KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Sunday, May 15, 2011

VIDEO - Amchinja Mtu na Kukimbia na Kichwa Chake Mtaani

Watalii katika mji wa Tenerife nchini Hispania hawakuamini macho yao pale mwanaume mmoja alipojitokeza ghafla na kumshambulia mwanamke raia wa Uingereza na kukikata kichwa chake na kuanza kutimua mbio mitaani akiwa amekishikilia mkononi kichwa hicho.
Mwanaume huyo anayeaminika kuwa ni raia wa Bulgaria ambaye alikuwa hana makazi maalumu akilala mitaani katika mji wa Tenerife, alimvamia mwanamke raia wa Uingereza na kumshambulia kwa panga hadi alipokinyofoa kichwa chake na kisha kutimua mbio mitaani akiwa amekibeba kichwa hicho.

Watalii hawakuamini macho yao kwa tukio hilo ambalo lilifananishwa na matukio ya kwenye sinema.

Mwanaume huyo alifanya mauaji hayo ndani ya supermarket baada ya kuiba panga toka kwenye duka la vitu vya kitamaduni la Wachina.

Mwanaume huyo mwenye rekodi ya uhalifu alimvamia mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 50, na kuanza kumshambulia kwa panga akijaribu kukikata kichwa chake kama anachinja kuku hadi alipofanikiwa.

Akizishikilia nywele kwenye kichwa cha mwanamke huyo, alianza kutimua mbio akikiacha kiwiliwili huku damu zikiendelea kuchuruzika kwa wingi.

Walinzi wa supermarket walianza kumkimbiza mwanaume huyo ambaye aliangushwa chini alipotandikwa na helmet ya mwendesha pikipiki alipokatiza mbele yake akiwa amekibeba kichwa hicho.


"Nilipaki gari langu na ghafla nilimuona mwanaume akitoka kwenye supermarket akiwa ameshikilia kitu chenye kuchuruzika damu kwenye mikono yake huku walinzi wakimkimbiza" alisema shuhuda mmoja wa tukio hilo.

"Alikitupa kitu hicho pembeni ya barabara, kiliangukia pembeni yangu nilipoangulia vizuri niligundua kilikuwa ni kichwa cha mwanamke", aliendelea kusema shuhuda huyo.

Taarifa ya polisi ilisema kuwa mwanaume huyo raia wa Bulgaria alikuwa akijulikana sana maeneo hayo na alikuwa hamjui mwanamke huyo aliyemchinja.VIDEO - Amchinja Mtu na Kukimbia na Kichwa Chake Mtaani

Mkwamo katika vita vya Libya
Mkuu wa jeshi la Uingereza, Jenerali Sir David Richards, ameihimiza NATO kuzidisha shughuli zake za kijeshi nchini Libya kwa kushambulia maeneo zaidi, ambayo inaruhusiwa kuyalenga.Akihojiwa na gazeti moja la Uingereza, The Sunday Telegraph, alisema kama NATO haikufanya hivo basi itashindwa, na Kanali Gaddafi atabaki madarakani.

John Nichol aliwahi kuwa rubani wa jeshi la wanahewa la Uingereza, RAF, ambaye alidunguliwa Iraq katika vita vya kwanza vya Ghuba.

Anasema matamshi ya Jenerali Richards yanaonesha kuwa kunahitajika mkakati mwengine, ama sivyo, kuna hatari kuwa NATO itakwama kwenye operesheni ya Libya, ambazo zitakwama kwa miaka:

"Sote tunaotazama hali hivi sasa tunajua, kweli tumewawahifadhi raia, na hilo ni jambo jema.

Hayo tunakubaliana.

Lakini jee, sasa tutafanya nini?

Tumewalinda raia kwa siku 57; hata hivo mamia au pengine maelfu wamekufa.

Lakini sasa tufanye nini?

Hichi kipengee cha kulinda mstari wa mbele hakifai, kwa sababu kuna watu wanaendesha malori kwenye bara-bara kuu na kuuwana.

Kuna wenye ufundi wa shabaha wanaotumia bunduki.

Bado kuna vikundi vinavouwa watu.

Tufanye nini?

Au tubaki kwenye mkwamo, huku majeshi ya wanahewa ya Uingereza, Utaliana na Ufaransa yakilinda upande mmoja wa nchi, huku serikali inadhibiti upande mwengine.

Na mkwamo huo unaweza kuendelea kwa miaka."
Wapalestina wanaandamanaAskari wa usalama wa Israil na waaandamanaji wa Palestina wamepambana ufukwe wa magharibi wa mto Jordan, wakati Wapalestina wanakumbuka kuundwa kwa taifa la Israil, mwaka wa 1948, ambapo Wapalestina wengi wakawa wakimbizi.
Katika eneo la Gaza, inaarifiwa watu kama 15 walijeruhiwa na mizinga na bunduki za rashasha.

Katika ufukwe wa magharibi, kwenye mji wa Ramallah, mamia ya polisi wa Israil wa kupambana na fujo pamoja na jeshi, walitumia moshi wa kutoza machozi na risasi za mpira dhidi ya Wapalestina waliokuwa wakirusha mawe.

Piya kuna taarifa kuwa risasi zilifyatuliwa katika milima ya Golan, wakati wakimbizi wa Kipalestina walioko Syria, walipovuka mpaka.

Piya watu zaidi ya 10 wamejeruhiwa kutokana na risasi, katika tukio kama hilo kwenye mpaka wa Israil na Libnan.

Misri inachelewesha mkataba wa Mto NileBaada ya mazungumzo ya masaa baina ya serikali mpya ya Misri na Ethiopia, kuhusu swala tete la kugawana maji ya Mto Nile, makubaliano yamefikiwa kuwa Ethiopia haitotia saini ya mwisho ya mkataba mpya wa Mto Nile, hadi serikali mpya ya Misri itaposhika madaraka na kujiunga na mazungumzo hayo.
Mto Nile ndio maisha ya Misri, ndio chanzo pekee cha maji cha nchi hiyo.

Jambo hilo lilitambuliwa kwenye mkataba wa mwaka 1929 baina ya Uingereza na Misri, ambao ulisema hakuna mabadiliko yoyote yatakayofanywa kwenye Mto Nile, ambayo yatapunguza maji yanayofika Misri.

Mkataba huo uliithibitishia Misri kuwa itapata thuluthi mbili ya maji ya Mto Nile daima.

Katika miaka ya karibuni, nchi nyengine kando ya Nile zilikataa mkataba huo wa kikoloni.

Mwaka jana, baada ya juhudi za mwongo mzima kujaribu kubadilisha msimamo wa Misri kushindwa, nchi 6 za Nile zilikubaliana kutayarisha mkataba mwipya ambao Rais Mubarak aliupinga kabisa.

Ndio sababu ya Waziri Mkuu mpya wa Misri Essam Sharaf, kuzuru Ethiopia.

Baada ya mazungumzo, Waziri Mkuu wa Ethiopia, Meles Zenawi alitangaza kuwa nchi yake haitotia saini mkataba mpya hadi serikali mpya ya Misri itapochukua madaraka kufuatia uchaguzi.

Hiyo itamaanisha kuwa Ethiopia itabidi kusimamisha ujenzi wa bwawa muhimu
Obama anahimiza uchimbaji mafutaRais Obama ametangaza hatua mpya za kuzidisha sekta ya mafuta nchini humo.

Katika hotuba yake ya kila juma kwenye redio, alisema uchimbaji wa mafuta huko Alaska na Ghuba ya Mexico, hatimaye utasaidia kuacha kutegemea sana mafuta kutoka nchi za nje.

Siku za nyuma Bwana Obama akipendelea kutafuta njia mpya za kutoa nishati, bila ya kuchafua mazingira.

Lakini hivi sasa Wamarekani wanalalamika juu ya kupanda kwa bei ya mafuta.

Wapinzani wa Rais Obama, wa chama cha Republican, wamekuwa wakidai kuwa sekta ya uchimbaji mafuta nchini Marekani kwenyewe itanuliwe.

Watu wawili wameuwawa katika mapigano kati ya Wakoptik na Waislam
Cairo:

Watu wawili wameuwa wakati machafuko yaliporipuka upya kati ya Waislam na Wakoptik mjini Cairo.Wengine wasiopungua 60 wamejeruhiwa.Habari hizo zimetangazwa na kituo cha matangazo ya televiheni cha Al Jazira.Kwa mujibu wa polisi machafuko hayo yamesababishwa na ugomvi kati ya vijana wa Kiislam na waumini wa madhehebu ya kikristo ya Koptik ambao kwa siku kadhaa sasa wamekuwa wakiandamana mbele ya kituo cha televisheni cha Misri kulalamika dhidi ya mashambulio ya hivi karibuni dhidi ya makanisa nchini Misri.Mawe na mabomu ya mikono yamevurumishwa na magari yasiyopungua kumi kutiwa moto.Polisi wametumia gesi za kutoa machozi kuwatawanya wafanya fujo.Machafuko kama hayo yaligharimu maisha ya watu wasiopungua15 na wengine 240 kujeruhiwa mjini Cairo.Machafuko kadhaa yameripotiwa katika maeneo yanayopakana na Israel.

