KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, May 7, 2011

Al-Qaeda yathibitisha kifo cha Osama




Al-Qaeda imethibitisha kifo cha kiongozi wake, Osama Bin aden, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kundi hilo na kutangazwa kupitia mitandao mbalimbali ya itikadi kali






Taarifa inayothibitisha kifo


Tarifa hiyo imesema damu ya kiongozi huyo "haitapotea" na kuwa al-Qaeda itaendelea kushambulia Marekani na washirika wake.

Kifo cha Bin Laden kitakuwa "laana" kwa Marekani, na kutoa wito kwa Pakistan kuanza harakani, imesema taarifa hiyo.

Bin Laden alipigwa risasi na kufa siku ya Jumatatu, wakati makomando wa Marekani walipovamia nyumba yake katika mji wa Abbottabad nchini Pakistan.







Osama Bin Laden


Uvamizi huo ulifanywa bila ya mamlka za Pakistan kufahamu, na hivyo kuongeza mvutano kati ya nchi hizo mbili.

Mikutano kadhaa ya hadhara inafanyika nchini Pakistan siku ya Ijumaa, kupinga hatua hiyo.

Taarifa hiyo iliyochapishwa katika mitandao yenye itikadi kali imesema sauti ya kiongozi huyo wa al-Qaeda iliyorekodiwa wiki moja kabla ya kifo chake itatolewa hivi karibuni.







Makazi ya Bin Laden, Pakistan


"Damu ya Osama Bin Laden itaendelea kubaki, kwa ruhusa ya Mwenyezi Mungu, laana inayowafuata wamarekani na jamaa zao, itawafuata ndani na nje ya nchi zao," imeonya taarifa hiyo.

"Furaha yao itakuwa masikitiko, na damu yao itachanganyika na machozi. Tunatoa wito kwa Waisilamu wenzetu nchini Pakistan, ambao katika ardhi yao Sheikh Osama aliuawa, wasimame na kupambana."

Waandishi wa habari wanasema Wapakistani wengi wamekasirishwa na kile wanachoona kama Marekani kuingilia uhuru wa nchi yao



Marekani wakisherekea kifo cha Osama



Pia wanaishutumu serikali ya Pakistan kwa kuruhusu makomando wa Marekani kufanya shughuli zao, ingawa maafisa wanakanusha kuwa walifahamishwa.

Karibu watu 1,000 walikusanyika katikati ya mji wa Abbotabad baada ya sala ya Ijumaa, limeripoti shirika la habari la AFP.

Walichoma moto matairi ya magari, kuweka vikwazo katika barabara kuu na kupiga kelele wakisema "Hapana Marekani" na "magaisi, magaidi, Marekani ni magaidi".

Hata hivyo mwandishi wa BBC mjini Rawalpindi amesema maandamano ya kupinga Marekani yalikuwa madogo kuliko yalivyotarajiwa, huku watu 50 wakijitokeza






Another Osama Dead Body Photo







This is the latest photo released of Osama Bin Laden Dead Body. The world hated Osama and now he is dead here are the pictures of his dead body to prove it. Osama is dead. Death to al qaeda. Osama Bin Laden pictures of body and death





Ouattara wa Ivory Coast aapishwa



Alassane Ouattara anatarajiwa kuapishwa kuwa Rais wa Ivory Coast na mtu ambaye mwanzo alimkatalia ushindi wake katika uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi Novemba.

Mwezi Desemba, kiongozi wa baraza la katiba alimwidhinisha Laurent Gbagbo kuwa mshindi, iliyosababisha nafasi hiyo kushikiliwa naye kwa muda wa miezi minne.

Bw Gbagbo pia anatarajiwa kuhojiwa juu ya madai ya kukiuka haki za binadamu wakati akiwa madarakani.



Bw Alassane Ouattara


Hata hivyo, imeripotiwa kuwa mawakili wake kutoka Ufaransa wamenyimwa ruhusa ya kuingia Ivory Coast.

Shirika la habari la AFP limesema walizuiwa kwenye uwanja wa ndege wa Abidjan na kutiwa kwenye ndege iliyofuata na kurejeshwa Paris.

Wakati huo huo, Umoja wa Ulaya unatarajiwa kuipa nchi hiyo msaada wa zaidi ya dola za kimarekani milioni 60.

Kamishna wa maendeleo wa Ulaya, Andris Piebalgs, ambaye yupo Ivory Coast, amesema inabidi waende kwa kasi.

Aliiambia BBC kuwa hali ilivyo nchini humo bado ina utata na kama maisha ya watu hayakuimarishwa haraka, ghasia zinaweza kuanza upya.

Alisema raia wa nchi hiyo wanahisi wamepoteza miaka 25 ya maendeleo kutokana na mapigano ya kisiasa na kikabila ya hivi karibuni.

Takriban watu 3,000 wanaaminiwa kuuawa wakati wa ghasia zilizotokea kwenye nchi inayozalisha kakao zaidi duniani, ambapo awali ilikuwa nchi yenye utajiri mkubwa Afrika magharibi.

Alipotokea

Alassane Ouatarra ni miongoni mwa kikundi kidogo cha watu ambao ni wasomi wa kisiasa nchini Ivory Coast, ambao harakati zao za kuwania madaraka zimeishia katika mapambano ya kupigania mji mkuu wa Abidjan mwezi uliopita.

Lakini mapambano hayo ya kuwania madaraka yalianza katika miaka ya mwanzo ya 1980.

