KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Monday, May 16, 2011

Mkuu wa Benki Kuu ya Ulaya asema hakuna mgogoro wa Euro
Mkuu wa Benki Kuu ya Ulaya, Jean-Claude Trichet, amekanusha kwamba sarafu ya Euro iko kwenye mgogoro licha ya kuwepo kwa matatizo ya madeni katika baadhi ya mataifa yanayotumia sarafu hiyo.

Katika makala yake kwa gazeti la Bild am Sonntag la hapa Ujerumani, Trichet amesema kwamba sarafu ya Euro imefanikiwa kukiweka kiwango cha ushukaji thamani katika eneo inamotumika kuwa chini ya asilimia mbili kila mwaka kwa kipindi cha miaka 12 tangu kuanzishwa kwake.

Hata hivyo, Trichet ameonya kwamba mataifa yote yanayotumia sarafu ya euro yanapaswa kudumisha misingi ya sera madhubuti za kifedha.

Katika toleo hilo hilo, gazeti la Bild am Sonntag limechapisha ripoti inayoonesha kuwa 58% ya Wajerumani sasa hawaiamini tena sarafu ya Euro, likiwa ni ongezeko la asilimia nne tangu mwezi Disemba mwaka jana.

Watu 27 wauawa katika mauaji ya maangamizi Guatemala
Kwa mujibu wa polisi nchini Guatemala, watu 27 wameuawa katika mauaji ya maangamizi kwenye mkoa wa kaskazini ya nchi hiyo unaoendeshwa na wafanyabiashara wa madawa ya kulevya.

Watu hao, wanaume 25 na wanawake wawili, waliuawa baada ya watu wenye silaha kuuvamia mji wa Saserio La Bomba kwenye jimbo la Peten.

Mamlaka za Guatemala zinasema zinachunguza ikiwa mauaji haya yana uhusiano na kuuawa kwa Haroldo Leon hapo Jumamosi.

Leon ni kaka wa mfanyabiashara mkubwa wa madawa ya kulevya nchini humo, Juan Jose Leon, ambaye aliuawa mwaka 2008 na kundi la madawa ya kulevya la Mexico la Zetas


Muhudumu wa kike amtambua Strauss-Kahn kuwa mkosaji wakeKatika maendeleo ya karibuni zaidi ya kesi inayomkabili Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Dominique Strauss-Kahn, anayetuhumiwa kujaribu kumbaka mhudumu wa hoteli moja jijini New York, polisi imesema kwamba mhudumu huyo wa kike ameweza kumtambua Strauss-Kahn kwamba ndiye mwanamme aliyetaka kumuingilia bila ya ridhaa yake.

Mashitaka haya ya shambulio la aibu, yanamuingiza kiongozi huyo wa IMF kwenye mgogoro wa kiuongozi katika wakati ambapo Shirika hilo likijaribu kusaidia kutatua mgogoro wa kifedha unaoendelea katika eneo linalotumia safaru ya Euro.

Sasa IMF imemteua msaidizi wa Strauss-Kahn, John Lipsky, kukaimu nafasi ya meneja mkurugenzi.

Polisi ya New York imesema Strauss-Kahn hana kinga ya kibalozi inayozuia kutoshitakiwa. Endapo atatiwa hatiani, mwanasiasa huyo wa Ufaransa anakabiliwa na kifungo cha kati ya miaka 15 na 20 jela.

Kesi yake iliyokuwa itajwe jana imeahirishwa hadi hivi leo na mwanasheria wake amesema kwamba mteja wake angelikana mashitaka dhidi yake.


IMF warns that crisis threatens democracyThe managing director of the International Monetary Fund (IMF), Dominique Strauss-Kahn, said that the world is immersed in a crisis of ‘extreme gravity’ and that it will not recover until the financial systems have been ‘cleaned.’ “To be frank, the situation is extremely serious,” he admitted at a meeting in Geneva organized by the International Labor Organization (ILO).

Strauss-Kahn warned that the current crisis can drag into poverty and unemployment of millions of people worldwide, bringing the risk of social unrest and even war. Hence, there is a demand for urgent action to combat the current crisis.

“This dramatically affects employment, and even beyond. For many countries, this could represent the root of social unrest and threats to democracy. In some, it could lead to war,” Strauss-Kahn warned.

The IMF believes, however, that there exists the possibility of achieving a recovery by 2010 if decisions are urgent and coordinated internationally.

Moreover, world trade in 2009 will fall by 9 percent due to the crisis. This shall be the biggest decline since World War II, according to a report released by the World Trade Organization (WTO).

”The contraction in developed countries will be particularly severe, and a fall in exports of 10 percent,” the report said. For developing countries, the decline will be from 2 to 3 percent

No comments:

Post a Comment