Jerusalem:

Machafuko ya umwagaji damu yameripotiwa katika maeneo matatu ya mpakani karibu na Israel,baada ya makundi ya itikadi kali ya Wapalastina kutoa mwito wa kuandamana hadi katika maeneo hayo.Watu wasiopungua wanne wameuliwa,na 11 kujeruhiwa pale makundi ya Wapalastina walipokuwa wanajongelea milima ya Syria ya Golan inayokaliwa na Israel.Katika machafuko kama hayo katika mpaka kati ya Israel na Lebanon,mashahidi wanasema watu6 wameuliwa na 71 kujeruhiwa pale wanajeshi wa Israel walipofyetua riasi za onyo.Hata katika kivukio cha Erez katika Ukanda wa Gaza wanajeshi wa Israel wamewafyetulia risasi Wapalastina waliokuwa wakielekea katika eneo hilo na kuwajeruhi 50 kati yao.Mnamo siku kama hii ya leo ya Nakba-au balaa,Wapalastina wanakumbuka jinsi walivyolazimika kuyapa kisogo maskani yao,dola ya Israel ilipoundwa mwaka 1948.Jeshi la Israel limelifunga eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan

Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa Domonique Strauss-Kahn amekamatwa New York

New-York/Paris:

Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF,Dominique Strauss-Kahn atafunguliwa mashtaka kwa tuhuma za kumsumbuwa na kutaka kumbaka mhudumu mmoja wa kike wa hoteli mjini New-York.Bwana huyo mwenye umri wa miaka 62 alikamatwa akiwa ndani ya ndege ,katika uwanja wa ndege wa John F. Kenndy,muda mfupi kabla ya kuondoka kuelekea Paris.Mhudumu huyo wa kike wa hoteli ndie aliyetowa malalamiko kwamba Dominique Strauss-Kahn alitaka kumbaka.Duru zinasema Dominique Strauss-Kahn aliondoka haraka hotelini na kusahau simu yake ya mkono na vitu vyake vyengine.Mfaransa huyo,aliyekuwa akipewa nafasi nzuri ya kukiwakilisha chama cha kisoshiliasti katika uchaguzi wa rais mwakani ,alipangiwa kukutana na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani hii leo mjini Berlin kuzungumzias mgogoro wa fedha wa Ugiriki.Wakili wa Domonique Strauss-Kahn William Taylor amewataka watu wasitaharuki kuhusiana na kisa hicho cha kukamatwa mkuu huyo wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF.Baadae hii leo Dominique Strauss Kahn amepangiwa kufikishwa mbele ya jaji mjini Manhattan.Mwenyekiti wa shirika la fedha la kimataifa anakanusha tuhuma dhidi yake na anapanga kujitetea kwamba hana hatia

Pakistan: Marekani inatuharibia jinaBunge la Pakistan limeitaka serikali izingatie tena uhusiano wa nchi hiyo na Marekani, baada ya Osama bin Laden kuuliwa na kikosi cha Marekani.

Bunge limedai ndege za Marekani zisokuwa na rubani ziache kufanya mashambulio katika ardhi ya Pakistani, na lilisema inafaa kufikiria kuacha kuruhusu vifaa vya NATO vinavokwenda Afghanistan, kupitia Pakistan.

Wabunge piya walitaka uchunguzi ufanywe kuhusu operesheni ya kumuuwa Osama bin Laden, ambayo waliilaani kuwa imevunja mamkala ya Pakistan.

Maazimio yaliyopitishwa na bunge hayakutaja swala la vipi kiongozi wa Al Qaeda alifika kuwa nchini humo. Badala yake, kikao hicho cha faragha cha bunge kilijadili uhusiano maalum baina ya Pakistan na Marekani.

Maazimio yamelaani sana shughuli za Marekani nchini humo, na kile kilichoelezewa kuwa "kampeni ya Marekani kuipa Pakistan jina baya".

Bunge halikuilaumu idara ya usalama ya Pakistani hadharani.

Wabunge waliohudhuria kikao hicho cha faragha, walisema, mkuu wa Idara ya Ujasusi, Jenerali Pasha, alichagizwa sana na baadhi ya wabunge, na alisema yuko tayari kujiuzulu; ingawa Waziri Mkuu hajakubali ombi la jenerali huyoMzozo wa katiba unasuluhishwa Zimbabwe
Vyama vya Zimbabwe vimetatua mzozo kuhusu matayarisho ya katiba mpya ya nchi.
Mazungumzo hayo yalivunjika mapema juma hili kuhusu namna ya kushirikisha maoni ya watu wa kawaida kwa kuwashauri nchini kote Zimbabwe.

Msemaji wa chama cha Waziri Mkuu, Morgan Tsvangirai, aliiambia BBC, tatizo hilo sasa limeondoka.

Katiba mpya inatarajiwa kutayarishwa ufikapo mwezi Septemba, na msemaji huyo, Douglas Mwonzora, alieleza bado ana matumaini kuwa lengo hilo litafikiwa iwapo polisi wataacha kubughudhi chama chao.

Kufwatana na mkataba wa amani kati ya wanasiasa wa Zimbabwe, ulioongozwa na Afrika Kusini, katiba mpya inahitajika kabla ya uchaguzi kufanywa


Maisha mafupi kusini mwa Afrika
Takwimu za Shirika la Afya Duniani, WHO, zinaonesha kuwa, kwa sababu ya UKIMWI kusini mwa Afrika, urefu wa wastani wa maisha ya Muafrika Kusini umepungua kwa miaka 9, na miaka 12 Swaziland na Zimbabwe, ikilinganishwa na mwaka 1990.Lakini watu wanaishi kwa muda mrefu zaidi katika nchi nyengine za Afrika na dunia.

Eneo la kusini mwa Afrika ndilo liloathirika vibaya kabisa na UKIMWI katika bara hilo.Waliofariki wafikia 92 SamungeWATU waliofariki Kijiji cha Samunge, wilayani Ngorongoro, kabla ya kupata tiba ya magonjwa sugu inayotolewa na Mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Masapila, wamefikia 92
Waliofariki wafikia 92 Samunge
baada ya wengine sita, wakiwamo raia watatu wa Kenya kufariki wiki hii.

Mganga Mfawidhi Zahanati ya Kata ya Samunge, Dk Elias Lubida, alisema watu sita wamefaniki kuanzia Jumatatu hadi jana.Dk Lubiba aliwataja watu hao kuwa, ni Stain Madokelo, mkazi wa Narock, Jospicke Kipati, mkazi wa Bometi na Lina Chilomo wa Wilaya ya Bomet, Kenya.

Alisema Watanzania waliofariki, ni Ernest Kileo, mkazi wa Hai, Edwin Yusto, mkazi wa Tarime na Sekunda Mmanda, mkazi wa Rombo.

"Wagonjwa hawa walifariki kabla ya kupata kikombe cha tiba, inavyoonekana walifika Samunge wakiwa mahututi," alisema Dk Lubiba.Kuhusu takwimu za waliofariki, Dk Lubiba alisema Aprili walifariki watu wanane na Machi kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Ngorongoro, Dominick Lusasi, watu 78 walifariki.

Lusasi alisema watu hao walifariki kutokana na msongamano uliokuwapo Samunge, hivyo kuzuia wagonjwa waliokuwa mahututi kupata huduma ya kwanza kabla ya kupata kikombe cha tiba.

Vifo hivi vya watu hao, vinaendelea kutokea licha ya serikali na Mchungaji Mwasapila, kutoa taarifa mara kwa mara kushauri wagonjwa mahututi kutopelekwa Samunge.

Mapema wiki hii, Mchungaji Mwasapila aliwataka Wakenya pia kuacha kumpelekea wagonjwa mahututi, ambao wanawaondoa hospitali hasa kutokana na kutokuwa na miundombinu mizuri ya kufika Samunge.

Wafuasi 80 wa Chadema Jimbo la Arusha watua Samunge.
Wananchi 80 wa Jimbo la Arusha wengi wao wakiwa wanachama wa Chadema, jana walifika Samunge kupata kikombe cha tiba kutokana na ufadhili wa Mbunge wa jimbo hilo, Godbless Lema na Taasisi ya Maendeleo ya Jimbo la Arusha (ArDF).

Wakazi hao wa Arusha, walifika Samunge saa 7:00 mchana, huku wakiimba nyimbo mbalimbali za Chadema.

Katibu Mwenezi wa Chadema Wilaya ya Arusha, Gabriel Lucas, aliyekuwa kiongozi wa msafara huo, alisema wamefarajika kufika Salama Samunge.Lucas alisema katika msafara huo, ambao unatokana na ahadi ya Lema na taasisi yao ArDF, kulikuwa na watu 80 kati yao watoto ni 20.

Naye Mwenyekiti wa ArDF, Elifuraha Mtowe, alisema watu hao 80 kutua Samunge ni awamu ya kwanza na kundi jingine linatarajiwa kufika kesho."Hili ni kundi la kwanza, kundi jingine litafika Samunge Jumapili, tunapenda kutoa shukrani kwa waliofanikisha safari za watu hawa, ambao tunaamini tiba ya babu itawasaidia kuboresha afya zao," alisema Mtowe.

Alisema ArDF na Chadema Arusha, wanampongeza Mchungaji Mwasapila kwa kutoa tiba hiyo kwa gharama ndogo na kuwezesha hata watu wa kipato cha chini kunufaika.

Mchungaji Mwasapila ataka wanaokunywa dawa wasiwe malaika.Mchungaji Mwasapila, jana amewataka wagonjwa wanaofika Samunge kupata tiba wasiache kunywa dawa zao wanapougua magonjwa mengine, kwani wao sio malaika.

