KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Sunday, May 8, 2011

Raha ya Kufumaniwa Kwenye Danguro
Mwanaume huyu wa nchini China amekuwa maarufu duniani kufuatia kusambazwa kwa picha zake online wakati akihatarisha maisha yake kwa kujaribu kushuka toka ghorofani akiwa uchi wa mnyama akiwakimbia polisi waliovamia danguro alilokuwa akijisevia uroda.
Mwanaume huyo alinaswa live akijaribu kushuka toka ghorofani kwa kuparamia mabomba na machuma yaliyojitokeza kwenye ghorofa hilo.

Mwanaume huyo akiwa uchi wa mnyama alikuwa akijaribu kuwatoroka polisi waliolivamia danguro ambalo mwanaume huyo alikuwa ndani akijisevia uroda toka kwa machangudoa.

Picha za tukio hilo zilipigwa kwa kutumia simu na mwanafunzi wa sekondari aliyekuwa akikatiza mitaa hiyo akienda kwa rafiki yake.

"Nilihofia nyeti zake zinaweza kuungua kutokana na msuguano wakati alipokuwa akishuka kwa kutumia bomba la maji taka lenye kutu", alisema mwanafunzi huyo.

Serikali ya China imeweka sheria kali za kutokomeza ukahaba ambapo miongoni mwa adhabu zinazotolewa ni adhabu ya kifo kwa mtu anayeuza wanawake kwaajili ya ukahaba

Ghasia za kidini zinazuka tena MisriWaziri Mkuu wa Misri, Essam Sharaf, amevunja safari ya kuzuru nchi za Ghuba baada ya ghasia kati ya Waislamu na Wakristo, zilizouwa watu kama sita.

Hii ilikuwa ziara muhimu kwa Waziri Mkuu, katika nchi za Ghuba ambazo zingeweza kutoa msaada anaohitaji sana, na nchi ambazo piya zina wasi wasi juu ya mwelekeo wa mapinduzi ya Misri.

Kwa kuvunja safari hiyo, Bwana Sharaf anaonesha anashughulishwa na ghasia nyengine zilizozuka baina ya makundi ya Waislamu na Wakristo.

Safari hii ghasia zimetokea kwenye mtaa wa kati-kati ya Cairo, pale kundi la Waislamu wa madhehebu ya Sunni, wanaoitwa Salafi, ambao hawapendi mabadiliko, lilipozingira kanisa ambamo likiamini Wakristo walikuwa wakimzuwia mwanamke, ambaye akitaka kubadilisha dini na kuwa Muislamu.

Risasi zilifyatuliwa, na kanisa na majengo mengine yalichomwa moto.

Ilichukua saa kadha kwa askari wa usalama kuzima mapigano.

Inafikiriwa kuwa Salafi ni wachache kati ya Waislamu, lakini wamekuwa na ghasia nyingi tangu Rais Hosni Mubarak kuondoka mwezi wa Februari.

Tangu wakati huo, kumetokea mapambano kadha baina ya Wakristo na Waislamu, na Wakristo wengi, ambao ni asili mia 10 ya watu wa Misri, wanahofia usalama wao, endapo makundi ya Waislamu wasiopenda mabadiliko, ndio yatashinda katika uchaguzi wa mwezi Septemba.Besigye kurudi UgandaBwana Besigye aliiambia BBC kwamba atarudi nyumbani na kuendelea kutembea kwa miguu hadi kazini kuonesha malalamiko juu ya kupanda kwa bei za bidhaa.Kizza Besigye


Kiongozi wa upinzani wa Uganda, Kizza Besigye, alizungumza jana kutoka Kenya ambako amekuwa akitibiwa macho yaliyodhurika wakati askari wa usalama wa Uganda walipompulizia gesi ya pili-pili.

Bwana Besigye alisema hana budi kurudi Uganda.

Na mshauri wa rais katika mawasiliano na vyombo vya habari, John Nagenda, anasema ni salama kwa Bwana Besigye kurudi Uganda iwapo hatochochea ghasia.

"Hakika atakuwa salama. Lakini ikiwa ataendelea kufanya kama yale aliyofanya; na ameshawahi kusema kuwa ataifanya Uganda isiweze kuongozwa...ikiwa hiyo ndio azma yake, basi atazuwiwa", aliongeza
Wataja sababu za Obama kutakaa kumuonyesha hadharani Osama


MSIMAMO wa Rais Barack Obama wa Marekani, kuzuia kuonyeshwa hadharani kwa picha za mwili wa Kiongozi wa Al Qaeda, Osama bin Laden, aliyeuawa mapema wiki hii nchini Paskatani, umesukumwa na sababu nane, imeelezwa.

Jana, Gazeti la The Monitor la Uingereza, liliorodhesha sababu hizo zilizoelezwa kuwa zimetokana na uchunguzi wa timu ya waandishi wake wa habari.

Uchunguzi huo unafautia msimamo wa Obama wa kutorohusu picha hizo, kuonyeshwa hadharani kama inavyoshinikizwa na watu wengi duniani .
Kwa mujibu wa gazati hilo, sababu hizo pamoja na kuhofia kuchochea hasira za waumini wa dini ya Kiislamu duniani, kuwachukia Wamarekani, kwa sababu hawako radhi kuona sura ya maiti.

Sababu nyingine ni sheria za adhabu za vifo nchini Marekani, inakataza uonyeshaji wa picha za watu waliouawa katika kutekeleza adhabu.

Pia imeelezwa kuwa jaribio lolote la kuonyesha picha hizo hadharani, litachochea zaidi vitendo vya ugaidi na baada ya kuonyesha kwa vitendo vya kikatili wanavyowafanyiwa mateka wa mtandao wa kigaidi.

Kulingana na gazeti hilo la Uingereza, sababu nyingine ya Marekani kukataa kuonyesha picha ni wafuasi wengi wa mtandao wa Al Qaeda, kukataa kuambiwa ukweli kuwa bin Laden amekufa.

Lakini pia uonyeshaji wa picha ya mtu aliyeuawa, unakiuka maadili yanayokataza watoto kuonyeshwa picha za aina hiyo.

The Monitor ilitaja sababu nyingine kuwa mwili wa Osama hauwezi kufananishwa na bidhaa ama kitu muhimu cha maonyesho. Jambo la msingi katika tukio hilo ni tabia yake mbaya ambayo ilikuwa ni ya kuua watu wasio na hatia ili kuridhisha nafsi ya chuki zake dhidi ya watu wengine.

Sababu ya saba, imeleezwa kuwa ni Marekanikuweka nguvu zaidi katika malengo ya kuudhofisha watu wengine wenye mikakati kama ya Osama.

Hali kadhalika Wamarekani kuamini kuwa kuna kasi kubwa ya watu katika nchi za Kiarabu, kumchukia bin Laden kutokana na tabia yake na kwa hiyo hakuna sababu ya kuendelea kuwaonyesha picha yakeWakristo Inabidi Wamsalie Osama

Wakristo inabidi wasali kumuombea makazi mema peponi Osama bin Laden ingawa alikuwa ni adui wao kwakuwa kutoa msamaha ndio mafundisho ya biblia.
Ingawa Osama alikuwa ni adui wa wakristo, wakristo inabidi wasimame kusali na kumuombea makazi mema Osama bin Laden.

Hayo yalisemwa na kardinali Albert Vanhoye mwenye umri wa miaka 87 wa kanisa katoliki nchini Italia ambaye alisema kuwa mafundisho ya biblia yanafundisha kusameheana.

"Mimi nimeusalia mwili wa Osama bin Laden, inatubidi tumuombee dua njema kama tulivyowaombea wahanga wa shambulio la septemba 11, hivyo ndivyo Yesu anavyowafundisha wakristo", alisema Kardinali Vanhoye.

"Yesu ametutaka tuwasamahe maadui zetu, tunaposali huwa tunasema "Baba, tusamehe kwa yale tuliyoyatenda kama vile tulivyowasamehe watu kwa yale waliyotutendea".

"Sala hii haiwezi kukubalika kama bado tutaendelea kuweka chuki kwa maadui zatu", alisema Kardinali Vanhoye, ambaye alichaguliwa kuwa Kardinali na Pope Benedict XVI mwaka 2006.

Kardinali Vanhoye anatambulika sana kwa mafundisho yake kuhusiana na biblia
Sababu za kumfukuza balozi wa UingerezaRais wa Malawi Bingu wa Mutharika ameeleza sababu ya kumfukuza balozi wa Uingereza mwezi uliopita.
Bingu wa Mutharika


Katika taarifa yake ya mwanzo hadharani kuhusu ugomvi huo Rais Mutharika alisema Balozi Fergus Cochrane-Dyet

alimtusi na hayuko tayari kukubali hayo eti kwasababu Malawi inapata msaada wake mkubwa kabisa kutoka Uingereza kushinda nchi nyengine.

Magazeti yalichapisha barua iliyofichuliwa ambamo Balozi Cochrane-Dyet alimuelezea Rais Mutharika kuwa anaongoza kimabavu na hakubali kukosolewa.

Uingereza ilimtaka balozi wa Malawi aondoke London kujibu kufukuzwa kwa Bwana Cochrane-Dyet kutoka Malawi.

Malawi ilimfukuza Cochrane-Dyet baada ya nyaraka za kisiri kufichuliwa ambazo zilikuwa zikitumwa kwa waziri wa mambo ya nje ya nchi wa Uingereza, William Hague, na kuwafikia waandishi habari.

Baada ya tukio hilo Ofisi ya mambo ya nje na jumuiya ya madola, FCO, mjini London ilimuamuru balozi wa Malawi Flossie Gomile-Chidyanga kuondoka Uingereza.

Uingereza hutuma paundi milionii 93 kwa Malawi kwenye mfuko wa msaada kwa nchi zinazooendelea na Malawi ni nchi inayopokea kiasi kikubwa cha msaada wa fedha.

Wakimbizi zaidi ya 400 waokolewa
Wakimbizi hao walikuwa kwenye boti iliyogonga mwamba katika kisiwa cha Lampedusa na watawasili Lampedusa tarehe 8 Mei walinzi wa mwambao walisema.Boti ya wakimbizi


Picha kwenye televisheni zilionesha baadhi ya wakimbizi wakiruka kutoka kwenye boti na kuanguka baharini.

Wengine walionekana wakining'inia kwenye kamba kati ya boti na ufukwe wa Italia huku walinzi hao wakijaribu kuwasaidia.

Tukio hili linakuja baada ya Papa Benedict kuwaomba Wakatoliki kuwa wavumilivu zaidi kwa wakimbizi wanaotoka Afrika Kaskazini.

Aliwaambia waumini katika mji mmoja wenye bandari kwamba Wakatoliki wanafaa kuwakaribisha na kuwa wakarimu kwa maelfu ya wageni wanaowasili kwenye bandari zao mwaka huu.

Idadi ya wakimbizi kutoka Afrika Kaskazini imezidi kwa sababu ya ghasia katika nchi za eneo hilo.

