KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, July 18, 2011

Misaada inapitia kwa al-Shabaab

Misaada inapitia kwa al-Shabaab







Mratibu wa shughuli za Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Mark Bowden, anasema msaada unatolewa katika baadhi ya makambi yaliyopewa idhini na kikundi cha wapiganaji wa Kiislamu, Al-Shabaab.
Wanawake wakisubiri msaada mtaa wa Shangani, Mogadishu

Bwana Bowden aliiambia BBC kwamba msaada unatolewa kwa kupitia kamati za Al-Shabaab, zinazohusika na ukame ambazo zinaendesha makambi hayo.

Bwana Bowden alisema ilibidi kufanya hivo, ingawa inajulikana kuwa Al-Shabaab ina uhusiano na Al-Qaeda, ikiwa msaada wenyewe unatolewa kufuatana na misingi ya utu, bila ya kuhusisha siasa.

Alisema ni lazima kuzidisha shughuli nchini Somalia katika miezi michache ijayo.











Jeshi la Nigeria linakosolewa







Gavana wa jimbo la Nigeria ambako kulitokea fujo karibuni, inayotokana na kikundi cha kiislamu cha Boko Haram -- amekiri kuwa jeshi lilitumia nguvu za kukithiri.
Usalama, Maiduguri, jimbo la Borno

Kashim Shettima, gavana wa jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria, aliiambia BBC kwamba wale ambao nyumba na magari yao yaliangamizwa, watalipwa fidia.

Piya aliwaambia watu waliohama maeneo yao, warudi nyumbani.

Mashirika ya haki za kibinaadamu yamelishutumu jeshi la Nigeria kwamba liliuwa watu kiholela, wakati wa kupambana na Boko Haram










Hammam apuuza wanaompeleleza




Shirikisho linalotawala mchezo wa Kandanda Duniani FIFA linasema kuwa Mwanachama wake Mohamed Bin Hammam amekataa kuzungumza na wakuu wake waliotumwa kupeleleza madai kuwa alijaribu kuwahonga wakuu wa vyama vya mpira vya kanda ya Caribbean.

Hammam amekataa kujadiliana na wapepelezaji

Bw.Hamam vilevile amekataa kutoa maelezo kuhusu akaunti zake za benki.

Taarifa iliyochapishwa na kundi lijulikanalo kama Freeh Group International, shirika huru la upelelezi linalomilikiwa na aliyekuwa mkuu wa FBI hapo zamani limehitimisha taarifa yake kwa kusema kuwa ''Hakuna ushahidi bayana unaomhusisha Bw.Hamam na jaribio la kutoa hongo moja kwa moja au malipo taslimu, kilichopo ni ushahidi wa dhana, kuwa raia huyo wa Qatari ndiye aliyetoa pesa hizo.


Bin Hammam

Mkuu huyo aliye kwenye Kamati ya utendaji ya FIFA akiwa pia Rais wa Shirikisho la mpira la bara Asia alisimamishwa na FIFA kuanzia tareh 29 May mwaka huu.

Ripoti ya Freeh iliyotolewa na wakili wa Bw.Hamam kwa vyombo vya habari imesema kuwa Bw.Hamam amekataa kuzungumza na wanaoendesha upelelezi huo ingawa amesema atakua tayari kuzungumza mbele Kamati ya maadili ya FIFA.

Mashirika saba kutoka kanda ya Caribbean yamewambia wapelelezi kuwa walipewa au walikubali zawadi za hadi dola za kimarekani 40,000 wakiwa kwenye chumba kimoja cha Hoteli ya Hyatt Regency mnamo tareh 10 mwezi May baada ya hotuba ya Bw.Hammam akijieleza katika kampeni za uchaguzi wa Rais wa FIFA.



Jack Warner

Jack Warner, Makamu wa Rais wa FIFA aliyetuhumiwa pamoja na Bw.Hammam na maofisa wengine wawili kutoka Kanda ya Caribbean, Debbie Minguell na Jason Sylvester.