Akizungumza na mamia ya watu kabla ya kuanza kutoa tiba jana, Mchungaji Mwasapila alisema, kama mgonjwa amepata kikombe na baadaye akaugua tena ugonjwa mwingine asisite kwenda hospitali."Ndugu kupata kikombe cha tiba hamjawa malaila, kuwa hamtaugua ugonjwa mwingine tena, kwani kikombe siyo kinga ni tiba hivyo mkiungua nendeni hospitali," alisema Mwasapila.

Alisisitiza kikombe cha tiba ambacho anatoa hakirejewi mara mbili, hivyo wale waliokunywa na sasa wanahisi ugonjwa kurejea wanaweza kurudi Samunge kwa maombi na ushauri mwingine siyo kikombe.

Msanii Dude atua Samunge.
Msanii maarufu wa kundi la bongo Dar es Salaam, ambalo linarusha michezo yake Kituo cha televisheni cha TBC1, Kulwa Kikumba, maarufu kama Dude jana alitua Samunge na kuwa kivutio.

Dude baada ya kufika Samunge, alishuka kwenye gari na kusalimiana na Mchungaji Mwasapila kicha akapata kikombe na kuondokaMan United mabingwa wa Ligi ya England


Bao la mkwaju wa penalti lililoonekana la utata lililofungwa na Wayne Rooney lilitosha kuipatia Manchester United ubingwa na kuvunja rekodi ya kunyakua ubingwa wa Ligi ya Soka ya England kwa mara ya 19 katika uwanja wa Ewood Park.Sir Alex Ferguson
Pointi moja ilitosha kwa meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu ya England kwa mara ya 12 tangu aanze kuifundisha timu hiyo katika pambano dhidi ya Blackburn.

Manchester United ilionekana ingepoteza mchezo huo hadi mlinda mlango wa Rovers Paul Robinson alipofanya makosa ya kumuangusha chini Javier Herndandez na wageni wakapatiwa nafasi ya kupiga mkwaju wa penalti.

Rooney alifunga mkwaju huo wa penalti na kuisawazishia timu yake na kuwafanya mashabiki wa timu hiyo kuhanikiza kwa shangwe za ubingwa.

Blackburn walikuwa wa kwanza kupata bao lililopachikwa na Brett Emerton baada ya ngome ya United kujichanganya akiwemo mlinda mlango wake Thomas Kuszczak.

Lakini bao la mkwaju wa penalti katika dakika ya 73 lilitosha kuibua shangwe za ubingwa kwa mashabiki ambapo sasa Manchester United imepata pointi 77 ambazo timu inayofuatia Chelsea hata ikishinda mechi zake zote mbili zilizosalia haitaweza kufikisha pointi hizo


Maharamia wa Somalia walipwa dola milioni 7


MOGADISHU

Maharamia wa Somalia wamepokea dola milioni saba kwa ajili ya kuachiliwa kwa mateka wawili wa Uhispania ambao walikuwa wakishikiliwa mateka kwa miezi minne na nusu.

Abdi Yare haramia wa mji wa bandari wa kaskazini mashariki wa Hobyo akizungumza kwa njia ya simu kutoka Mogadishu amesema fedha hizo zilidondoshwa kutoka angani kwenye jengo la Italia linalomilikiwa na maharamia hao na kwamba mateka hao wawili wako huru na wanasubiri kurudishwa makwao.Kwa mujibu wa mzee mmoja wa mji wa Hobyo Mohamed Duale aliezungumza na shirika la habari la AFP fedha hizo zilidondoshwa na helikopta na kima hicho ni kikubwa kabisa kuwahi kulipwa kwa ajili ya mateka wawili tu.Wizara ya mambo ya nje ya Uhispania hapo jana imesema haiwezi kuthibitisha kuachiliwa kwa mateka hao, nahodha Juan Alfonso Rey Echeverri na msaidizi wake Jose Alfonso Garcia.

Mwezi Novemba mwaka jana ilivunjwa rekodi ya kulipa kima kikubwa cha fedha cha kuwagombowa mateka wakati dola milioni tisa zilipolipwa kwa ajili ya kuachiliwa kwa meli ya Samho Dream iliotekwa mwezi wa April mwaka uliopita ikiwa na mabaharia watano wa Korea Kusini na Wafilipino tisa na shehena ya mafuta ya Iraq iliokuwa inapelekwa Marekani
FDPMkutanao mkuu wa chama cha FDP wakurubia kumalizika mjini Rostock

Rostock:

Wajumbe katika mkutano mkuu wa chama cha Kiliberali cha FDP wanaendelea kuwachagua wanachama wa halmashauri ya uongozi.Mnamo siku ya mwisho ya mkutano huo mkuu wa siku tatu mjini Rostock,zaidi ya wajumbe 600 wanapanga pia kujadili namna ya kuachana na nishati ya kinuklea.Mada nyengine mkutanoni hii leo inahusu elimu.Katika hotuba yake ya mwanzo kama mwenyekiti wa chama cha Kiliberali cha FDP,waziri wa uchumi Philipp Rösler alisema jana wanataka kuutakasa wajih wa FDP kama mshirika katika serikali ya muungano pamoja na vyama ndugu vya CDU/CSU.Philipp Rösler amerithi wadhifa uliokuwa ukishikiliwa na Guido Westerwelle ambae ameamua kujishughulisha na wizara ya mambo ya nchi za nje tu.Marais, mfalme watarajiwa kutua Samunge kwa BabuAbiria waliofika kwa mchungaji Ambilikile Mwasapila katika kijiji ch Samunge kunywa dawa jana, wakiteremka kutoka katika helikopta inayomilikiwa na kampuni ya Akagera aviation ya Rwanda. Picha na Mussa Juma

MARAIS kadhaa wa nchi za Afrika akiwamo mfalme, wanatarajiwa kwenda Samunge, Loliondo kupata tiba ya magonjwa sugu inayotolewa na Mchungaji Ambilikile Mwasapila.

Kutokana na ujio huo, ulinzi umeimarishwa kuanzia jana. Ofisa mmoja wa polisi wa Wilaya ya Ngorongoro, alithibitisha ujio wa wakuu hao bila ya kutaka kutoa maelezo zaidi. Hakutaja siku wala muda ambao watawasili hapa.
Jana kulikuwa na idadi kubwa zaidi ya polisi kijijini hapa. Ofisa mwingine wa polisi ambaye pia hakutaka jina lake liandikwe alisema, wamepokea taarifa za ujio wa marais hao na walitegemea kwamba wangewasili Samunge kuanzia jana.

"Ni kweli, kuna wageni watakuja. Nadhani ni wakubwa bado taarifa kamili hazijatufikia watatua lini," alisema.
Helikopta kutoka Rwanda inayomilikiwa na Kampuni ya Akagera Aviation, imeanzisha safari za kwenda Samunge kila siku ikitokea Uwanja wa Ndege wa Arusha.

Helikopta hiyo ni kubwa kuliko nyingine ambazo zimekuwa zikitua Samunge kuleta wagonjwa kupata tiba ya kikombe kwa Babu.Ujio wa helikopta hiyo, sasa unalifanya anga la Samunge kutawaliwa na helikopta nne, zinazofanya safari takriban mara tatu kwa siku kwenda na kutoka Samunge.

Gharama za nauli kwa abiria mmoja kutoka Arusha hadi Samunge kwa helikopta hiyo ya Rwanda ni Dola za Marekani 1,000 hivyo kufanya usafiri huo kuwa wa watu wenye uwezo mkubwa kifedha.
Baada ya kuongezeka wimbi la viongozi kutoka nchi jirani ya Kenya wanaofika Samunge na habari zao kuandikwa, sasa vigogo wengi wa huko wamebuni njia nyingine ya kufika kijijini hapo bila kujulikana.

Vigogo hao sasa wanafika Samunge kupitia mpaka wa Narock ambako huenda moja kwa moja hadi Loliondo na kukodi magari ya wenyeji ili kuwapaleka Samunge. Kwa takriban wiki mbili sasa, viongozi kadhaa wa Serikali ya Kenya, wakiwamo maofisa wa Ikulu ya Kenya, mawaziri na wabunge wamekuwa wakitua Samunge.

Babu: Wagonjwa waruhusiwe
Mchungaji Mwasapila ameomba vituo vinavyoratibu magari yanayokwenda Samunge, kuruhusu magari zaidi kupeleka wagonjwa ili wapate huduma kutokana na kupungua kwa foleni.Msaidizi wa Mchungaji Mwasapila, Frederick Nisajile alisema jana kwamba kutokana na huduma kuboreshwa, idadi ya magari yanayopaswa kuingia Samunge kwa siku yanapaswa kuongezeka.

"Tunaomba wawe na mawasiliano na sisi ya mara kwa mara kwani sasa kama unavyoona hakuna foleni, lakini kuna magari yamezuiwa maeneo ya vituo yasije huku," alisema Nisajile.

Jana, zaidi ya magari 500 yakiwamo mabasi makubwa kutoka Mikoa ya Kigoma, Dodoma, Mwanza na Arusha yalifika Samunge na abiria kupata kikombe na kuondoka.Hadi majira ya tisa jioni jana, foleni ya magari ilielekea kumalizika kabisa.