Jana usiku meli ya wavuvi iliyobeba mamia ya watu kutoka Libya iligonga mwamba, ilipojaribu kutia nanga katika kisiwa cha Utaliana cha Lampedusa.

Taarifa zinasema abiria wote walinusurika, na wengine walisaidiwa walinzi wa mwambao wa Utaliana
Maiti ya Osama Imefanywa Nini?Maafisa wa Marekani wamesema kuwa maiti ya Osama bin Laden ilipewa heshima zote na kusaliwa kiislamu kabla ya kuzikwa baharini, lakini maswali mengi yamezuka kwanini azikwe baharini wakati Marekani ingeweza kumzika kwenye ardhi ya sehemu yeyote ile?.
Taratibu za kiislamu zinataka maiti izikwe mapema iwezekanavyo badala ya kucheleweshwa isipokuwa iwapo uchunguzi wa kifo cha mtu aliyefariki utahitajika.

Maafisa wa Marekani wanasema kuwa walizingatia sana taratibu za kiislamu kwa kuuzika mwili wa Osama bin Laden ndani ya masaa machache.

"Taratibu za mazishi katika dini ya kiislamu zilifuatwa, maiti yake ilifanyiwa taratibu zote za kidini kwenye kambi ya jeshi, mwili wake ulivalishwa sanda nyeupe, uliwekwa ndani ya mfuko uliowekwa vitu vizito ili uweze kuzama baharini na kisha ulidondoshwa kwenye peninsula ya Uarabuni katika bahari ya Hindi.

Maafisa wa Marekani walisema kuwa tukio hilo lilitokea masaa 12 baada ya Obama kuuliwa kwa kupigwa risasi ya kichwa. Taarifa ya televisheni ya ABC ilisema Osama alipigwa risasi ya pili kwenye kichwa ili kuhakikisha kuwa amefariki dunia.

Mwili wake ulisafirishwa hadi kwenye kambi ya jeshi la Marekani nchini Afghanistan ambapo sampo yake ya DNA ilipimwa ambapo ilionekana kushahibiana kwa asilimia 99 na sampo za ndugu kadhaa wa Osama.

Ulichukuliwa na kuwekwa kwenye meli ya kivita ya Marekani, USS Carl Vinson iliyopo kaskazini mwa bahari ya Uarabuni ambapo taratibu za kidini zilifanyika na baadae mwili wake ulizikwa baharini.

Marekani ilisema kuwa iliamua kumzika Osama baharini baada ya kukosekana kwa mtu ambaye angeikubali kuizika maiti yake. Iliripotiwa kuwa Saudi Arabia iliukataa mwili wa Osama bin Laden.

Hata hivyo kumekuwa na maswali mengi kwanini Marekani iliamua kumzika Osama bin Laden baharini.

Kwa mujibu wa imamu Dr Abduljalil Sajid wa Uingereza ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la waislamu nchini Uingereza alisema kuwa si kweli kwamba hakuna mtu ambaye angejitolea kuupokea na kuuzika mwili wa Osama bin Laden.

Imamu Sajid alisema kuwa lazima kungekuwepo na mtu ambaye angejitolea kumzika kati ya ndugu zake wengi au mmoja wa watu wanaoshabikia itikadi zake za kigaidi.

Naye profesa wa sheria za kiislamu katika chuo kikuu cha University of Jordan, Mohammed Qudah alisema kuwa kumzika mtu baharini haikatazwi katika dini ya kiislamu lakini kwa sharti la kukosekana kwa mtu atakayekubali kuipokea maiti na kuizika kiislamu.

"Si kweli na wala si sahihi kusema kwamba hakuna mtu katika ulimwengu wa waislamu ambaye angekuwa tayari kuupokea mwili wa Osama bin Laden", alisema profesa Qudah.

"Kama familia imekataa kuipokea maiti, ni jambo rahisi katika uislamu, chimba kaburi kwenye ardhi yoyote ile hata porini, isalie maiti na kuizika", alisema mufti mkuu wa Dubai, Mohammed al-Qubaisi alipohojiwa kuhusiana na suala hilo.

Marekani katika kutoa maelezo ya mjadala huu imetoa sababu mbili za kuamua kuizika maiti ya Osama baharini, kwanza ili kuepuka kaburi lake kufanywa kama kaburi la shujaa na hivyo kujijengea umaarufu kwa watu wengi kulitembelea.

Pili serikali ya Marekani imesema kuwa haikuwa na muda wa kujaribu kutafuta muafaka na nchi zingine kuukubali kuuzika mwili wa Osama bin Laden

Pakistan wito wa viongozi kujiuzulu

Marekani inasema Osama Bin Laden alikuwa hakujitenga bali akiongoza Al Qaeda hadi alipouliwa na kikosi cha Marekani nchini Pakistan juma lilopita.
Osama Bin Laden


Na nchini Pakistan viongozi wa serikali na jeshi wamekuwa na kikao cha dharura huku kuna wito kuwa Waziri Mkuu na Rais wanafaa kujiuzulu.

Rais wa Pakistan, Waziri Mkuu na mkuu wa jeshi wamekuwa na kikao hicho baada ya kuuwawa kwa Osama Bin Laden.

Inaelekea wana hamu ya kutafuta njia ya kuokoa jahazi kuna ripoti kuwa taarifa rasmi itatolewa kesho bunge likikutana.

Swala muhimu ni nani alikuwa akijua kuwa bin Laden alikuwa ndani ya nchi na kama wanasiasa waliambiwa.Nguvu ziko mikononi mwa jeshi nchini Pakistan.

Na kama jeshi llikuwa linajua kuwa Bin Laden akiishi nchini na likaificha serikali basi itaonesha kuwa serikali haina mamlaka juu ya nchi.

Tangu hapo serikali ilikuwa imeshadhoofika kutokana na shida za kiuchumi lawama wakati wa mafuriko makubwa ya mwaka jana na uhusiano wake na Marekani, huku ndege za Marekani zisokuwa na rubani zinaendelea kufanya mashambulio katika ardhi ya Pakistan
Hivi ni ugumu wa maisha?


Wimbi la wanaojinyonga wenyewe linazidi kuongezeka siku hadi siku sababu ambayo wananchi wanashindwa kuelewa linatokana na chanzo gani kutokana na watu kuamua kukatiza uhai wao wenyewe
Mbali na kujiondoa uhai watu wameonekana kubadilika mioyo yao na utu umeisha kutokana na watu kushindwa kuaminiana kufanyiana mambo ya kinyama hali ambayo inatishia maisha kwenye jamii

Inawezekana ugumu wa maisha unachingia auu? Mana siku hizi ukitembea barabarani kukuta mtu anaongea peke yake imekuwa ni kawaida na idadi hiyo inazidi kuongezeka kila kukicha.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke, David Miseme, ametoa taarifa jana kuwa, mkazi wa Mbagala, Abdallah Mohamed (25), amekufa baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya manila aliyokuwa ameitundika kwenye dari chumbani kwake.

Amesema tukio hilo lilitokea juzi saa 12 jioni huko Mbagala anakoishi.

Amesema sababu ya kujinyonga haikupatikana mara moja uchunguzi unafanyika.

Matukio haya yamekithiri sana kila kukicha makamanda wanatoa taarifa kuhusiana na watu kujiua wenyewe kwa kutumia vitu mbalimbali vikiwemo sumu na vinginevyo vinanyoua

Aliyejichoma majimoto afunguliwa mgahawaMwanamke mmoja [32] mkazi wa jijini Dar es Salaam, aliyeweza kujiunguza na maji ya moto ili aweze kuomba barabarani apatiwe mtaji, nduguze wamfungulia mradi wa kuendesha mgahawa eneo la Buguruni.
Chanzo cha habari hii kilidai kuwa, ndugu waliomkataza aachane na kuomba barabarani kwa pamoja walishirikiana kumtafutia mtaji na kumfungulia mgahawa ikiwa ni kumtaka aendeshe maisha yake pasipo kuomba.

Imedaiwa kuwa, mwanamke huyo tayari ameshaanza biashara hiyo mwanzoni mwa wiki hii na kudaiwa kuwashukuru ndugu zake waliojitolea kumfungulia biashara hiyo.

Imedaiwa kuwa, mwanamke huyo anaapa kutokuwa na hamu ya kuolewa kwa kuwa tayari alishapata mateso kutoka kwa mtalaka wake ambaye alimtelekeza na mtoto na kuishi maisha magumu yaliyompelekea kuomba ili ndugu zake waweze kumsaidia.

Imedaiwa kuwa mwanamke huyo alitumia mbinu ya kuomba barabarani ili aweze kupatiwa msada na ndugu zake kwa kuwa ndugu hao hakuna aliyeamini kama angekosa mtaji kwa kuwa ilidaiwa alikuwa na maisha ya juu alipokuwa na mumuwe huyo


Wahama kuogopa ulipuaji wa mabomuBaadhi ya wakazi wa Gongo la Mboto walilazimika kuhama kwa kuogopa zoezi la ulipuaji wa mabaki ya mabomu katika kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Gongolamboto na kurejea makazi yao jeshi hilo lilipotangza kusitisha zoezi hilo.


Wakazi hao waliondoka kwenye makazi hayo kwa hofu ya kulipukiwa na mabomu hayo kama awali japo jeshi hilo kutngaza hakutakuwa na athari yoyote kwa wakazi hao.

Jumatatu ya wiki hii jeshi hilo lilitangaza kumalizia kulipua masalia ya mabomu katika kambi hiyo na zoezi hilo kuahirisha jana na kutangazwa.

Taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Habari wa JWTZ zilidai kuwa walipanga kulipua mabomu hayo ndani ya kambi hiyo kwa kuhofia kya lipua kwa kuyabeba kuyahamisha mahali pengine kwani kuwa kungeweza kuleta madhara makubwa

Februari 16, mwaka huu, katika ghala la kambi ya Gongolamboto mabomu yalilipuka na kusababisha vifo vya watu 30 na wengine zaidi ya 300 kujeruhiwa huku wakazi wengine kukosa makazi na wengine kuharibiwa mali zao na mifugo

Wanaharakti wa Misri wanajadili uchaguzi
Zaidi ya wawakilishi elfu mbili wa makundi yaliyoshiriki katika maandamano kumfanya Rais Hosni Mubarak aondoke mwezi Februari, wanakutana leo nchini Misri kwa mara ya kwanza, kupanga mustakbali wa siasa wa nchi hiyo.Tangu Rais Mubarak kuondoka madarakani, Misri imekuwa ikiongozwa na halmashauri ya siri ya kijeshi; wanaharakati walioanzisha maandamano katika medani ya Tahrir hawakuchangia katika mabadiliko yanayotokea.

Katika mkutano wa mwanzo wa Halmashauri ya Taifa ya demokrasi, wanaharakati wanataraji kuwa wataweza kukubaliana juu ya njia za kuendeleza shime katika mapinduzi.

