuhusu haki za binadamu ilisema.

Taarifa hiyo ilionya juu ya "kuongezeka kwa ukatili wa serikali" Kusini, huku pesa na mamlaka vikilundikwa Juba, na usalama ukichukua sehemu kubwa ya bajeti.

Chama cha SPLA kimekuwa kikipambana na takribani vikundi vya wapiganaji vipatavyo saba kwa mwaka. UN inasema pande zote mbili zilikuwa zikilenga raia.

Zaidi ya watu 1,800 wameuawa mwaka huu Sudan Kusini na wengine 264,000 kwa mujibu wa makisio ya UN.

Serikali ya Kusini imerejea kusisitiza kuwa inafanya kazi kwa manufaa ya siku za usoni, na inasema wakati makosa tayari yameshafanyika, mabadiliko kutoka vita vya msituni hadi serikali si kitu rahisi.

"Sudan Kusini itaheshimu haki za watu wote wanaoishi katika milki yake wawe wa kutoka mchanganyiko wa makabila , utamaduni, lugha dini na asili " ilisema taarifa rasmi ya serikali iliyotolewa sasa kabla ya kutangazwa uhuru ikiahidi kuzingatia tamko la Haki za msingi za Binadamu.




Uwanja wa Makaburi


Chumba cha mateso
Baada ya sherehe za furaha za uhuru kumalizika, kazi kubwa ya siku za usoni itakuwa ni kuhakikisha ahadi zinalinda haki kwa ujasiri, kuwa na vyombo vya habari na jamii iliyo tayari.

Vikosi vya kaskazini vimeacha chumba hicho cha ‘White House,’ lakini eneo la jirani bado ni kambi hai ya kijeshi kwa sasa ikiendeshwa SPLA.

Jengo halisi lililotoa jina gumu ni mwendo mfupi kutoka kwenye handaki: Wafungwa walikuwa wakiburutwa nje ya eneo hilo wakienda kunyongwa, alisema askari.

Jengo la kawaida, lililopakwa rangi nyeupe sasa linatumika kama duka na bweni

Meja Jenerali Marial Chanoung, kamanda anayesimamia kambi ya jeshi anasema hakuna anayeweza kueleza wasudani maelfu mangapi waliokufa hapa.

"Kulikuwa na mateso. Ni sehemu iliyojulikana kuua watu wengi,” alisema.

Karibu na jengo kuna kifusi cha majani ya kijani, alama ya fuvu jekundu na mifupa miwili ikionyesha kuna bomu ambalo halijalipuka.

Askari wanasema wakati wa kiangazi mifupa ilikuwa ikionekana nje ya kaburi la pamoja.

SUDAN: Ni nchi mbili sasa










Hofu ya vita wiki moja kabla Uhuru



Hata kabla ya Sudan ya kusini kutangaza kuwa Taifa huru wiki hii, tayari nchi hiyo inakabiliana na zaidi ya makundi sita ya wapiganaji walioasi.

Nguvu ya waasi


Kwenye picha ya video iliyo mikononi mwa BBC, mamiya ya wapiganaji kutoka kusini mwa Sudan wanaonekana wakifanya mazowezi ya kijeshi kwa kuimba na kujaribu silaha zao mpya.



Tabasamu za viongozi


Sura za tabasamu zinazojitokeza kwenye video hii ni kinyume kabisa na ukweli wa matayarisho ya vita vikali. Makundi haya ya waasi yamepigana mara kadhaa na jeshi la kusini, na ni tishio kubwa kwa utulivu wa Taifa hili changa.

Vishawishi vilivyosababisha waasi kuasi serikali yao ni vingi, lakini wengi wa viongozi wao waliwahi kuwa maofisa wakuu katika vikosi vya kusini,Sudan People's Liberation army(SPLA), au hata viongozi wa mgambo waliopambana na serikali ya Sudan kwa kipindi cha miaka 21 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, vilivyomalizika kwa amani ambayo imewezesha Uhuru wa sehemu ya kusini.

Peter Gadet wa SSLA

Mojapo ya makundi hayo ya waasi, lijulikanalo kama South Sudan Liberation Army(kifupi -SSLA) likiongozwa na Peter Gadet linadai kuwa linapiga vita rushwa, ukosefu wa maendeleo na umiliki wa nyadhifa unaofanywa na kabila la Dinka.

Makabila ya Dinka ndiyo kabila moja kubwa kuliko yote ya Sudan ya kusini, na linalaumiwa kwa kushikilia nyadhifa nyingi muhimu katika jeshi la kusini pamoja na serikalini.

Kiwango kikubwa cha fedha hutumika kwa gharama za jeshi ikiwa ni robo ya mapato ya Sudan ya kusini, vilevile ni sawa na mara tatu ya jumla ya fedha zinazotumiwa kwa huduma ya Afya na Elimu kwa pamoja.
Kwa kifupi, hii ni sehemu tu ya wasiwasi unaoikabili serikali mpya wa makundi ya waasi pamoja na maadui wa kale katika utawala wa Sudan ya kaskazini huko Khartoum.



Ushauri lipunguzwe nusu
Ingawaje pesa nyingi hutumiwa kwa mishahara ambapo afisa mmoja wa Umoja wa Mataifa aliyeko Sudan ya kusini, David Gressley alinena hivi karibuni akishauri kuwa bora jeshi lipunguzwe kwa nusu baada ya Uhuru.


Mkono wa kaskazini upo?

Wapiganaji wa kundi la SSLA wamepambana na SPLA mara kadhaa karibu na makao yao makuu katika Jimbo la Unity.



Rais al Bashir
Kwa mujibu wa SPLA, makundi yote yanafanana kwa kitu kimoja;Yote yanadhaminiwa na aliyekuwa adui yao wote aliye mjini Khartoum.

Video iliyotoa sura ya hali ya mambo ilivyo huko Kusini mwa Sudan ilikabidhiwa kwa BBC na kiongozi wa waasi ambaye wakati huo alikuwa mjini Khartoum.

Ikiwa kuna ukweli au hata kama hapana ukweli, serikali ya Sudan ya kusini inaonelea kila hatua ya njama inayofanywa na wakuu wa Khartoum na yote haya yakiashiria uhusiano mbovu baina yao.

Katika kipindi cha vita vya miongo miwili, eneo la kaskazini lilikuwa na tabia ya kuyapa silaha makundi yanayohasimiana ili kulilegeza jeshi la SPLA.

Riek Machar


Hata Makamu wa Rais wa Sudan ya kusini, Riek Machar wakati mmoja alijitenga kutoka SPLA.

Hata hivyo Chama cha NCP cha Rais Omar al-Bashir kinakanusha kuwa kinaunga mkono kizazi kipya cha makundi ya waasi.

"Peter Gadet na wengine kama yeye hawakuwa sehemu ya Chama cha Rais Bashir cha NCP wala jeshi la Sudan, alikuwa ni sehemu ya mgambo wa SPLA, walioasi kufuatia kuibia kura baada ya Uchaguzi mkuu wa Sudan ya kusini, kwa mujibu wa afisa wa Chama cha NCP Ibrahim Ghandour.

Habari zisizokuwa za kufurahisha ni kwamba waasi hao wanapanga kutumia silaha zao kabla au baada ya sherehe za Uhuru wa Sudan ya kusini.

No comments:

Post a Comment