Bei ya kikombe iko palepale
Mchungaji Mwasapila jana alitoa ufafanuzi kuhusu malipo ya kikombe akieleza kuwa hajawahi kupandisha gharama zake tangu mwanzo. Alisema Watanzania wanalipa Sh500 na wageni kutoka nje ya nchi, wanalipa Dola moja au Sh1,500.TP Mazembe kukata rufaa uamuzi wa Caf


Mabingwa wa sasa wa soka barani Afrika TP Mazembe, wamesema watakata rufaa kutokana na uamuzi wa Shirikisho la Kandanda Afrika- Caf, kuiondoa katika Ligi ya Ubingwa wa Vilabu kutokana na kumchezesha mchezaji asiyestahiki.


Wachezaji wa TP Mazembe


Katika taarifa iliyotolewa muda mfupi baada ya uamuzi wa Kamati ya Maandalizi ya Caf kwa mashindano ya vilabu, klabu hiyo ya Congo imesisitiza haijavunja sheria kwa kumchezesha Janvier Besala Bokungu, ambaye klabu ya soka ya Simba ya Tanzania imemshutumu alivunja mkataba wake na klabu ya Esperance na kujiunga na Mazembe, hali iliyomfanya asistahili kucheza katika michuano ya Caf.

“Uongozi wa Mazembe unauona uamuzi wa Caf haukubaliki ndio maana haraka tutakata rufaa kutokana na uamuzi huo. Meneja wetu Mkuu Frederick Kitenge kwa sasa yupo Cairo akiangalia vipengele vyote vya kupata haki kwa klabu yetu,” Taarifa hiyo ya Caf imesomeka katika mtandao rasmi wa Corbeaux.

Iwapo rufaa ya Mazembe itagonga mwamba, watakosa nafasi ya kutetea ubingwa wao na pengine kuweka rekodi ya kuwa mabingwa wa vilabu barani Afrika kwa mwaka wa tatu mfululizo, ambapo klabu hiyo imesema ndio lengo lao kuu msimu huu.

Katika hali nyingine, Chama cha taifa cha kandanda cha Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, kimetupilia mbali maombi ya Mazembe ya kutaka kuahirishwa mechi yake ya mwishoni mwa wiki dhidi ya DCMP, kwa sababu mabingwa hao wana ziara ya mazoezi nchini Brazil.

DCMP itadai pointi zote tatu iwapo Mazembe haitatokea uwanjani siku ya Jumapili. Kuna mashaka kama timu hiyo itasafiri kuelekea Marekani Kusini ili ikabiliane na DCMPWalumbana juu ya sababu za elimu duni


KUSHUKA kwa ufaulu wa wanafunzi wa shule za sekondari kwa kidato cha nne, juzi kuliibua mjadala mkali jijini Dar es Salaam baada ya makundi yaliyoshiriki semina iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia (TGNP) kutofautiana kuhusu sababu zake. Hali hiyo ilijidhihirisha juzi katika semina zinazoratibiwa na TGNP ambapo wachangiaji waliojitambulisha kuwa ni wanasiasa kutoka katika vyama vya CCM na Chadema waliposimama kuchangia.

Ofisa Mwandamizi wa CCM, Idara ya Mahusiano ya Kimatifa, Amos Robert ambaye alisimama na kuanza kutetea serikali ya CCM kwa kudai kuwa haisitahili kulaumiwa kwa kushuka kwa ufaulu huo.

“Suala la kushuka kwa elimu serikali isilaumiwe pekee, Serikali ya CCM ni sikivu na inayo mazuri mengi imeyafanya katika awamu zote za uongozi wake”, alisema Robert na kuongeza “Wachangiaji wengi wanazungumzia shule za kata kuwa zina kiwango duni cha utoaji elimu,huo ni utekelezaji wa ilani ya CCM awamu ya kwanza ya kujenga shule, sasa mpango unaokuja ni wa uboreshaji shule hizo kwa kujenga maabara na kupeleka walimu”alisema.

Amos aliwataka wachangiaji kutambua kuwa hakuna mfumo wa elimu duniani usio na mapungufu na kusisitiza yeye ametumwa kutoka makao makuu ya chama ili kusikiliza mawazo ya wanaharakati na kuyafikisha makao makuu ili yakafanyiwe kazi.Kauli ya kada huyo wa CCM ilimuinua Mbunge wa SuzanLyimo9Viti Maalumu Chadema) ambaye kama mtangulizi wake alijitambulisha kuwa yeye ni mwanasiasa kutoka Chadema.

Lyimo alisema kuhusu kushuka kwa elimu serikali ya CCM haiwezi kukwepa lawama sababu imevurugu mitalaa na kuwatelekeza walimu makusudi ili kuwafanya Watanzania wawe wajinga iweze kuwatawala. “Mimi ni mwalimu,walimu wamedharauliwa na kutelekezwa,mitalaa imevurugika,ziko wapi shule za sekondari za serikali ambazo ndizo zilizokuwa zikitamba kwa kutoa elimu bora,huu ni kuporomoka kwa elimu ni mpango wa Serikali ya CCM wenye lengo la kuwafanya watu wabaki na maskini ili wao waendelee kutawala”alisema Lyimo.

. Katika mjadala huo wachangiaji waliendelea kutofuatina juu ya nani wa kulaumiwa ambapo Hussen Bondei aliitetea serikali kuwa haistahili lawama katika hilo. Kwa upande wake alihoji sababu za wazazi kuruhusu uwepo wa shule za kata bila kuwa na mabweni na kusema hali hiyo inatoa fursa kwa watoto hao kupata mimba wakiwa mashuleni.

“Serikali imekosea! mimi sitaki kusema hivyo, je wazazi wana moyo wa kuchangia katika elimu?”alihoji Bondei.
Naye Lecat Nkya aliyejitambulisha kuwa ni Mwalimu aliwatupia lawamu wananchi kwa kuwachagua viongozi wasiotimiza wajibu wao kwa kushindwa kutambua umuhimu wa elimu hapa nchini.


Manchester City yashinda kombe la FA


Bao pekee la Yaya Toure limemaliza ukame wa makombe kwa Manchester City, baada ya kuishinda Stoke City kwa bao 1-0 kwenye uwanja wa Wembley.


Yaya Toure akishangilia


Licha ya timu hizo kukamiana, zilikwenda mapumziko zikiwa hazijafungana.

Man City walicheza mchezo wa kuonana na pasi za uhakika, huku Stoke zaidi wakitegemea mipira ya kurusha.

Kipa Joe Hart wa Man City hakuwa na kazi ngumu kama kipa wa Stoke.

Licha ya matokeo hayo, Stoke ity bado wanacheza kombe la Europa msimu ujao, kutokana na Man City kumaliza katika nafasi ya nne, na hivyo itacheza klabu bingwa Ulaya.

Mafuriko yawakosesha maelfu makazi Kilombero


WATU 9,000 wa Kata ya Mbingu wilayani Kilombero mkoani Morogoro, hawana mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kubomoka na nyingine kuzingirwa na maji kutokana na mafuriko yaliyolikumba eneo hilo.Vijiji vilivyokumbwa na mafuriko hayo yaliyosababishwa na mvua zilizoanza kunyesha mwanzoni mwa
mwezi uliopita ni pamoja na Mofu, Ikwambi, Mbingu, Igima na Mpofu.

Kutokana na mito kujaa maji baadhi ya mamba walisombwa na maji mpaka katika makazi ya watu ambapo Aprili 26, mwaka huu mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kisoma, Jackson Kisoma (14), ambaye ni mkazi wa kata hiyo aliliwa na mamba wakati akitoka shuleni.

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Injinia Evarist Ndikilo aliwaeleza maofisa wa Shirika la Plan International waliokwenda kutoa msaada wenye thamani ya dola 100,005 kuwa nyumba zilizobomoka kutokana na mafuriko hayo ni 663 huku zilizozingirwa na maji zikiwa 2,942.

“Kaya zilizoathirika ni 1807 na idadi ya watu ambao ambao mpaka sasa hawana makazi ni 8,586, mashamba yaliyoharibiwa ni 2,256 na idadi ya watu waliopoteza mashamba ni 1,003,” alisema Ndikilo.

Alisema kutokana na hali hiyo, Halmashauri ya Wilaya hiyo imechukua hatua kadhaa ikiwa ni pamoja na kutoa msaada wa vyakula na mahema.

Mwananchi lilishuhudia baadhi ya nyumba zikiwa zimebomolewa na maji huku Shule ya Msingi ya Mbingu, Chiwachiwa, Londo na Upendo zikifungwa kwa muda kutokana na kuzingirwa na maji.Akielezea jinsi James alivyoliwa na mamba, diwani wa Kata hiyo, Seleni James alisema kuwa tukio hilo lilitokea Aprili 26 na kwamba mwanafunzi huyo aliliwa na mamba wakati akitoa shuleni.

“Unajua mito imejaa maji hivyo mamba walisombwa na maji mpaka katika makazi ya watu, hivi sasa tumeshatoa tahadhari kwa wananchi, lakini pia tumeanza kufanya msako kwa mamba hao,” alisema James.

Alisema kuwa mbali na tukio hilo, Negiris Mkemwa (2), alifia njiani wakati akipelekwa hospitali kutokana na barabara kutoka Mbingu kwenda Ifakara Mjini kujaa maji na kusababisha magari kukwama.