Wasi wasi wao mkubwa ni kuwa chama cha Muslim Brotherhood kitahodhi uchaguzi uliopangwa kufanywa mwezi Septemba, kwa sababu hakuna chama kisichokuwa cha kidini kilichoundwa kuchukua nafasi ya chama cha Bwana Mubarak, ambacho kimepigwa marufuku.

Mkutano unazungumza juu ya wagombea uchaguzi na mabadiliko zaidi ya katiba.

Lakini wanaharakati wengi hawana uzoefu, na wengine hawataki kuingia kwenye siasa.

Haijulikani vipi mkutano wa siku moja utaweza kuleta msimamo mmoja kati ya waakilishi wengi hivo.

Na uchaguzi unakaribia, hakuna muda wa kuunda chama kipya cha siasa.

Jaji Samatta ataka mafisadi wabanwe

KASI ya ufisadi na matumizi mabaya ya rasilimali za umma, imemtisha Jaji Mkuu mstaafu Barnabas Samatta, ambaye amevitaka vyombo vya habari kukemea bila uwoga.Jaji Samatta alisema kutokana na ufisadi huo kufanywa kwa sura tofauti, Watanzania hawawezi kushinda vita dhidi yake bila vyombo vya habari na waandishi.Alitoa kauli hiyo juzi usiku kwenye hafla ya utoaji tuzo kwa waandishi bora wa habari kwa mwaka 2010.

Tuzo hizo ziliandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT).“Mheshimiwa Rais (Rais wa MCT ) kama sote tujuavyo, nchi yetu imekuwa inapata mapigo makubwa ya ufisadi katika sura zake mbalimbali," alisema na kuongeza: "Ningependa kutumia fursa hii kuvipongeza vyombo vya habari, ambavyo vimejitokeza kwa ujasiri mkubwa kushiriki mapambano dhidi ya maovu hayo.”

Kwa mujibu wa Jaji Samatta, mafisadi wanaamini kuwa nchi inawahitaji zaidi kuliko wao wanavyoihitaji fikra ambazo ni finyu na hazina tija.“Naogopa sana kufikiri kitu gani kitatokea iwapo watu jasiri wakiweka chini silaha zao na kutangaza kuwa mafisadi wameshinda vita.

Au wanahabari mkiamua kuwa kalamu, kompyuta, 'microfone' na kamera zenu, sasa havitatumika katika vita dhidi ya mafisadi,” alisema Jaji Samatta na kuongeza:”Wanahabari msimwonee mwananchi yeyote, lakini, vilevile msimwogope mtu. Lishughulikieni kila suala linalojitokeza kwa mujibu wa sheria za nchi na kanuni za maadili ya taaluma yenu,Pambaneni na wale wote nchini wanaokubaliana na matamshi ya kutisha aliyotoa Napolean Bonaparte, mtawala wa Ufaransa kwenye karne ya 19 aliposema:Kuna kitu kimoja tu hapa duniani, nacho ni kuendelea kupata fedha na fedha zaidi, mamlaka na mamlaka zaidi.

Vitu vingine vinavyobaki havina maana.”Alisema mafisadi wasipate picha kuwa, falsafa hiyo inakubalika hata Tanzania, ili vizazi vinavyokuja visipate shida kuona au kutambua kuwa kwenye vita dhidi ya ufisadi, waandishi wa habari hawakusita kuwa upande wa wanyonge.Jaji Samatta alisema bila kuwashinda mafisadi, siku zote uhuru wa mwananchi, demokrasia na utawala wa sheria vitakuwa hatarini.Alisema taarifa zinaonyesha mafisadi wapo hadi ngazi ya serikali ya vijiji na kwamba, kwa kupitia vyombo vya habari anapata nguvu ya kuamini taifa halijaishiwa watu jasiri.

”Mafisadi inasemekana sasa wako hadi ngazi ya serikali za vijiji. Nisomapo baadhi ya makala katika magazeti na kusikiliza baadhi ya maoni kwenye runinga, au redio, napata nguvu kuamini kuwa nchi yetu haijaishiwa watu ambao ni jasiri kupambana na ufisadi,” alisema.Kuhusu uhuru wa vyombo vya habari, alimnukuu mmoja wa viongozi wa Marekani, Thomas Jefferson, aliyesema: Kama ningepewa na uwezo wa kuamua kama tuwe na serikali bila magazeti, au magazeti bila serikali, ningependelea bila kusita hilo la pili.

”Jaji Samata alisema hakuna mashaka kuwa, kuna watu wengi duniani ambao hawatakubaliana na maoni hayo, lakini anaamini hakuna mpenda demokrasia na utawala wa sheria anayeweza kusita kukubali kuwa vyombo vya habari vina umuhimu wa kipekee kwenye maisha ya binadamu. Alisema kwenye vyombo vya habari vinavyowajibika ipasavyo, madikteta, mafisadi, wala rushwa, wakandamizaji na wabaguzi hupata shida kufanikisha matakwa yao.

“Kuvifunga minyororo vyombo vya habari, ni kuwafunga minyororo wananchi,” alisema Jaji Samata.Pia, Jaji Samatta alivitaka vyombo vya habari vya umma, kutoa nafasi sawa kwa vyama vya siasa vinavyotambulika kisheria, badala ya kupendelea chama tawala.

Katika hatua nyingine, Jaji Samatta alisema sekta ya mahakama ni moyo wa demokrasia, lakini mahakama zilizo huru na zisizo na uwoga.Jaji Samata alivitaka vyombo vya habari kutoa mchango wake kuwezesha wananchi na viongozi kuheshimu uamuzi wa mahakama.Kuhusu katiba mpya, Jaji Samata alisema kama taifa likipata katiba isiyoridhisha, haitakuwa rahisi kwa vyombo vya habari kukwepa kuwa kwenye makundi yatakayolaumiwa.Mwisho
Mabomu mtawanyiko yanatumiwa Misrata
Majeshi ya Kanali Gaddafi wa Libya yametumia mabomu ya mtawanyiko, katika shambulio jengine katika mji wa bandari ya Misrata, ambao umezingirwa na jeshi hilo.Msimamizi wa bandari alisema mabomu hayo yaliripuka chini ya lori na kujeruhi watu wawili.

Mwandishi wa BBC mjini Tripoli anasema, waandishi wana picha ambazo zinaonesha wazi mabomu yaliyojizika ardhini, yaliyofyatuliwa kutoka kombora linalorusha mabomu mtawanyiko, ambayo yamepigwa marufuku katika nchi nyingi.

Juma lilopita NATO ilitegua mabomu yaliyolengwa dhidi ya meli katika pwani ya Misrata.

Na mizinga iliyofyatuliwa na jeshi la Gaddafi nchini Libya, inaarifiwa kuwa imepiga ardhi ya Tunisia kwenye mji wa Dehiba, ulio mpakani.

Vita baina ya jeshi la wapiganaji na jeshi la Kanali Gaddafi vimezidi kuwa vikali katika juma lilopita, kwenye milima ya magharibi mwa Libya.Nitajiuzulu ikithibitishwa- SadickKAIMU Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Saidi Meck Sadiki, ametishia kujiuzulu endapo itathibitika kuwa amechakachua posho katika milipuko wa mabomu iliyotokea katika kambi ya Jeshi Gongo la Mboto.
Sadiki amesema kuwa, licha ya wakazi kuwa na wasiwasi juu ya ujenzi wa nyumba na kuhisi huenda zoezi hilo halitakamilika amesema zoezi hilo litakamilka na kudai atajiuzulu endapo itathibitishwa kula fedha hizo na kutengwa kwa fungu la watoa tathimini.

Aliyasema hayo jijini Dar es Salaam, na kusema kazi ya kufanya tathmini ni ya serikali.

Hayo yamekuja baada ya malalamiko ya maofisa wanaofanya tathimini za nyumba kudai posho na ambapo fungu la posho hizo hazikutengwa na serikali na maofisa hao kudai kutafunwa kwa posho.

Amesema ujenzi wa nyumba utaanza mara baada ya kukamilika kuwalipa fidia watu wote ambao nyumba zao zilipigwa na milipuko ya mabomu

Pia Sadiki alisema zoezi la ufyatuaji wa matofali ya kujengea utaanza mara baada ya kumalizika kwa tatizo la umeme kumalizika katika mitambo ya kufyatulia matofali ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).


MCL yazoa tuzo sita za waandishi bora


WAANDISHI sita wa habari wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), juzi usiku walitwaa za ubora wa kazi zao katika kundi la magazeti kwa mwaka 2010 katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam.
MCL ndiyo inayochapisha magazeti ya Mwananchi, Mwanaspoti na The Citizen.Katika tuzo hizo zilizotolewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT), Mwandishi Mkuu wa The Citizen Lucas Liganga alitwaa Tuzo ya Malaria. Mwandishi wa Mwananchi, Tumaini Msowoya alipata Tuzo ya Kundi la Walemavu.

Mwandishi mwingine wa Mwananchi, Florence Majani alipata Tuzo ya Habari za Jinsia, Sheila Sezzy pia wa Mwananchi, alipata tuzo ya Habari Nzuri ya Afya. Salome Gregory wa The Citizen alipata Tuzo ya Habari Bora ya Majanga. Tuzo ya Mchora Katuni Bora ilikwenda kwa Samuel Mwamkinga wa The Citizen.

Mwandishi wa Daily News ambaye pia aliwahi kuandikia Gazeti la The Citizen kwa muda mrefu, Orton Kiishweko, alipata Tuzo ya Mwandishi Bora wa Habari za Utawala Bora, Tuzo ya Habari za Ukimwi na kuibuka mshindi wa jumla na hivyo kutangazwa kuwa mwandishi bora wa habari kwa mwaka 2010.

Wandishi wengine wa magazeti waliofanya vizuri ni pamoja na Bashiru Nkoromo kutoka Uhuru na Mzalendo aliyeibuka na Tuzo ya Mpigapicha Bora na Happy Severine akichukua Tuzo ya Mwandishi Bora wa Habari za Elimu.
Kwa upande wa redio na televisheni, Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) liliibuka kidedea baada ya waandishi wake kutwaa tuzo katika nyanja karibu zote.

Jaji Mkuu wa shindano hilo, Anthony Ngaiza, alisema jopo la majaji lilitafanya kazi yake kwa weledi wa hali ya juu na hivyo washindi waliopatikana wanakidhi vigezo.Hata hivyo, alitoa changamoto kwa waandishi wa habari kufanya kazi zao kwa kina ili kukidhi vigezo na pia kuisaidia jamii.Alitoa wito kwa wamiliki na wahariri wa vyombo vya habari kuwawezesha waandishi kwenda vijijini kuibua matatizo ya msingi yanayowakabili wananchiTaliban inashambulia vikali Kandahar
Shughuli zimesimama katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Afghanistan, mji wa Kandahar, kusini mwa nchi, kwa sababu ya mapigano makali, yaliyozushwa na mashambulio kadha yanayofikiriwa kufanywa na wapiganaji wa Taliban dhidi ya majengo ya serikali.