Jack Warner hata hivyo, hatotakiwa kufika mbele ya Kamati ya maadili kutokana na kwamba FIFA ilimuondolea tuhuma zote baada ya uwamuzi wake wa kujiuzulu kutoka shughuli zote za FIFA.










Msaada unaingia Somalia








Waziri wa Misaada wa Uingereza, Andrew Mitchell, anasema msaada mpya wa Uingereza utalenga walioathirika na ukame, katika Pembe ya Afrika, wanawake na watoto nchini Somalia.
Mama amebeba mtoto anayetapia mlo

Bwana Mitchell alisema ni muhimu kuhakikisha kuwa watu hao hawalazimiki kufanya safari ndefu, kuvuka mipaka hadi Kenya na Ethiopia, ili kufika katika makambi ambayo yamejaa sana.


Juhudi za kuwasaidia watu walioathirika vibaya zaidi na ukame nchini Somalia, hadi sasa zimekuwa zikilenga makambi yalioko Ethiopia na Kenya.

Lakini sasa kunafanywa juhudi piya za kuwasaidia wale walionasa nchini Somalia kwenyewe, na kupeleka misaada Somalia sasa kunapewa kipa umbele.

Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, linakisia kuwa karibu Wasomali milioni moja na nusu waliohama makwao kwenda kutafuta chakula, wako ndani ya nchi.

Lakini imekuwa shida sana kuweza kuwasaidia.

Wapiganaji wa Kiisalmu, al-Shabaab, ambao wanadhibiti karibu eneo lote la kusini na kati la Somalia, ni hivi karibuni tu wameridhia mashirika ya misaada kuendesha shughuli zao humo.

Na Shirika la Chakula Duniani, WFP, sasa linachunguza njia za kuchukua fursa hiyo.

Mashirika mengine tayari yameanza shughuli.

Shirika la Watoto wa Umoja wa Mataifa, Unicef, limesafirisha chakula kukipeleka Baidoa, kaskazini magharibi ya mji mkuu, kwa mara ya kwanza kwa muda wa miaka kadha.

Nalo Shirika la Msalaba Mwekundu, linafungua vituo 10 vipya vya kuwapatia watu chakula, katika eneo la Afgoye, karibu na Mogadishu.

Shirika la Matibabu, MSF, linawalisha watoto kama elfu-tano kwenye makambi huko Jilib, kando ya Mto Juba.

Na al-Shabaab yenyewe inawapatia chakula watu kama elfu 4, katika eneo la kusini-magharibi ya Mogadishu.

Huu ni mwanzo tu - janga hilo litahitaji operesheni kubwa zaidi.

Lakini shughuli zote hizo zinaonesha kuwa angalau msaada sasa unaweza kufika kwenye maeneo yanayodhibitiwa na wapiganaji wa al-Shabaab, ambako kabla ya hapo, mashirika ya msaada yalikuwa yamepigwa marufuku na wapiganaji hao.












Charles N'Zogbia awindwa na Aston Villa



Klabu ya Aston Villa imepeleka maombi rasmi ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa pembeni wa Wigan Athletic Charles N'Zogbia.
Charles N'Zogbia akikata mbuga




Charles N'Zogbia akikata mbuga

Meneja mpya wa Aston Villa Alex McLeish anamuhitaji sana N'Zogbia ili azibe pengo litakaloachwa na Stewart Downing, ambaye yupo katika mazungumzo ya kujiunga na klabu ya Liverpool baada ya klabu hizo mbili kukubalia dau siku ya Jumanne.

Villa pia imo katika kujiimarisha baada ya mshambuliaji wake wa pembeni na wa kutegemewa Ashley Young kujiunga na Manchester United mapema msimu huu.

N'Zogbia, mwenye umri wa miaka 25, ameshacheza michezo soka ya England mara 250 akiwa na klabu ya Wigan pamoja na klabu yake ya zamani ya Newcastle.