Wafanyabiashara wanaosafirisha mazao kutoka katika Kata hiyo kuelekea maeneo mbalimbali magari yao yamekwama kutokana na barabara kujaa tope.Blackpool, Wolves na West Brom zashinda
Blackpool imeweka hai matumaini ya kutoshuka daraja baada ya ushindi mnono wa mabao 4-3 dhidi ya Bolton katika mchezo uliokuwa wa vuta nikuvute.
DJ Campbell
Kevin Davies wa Bolton alikuwa wa kwanza kuipatia timu yake bao mapema dakika ya sita, lakini dakika tatu baadae DJ Campbell aliisawazishia Wolves na dakika kumi baadae Jason Puncheon akaandika bao la pili kwa mkwaju wa yadi 18.

Matt Taylor aliisawazishia Bolton na alikuwa kwa mara nyingine Campbell aliyeandika bao la tatu kwa Wolves kabla ya mapumziko.

Daniel Sturridge aliisawazishia Bolton na kufanya ubao wa mabao uoneshe 3-3, lakini Charlie Adam akakamilisha kazi kwa kupachika bao la ushindi la nne kwa Wolves..

Kwa matokeo hayo, Blackpool wanaendelea kubakia nafasi tatu kutoka chini wakiwa na pointi 39, lakini timu nne zilizo juu yake kimahesabu zinaweza nazo kuporomoka na kushuka daraja.

Wolves nayo imepata ushindi muhimu katika hekaheka zao za kuwania kubakia Ligi Kuu ya England msimu ujao, baada ya kuilaza Sunderland ugenini kwa mabao 3-1.


Charlie Adam
Ushindi huo umeifanya Wolves kufikisha pointi 40 wakiwa nafasi ya 16, nafasi mbili tu chini ya timu tatu zilizo mstari wa kuteremka daraja.


Huo unakuwa wa kwanza kwa meneja Mick McCarthy katika uwanja wa Stadium of Light akiwa meneja katika timu ya Ligi Kuu ya England.

Bao la Youssouf Mulumbu katika dakika ya10 liliihakikishia ushindi mzuri West Brom kumaliza mechi zao za Ligi katika uwanja wa nyumbani dhidi ya Everton waliocheza pungufu ya mchezaji mmoja
Youssouf Mulumbu
Mulumbu alifunga kwa mkwaju wa karibu na lango baada ya kazi kubwa iliyofanywa na Peter Odemwingie kufuatia krosi safi iliyochongwa na Chris Brunt.

Victor Anichebe, Johnny Heitinga na Leon Osman wote walikaribia kuipatia bao Everton, lakini tatizo lao la kufunga liliongezwa zaidi baada ya Diniyar Bilyaletdinov aliyeingizwa kipindi cha pili, kutolewa kwa kadi nyekundu.

Bilyaletdinov alioneshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumchezea vibaya James Morrison.

Matokeo hayo yameifikisha West Brom nafasi ya 10 wakiwa na pointi 46, huku Everton wakiwa nafasi ya saba na pointi 51
Ndugu wa Pinda wapata kikombeUJUMBE wa watu zaidi ya kumi ambao ni ndugu wa karibu wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, jana walifika kijijini Samunge wakiwa na ulinzi mkali ili kupata kikombe cha tiba, kinachotolewa na Mchungaji Ambilikile Mwasapila.
Ndugu hao wa Pinda, walifika Samunge saa saba mchana na magari matatu aina ya Toyota Land Cruiser, VX na Prado yenye namba binafsi na walikuwa wamewekewa ulinzi usiokuwa wa kawaida.

Mara baada ya kufika Samunge, ndugu hao wa Waziri Mkuu walipokelewa na maofisa wa Serikali na wale wa usalama ambapo walipelekwa moja kwa moja kwa Mchungaji Mwasapila kupata kikombe.

Ofisa wa Serikali, ambaye alishiriki katika mchakato wa mapokezi ya ndugu hao, alisema ni ndugu wa karibu wa Waziri Mkuu Pinda, ambao wametoka nyumbani kwake na ndio sababu wamepewa upendeleo maalumu katika kupata tiba hiyo.

"Ni kweli, hawa ni ndugu wa Waziri Mkuu, wamo kaka yake aliyeambatana na mkewe pamoja na watoto, pia wamo wajomba na wadogo zake na tangu asubuhi tumekuwa tukiwasubiri ili wapate huduma ya kikombe kutoka kwa Babu,"alisema ofisa huyo.

Hata hivyo, haikuwa rahisi kupata picha zao wakati wakinywa dawa baada ya maofisa wa usalama kuzuia wasipigwe picha kwa maelezo kwamba safari yao hiyo ni ya binafsi.Ujio wa ndugu hao, unafanya iwe familia ya pili ya vigogo wa Serikali kutua Samunge, familia nyingine iliyofika ni ya Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi ambapo watoto wake na wake zao walifika Samunge kupata kikombe cha Babu.

Bugudha kwa wageni
Mchungaji Mwasapila ameomba maofisa wa Serikali na Jeshi la Polisi kuacha kuwabugudhi wagonjwa kutoka nje ya nchi wanaokwenda Samunge kupata tiba.

Akizungumza na mamia ya watu kijijini Samunge jana kabla ya kuanza kutoa tiba, Mchungaji Mwasapila alisema amepata taarifa za kubughudhiwa kwa raia wa kigeni ambao wanakwenda Samunge. "Jamani watu wanapokuja hapa Samunge ni kwa shida, hivyo muwatendee mambo mema, wafike salama na kupata tiba,"alisema Mwasapila.

Hata hivyo, mchungaji huyo aliwataka wageni wanaofika Samunge kufuata taratibu za nchi ikiwa ni pamoja na vibali vinavyowaruhusu kuingia nchini.

Serikali na njia za panya
Serikali wilayani Ngorongoro imesema itaimarisha udhibiti wa matumizi ya njia za panya ikiwa ni pamoja na wale wanaotumia njia hizo, hasa wageni kutoka nchi jirani.
Mkuu wa wilaya hiyo, Elias Wawa Lali, alisema tayari Serikali imepiga marufuku magari kutoka nchi jirani kufika Samunge bila kupitia mipaka inayotambuliwa kisheria.

Akizungumza na Mwananchi jana, Lali alisema hatua hiyo, imechukuliwa ili kudhibiti wimbi kubwa la magari yanayofika Samunge kutoka nchi jirani kwa kupitia njia za Panya."Ili kukabiliana na wimbi hili baadhi ya wajumbe wa Kamati za Ulinzi na Usalama tumewatuma kuchunguza hiyo mipaka na kuona ni jinsi gani tutadhibiti,"alisema Lali.

Ushuru wachunguzwa
Katika hatua nyingine, Serikali imeanza kuchunguza ushuru wa Sh500 za Kenya ambazo, hutozwa madereva wa magari yanayotoka nchi hiyo jirani kupitia mpaka wa kijiji cha Soitsambu.Lali, alithibitisha kuanza uchunguzi huo jana na kutumwa kwa maofisa wa Serikali katika Kijiji hicho.

"Ni kweli tumepata taarifa za ushuru huo na tunafuatilia kujua uhalali wake,"alisema Lali.Kwa mujibu wa diwani wa Kata ya Soitsambu, Ngoitika Daniel, wao wanakusanya ushuru huo kwa kufuata taratibu na wamekuwa wakigawana fedha nusu kwa nusu na Halmashauri ya Ngorongoro.

"Fedha ambazo tunakusanya, zinatumika katika masuala ya usafi na ulinzi kama unavyojua kule ni mpakani na mazingira yameanza kuchafuliwa sana,"alisema Daniel.

Hata hivyo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ngorongoro, Dominick Lusasi alipotakiwa kuelezea ushuru huo wa magari kutoka nchi jirani ya Kenya, alisema yeye sio msemaji na anayepaswa kuulizwa ni Mkuu wa Wilaya


Polisi Arusha wajipanga kuwalinda Wamarekani
POLISI kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB),wameandaa mkakati maalumu wa kuimarisha ulinzi katika mji wa Arusha kufuatia ujio wa wageni 260 kutoka Marekani na Mexico.

Wageni hao, wanatarajia kuwasili nchini Mei 18 mwaka huu na watatembelea Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Kituo cha kulelea Watoto Yatima cha Moshi mkoani Kilimnjaro.

Pia watapanda Mlima Kilimanjaro.

Hatua ya kuimarishwa kwa ulinzi katika mji huo wa kitalii, inakuja huku kukiwa na hofu ya mtandao wa kigaidi duniani wa Al Qaeda, kulipiza kisasi cha kuuawa kwa kiongozi wake, Osama bin Laden, nchini Pakistani.

Kundi hilo limekuwa likitishia kuwashambulia raia wa Marekani popote watakapokuwa duniani.

Ofisa Uhusiano Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania, Geofrey Tengeneza wageni hao watakuwa nchini kwa wiki mbili.

"Kuanzia siku watakayowasili, wageni hao watafanya shughuli mbalimbali zikiwao za michezo na baadaye, watetembelea Hifadhi ya Taifa ya Tarangire,"alisema.

Alisema wageni hao watagawanyika katika makundi matatu na kwamba la kwanza litatembelea hifadhi hiyo Mei 22 wakati , kundi la pili litafanya hivyo Mei 23 na kundi la tatu litatembelea hifadhi, Mei 24.

Alisema baadaye, watakwenda Moshi ambako watapata fursa ya kutembelea miradi ya kituo cha watoto yatima kinachoratibiwa na vikundi vya hiari vya IRS na STEMM.