Mashambulio kama sita yamefanywa na watu waliojitolea mhanga.

Mapigano mengi yametokea kwenye maeneo ya biashara.

Watu wengi walijeruhiwa.

Rais wa Afghanistan, Hamid Karzai, alisema Taliban wanajaribu kuficha kuwa wameshindwa kwa Osama Bin Laden kuuwawa, kwa kulipiza kisasi kwa kushambulia raia wasiokuwa na hatia.

Taliban imekanusha kuwa mashambulio hayo ni ya kujibu mauaji ya Bin Laden, na wamesema mashambulio hayo yalipangwa kitambo.

DPP akaribisha ushahidi kuhusu Kagoda
MKURUGENZI wa Mashtaka Nchini, Eliezer Feleshi, amewataka wananchi wenye ushahidi kuhusu Kampuni ya Kagoda Agricultural Limited, inayodaiwa kuchota Sh40 bilioni za EPA, kuwasilisha katika ofisi yake au polisi, ili ufanyiwe kazi.

Akizungumza na Mwananchi katika mahojiano maalumu jijini Dar es Salaam juzi, Feleshi alisema, ofisi yake inahitaji ushahidi kuhusu kampuni hiyo ili kurahisisha kazi ya upelelezi.Wito huo wa Mkurugenzi, unafuatia madai ya baadhi ya wanasiasa kuwa wana ushahidi kuhusu wamiliki halali wa kampuni hiyo na kwamba serikali ikiwahitaji, watakuwa tayari kutoa ushirikiano.

Alisema ofisi yake anawakaribisha watu wote wenye ushahidi au taarifa kuhusu kampuni hiyo ili iufanyie kazi, itakayowawezesha wamiliki, kufikishwa mahakamani."Nawakaribisha wananchi wenye ushahidi au taarifa kuhusu Kampuni ya Kagoda, kuwasilisha katika ofisi yangu ili tuweze kuufanyia kazi," alisema Feleshi.

Mkurugenzi huyo wa mashtaka pia aliwataka wananchi kuwa na tabia ya kusaidiana na polisi au ofisi yake katika kukabiliana na uhalifu ili kumaliza tatizo hilo.

Alisema haipendezi watu kulalamikia mambo hayo nje ya utaratibu au taasisi zilizowekwa kisheria, kuyashughulikia mambo.Feleshi, alisema serikali ni ya watu wote na sheria zinampa kila mtu nafasi ya kutoa ushahidi kuhusu taarifa mbalimbali,iwe Kagoda au nyingine. "Lengo ni kuisadia serikali kupambana na ufisadi," alisema .

Alisema, kila idara imetengewa majukumu yake na wajibu wa ofisi yake ni kusikiliza ushahidi au taarifa mbalimbali ikiwamo ushahidi kuhusu tuhuma za ufisadi wa Kagoda ili ziweze kufanyia kazi."Jamii inaweza kuwa chanzo kizuri cha taarifa kamili kuliko ofisi yangu, kwa hiyo jamii inapaswa kutoa ushirikiano
Kampuni ya Kagoda Agricultural Limited ni miongoni mwa kampuni 22 zinazodaiwa kuchota Sh133 bilioni za EPA.

Imedaiwa kuwa kampuni hiyo inamilikiwa na baadhi ya vigogo wa kisiasa na wafanyabiashara wakubwa.Hata hivyo,Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA),wamedai kuwa, wamiliki wa kampuni hiyo ni John Kyomuhendo na Francis William na kwamba ilisajiliwa Septemba 22 mwaka 2005 na kupata hati yenye namba 54040.

Inadaiwa kuwa ofisi yake iko katika kiwanja namba 87 kilichoko katika eneo la Viwanda la Kipawa, jijini Dar es Salaam

Vifaru vinaingia Banias, Syria
Taarifa kutoka Syria zinaeleza kuwa vifaru vimepelekwa katika mji wa bandari wa Banias, ambao umekuwa na maandamano kadha dhidi ya serikali yaRais Bashar al-Assad.

Ripoti zinasema vifaru vinaelekea maeneo ya watu wa madhehebu ya Sunni, lakini siyo ya Alawi, koo za Kishia anakotoka Rais Assad.

Mwandishi wa BBC anasema ripoti hizo zikithibitishwa, basi ni tukio la hatari, kwa sababu linaweza kuleta mgawanyiko kati ya madhehebu tofauti.Siku ya Ijumaa watu zaidi ya 20 waliuliwa na askari wa usalama, wakati wa maandamano dhidi ya serikali nchini Syria.

Marekani imeonya kuwa itachukua hatua zaidi dhidi ya Syria iwapo serikali ya Rais Assad itashindwa kuacha kukandamiza waandamanaji kwa nguvu.

Lakini Marekani haikueleza itachukua hatua za namna gani


Besigye ametoka hospitali Nairobi


Siku moja baada ya kutoka hospitali mjini Nairobi, kiongozi wa upinzani nchini Uganda anasema anajiandaa kurudi nyumbani.Dr. Besigye anasema ataporudi huko ataendelea na harakati zake, za kutembea hadi kazini.

Kwa sasa anasema afya yake imetengenea kiasi na anaweza kuona, japo macho bado yanamsumbua.

Alikuwa akizungumza mjini Nairobi alipokuwa anapata matibabu.

Alisema "bila ya shaka nitarudi Uganda, sina nchi nyengine, ni nchi yangu na ni lazima nirudi Uganda.

Vitendo tunavoshughulika navyo hivi sasa, siyo vitendo vyangu, ni vitendo vya wananchi wa Uganda, ambao wameamua lazima wajirudishie uwezo na kuona kwamba mali ya umma inawahudumia, siyo inawahudumia wale wachache.

Na wakati wanapigania haki zao, sisi wote viongozi tutaendelea kuwaunga mkono, na kufanya chochote ambacho kitasaidia kuleta mabadiliko yanayohitajika nchini mwetu."Ridhiwani Kikwete Aukana Ubilionea


MTOTO wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete ameukana ubilionea aliovishwa na wanasiasa wa vyama vya upinzani
Amekanusha hayo baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa na Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila, kuutangazia umma kuwa ni Ridhiwani Kikwete ni bilionea na kuhoji ubilionea wake umetoka wapi.

Ridhiwani aliwataka Watanzania wasimhukumu kwa kumuona mitaani akiendesha magari ya bei ghali.

“Mi naishi na watu vizuri hapa mjini jamani, tunaishi kimjini mjini na si kila kitu unachomuona nacho mtu ni cha kwake,”, alisema Ridhiwani.

"Hii inatokana na malezi ya wazazi wangu yaliyonieleza kuishi na watu vizuri”, alieleza Ridhiwani

“Hayo wanayonizushia mimi kuwa ni bilionea na namiliki kampuni ya malori 150 na kampuni ya ujenzi pamoja na ghorofa za kupangisha mjini mimi nasema si kweli”.

Alibainisha kuwa habari hizo ni za uongo na uzushi na zimelenga kumchafua yeye na mzazi wake na kupandikiza chuki dhidi ya familia yake na jamii.

Alisema hatua waliyochukua si nzuri na kubainisha kuwa anawaheshimu sana kutokana na umri wao na kuwataka watoe ushahidi wa hayo kwenye vyombo vya habari

Hata hivyo Ridhiwani alibainisha mali zake anazomiliki kuwa ni shamba la hekari moja na nusu lililopo Bagamoyo, gari aina ya Toyota Cami na akaunti mbili katika benki za Stanbic na NBC


Babu ataka apelekewe wafungwa

MCHUNGAJI Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapila ameomba wafungwa waliopo magerezani na watoto yatima ambao ni wagonjwa wapelekwe Samunge ili wapatiwe kikombe cha tiba.
Mwasapila ambaye anatoa tiba ya magonjwa Sugu aliliambia Mwananchi kijijini Samunge jana kuwa, Mungu amemwonyesha uhitaji wa tiba kwa watoto yatima na wafungwa.

"Nimeonyeshwa ujio wa yatima kwa wingi hapa, lakini siwaoni, naomba Serikali na wengine wanaohusika wawalete wapate dawa,"alisema Mwasapila na kuongeza kuwa wafungwa ambao ni wagonjwa, pia wana haki ya kupata tiba, hivyo kutaka wapelekwe kwake ili wapate kikombe cha tiba.

Babu akemea rushwa
Katika hatua nyingine, Mchungaji Mwasapila amekemea vitendo vya rushwa na urasimu ambavyo vinadaiwa kufanywa na watu wanaoruhusu magari yanayokwenda Samunge, hivyo kusababisha malalamiko kutoka kwa wagonjwa."Wanakuja hapa wanalalamikia kunyanyaswa katika vituo vya kupitisha magari, naomba jambo hili liachwe na wahusika,"alisema Mwasapila.

Alisema utaratibu uliowekwa na Serikali wa kuruhusu kwa mpangilio maalumu wa magari yanayokuja Samunge ni mzuri na unapaswa kutekelezwa na pande zote bila ya malalamiko.

Asisitiza kikombe ni kimoja
Kadhalika, Mchungaji Mwasapila aliendelea kusisitiza kuwa kikombe cha dawa anachopaswa kupewa mgonjwa ni kimoja tu, licha ya kuwapo kwa madai ya baadhi ya watu waliopewa dawa hiyo kutopona.
Maelezo ya Mchungaji huyo yamekuja wakati baadhi ya watu waliokunywa dawa kusema bado hawajapona vizuri, hivyo kuhitaji kikombe cha pili.

Kadhalika, tafiti za kitaalamu zilizofanywa zimekuwa zikipendekeza kuchunguzwa kwa kiwango cha dozi kinachotolewa na mchungaji huyo ili kubaini kama kinakidhi kutibu magonjwa husika kufuatia tafiti hizo kubaini uwezo mkubwa wa kitiba katika mti wa Murigariga unaotumiwa na Mchungaji Mwasapila.

Mtaalamu mmoja wa afya mkoani Arusha, aliyeomba kutotajwa jina alisema, dawa ya Mchungaji Mwasapila ina uwezo mkubwa ila kama akishauriwa kitaalamu ikaboreshwa itakuwa na manufaa makubwa.Hata hivyo, Mwasapila jana alipinga mawazo hayo na kusisitiza kuwa wagonjwa ambao wamepata kikombe na wakapata nafuu na baadaye hali zao kurejea kuumwa wanapaswa kuwasiliana naye kwa maombi na sio kunywa kikombe kingine.

Maofisa wa Kenya Samunge
Maofisa wa Serikali ya Kenya, wakiwamo wanaotoka katika ofisi ya Rais Mwai Kibaki pamoja na familia zao, jana walitinga Samunge ambapo walipata kikombe cha tiba.Akizungumza na Mwananchi, mmoja wa maofisa hao, ambaye ni Chifu wa eneo la Frans Mara, Olenantea Labora alisema yeye na maofisa wenzake kutoka Kenya wamefika Samunge kupata tiba."Tumekuja kupata kikombe cha dawa na familia yangu na wenzangu, tumepata taarifa za dawa hii kutibu wengi nasi tumekuja," alisema Labora ambaye alikuwa na sare za Serikali ya Kenya.