Murdoch anaomba msamaha







Tajiri anayemiliki vyombo vya habari kadha duniani, Rupert Murdoch, ameomba msamaha kwa wananchi wa Uingereza, kwa makosa yaliyofanywa na gazeti lake moja, News of the World.
News Internationa inaomba msamahama

Gazeti hilo lilifanya udaku katika maelfu ya simu za mkononi za watu.

Msamaha huo umetolewa kama tangazo lilochapishwa kwenye magazeti kadha lenye kichwa cha maneno: "tunaomba msamaha", na ambalo limetiwa saini na Bwana Murdoch.

Anasema anaomba msamaha kwa makosa makubwa na kwa kuwaumiza watu walioathirika na udukuzi huo.

Mwandishi wa BBC anasema siyo mara nyingi kwa watu wakubwa duniani kuomba radhi hadharani.

Lakini tajiri huyo anayemiliki vyombo vya habari kadha, ilimbidi kufanya hivo, baada ya gazeti lake la Uingereza, lilokuwa likisomwa na watu wengi kabisa nchini, kugunduliwa kuwa likifanya udaku kwa kusikiliza ujumbe kwenye simu za maelfu ya watu.

Kati yao walikuwamo watu wa ukoo wa kifalme wa Uingereza, wachezaji sinema na waimbaji maarufu, na piya familia za wanajeshi waliouwawa vitani nchini Iraq na Afghanistan -- na hata simu ya msichana aliyeuliwa.

Katika barua yake Bwana Murdoch piya anasema kampuni yake ya News International, itachukua hatua zaidi kutatua maswala yaliyozuka kutokana na kashfa hiyo ya udukuzi kwenye simu.

Hapo jana, wakurugenzi wawili wa kampuni ya bwana Murdoch walijiuzulu.






Will Rupert Murdoch be locked out of British politics?



“In so many ways, a vote for the Lib Dems is a vote against Murdoch and the media elite.”

Amid all the media hysteria about the prospects and consequences of a hung parliament, possibly the most noteworthy contribution was David Yelland’s surprisingly thoughtful piece in Monday’s Guardian. Yelland speculates that an unexpected by-product of no one party achieving a parliamentary majority would be that Rupert Murdoch’s lengthy and malign influence over British politics may be dealt an unlikely blow.

This might explain the ludicrous tone of the General Election coverage in Monday’s edition of Murdoch’s Sun newspaper. The paper’s YouGov election poll (which put the Lib Dems in the lead on 33%) clearly demonstrated that The Sun’s six month propaganda campaign on behalf of the Conservatives has had precious little effect on its own readership. Undaunted, they went for the Lib Dem jugular. Page after page attempted to whip the reader into a frenzy of terror at the prospect of life under “loony” Lib Dem overlords. Scrapping the Trident replacement would inevitably lead to the humiliation of Brittania before the enemies of the Empire, the country would prostrate itself at the feet of the evil European socialist conspiracy, and (worst of all) the place would be bloody well crawling in immigrants.

I suppose Nick Clegg should be flattered. If (arguably) the world’s most powerful man has unleashed his principle attack dog on them, then the Lib Dems must be doing something right. Moreover, NewsCorp must fear something unwelcome around the corner if Clegg has a hand in the next government. As we know, Murdoch’s operation is only concerned with one thing: continued business success. In the case of his British media interests, this has always been inextricably linked with being on the right side of the people who regulate the industry. The Sun’s opportunistic switch last year from Labour to the Tories was a classic example of this: NewsCorp judged that Cameron was going to win, so it was time to reignite the flame that burned so strongly during the union-filleting Thatcher years.

Perhaps their biggest fear, as David Yelland speculates, is having people in charge with whom they have no relationship. They’ve never bothered with Clegg and they’ve burned their bridges with Brown, and if Cameron fails to seal the deal on 6th May Murdoch won’t have anyone to play with. The news coverage would inevitably be spiteful and dishonest but, perhaps only for a short time, the government could go about its business without having to run things by the editor of The Sun. Perhaps as part of that process we might even end up having a sensible debate about the nature of media ownership in Britain.

No comments:

Post a Comment