Tengeneza alisema ziara hiyo itafuatiwa na safari ya kupanda Mlima Kilimamnjaro.

"Katika kupanda mlima huo, wageni watagawanywa katika makundi mawili na kundi la kwanza ni litakuwa la Wamexico na kundi la pili ni Wamarekani,"alisema.

Alisema kundi hilo la kwanza litapanda mlima kwa kutumia njia ya Machame na kushuka kwa kutumia njia ya Mweka wakati kundi la pili litapanda kupitia njia ya Rongai na kushukia ile ya Marangu.


Pi alisema bodi hiyo imeandaa nakala za jarida yanayoelezea vivutio vya kitalii vilivyopo nchini na mifuko yenye picha mbalimbali itakayotolewa kwa wageni hao


Kimaro ahoji usafi wa Waziri Magufuli


ALIYEKUWA Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro, amemshangaa Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, kuendelea kug’ang’ania kung’oa mabango ya matangazo ilhali barabara zake ni chafu kuliko mabango hayo.

Akizungunmza ofisini kwake jana, Kimaro alimtaka Dk Magufuli kuacha malumbano na serikali za mitaa na kwamba, mabango ya matangazo yanapendezesha mji na hivi sasa yanawasha taa za barabara, kitu ambacho wizara imeshindwa.

“Mabango yanawasha taa za barabara. Dodoma imewasha taa za barabarani kwa mabango. Aende New York, Mtaa wa Tuime Square aone jinsi mabango yalivyogeuza mtaa kuwa kivutio cha utalii,” alisema na kuohoji:

“Lakini usafi wa Magufuli unatoka wapi? Magufuli huyo huyo ndiye aliyesimamia uuzaji wa nyumba za serikali kwa ulafi wa kupata nyumba mjini, wakauza nyumba hata za wilayani, hivi sasa watumishi wanahangaika. Hiyo ni dhambi ya mauti, ni dhambi mbaya haimtoki hiyo.”

Kuhusu mabango ya matangazo, Kimaro alisema hakutakiwa kulumbana na halmashauri, bali angekaa na Waziri mwenzake wa tamisemi kuangalia jinsi ya kutatua suala hilo.

Kimaro alisema iwapo Dk Magufuli alifikiri serikali iliyokuwapo ndio ya mwisho, imekuwaji anaendelea kutumia iliyopo sasa na kwamba, hata kama ni utekelezaji wa sheria, unatakiwa kutumia busara zaidi.

Alisema kinachomuumiza ni jeuri ya waziri huyo kwa viongozi wake na kwamba, semina elekezi inayomalizika Dodoma leo ilitakiwa imwelekeza kuacha malumbano na Rais na Waziri Mkuu.

“Magufuli ni rafiki yangu, lakini amekuwa mbabe mno, anachonganisha serikali ya CCM na wananchi bila sababu yoyote. Analeta chuki ndani ya jamii kwa kuweka alama za X,” alisema.

Kimaro alisema Dk Magufuli ametumia mabilioni ya shilingi kutengeneza vigingi vya mipaka ya barabara, hivyo waliopo ndani ya hifadhi wanatambua na wale wanaostahili kulipwa lazima haki itendeke pindi ujenzi wa barabara utakapoanza.

“Kitendo cha kuweka alama X nchi nzima ni uchafu, hizo rangi zilizotumika ni ubadhirifu wa fedha za serikali. Ameweka alama X hata vibao vinavyoelekeza shule, umbali havitaki kwa sababu vinaendana na tangazo, ingawa alitakiwa aviweke yeye (Magufuli),” alisema na kuongeza:

“Fedha alizotumia angezitumia kufyeka majani pembeni mwa barabara. Amefika sehemu amejenga jeuri, anakaidi Waziri mkuu wake, rais karudia Magufuli acha ubabe, kitendo cha kuendelea kuonyesha dharau ya maagizo ya wakubwa zake, kinakwenda kinyume na uwajibikaji wa pamoja wanaofundishwa Dodoma.”
TP Mazembe yatolewa, Simba kusonga mbele
Mabingwa watetetezi wa Klabu Bingwa Afrika TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imeondolewa katika michuano ya klabu bingwa Afrika.TP Mazembe


Shirikisho la Soka barani Afrika Caf limechukua hatua hiyo kufatia malalamiko ya Simba ya Tanzania kuhusu kuchezeshwa kwa Janvier Besala Bokungu.

Mazembe iliichapa Simba 6-3 katika mechi mbili walizocheza.

Simba sasa itapambana na Wydad Casablanca ya Morocco, ambayo ilifungwa na Mazembe katika raundi ya tatu, kupata nafasi ya katika ngazi ya makundi.

Simba na Wydad casablanca watakutana katika uwanja utakaotangazwa wiki ijayo.

Mazembe imeshinda ligi ya mabingwa Afrika kwa miaka miwili iliyopita, na kufika fainali ya klabu bingwa ya Dunia mwaka jana, na kutolewa na Inter Milan ya Italia kwa mabao 3-0


Tatizo la watoto kukataa Dawa za ukimwi
Utafiti wa kwanza kufanywa kuhusu dawa ya kinga ya ukimwi miongoni mwa vijana wanaoishi na virusi vya ukimwi imeonyesha kuwa mwili wa mtoto 1 hadi 8 anaweza kuwa sugu dhidi ya dawa muhimu zilizotengenezwa kwa ajili ya kupunguza makali ya virusi vya ukimwi.

Utafiti huo ulichunguza hali za watoto 1000 kote barani Ulaya. Wataalamu wanasema kuwa mojapo ya matatizo nyeti ni ladha ya dawa, ambayo inaweza kuwachukiza wagonjwa na kukwepa kuitumia kama wanavyohitajika kufanya.

Tiba kuu ya ukimwi ni dawa ijulikanayo kama antiretroviral. Mchanganyiko wa dawa hizi hutumika kwa kupunguza kiwango cha makali ya virusi vya ukimwi mwilini. Hilo husaidia kwa kumpunguzia mgonjwa hali ya kudhoofika na kumsaidia kupata nafuu ya athari nyingine zinazosababishwa na ukimwi.

Kwa utafiti huu pekee Madaktari wa Baraza la utafiti wa matibabu nchini Uingereza walichunguza watoto kutoka nchi nane za Ulaya ikiwemo Uhispania,Ireland na Uholanzi.

Utafiti wao uligundua kwamba 1 kati ya watoto 8 alikuza kikwazo cha mwilini dhidi ya dawa aina tatu zilizopo kwa ajili ya vijana, waliotumia dawa hizo kwa kipindi cha miaka mitano idadi kubwa kuliko miongoni mwa watu wazima.

Utafiti huu unazua masuali juu ya ubora wa dawa hizi kwa watoto hao wanaoishi na virusi na ukimwi. Virusi vinaweza kuwa sugu kwa dawa ikiwa mgonjwa hatotumia dawa kwa kila siku - mara nyingi kwa siku kwa maisha yake yote.

Wataalamu wanaoendesha utafiti huu wanadokeza kuwa ni kazi kubwa kuwashawishi watoto na wavulana kuendeleza tabia ya kutumia dawa zenye ladhaa inayochukiza.

Kutokana na utafiti huo wataalamu hawa wameyataka makampuni yanayotengeneza dawa pamoja na wachunguzi wa ubora wa dawa wajitahidi kutengeneza dawa nyembamba, rahisi kutumia bila ya kuwa na ladhaa ya kuchukiza. Wanahisi kuwa hili huenda likasaidia kunusuru maisha ya watoto milioni 2 wanaoishi na maradhi ya ukimwi kote duniani.
Israel imeuzingira ukingo wa magharibi mnamo wakati huu wa Nakba

Jerusalem:

Jeshi la Israel limeuzingira Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kwa hofu ya kutokea mashambulio ya wafuasi wa itikadi kali wa Kipalastina.Kwa mujibu wa jeshi,wanaokwenda kwa ajili ya kufanya matibabu tu au kwa ajili ya huduma za kiutu ndio watakaoruhusiwa kuingia Israel.Chanzo cha hali hiyo ni Nakba,siku ya balaa ambayo Wapalastina wanakumbuka kila mwaka jinsi walivyotimuliwa na kulazimika kuyapa kisogo maskani yao,taifa la Israel lilipoundwa mnamo mwaka 1948.Kupitia mtandao wa Internet,Wapalastina wametoa mwito wa kuandamana hii leo dhidi ya Israel.Mkutano mkubwa wa hadhara unapangwa kuitishwa hii leo huko Ramallah.Huko Gaza ,Wapalastina wanapanga kuandamana hadi katika eneo la mpakani lililozungushwa senyen'ge na Israel.Nchini Misri,mabasi yameshawekwa tayari katika uwanja wa Tahrir mjini Cairo kuwasafirisha waandamananji hadi Rafah-ujia wa mpakani kati ya Misri na Ukanda wa Gaza
Mauaji ya Wagalla

Kwa kipindi kirefu koo za Ajuran na Degodia kutoka jamii ya wasomali wamekuwa wakizozana, kuhusu masuala tofuati ikiwemo malisho na maji ya mifugo.
Ramani ya KenyaWakati wa makabiliano hayo silaha nzito nzito zilikuwa zikitumika.