Foleni yaongezeka Samunge
Foleni ya magari ambayo yanaingia kijiji cha Samunge, imeongezeka tena, ambapo jana ilikuwa imekwenda zaidi ya kilometa tatu kutoka nyumbani kwa Mchungaji Mwasapila.Magari mengi yaliyopo kwenye foleni hiyo, ni kutoka nchi jirani ya Kenya, mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kanda ya Kaskazini.

Wakati magari yakiongezeka, mvua ambazo zimeanza kunyesha zimetishia tena kuzuia watu kufika Samunge baada ya juzi usiku kunyesha mvua ambayo imesababisha magari kadhaa kukwama barabarani.Baadhi ya madereva wakizungumza na Mwananchi, waliitaka halmashauri ya Ngorongoro, kukarabati barabara ya kutokea njia panda ya Arusha na Loliondo kwenda kijiji cha Samunge ambayo magari yote yanaitumia kufika Samunge.

Jonathan Mathayo, alisema barabara hiyo ambayo ipo chini ya halmashauri ni mbaya sana na sasa imeanza kusababisha magari kukwama. "Mbona hawa halmashauri wanapokea fedha hakuna lolote, barabara zao mbaya, hakuna huduma za afya, Samunge pachafu ....tunaomba katika fedha za ushuru tunaolipa watengeneze barabara," alisema Mathayo.

Mchungaji Mwasapila, pia jana alizungumzia tatizo hilo, la barabara na kuiomba Serikali kuifanyia ukarabati ili kuwezesha watu kufika Samunge bila tatizo. "Nimeonyeshwa maelfu ya watu wa mataifa mbalimbali kwenda Samunge sasa naomba Serikali irekebishe hii miundombinu ili wafike na kupata tiba," alisema Mwasapila

Dawa ya Babu inawezekana kuwa katika mfumo wa vidonge -WHO


UTAFITI unaoendelea kufanyika wa dawa ya Mchungaji Ambilikile Mwasapile wa kijiji cha Samunge umebainika kuwa dawa inatibu maradhi sugu na Shirika la Afya Duniani [who] Kuikubali dawa hiyo
Hayo yamebainishwa na Askofu wa Kanisa la KKKT na kubainisha kuwa shirika hilo limekubali kuwa dawa hiyo inatibu maradhi sugu kama ilivyobainishwa awali katika utafiti wa kina walioufanya.

Imesemekana kuwa dawa hiyo inawezekana kuwa katika mfumo wa vidonge na chupa.

Shirika la Afya Duniani WHO ambalo lilituma wataalamu wake kuichunguza dawa ya babu, limebainisha hilo na kulifanyia kazi mikakati hiyo ya kuweka dawa hiyo katika mifumo hiyo na si kikombe pekee kama ilivyozoeleka, alisema Askofu huyo.

Pia dawa hiyo imethibitishwa na taasisi ya TMF na kubainisha kuwa dawa hiyo inatibu maradhi sugu.

Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa TMF, Marwa Gonzaga jijini Dar es Salaam.

Alisema wakati wakiendelea na utafiti huo walibaini kuwa tiba hiyo ni mchanganyiko wa mizizi ya miti shamba ya aina mbili ambayo ni kisayansi unafahamika kama Carissa Spinarum na mti wa Ntuntwa.

Tayari dawa ya babu imeshajizolea sifa ndani na nje ya nchi ambapo watu wameendelea kumiminika kijijini hapo kunywa dawa hiyo.

Hata hivyo taarifa zilizopatikana baadae zimesema kuwa babu amekataa dawa yake kufanyiwa mabadiliko yoyote kwakuwa Mungu hapendi.

Babu alisema kuwa kwakuwa dawa hiyo ni ya miujiza alioteshwa na Mungu, masharti aliyopewa na mungu kwenye ndoto yake hayaruhusu dawa hiyo ifanyiwe mabadiliko yoyote yale. Labda kama ataoteshwa ndoto nyingine ya kupewa ruhusa kufanya hivyo.

Kifo cha Osama kitazaa vita kubwa ya ugaidi-wanasiasa

BAADHI ya wanasiasa nchini, wamesema kuuawa kwa kiongozi wa Kundi la Al Qaeda, Osama bin Laden, sio mwisho wa ugaidi duniani, huku wakisisitiza kuwa mauaji hayo huenda yakaibua vita mpya baina ya wafuasi wa kundi hilo na mataifa mbalimbali duniani.

Wamesema mtandao wa kundi hilo ni mpana na kwamba kuna uwezekano mkubwa wa wafuasi wake, kuwapo nchini na hasa iizingatiwa kuwa aliyehusika kulipua ubalozi wa Marekani nchini Ahmed Khalfan Ghailan, alikuwa ni Mzanzibari.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, alisema hakukua na ulazima wa Marekani kumuua kiongozi huyo Al Qaeda na badala yake, wangemkamata na kumfikisha katika vyombo vya sheria.

“Ugaidi ni kulipiza kisasi, Wamarekani walikuwa na uwezo wa kumkamata Osama na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria, kama hilo lingekuwa gumu pia wangeweza kukaa naye meza moja na kumhoji ili kujua nini hasa alichokuwa akikitafuta kutokana na matendo aliyokuwa akiyafanya,” alisema Mbatia.


Huku akitolea mfano wa kukamatwa na kunyongwa kwa Rais wa zamani wa Iraq, Saddam Hussein, Mbatia alisema licha ya tukio hilo, bado mauaji yanaendelea nchini Iraq.“Wapo wanapambana na ugaidi, lakini leo hii raia wema wanazidi kupoteza maisha nchini Libya, sasa mauaji ya Libya yana tofauti gani na mauaji mengine duniani,” alihoji Mbatia.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro, alisema mashambulizi yanayoendelea kufanywa nchini Libya na majeshi ya nchi za Jumuiya ya Nato, yatazidisha ugaidi duniani.

“Dunia ingependa kuona Osama anafikishwa kortini, ugaidi hauwezi kwisha wakati unyanyasaji bado unaendelea duniani, wapo wanaowapiga wenzao kwa kudhani kuwa wana haki kumbe siyo, sasa hapo ndipo unapoanza uhasama,” alisema Mtatiro.

Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, alisema Wamarekani wasidhani wamemaliza kazi kwa kumuua Osama.

“Kwa taarifa nilizonazo Osama alikuwa amestaafu lakini ugaidi ulikuwa ukiendelea kama kawaida, hivyo basi hawa watu sidhani kama watakaa kimya lazima watafanya kitu tu ili kulipiza kisasi,” alisema Mtikila

Ramani ya Sudan Kusini inachorwa


Benki ya Dunia inashirikiana na mtandao wa Google kuisaidia Sudan Kusini kabla ya nchi hiyo kuwa huru mwezi July.

Lengo ni kutoa ramani kamilifu, kulingana na picha za satalaiti.

Kwenye mkutano mjini Washington na wajumbe wa raia wa Sudan wanaoishi ng'ambo, mamia ya hospitali mpya, barabara na vijiji viliongezwa kwenye ramani za Google za Sudan Kusini.


EU kusherekea wiki kwa kujitolea


UMOJA wa Ulaya (EU), umezindua wiki ya umoja huo kwa kujishughulisha na shughuli mbalimbali za kujitolea nchini.Akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye uzinduzi wa wiki hiyo jana, Mkuu wa umoja huo nchini, Balozi Tim Clarke, alisema katika wiki hiyo kutakuwa na shughuli mbalimbali zitakazofanyika nchini kwa ajili ya kukuza uelewa juu ya watu wanaojitolea.

Clark alisema shughuli hizo zitahusisha masuala yote, yakiwamo ya afya, elimu na mazingira, kaulimbiu ya mwaka huu itakuwa ni ‘Kujitolea’.“Huu ni wakati muafaka kwa Tanzania, wananchi wanaangalia mafanikio waliyoyapata katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru, tunadhani ni vyema sisi pia tusherehekee juhudi za wale waliojitolea kwa ajili ya kuwasaidia wengine,” alisema Balozi Clarke.

Balozi huyo alisema kila mtu anaweza kuleta mabadiliko na kutaka watu wajitolee muda wao, nguvu na ari na ujuzi wao wa maarifa kwa ajili ya kuwasaidia wengine ili kuleta mabadiliko.

Clark alisema shughuli zitakazofanywa katika wiki hiyo, ni kufanya usafi wa mazingira na kufukia mazalia ya mbu kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa wa malaria, ambayo itafanyika katika masoko ya Kisutu na TX Kinondoni.Kwa mujibu wa balozi huyo, shughuli nyingine zitakazofanywa ni msafara wa baiskeli ambao utahusisha wanaume, wanawake, watoto, vijana, wazee na walemavu.

Alisema msafara huo wa baiskeli una lengo la kutoa elimu juu ya umuhimu wa kuboresha usalama barabarani kwa wapanda baiskeli.Pia, alisema shughuli hizo zitafanyika visiwani Zanzibar kwenye Shule ya Msingi Lumumba iliyoko Unguja, ambako kutatolewa mafunzo kuhusu usalama barabarani kwa wanafunzi, walimu na jamii inayozunguka shule hiyoKenyan Parliament-Full Of Kenyan Prisoners On The Run!!!The picture on the left is of a Kenyan parliament, and the picture on the right is of a Kenyan prison. I drown in my own blood when I see this picture of our parliament building because this is where the most corrupt Kenyans hide, infact the building should be turned into a prison when all the members of parliament are seated.They should be let to spend ONLY 2 nights as the Kenyan prisoners on the right ,most of whom are charged for petty crimes,like stealing a cow,stealing maize,and maybe even for not committing any crime.The big offenders go jail free while the petty offenders suffer. The big offenders can only be suspended from their duty,while the petty offenders are not even given a day for investigation before they are loaded on a truck and poured to jail.

In that building you are seeing, we have people who have made themselves filthy rich for stealing millions of shillings from their own ministries or organisations, they have stolen from the poor Kenyans you are seeing sleeping like pigs in a prison.I think even pigs sleep better.

Most of them are old, they have nothing to loose if the country drowns into a bloodshed,they have their children abroad and they have the money to enable them charter a flight and flee the country when things get hot.

In the prison you are seeing on the right, thats where we have an innocent Kenyan, who has been jailed because he could not agree with his boss and for that reason, the boss sent cops to pick him and jail him for selling cannabis,a crime they did not do, he will serve upto five years or more.This is one person that had a good vision and good ambitions, he has a wife and children, he was young, had a good home,but by the time he comes out, all that is gone.We can get a good leader from this prison than from the parliament building we are seeing…..

2012 is around the corner and yet our leaders are still squabbling…..how stupid will we be to re-elect them back?

Clay Onyango.


Mamia Wajitokeza Kumzika Mtoto wa GaddafiMamia ya wakazi wa jiji la Tripoli walijitokeza jana kumzika mtoto wa Gaddafi, Saif al-Arab Gaddafi ambaye aliuliwa katika shambulio la mabomu ya NATO kwenye nyumba ya Gaddafi.
Saif al-Arab Gaddafi, 29, pamoja na wajukuu watatu wa Gaddafi waliuliwa jumamosi wakati majeshi ya Nato yalipofanya shambulizi la kijeshi kwenye makazi ya watu matajiri jijini Tripoli.Shambulizi hilo liliamsha hasira za raia wa Libya ambao waliamua kuzishambulia balozi za Ufaransa, Uingereza na Marekani zilizopo mjini Tripoli.

Maafisa wa Libya wameyashutumu majeshi ya NATO kwa kuua raia wasio na hatia na kujaribu kumuua kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi.

Mamia ya watu akiwemo mtoto maarufu wa Gaddafi, Saif al-Islam walihudhuria mazishi hayo ambapo bendera za Libya na makelele ya kumsifu Gaddafi yalisikika.

Kanali Gaddafi hakuhudhuria mazishi hayo ambayo yalifanyika kwenye makuburi ya Hani mjini Tripoli.

Shambulizi la NATO limezua mjadala kama majeshi ya NATO yana lengo la kweli la kuwalinda raia.

Serikali ya Afrika Kusini ambayo awali ilianzisha mjadala wa kutafuta muafaka wa vita hivyo ililaani shambulizi la NATO na kusema kuwa umoja wa Mataifa haukutoa ruhusa ya kuuliwa kwa raiaRAIS Jakaya Kikwete amesema,mauaji dhidi ya kiongozi wa Mtandao wa kigaidi wa Al- Qaeda, Osama bin Laden si jambo la kufurahia, lakini yametoa ahueni katika vita dhidi ya ugaidi.
Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam jana na kubainisha kuwa ingawa haki haikutendeka dhidi yake kwa kufuata sheria na si vizuri kufurahia jambo hilo bali limeleta ahueni dhidi ya ugaidi duniani

Jana, Rais Barack Obama wa Marekani alitangaza kifo cha Gaidi huyo baada ya kutafutwa kwa kipindi kirefu baada ya shambulizi la ugaidi lilitokea Septemba 11, mwaka 2001 Marekani na kuua zaidi ya watu 3,000.

Agosti 7, 1998 Ubalozi wa Marekani nchini ulilipuliwa na kusababisha vifo vya Watanzania 11 na siku hiyo hiyo karibu muda sawa, Ubalozi wa Marekani nchini Kenya nao ulilipuliwa.

Katika uchunguzi uliofanywa Rais Kikwete alisema baadhi ya watu walihisiwa kuhusika, lakini mhusika mkuu alikuwa Osama.


Al-Qaeda yathibitisha kifo cha Osama
Al-Qaeda imethibitisha kifo cha kiongozi wake, Osama Bin aden, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kundi hilo na kutangazwa kupitia mitandao mbalimbali ya itikadi kali


Taarifa inayothibitisha kifo


Tarifa hiyo imesema damu ya kiongozi huyo "haitapotea" na kuwa al-Qaeda itaendelea kushambulia Marekani na washirika wake.

Kifo cha Bin Laden kitakuwa "laana" kwa Marekani, na kutoa wito kwa Pakistan kuanza harakani, imesema taarifa hiyo.

Bin Laden alipigwa risasi na kufa siku ya Jumatatu, wakati makomando wa Marekani walipovamia nyumba yake katika mji wa Abbottabad nchini Pakistan.Osama Bin Laden


Uvamizi huo ulifanywa bila ya mamlka za Pakistan kufahamu, na hivyo kuongeza mvutano kati ya nchi hizo mbili.

Mikutano kadhaa ya hadhara inafanyika nchini Pakistan siku ya Ijumaa, kupinga hatua hiyo.

Taarifa hiyo iliyochapishwa katika mitandao yenye itikadi kali imesema sauti ya kiongozi huyo wa al-Qaeda iliyorekodiwa wiki moja kabla ya kifo chake itatolewa hivi karibuni.Makazi ya Bin Laden, Pakistan


"Damu ya Osama Bin Laden itaendelea kubaki, kwa ruhusa ya Mwenyezi Mungu, laana inayowafuata wamarekani na jamaa zao, itawafuata ndani na nje ya nchi zao," imeonya taarifa hiyo.

"Furaha yao itakuwa masikitiko, na damu yao itachanganyika na machozi. Tunatoa wito kwa Waisilamu wenzetu nchini Pakistan, ambao katika ardhi yao Sheikh Osama aliuawa, wasimame na kupambana."

Waandishi wa habari wanasema Wapakistani wengi wamekasirishwa na kile wanachoona kama Marekani kuingilia uhuru wa nchi yaoMarekani wakisherekea kifo cha OsamaPia wanaishutumu serikali ya Pakistan kwa kuruhusu makomando wa Marekani kufanya shughuli zao, ingawa maafisa wanakanusha kuwa walifahamishwa.

Karibu watu 1,000 walikusanyika katikati ya mji wa Abbotabad baada ya sala ya Ijumaa, limeripoti shirika la habari la AFP.

Walichoma moto matairi ya magari, kuweka vikwazo katika barabara kuu na kupiga kelele wakisema "Hapana Marekani" na "magaisi, magaidi, Marekani ni magaidi".

Hata hivyo mwandishi wa BBC mjini Rawalpindi amesema maandamano ya kupinga Marekani yalikuwa madogo kuliko yalivyotarajiwa, huku watu 50 wakijitokeza


Another Osama Dead Body PhotoThis is the latest photo released of Osama Bin Laden Dead Body. The world hated Osama and now he is dead here are the pictures of his dead body to prove it. Osama is dead. Death to al qaeda. Osama Bin Laden pictures of body and death

Ouattara wa Ivory Coast aapishwaAlassane Ouattara anatarajiwa kuapishwa kuwa Rais wa Ivory Coast na mtu ambaye mwanzo alimkatalia ushindi wake katika uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi Novemba.

Mwezi Desemba, kiongozi wa baraza la katiba alimwidhinisha Laurent Gbagbo kuwa mshindi, iliyosababisha nafasi hiyo kushikiliwa naye kwa muda wa miezi minne.

Bw Gbagbo pia anatarajiwa kuhojiwa juu ya madai ya kukiuka haki za binadamu wakati akiwa madarakani.Bw Alassane Ouattara


Hata hivyo, imeripotiwa kuwa mawakili wake kutoka Ufaransa wamenyimwa ruhusa ya kuingia Ivory Coast.

Shirika la habari la AFP limesema walizuiwa kwenye uwanja wa ndege wa Abidjan na kutiwa kwenye ndege iliyofuata na kurejeshwa Paris.

Wakati huo huo, Umoja wa Ulaya unatarajiwa kuipa nchi hiyo msaada wa zaidi ya dola za kimarekani milioni 60.

Kamishna wa maendeleo wa Ulaya, Andris Piebalgs, ambaye yupo Ivory Coast, amesema inabidi waende kwa kasi.

Aliiambia BBC kuwa hali ilivyo nchini humo bado ina utata na kama maisha ya watu hayakuimarishwa haraka, ghasia zinaweza kuanza upya.

Alisema raia wa nchi hiyo wanahisi wamepoteza miaka 25 ya maendeleo kutokana na mapigano ya kisiasa na kikabila ya hivi karibuni.

Takriban watu 3,000 wanaaminiwa kuuawa wakati wa ghasia zilizotokea kwenye nchi inayozalisha kakao zaidi duniani, ambapo awali ilikuwa nchi yenye utajiri mkubwa Afrika magharibi.

Alipotokea

Alassane Ouatarra ni miongoni mwa kikundi kidogo cha watu ambao ni wasomi wa kisiasa nchini Ivory Coast, ambao harakati zao za kuwania madaraka zimeishia katika mapambano ya kupigania mji mkuu wa Abidjan mwezi uliopita.

Lakini mapambano hayo ya kuwania madaraka yalianza katika miaka ya mwanzo ya 1980.

Bw Ouatarra, ambae ni mtalamu wa uchumi aliyesomea Marekani, aliwahi kutumikia shirika la fedha la kimataifa IMF wakati huo na kwa muda mfupi aliteuliwa kuwa waziri mkuu.

Huo ndio ulikuwa mwanzo wa mchuano mkali kati ya Bw Ouatarra na watu wengine wawili.

Wote walikuwa vigogo kutoka chama kilichotawala wakati huo, Henri Konan Bedie, na Profesa wa Historia ambae wakati huu alijinasibu kuWa mwanaharakati wa kutetea demokrasia Laurent Gbagbo.

Silaha walizozitumia watu hao watatu katika vita vyao vya kisiasa zilikuwa ni asili yao ya mikoa ama makabila walikotoka na ushawishi wao wa kifedha.

Ni mwaka uliopita tu kwa msaada wa Umoja wa mataifa ndio kulianzishwa kitu kilichokaribia kuwa demokrasia ya vyama vingi.

Bw Ouatarra alishinda uchaguzi wa kwanza kabisa wa rais kwa njia ya mashindano wazi.

Lakini Bw Gbagbo, akipuuza madai yake ya kuwa mwanademokrasia alikataa kuachia madaraka.

Mapigano yaliyofuata yalisababisha zaidi ya watu 1,000 kuuawa, maelfu kupoteza makazi yao na kuangamiza uchumi wa taifa hili kuu la Afrika Magharibi.

Demokrasia ya Ivory Coast imekuja kwa gharama kubwa.

Alassane Ouatarra ameapishwa rasmi leo kuwa Rais wa Ivory Coast baada ya mgogoro wa kisiasa ulioifanya nchi hiyo kuingia katika vita.

Rais wa zamani Laurent Gbagbo alikataa kuachia madaraka baada ya kushindwa kwenye uchaguzi ulioshuhudiwa na ujumbe wa Umoja wa mataifa mwaka jana.

Gbagbo aliondolewa madarakani mwezi uliopita katika mapigano yaliyohusisha msaada wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa na Ufaransa.


Tendwa avibana vyama vya siasa
MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, ametaka vyama vya siasa kuwasilisha gharama za uchaguzi kuanzia ngazi ya Rais hadi madiwani ifikapo Julai 30.

Katika uchaguzi wa mwaka jana, vyama vya siasa vilianza kutekeleza sheria ya Gharama za Uchaguzi ambayo, ilivibana kwa kuweka viwango vya matumizi kwa kila ngazi huku kiti cha urais kikomo cha juu kikiwa ni Sh5 bilioni.
Akizungumzia utekelezaji wa sheria ofisini kwake Dares Salaam jana, Tendwa alisema vyama vyote vinapaswa kuitekeleza ifikapo Julai 30, mwaka huu.