Hali ambayo ilitatiza serikali ya Rais Daniel arap Moi wakati huo, kutokana na utovu wa usalama katika eneo hilo la kaskazini mwa Kenya kwenye mpaka na Somalia.

Silaha haramu

Kufuatia hali hiyo serikali ilianzisha mikakati ya kuwapokonya raia silaha katika eneo hilo la Wajir. Jamii ya Ajuran walitii amri lakini wenzao wa Degodia wakakaidi.

Wiki hiyo ilioanza Februari tarehe 10 mwaka 1984, vikosi vya usalama likiwemo jeshi, viliingia wilaya ya Wajir kufuatia shambulio kwenye kijiji kimoja. Kwenye harakati hizo za kutafuta silaha haramu, wanaume, vijana na wanawake wengine wakiwa wamebeba watoto wao mgongoni, walitiwa nguvuni na kusafirishwa kwenye malori ya jeshi hadi kwenye uwanja wa Wagalla.

Kulala uchi

Wakiwa kwenye uwanja wa ndege wa Wagalla, baada ya kukataa au kushindwa kuwaelekeza maafisa wa uslama palipo silaha. Mateso yalianza. Waume na wake waliamrishwa kuvua nguo na kulala uchi kwenye uwanja huo.

Walitembezewa kichapo kwa kipindi cha siku tano, bila chakula wala maji licha ya viwango vya joto kuwa juu kupita kiasi cha kawaida. Walionusurika walilazimka kunywa mikojo yao.

Mateso yalipozidi baadhi walijaribu kutoroka ndipo wakapigwa risasi. Miili ya waliouawa ikatupwa kwenye msitu, ili iliwe na wanyama pori, kulingana na wakaazi wa Wajir lengo lilikuwa kuficha ushahidi wa tukio hilo.

Msamaha

Kufikia leo hakuna aliyehusika amechukuliwa hatua na wala haijulikani aliyetoa amri maafa hayo yatendeke. Je rais ndiye aliyeamrisha au ulikuwa uamuzi wa wakuu wa usalama waliokuwa na hamaki ya kuonyesha wamefanya kazi?

Jibu hilo ndio tume hii ya haki na maridhiano inajukumu la kutafuta, baada ya hapo ipendekeze msamaha kwa wale watakao kiri makosa waliotenda au kufunguliwa mashataka kwa wale itakaopata ushaidi wa kutosha dhidi yao.Vyuo Vikuu Afrika havitambuliwi


Chuo kikuu cha Khartoum
Kuorodhesha vyuo vikuu kulingana na umaarufu ni desturi inayokua kwa kasi sana katika sekta ya elimu ya juu.

Orodha hiyo, inayojumuisha vyuo vikuu vilivyo maarufu zaidi duniani, ina walakini kwani bara zima halimo.

Hutapata hata chuo kimoja kutoka bara la Afrika kwenye orodha hiyo.

Vyuo vikuu vilivyoorodheshwa ni vya Marekani, Ulaya na baadhi kutoka China na Korea Kusini huku Afrika ikiwa imesahaulika.

Mazungumzo yanayohusu utandawazi wa vyuo vikuu yanatumia lugha ya kuvutia iliyorembwa kwa mada ya ushirikiano wa kimataifa, pamoja na mzunguko wa fedha katika mitandao ya kimataifa.

Ni rahisi sana kupotoshwa na mafanikio ya vyuo hivi ambavyo mazoea ni kuwatunukia watu tuzo na kujionyesha.

Swali ni, ikiwa ushindani wa kimataifa wa vyuo hivi utajikita katika hadhi na uwezo wa vyuo vichache, na hivyo basi bara zima likasahaulika, mambo yatakuwa vipi?
Idadi yaongezeka

Kwa mujibu wa taasisi ya takwimu ya shirika la elimu, sayansi, na utamaduni la Umoja wa Mataifa, kuna wanafunzi milioni 4.5 kusini mwa jangwa la Sahara.

Kulingana na orodha hiyo, wanafunzi hawa kutoka bara la Afrika ni kama hawapo.Bw Thandika Mkandawire
Lakini idadi hii inawakilisha kuwepo kwa ongezeko kubwa. Mwaka 1970, idadi ya wanafunzi Ilikuwa 200,000 katika eneo hilo la Afrika na sasa idadi ya vijana wanaojiunga na chuo kikuu imeongezeka kutoka aslimia moja hadi sita.

Katika takwimu hizi kuna tofauti kubwa zinazojitokeza. Nchini Malawi, takriban asilimia 0.5 ya vijana watajiunga na chuo kikuu wakati Cameroon kiwango kimefikia asilimia tisa.

Pia kuna mienendo tofauti kwa wale wanaoamua kusomea ng'ambo.

Wanafunzi wanaotoka kusini mwa jangwa la Sahara wengi wao husomea nchi za Afrika Kusini na Ufaransa.

Pia wanafunzi kutoka Afrika Kaskazini huenda kusomea Ufaransa.

Tatizo lingine ni kwamba wanawake kutoka bara la Afrika huwa hawajiungi na chuo kikuu kwa wingi.

Ukilinganisha idadi ya wanawake na wanaume katika vyuo vikuu, idadi ya wanaume ndio kubwa zaidi.

Nchini Chad - nchi iliyo kubwa zaidi kushinda nchi za Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zikijumuishwa pamoja - asilimia 0.6 pekee ya wanawake ndio wanaojiunga na chuo kikuu.

Ingawa idadi ya wanafunzi kuongezeka barani Afrika ni jambo zuri, hii itaathiri mambo mengine pia.

Kwa mujibu wa Benki Kuu ya Dunia, ongezeko la idadi ya wanaojiunga na chuo kikuu imeongezeka mno hata kuzidi uwezo wa kifedha wa vyuo hivyo kuajiri wafanyakazi na kununua vifaa.
Mwelekeo tofauti wa ufadhili

Profesa Thandika Mkandawire, mkufunzi wa maendeleo barani Afrika 'African Development' katika chuo kikuu cha LSE alisema, vyuo vikuu vya Afrika bado vinajaribu kurudi katika hali yake kutokana na kukosa ufadhili miaka ya 80 baada ya fedha hizo kuhamishwa kwenye shule za msingi.

Katika enzi za baada ya ukoloni kwenye miaka ya 60 na 70, vyuo vikuu vingi viliibuka barani Afrika lakini hali hii ilisitishwa ghafla. Na wakati maeneo mengine duniani yalikuwa yakiwekeza kwenye elimu ya juu, bara la Afrika lilikosa fursa hiyo.

Profesa Mkandawire alisema "Ukishaangamiza chuo kikuu, ustawishaji wa chuo hicho tena utakuwa si rahisi."Waandamanaji wadai uwekezaji kwenye elimu

Huenda itakuwa vigumu sana kujaribu kukaribia vipimo vya maendeleo vilivyoko katika vyuo vikuu vingine duniani baada ya 'miaka mingi' iliyopotezwa.

Prof Mkandawire alisema, watu wenye kipato cha kawaida wanajitahidi kushinikiza kuwepo kwa vyuo bora zaidi ili ijadiliwe kwenye duru za kisiasa.

Pia kuna ufahamu kuwa vyuo vikuu ni sekta mojawapo iliyo muhimu katika kuujenga uchumi wa kisasa.

Jo Beall, makamu mkuu wa chuo kikuu cha Cape Town Afrika Kusini (chuo pekee kutoka Afrika kuwa miongoni mwa vyuo vikuu 200 vilivyo bora) alisema "Vyuo vikuu ndio pahala panapo fursa ya kujipandisha katika tabaka za kijamii."
Rasilmali yaadimika


Bi Beall alielezea jinsi alivyoona barabara za kuelekea chuo kikuu kimoja Afrika ya kati zikiwa zimejaa foleni za watu wakiwa na mashine ya kupiga chapa ili kutoa huduma kwa wanafunzi, zikiwa zinaendesha na betri za gari, wakiwa wananakili vitabu vya miaka ya 50.

Wanafunzi hulazimika kusafiri kwa saa tatu au nne ili kufika chuo kikuu.Wasiwasi wa kisiasa umekuwa kikwazo kwa uwekezaji barani Afrika.


Isitoshe, ukumbi wa mihadhara hujaa kupindukia hadi kuna walinzi na lango la kudhibiti msongamano wa watu.

Profesa Beall ambaye atajiunga na taasisi ya 'British Council' baadaye mwaka huu alisema, licha ya hayo, bado ana matumaini kuhusu mustakabali wa mfumo wa elimu ya juu Afrika.

Kuna vyuo vikuu vinavyojitahidi kuwa taasisi zinazojishughulisha na utafiti wa hali ya juu.

Phillp Altbach, mkurugenzi wa 'Centre for International Higher Education Boston College' Marekani alisema udhaifu wa vyuo vikuu barani Afrika haitokani tu na ukosefu wa fedha bali kuna kasoro kadha wa kadha ikiwa ni pamoja na msukosuko wa kisiasa na ubadhirifu wa mali.
Kushindwa kuvutia

Soko la wanafunzi kutoka nje halijafanikiwa kuwavutia wanafunzi kwenda barani Afrika. Badala yake, wasomi wamelihama bara hilo kwenda kuishi ng'ambo.Chuo kikuu Tunis
Vyuo vikuu vya Marekani na Uingereza vimewekeza katika matawi ya vyuo vyao barani Asia na Mashariki ya kati badala ya Afrika.