Kwa mujibu wa Tendwa, kila chama kitapaswa kuwasilisha taarifa hiyo kuanzia ngazi ya urais, ubunge hadi udiwani.Msajili huyo alisema wapo wagombea ambao walifadhiliwa na chama na wengine kujifadhili wenyewe, watapaswa kuonyesha nyaraka halali za ufadhili huo.

"Tunajua kuna watakaosema walifadhiliwa na chama katika kampeni, hawa tutahitaji kupata uthibitisho wao na wapo watakaosema, wamejifadhili wenyewe nao watapaswa kufanya hivyo, ili nasi tumkabidhi CAG," alifafanua Tendwa.

Aliweka bayana kwamba, wapo wagombea ambao hawakutumia gharama zozote kutokana na kutoshiriki uchaguzi, huku wengine wakiwa wametumia chini ya kikomo cha juu cha matumizi, nao watapaswa kuwasilisha taarifa.
Kwa ufafanuzi zaidi, Tendwa alisema yupo mmoja wa wagombea urais (Fahmi Dovutwa), alijitoa ikiwa zimebaki siku chache za uchaguzi, lakini akaweka bayana kuwa naye anapaswa kuwasilisha taarifa.

"Kwa sababu alijitoa wakati tayari alishaingia kwenye orodha ya wagombea, atapaswa pia kuleta taarifa zake. Maana mwenyewe alijitoa akisema sijui jina lake limekosewa, lakini tayari alikuwa mgombea si haba naye amepata kura zake na niliwahi kumpa mkono wakati wa kutangazwa mshindi naye alihudhuria," alisema.

Dovutwa alijitoa kwa hiari kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa rais kwa tiketi ya UPDP, kutokana na kile alichokiita ni kukosewa kwa jina lake, hivyo akataka wapigakura wake walekeze nguvu zao kwa aliyekuwa mgombea wa CCM Rais Jakaya Kikwete, ambaye aliibuka mshindi kwa asilimia 61

Sheryl Cwele, afungwa miaka 12
Bi Sheryl Cwele


Sheryl Cwele, mke wa waziri wa masuala ya kijasusi, amehukumiwa kifungo cha miaka 12 jela kwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Cwele, aliyeolewa na Siyabonga Cwele, alikuwa akiajiri wanawake kuingiza dawa hizo nchini Afrika kusini kutoka Uturuki na Marekani ya kusini.

Cwele alikutwa na hatia pamoja na mwenzake Frank Nabolisa, raia wa Nigera, katika mahakama kuu ya Pietermaritzburg.

Mshirika wake huyo Nabolisa naye amepewa hukumu hiyo hiyo ya miaka 12.

Madai ya biashara ya dawa za kulevya yalianza mwaka 2009 baada ya kukamatwa kwa mwanamke mmoja raia wa Afrika kusini aliyekamatwa Brazil na aina ya cocaine yenye thamani ya dola za kimarekani 300,000.

Tessa Beetge kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka nane gerezani mjini Sao Paulo.

Alikutwa na kilo 10 za coaccaine kwenye mkoba wake.

Akitoa hukumu hiyo, Jaji Piet Koen alielezea makosa yao kuwa mazito mno.

Alisema, " Familia nyingi zinaathiriwa na dawa za kulevya zinazoletwa hapa kinyume cha sheria. Huteseka kutokana na wafanyabiashara wanaosababisha kutawaliwa na usambazaji wa mara kwa mara na kujikuta wakiwa wanaendela kutumia dawa hizo.

Watu hao wawili, ambao walikana mashtaka, walisema watakata rufaa dhidi ya hatia yao ya kufanya biashara hiyo.

Wangeweza kuhukumiwa kifungo cha miaka 15 jela.

Upinzani umetoa wito wa kumtaka Bw Cwele ajiuzulu, ukisema kama hajui shughuli za mkewe zilizo kinyume cha sheria, basi hana haja ya kuendelea kuongoza kitengo cha kijasusi nchini humo

TRA 'wambana' Dk Slaa

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), 'imemkaba kooni' Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) Dk. Willibrod Slaa, kufuatia tuhuma alizozitoa dhidi ya ofisa wa mamlaka hiyo kuisababishia serikali hasara ya mabilioni ya fedha.

Hivi karibu, gazeti moja lilimkariri Dk. Slaa akitaja majina ya watu mbalimbali wanaotuhumiwa kuwa ni mafisadi.Pia wakati akihutubia katika mkutano wake wa hadhara mkoani Tabora, alitaja orodha ya watuhumiwa hao akiwamo oafisa wa TRA, Placidus Luoga.Gazeti hilo lilimkariri Dk. Slaa akidai kuwa Luoga aliingizia serikali hasara ya Sh800 bilioni kwa kuzuia magari ya Kampuni ya Tango, Transport ya jijini Dar es Salaam kwa miaka 10 kwa kisingizio cha kutolipa kodi.

Alidai kuwa kitendo hicho, kiliilazimisha kampuni hiyo, kufungua kesi mahakamani ambako ilishinda na serikali kuamriwa kuilipa kiasi hicho cha fedha.Gazeti hilo lilimkariri kiongozi huyo wa Chadema akidai kuwa tayari serikali imeshailipa kampuni hiyo Sh500 milioni.

Hata hivyo jana TRA kupitia taarifa yake iliyotolewa na Idara ya Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi, imekanusha madai hayo na kuyaita kuwa uzushi tu wa Dk Slaa na kumtaka atoe uthibitisho wa madai yake hadharani.

"Huu ni uzushi unaopaswa kulaaniwa vikali kwa sababu unapotosha wananchi na hasa wasomaji wa magazeti. Dk. Slaa atoe nakala ya hukumu hiyo ili wananchi wamwamini. Bila kufanya hivyo kutaonyesha kuwa ametoa habari za uongo kwa kusingizia mahakama," ilisema taarifa.

Taarifa hiyo ilimtaka Dk. Slaa kutoa vielelezo vya maelezo yake hadharani na kwenye mkutano ili awathibitishie wananchi kuwa alichosema ni cha kweli.

TRA ilisema kama Dk. Slaa atashindwa kufanya hivyo, ni dhahiri kuwa yeye si mtu makini na ni mtu mwenye nia ya kupotosha umma wa Watanzania na kuchafua heshima ya Mamlaka ya Mapato Tanzania.

"Kudanganya watu kwa siri au hadharani ni aina mojawapo ya aina nyingi za kutokuwajibika. Kutokuwajibika kuna sura nyingi na uongo ni mojawapo. Dk. Slaa lazima ajisafishe na hili," ilisisitiza taarifa ya TRA. Taarifa hiyo ya TRA ilisema Luoga hajawahi kuzuia wala kukamata magari yanayodaiwa na Dk. Slaa.

"Hakuna ofisa wa TRA mwenye akili timamu anayeweza kukaa na mali ya mtu anayedaiwa kodi kwa miaka 10 huku akijua kuwa anatakiwa kukomboa kodi hiyo. Anatakiwa kuuza mali hiyo ili serikali ipate kodi; Kwa afisa yoyote aliye kwenda shule hawezi kufanya hivyo akishuhudia mlipa kodi anapeleka kesi Mahakamani ambako atapata fidia ya sh.800 bilioni," ilisema sehemu ya taarifa.


Ilisema hata kama ofisa huyu hajaenda shule, lakini hawezi kuhusika na mpango kama huo.
Ilisemwa mujibu wa maelezo ya Dk. Slaa,mahakama iliona kuwa Tango Trasport ya Dar es Salaam ilipata hasara ya wastani wa Sh80 bilioni kwa mwaka."Kwa biashara ya kawaida Tanzania, mahesabu kama haya hayawezi kuingia vyema kichwani kwa yeyote mwenye busara," imesisitiza TRA.

Hata hivyo TRA katika taarifa yake ilisisitiza kuwa Luoga haifahamu Kampuni ya Tango Transport ya jijini Dar es Salaam ambayo magari yake yamewahi kuzuiwa kwa muda wa miaka 10.

Imefafanua kuwa kumbukumbu zilizoko TRA zinaonyesha kuwa kampuni ya Tango Transport ni ya Arusha na kusisitiza kwamba hakuna taarifa zinazoeleza kuwa TRA imewahi kukamata magari ya kampuni hiyo kwa miaka 10.
Juhudi za gazeti hili kumpata Dk. Slaa kuzungumzia taarifa ya TRA hazikufanikiwa kwa kuwa simu yake ya mkononi haikuwa hewani


Libya: Waasi wajipanga baada ya Gaddafi


Chakula kimepungua maeneo ya waasi
Waasi wa Libya wametoa mwelekeo wa kisiasa kwa nchi hiyo iwapo Kanali Gaddafi ataondoka madarakani.

Mwelekeo huo unaonyesha kuanzishwa kwa serikali ya mpito wakati katiba mpya inaandikwa na uchaguzi kufanyika.

Mahmoud Jibril alitoa pendekezo la Libya baada ya Kanali Gaddafi katika mkutano wa kwa wajumbe wa nchi zinazounga mkono waasi uliofanyika Rome Italia.

Alifafanua kuwa serikali ya mpito itaanza kazi mara moja ili kutoa maekezo ya utendaji wa siku kwa siku na kuweka ulinzi, shirika la habari la AFP imeripoti.

Mahmoud Jibril,kiongozi wa Baraza la Kitaifa la Mpito (NTC) amekubaliana na mpango wa misaada uliopitishwa na nchi 22 zinazounga mkono waasi hao.

Katika habari nyingine, Ufaransa imewaamuru wanadiplomasia 14 wa Libya wanaomuunga mkono Kanali Gaddafi kuondoka nchini humo ndani ya siku mbili.

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa alisema maafisa hao wametajwa kuwa 'watu wasiotakiwa nchini humo.
JK aahidi ongezeko la mshahara kima cha chiniRAIS Jakaya Kikwete ameahidi kuongeza mshahara wa kima cha chini kwa wafanyakazi nchini katika bajeti ijayo.
Hayo yalisemwa na Rais Kikwete mjini Morogoro jana, katika viwanja vya Jamuhuri katika sherehe za Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani[May Day] yaliyofanyika mjini humo kitaifa.

Mchakato huo utaenda sambamba na maandalizi ya bajeti ya serikali kwa mwaka ujao wa fedha wa 2011/12.

Kipindi cha miaka mitano, serikali iliweza kupandisha kima cha chini cha mshahara kutoka shilingi. 48,000 hadi 180,000 ikiwa ni dhamira ya serikali ni kuimarisha na kuboresha maslahi ya watumishi kadri inavyowezekana.

Raisi Kikwete pia aliwataka na kuwaonya waajiri kote nchini kujali maslahi ya wafanyakazi wao ili kuboresha gharama za upandaji wa maisha na kutoa onyo kwa ambaye atakaidi ongezeko hilo

Bin Laden 'alipanga shambulizi jipya'
Usafiri wa reli MarekaniNyaraka zilizopatikana katika nyumba ya Osama Bin Laden zinaonyesha kuwa alikuwa na mipango ya kuishambulia tena Marekani ikiwemo wakati wa maadhimisho ya miaka kumi ya Septemba 11, taarifa kutoka Marekani zimearifu.