Pia Afrika, ambapo utajiri mkubwa sana na umaskini uliokithiri, umekosa watu wenye uwezo wa wastani Afrika hawana ushawishi kama wale wanaoishi nchi za China na India ambako wamechochea ustawishaji wa elimu ya juu nchini mwao.

Pamoja na uwekezaji wa fedha, alisema kunahitajika mabadiliko ya kitamaduni kama vile kulinda uhuru wa kitaaluma ili kuweka hali itakayoimarisha vyuo vikuu.

Lakini hakuna kuepuka pengo la kiuchumi.

Aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair ameunda wakfu inayofanya kazi na mtandao wa vyuo vikuu duniani kote, ikiwemo Afrika na Marekani.

Alisema chuo kikuu cha Yale, Marekani si tu kwamba kina uwezo mkubwa kifedha na chuo kama cha Fourah Bay College Sierra Leone - mali iliyowekwa wakfu ya Yale ni mara chungu nzima zaidi ya utajiri wa nchi nzima.

Ruth Turner mkurugezi mkuu wa wakfu hiyo alisema tofauti hii illiopo kwa sasa haitokani na hali ya uchumi tu bali kunahitajika kuliangalia suala hili kwa misingi ya maadili.

"Sote tunaishi katika dunia ya utandawazi lakini tunakosa namna ya kujadili tatizo hili tukizingatia maadili."Maendeleo ya kiuchumi

Katika utandawazi duniani, vyuo vikuu vyenye uwezo vinaonekana kunufaika zaidi na vile vilivyo maarufu zaidi.Chuo kikuu cha Free State
Vyuo vikuu vilivyo katika mstari wa mbele ni "taasisi za kimataifa. Vyuo hivi vinaweza kuwavutia wakufunzi waliobobea na vina uhusiano na sekta ya biashara pamoja na kuwa na ushawishi uliovuka mipaka" alisema Keith Harman ambaye anafanya kazi kwenye mradi unaofadhiliwa na jumuiya ya madola kuendeleza vyuo vikuu nchini Uganda ili kuwavutia wanafunzi wa Afrika mashariki na kusini.

Kwa upande mwingine, vyuo vikuu vingi barani Afrika ambavyo havina uhusiano kama huo "manufaa ya utandawazi "

"Vyuo vikuu ni misingi muhimu ya kuwaleta watu waliostadi na pia vina umuhimu katika kuleta maendeleo ya kiuchumi" alisema Bw Harman lakini vyuo vingi Afrika vinapoteza fursa ya kupanda daraja kwani havijafanikiwa katka uwekezaji na utafiti zaidi, pamoja na uwezo wa kuwavutia wanafunzi kutoka ng'ambo.

Profesa Makandawire alisema hata hivyo, kuna dalili za kuwepo na matumaini. " Kuna mabadiliko, mambo yanakuwa wazi zaidi ; ukandamizaji umepungua."

Alisema pia kuna ufahamu kuwa kusitisha uwekezaji katika vyuo vikuu ilikuwa ni makosa ambayo sasa yanarekebishwa.

Aliongezea "Kuna matokeo mazuri ambayo yanayojitokeza" lakini alitoa ilani kuwa maendeleo yatachukua miaka mingi ya kazi ngumu.


Makinda azuia watu kutumia barabara
SPIKA wa Bunge, Anne Makinda anadaiwa kufunga njia inayounganisha eneo la Kijitonyama na Sinza, Dar es Salaam na kusababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji.Habari zilizolifikia gazeti hili jana na kuthibitishwa na baadhi ya wakazi wa sehemu hiyo zimeeleza kuwa kutokana na kufungwa kwa njia hiyo, sasa wanalazimika kutumia dakika 45 kufika Sinza kwa miguu badala ya dakika tano hadi 10 walizokuwa wakitumia awali.

Mkazi wa eneo hilo, Juma Mbegu alieleza kuwa njia hiyo imefungwa katika Mtaa wa Sahara, jirani na Kituo Kidogo cha Polisi cha Mabatini: "Njia hiyo imefungwa eti kuruhusu ujenzi wa nyumba yake ya ghorofa moja. Unajua mtu hadi agundue kuwa njia hiyo imefungwa, inambidi atembee kama dakika tano hivi ndipo akutane na uzio wa mabati."

Kwa mujibu wa Mbegu, kibao kilichowekwa mwanzoni mwa Mtaa wa Sahara jirani na Kituo hicho cha polisi kuonyesha kuwa barabara imefungwa, nacho kina utata kwani watu wengi wanajua kuwa imefanyika hivyo kwa magari pekee. Alisema kufungwa kwa njia hiyo inayopita jirani na Kiwanja namba 630 katika Kitalu namba 47, kinachomilikiwa na Makinda, kumesababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi wa eneo hilo na vitongoji vyake.

Mkazi mwingine ambaye hakutaka kutajwa gazetini alisema kutokana na kufungwa kwa njia hiyo, watu wanalazimika kuzunguka hadi Barabara ya Shekilango eneo la Afrika Sana, ili kufika eneo la Mori, mwendo ambao ni takriban dakika 45.

Kauli ya uongozi wa Mtaa
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kijitonyama, Philip Komanya alipoulizwa jana kuhusu suala hilo alisema hana taarifa ya kufungwa kwa njia hiyo."Sina taarifa na ndiyo kwanza nasikia kwako. Mbona hawajanifahamisha?" alihoji mwenyekiti huyo na kuongeza:"Njia hiyo imekuwa ikitumika pia wakati wa mvua kwani njia inayounganisha ile inayopita katika Kituo Kidogo cha Polisi Mabatini, huwa haipitiki kutokana na ubovu."

Mwenyekiti huyo alisema anachojua ni kuwa Mei mwaka jana, wakazi wa eneo hilo kwa kumtumia Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wao, Athanas Mapunda waliwasilisha maombi ya kutaka kufungwa kwa njia hiyo kwa sababu za kiusalama, ombi ambalo hata hivyo, lilikataliwa.

"Walileta ombi la kutaka hilo lifanyike lakini kikao cha kamati ya maendeleo ya kata kilikataa ombi hilo kwa sababu ni njia pekee katika eneo hilo ambayo inaunganisha maeneo mawili tofauti," alisema.
Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, aliwashauri watafute jinsi ya kufanya ikiwa ni pamoja na kuweka lango la kuingilia katika mtaa huo na walinzi.

"Pia nilishauri waweke muda wa kupita kwa watu wote na muda wa kupita wenyeji tu. Niliwaambia waweke geti, walinzi na waaandike muda wa mwisho kupita kwa watu wa kawaida lakini siyo kufunga njia."

Mwenyekiti huyo aliahidi kufika katika eneo la tukio kujionea kinachoendelea akieleza kuwa kisheria, kabla ya kufunga barabara hiyo, mmiliki alipaswa kuwasiliana na ofisi yake.

"Ngoja nifike hapo baadaye nitakupigia. Unajua wakati mwingine kuna watu huwa wanatumia njia za mkato kwenda manispaa kuomba vibali bila kushirikisha mamlaka nyingine halali. Huu ni ukiukwaji wa utaratibu na ni kinyume kabisa na misingi ya utawala bora."

Kauli ya Spika
Spika Makinda alipigiwa simu kutoa ufafanuzi wa madai hayo. Hata hivyo, mara baada ya mwandishi kujitambulisha kwake na kabla ya kumweleza lolote alisema: "Naomba niacheni kwanza. Wasiliana na katibu, tafadhali sana."

Alipodokezwa kuwa suala lenyewe halihusu ofisi yake, bali yeye binafsi tena ni kuhusu kudaiwa kufunga barabara na kusababisha usumbufu kwa wakazi wa eneo hilo, alikata simu.Baadaye Msaidizi wa Spika, Herman Berege alipiga simu na kukiri kufungwa kwa barabara hiyo akisema hatua hiyo imefikiwa kwa sababu za kiusalama na bosi wake alifuata taratibu zote.

Alisema Makinda alipeleka maombi ya kufanya hivyo katika Manispaa ya Wilaya ya Kinondoni ambako kwa kuwashirikisha maofisa wa mipango miji na watendaji wengine, walikubali kuifunga njia hiyo. Alipoelezwa kauli ya mwenyekiti wa mtaa kwamba maombi hayo yalipelekwa kwenye Kamati ya Maendeleo ya Kata lakini yakakataliwa, msaidizi huyo wa Makinda alisema si kweli.

"Tulikwenda na hadidu za rejea za kikao kilichopitisha uamuzi wa kufungwa kwa njia hiyo na makubaliano yalikuwa ama yawekwe matuta, ziwekwe nguzo kuzuia magari au uzio. Barabara hiyo ilikuwa lazima ifungwe kuzuia vitendo vya uhalifu."Alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya Spika Makinda kutaka aishi nyumbani kwake awapo Dar es Salaam badala ya kukaa hotelini kwa gharama za Serikali.

"Lengo la mheshimiwa ni zuri tu, kunusuru pesa ya Serikali ambayo ingetumika kulipia anapoishi," alisema na kuongeza:"Alikopa kutoka taasisi tofauti ili kujenga nyumba hiyo na kulingana na hadhi yake, watu wa usalama waliona kuna haja ya kuifunga njia hiyo."
"Nasisitiza kwamba utaratibu ulifuatwa na kama manispaa hawajaifahamisha serikali ya mtaa, hilo si kosa lake (Spika)."

No comments:

Post a Comment