Mpango mmoja ulilenga kushambulia usafiri wa reli Marekani, ripoti zinasema, ingawa hakukuwa na taarifa za tishio la moja kwa moja lililogunduliwa.

Maafisa wanachunguza kompyuta, DVDs na nyaraka nyingine zilizochukuliwa kutoka kwenye nyumba hiyo Abbottabad ambako wanaamini Bin Laden alijificha kwa miaka sita.

Rais Obama anatarajia kukutana na baadhi ya vikosi vilivyohusika katika operesheni hiyo.

Atakuwa na mkutano wa faragha Fort Campbell, Kentucky, na baadhi ya Wanamaji walioendesha operesheni hiyo.

Alhamis, Rais Obama alizuru eneo la Ground Zero lililokumbwa na shambulio la Septemba 11 2001 mjini New York , na kuweka shada la maua ikiwa ni kumbukumbu ya karibu watu 3,000 waliothiriwa na shambulio hilo.

Aliziambia familia za waliothiriwa kuwa haki sasa imetendeka lakini Marekani 'haitasahau.
Magari ya mitumba yaitikisa Chadema

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimekiri kwamba suala la ununuzi wa magari yaliyotumika lilizua mjadala kwenye kikao chake cha Kamati Kuu kilichomalizika Jumatatu wiki hii.

Maelezo ya mvutano huo yalitolewa jana na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari baada ya gazeti hili toleo la Jumatatu kuandika juu ya suala hilo.

Hata hivyo, Dk Slaa alisisitiza kuwa mvutano huo ulikuwa wa kawaida hasa ikizingatiwa kuwa ni suala ambalo haliepukiki penye mjadala wa watu wengi akisisitiza kwamba demokrasia ndiyo iliyoamua.
Gazeti hili liliripoti kuwa mkutano huo ulitokana na baadhi ya wajumbe kupinga na wengine kuunga mkono suala la ununuzi wa magari yaliyotumika yenye thamani ya Sh480 milioni.

Baadhi ya waliokuwa wanapinga mkakati huo walisema kuwa ulikuwa unalenga kumnufaisha Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe ambaye alikuwa achukue nafasi hiyo kukiuzia chama magari ambayo tayari ameyatumia.

Miongoni mwa wajumbe wa Baraza hilo, Profesa Mwesiga Baregu na Dk Kitila Mkumbo walinukuliwa wakisema kwamba isingekuwa sahihi kwa chama hicho kinachopinga ufisadi kufanya ufisadi kwa kununua magari chakavu wakati wamekuwa wakiibana serikali.

Akitoa ufafanuzi huo jana, Dk Slaa alisema msuguano huo ulikuwa ni wa kawaida na ulikuwa sehemu ya kuwezesha demokrasia kuchukua mkondo wake. Alikiri kuwa kwenye mchakato huo, Mbowe ana magari matatu ambayo chama kinataka kuyanunua.

Alisema hoja hiyo ilimalizika kwa Baraza kuamua kuwa Mbowe aendelee kushawishiwa ili akubali kukiuzia chama magari hayo. Alielezea kuwa magari hayo aliyanunua na yakaanza kutumiwa na chama kwenye kampeni za uchaguzi uliopita.

"Magari hayo Mheshimiwa Mbowe aliyanunua kwa ajili ya biashara zake lakini kwa kuwa chama kilikuwa katika matatizo ya usafiri, akakubali kuyatoa yakisaidie ili baadaye tumrejeshee," alisema Dk Slaa na kuongeza kuwa magari mawili yanaendelea kutumiwa na chama hivyo ni vyema wayanunue.

Kuhusu chama hicho kununua vitu vilivyotumika wakati kimekuwa kikiipinga vikali serikali kutumia vitu vilivyotumika, Dk Slaa alisema njia inayotumiwa na Chadema iko wazi zaidi ukilinganisha na ile ya serikali.
Alidai kuwa kwenye michakato ya ununuzi serikalini kuna mazingira mengi yanayoruhusu ufisadi hasa katika kujadili bei lakini suala la kununua magari ya Mbowe, suala kama hilo haliwezi kupata nafasi.

Mshahara wa Dk Slaa
Katika hatua nyingine, Mbowe alisema kuwa chama hicho kimeamua kumlipa Dk Slaa mshahara na maslahi yanayolingana na anayopata mbunge.Alisema hiyo ni kwa sababu chama hicho ndicho kilichokuwa kimemshawishi aache kugombea ubunge katika Jimbo la Karatu, Arusha ambako alikuwa na nafasi kubwa ya kushinda na kumtaka agombee urais ambao mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete alitangazwa kuwa mshindi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mbowe alisema uamuzi huo ulifuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na vikao vikuu vya chama hicho, kama vile Kamati Kuu na kisha kuidhinisha malipo hayo.

"Itakumbukwa kuwa Mheshimiwa Dk Slaa hakuomba nafasi ya kugombea uraisi, aliombwa. Tunajua alikuwa mbunge na alikuwa na nafasi kubwa ya kushinda tena nafasi hiyo, lakini akakubali ombi la chama," alisema Mbowe na kuongeza: "Hii siyo mchezo! Uamuzi wa namna hiyo ni wa kujitoa. Ndiyo maana Kamati Kuu ikakubali apate mshahara na marupurupu sawa na yale ya mbunge."

Mbunge anakadiriwa kuwa anapata mshahara pamoja na marupurupu yanayokaribia kufikia Sh7 milioni kwa mwezi.

Chadema kilitumia Sh1.3 bilioni kusaka urais 2010
Akizungumzia Uchaguzi Mkuu uliopita, Mbowe aliwaambia waandishi wa habari kuwa chama chake kilitumia Sh1.3 bilioni katika kampeni za uras.

Alivitaja vyanzo vya fedha hizo kuwa ni Sh 338.9 milioni za ruzuku, Sh 235.9 milioni kutoka kwa marafiki, Sh32 milioni michango mbalimbali ya wanachama na mali mbalimbali za watu zenye thamani ya Sh719.7 milioni.

Jeshi la Polisi lawatahadharisha wanawake
JESHI la polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewatahadharisha wanawake nchini, kutodanganyika kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na wanaume papo kwa papo kwa kuwa kumekuwa na wimbi la mauaji wanawake baada ya kujitokeza mwanaume anayewarubuni
Akizungumza na wanahabari Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suileman Kova, amesema amejitokeza mwanaume anayetuhumiwa kuua wanawake waliofikia wanne jijini Dar es Salaam katika maeneo ya Tandika, Keko, Mtoni kwa Azizi Ally na Buguruni kwa Mnyamani katika kipindi cha miezi mitatu.

Amesema mwanaume huyo amekuwa akirubuni wanawake hao kimapenzi kwa kuwaahidi donge nono la fedha na kisha kwenda nao katika nyumba za kulala wageni na kuwalazimisha kufanya mapenzi kinyume na maumbile na anapomaliza haja zake kuwanyonga.

Kova amesema katika uchunguzi uliofanywa na jeshi la polisi limebaini kuwa katika nyumba zote za wageni walizouawa wanawake hao wamebaini ni mwanaume wa aina moja ambaye wahudumu wa nyumba hizo walipoeleza mazingira na maelezo yao yamefafana na kudai kuwa mwanaume huyo hupendelea kuvaa vazi la T-shirt na suruali aina ya jeans, mweupe, mtanashati na kukadiriwa kuwa na miaka 30 hadi 32.

Kova amesema mtuhumiwa huyo ambaye anasakwa ameonekana kuwalenga wanawake ambao wako ndoani [wake za watu] kwa kuwarubuni kuwaahidi fedha nzuri na kasha kuwanyonga na kutokome bila hata kuiba kitu chochote kutoka kwa marehemu.
.
Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi kumsaka mtuhumiwa huyo kumkamata na kumchukulia hatua zinazostahili na jamii wametakwi kutoa ushirikiano katika suala hilo
Obama azuru eneo la mashambulizi 9/11


Rais Obama akiweka shada la maua katika eneo la mashambulizi mjini New York.Rais wa Marekani Barack Obama amezuru eneo ambalo mashambulizi ya 11 Septemba yalitokea mjini New York.

Ziara hiyo inafanyika siku nne baada ya kuuawa kwa kiongozi wa kundi la Al-Qaeda Osama Bin Laden, nchini Pakistan.

Inaaminika Bin Laden ndiye aliyepanga mashambulizi hayo ya 9/11 mwaka wa 2001.

Rais Obama aliweka shada la maua kuwakumbuka takriban watu 3000 waliofariki na pia kuzungumza na jamaa zao katika eneo hilo.

Awali Obama aliwaambia maafisa wa kikosi cha kuzima moto kuwa: ''Wakati tunaposema hatuwezi tukasahau, tunamaanisha vivyo hivyo''.

Ziara hiyo inakuja siku moja baada ya rais wa Marekani kusema hatachapisha picha ya mwili wa Osama Bin Laden.

Kiongozi huyo wa Al-Qaeda aliuwawa na vikosi maalum vya jeshi la Marekani kaskazini mwa Pakistan siku ya Jumatatu.

Baadaye mwili wake ulizikwa kwenye bahari kutoka kwa ndege ya Marekani iliyokuwa imembeba.

Majeshi ya Pakistan yalikiri kushindwa kugundua alikojificha Bin Laden na kusema wataanzisha uchunguzi.

Pakistan pia imedokeza kuwa itatizama upya ushirikiano kati yake na Marekani iwapo kutatokea uvamizi mwingine bila ya wao kufahamishwa kama ilivyofanyika na Osama bin Laden

Besigye kupelekwa ng'ambo kwa matibabu
Kiongozi wa Upinzani nchini Uganda Dkt Kizza Besigye atapelekwa ng'ambo kwa matibabu zaidi.

Mkewe kiongozi huyo Bi Winnie Byanyima aliambia BBC kuwa madaktari wanaomshughulikia mwanasiasa huo katika hospitali moja Mjini Nairobi wanahofia kuwa Besigye alipata madhara makubwa ya sumu kwenye ngozi na macho yake.

Kiongozi huyo wa upinzani alisafirishwa hadi Nairobi kwa matibabu zaidi baada ya kupigwa na polisi wa Uganda wakati wa kuzima maandamano aliyokuwa akiongoza ya kutembea kwa miguu hadi kazini kupinga kuongezeka kwa gharama ya maisha nchini Uganda.

Bi Byanyima amemuomba Rais Yoweri Museveni kufanya mashauriano na upinzani pamoja na viongozi wa Kidini ili kutafuta suluhu juu ya matatizo yanayoikumba Uganda badala ya kuwa timua nguvu kupita kiasi kutawanya maandamano

No comments:

Post a Comment