Bw Ouatarra, ambae ni mtalamu wa uchumi aliyesomea Marekani, aliwahi kutumikia shirika la fedha la kimataifa IMF wakati huo na kwa muda mfupi aliteuliwa kuwa waziri mkuu.

Huo ndio ulikuwa mwanzo wa mchuano mkali kati ya Bw Ouatarra na watu wengine wawili.

Wote walikuwa vigogo kutoka chama kilichotawala wakati huo, Henri Konan Bedie, na Profesa wa Historia ambae wakati huu alijinasibu kuWa mwanaharakati wa kutetea demokrasia Laurent Gbagbo.

Silaha walizozitumia watu hao watatu katika vita vyao vya kisiasa zilikuwa ni asili yao ya mikoa ama makabila walikotoka na ushawishi wao wa kifedha.

Ni mwaka uliopita tu kwa msaada wa Umoja wa mataifa ndio kulianzishwa kitu kilichokaribia kuwa demokrasia ya vyama vingi.

Bw Ouatarra alishinda uchaguzi wa kwanza kabisa wa rais kwa njia ya mashindano wazi.

Lakini Bw Gbagbo, akipuuza madai yake ya kuwa mwanademokrasia alikataa kuachia madaraka.

Mapigano yaliyofuata yalisababisha zaidi ya watu 1,000 kuuawa, maelfu kupoteza makazi yao na kuangamiza uchumi wa taifa hili kuu la Afrika Magharibi.

Demokrasia ya Ivory Coast imekuja kwa gharama kubwa.

Alassane Ouatarra ameapishwa rasmi leo kuwa Rais wa Ivory Coast baada ya mgogoro wa kisiasa ulioifanya nchi hiyo kuingia katika vita.

Rais wa zamani Laurent Gbagbo alikataa kuachia madaraka baada ya kushindwa kwenye uchaguzi ulioshuhudiwa na ujumbe wa Umoja wa mataifa mwaka jana.

Gbagbo aliondolewa madarakani mwezi uliopita katika mapigano yaliyohusisha msaada wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa na Ufaransa.










Tendwa avibana vyama vya siasa




MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, ametaka vyama vya siasa kuwasilisha gharama za uchaguzi kuanzia ngazi ya Rais hadi madiwani ifikapo Julai 30.

Katika uchaguzi wa mwaka jana, vyama vya siasa vilianza kutekeleza sheria ya Gharama za Uchaguzi ambayo, ilivibana kwa kuweka viwango vya matumizi kwa kila ngazi huku kiti cha urais kikomo cha juu kikiwa ni Sh5 bilioni.
Akizungumzia utekelezaji wa sheria ofisini kwake Dares Salaam jana, Tendwa alisema vyama vyote vinapaswa kuitekeleza ifikapo Julai 30, mwaka huu.

Kwa mujibu wa Tendwa, kila chama kitapaswa kuwasilisha taarifa hiyo kuanzia ngazi ya urais, ubunge hadi udiwani.Msajili huyo alisema wapo wagombea ambao walifadhiliwa na chama na wengine kujifadhili wenyewe, watapaswa kuonyesha nyaraka halali za ufadhili huo.

"Tunajua kuna watakaosema walifadhiliwa na chama katika kampeni, hawa tutahitaji kupata uthibitisho wao na wapo watakaosema, wamejifadhili wenyewe nao watapaswa kufanya hivyo, ili nasi tumkabidhi CAG," alifafanua Tendwa.

Aliweka bayana kwamba, wapo wagombea ambao hawakutumia gharama zozote kutokana na kutoshiriki uchaguzi, huku wengine wakiwa wametumia chini ya kikomo cha juu cha matumizi, nao watapaswa kuwasilisha taarifa.
Kwa ufafanuzi zaidi, Tendwa alisema yupo mmoja wa wagombea urais (Fahmi Dovutwa), alijitoa ikiwa zimebaki siku chache za uchaguzi, lakini akaweka bayana kuwa naye anapaswa kuwasilisha taarifa.

"Kwa sababu alijitoa wakati tayari alishaingia kwenye orodha ya wagombea, atapaswa pia kuleta taarifa zake. Maana mwenyewe alijitoa akisema sijui jina lake limekosewa, lakini tayari alikuwa mgombea si haba naye amepata kura zake na niliwahi kumpa mkono wakati wa kutangazwa mshindi naye alihudhuria," alisema.

Dovutwa alijitoa kwa hiari kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa rais kwa tiketi ya UPDP, kutokana na kile alichokiita ni kukosewa kwa jina lake, hivyo akataka wapigakura wake walekeze nguvu zao kwa aliyekuwa mgombea wa CCM Rais Jakaya Kikwete, ambaye aliibuka mshindi kwa asilimia 61

Sheryl Cwele, afungwa miaka 12








Bi Sheryl Cwele


Sheryl Cwele, mke wa waziri wa masuala ya kijasusi, amehukumiwa kifungo cha miaka 12 jela kwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Cwele, aliyeolewa na Siyabonga Cwele, alikuwa akiajiri wanawake kuingiza dawa hizo nchini Afrika kusini kutoka Uturuki na Marekani ya kusini.

Cwele alikutwa na hatia pamoja na mwenzake Frank Nabolisa, raia wa Nigera, katika mahakama kuu ya Pietermaritzburg.

Mshirika wake huyo Nabolisa naye amepewa hukumu hiyo hiyo ya miaka 12.

Madai ya biashara ya dawa za kulevya yalianza mwaka 2009 baada ya kukamatwa kwa mwanamke mmoja raia wa Afrika kusini aliyekamatwa Brazil na aina ya cocaine yenye thamani ya dola za kimarekani 300,000.

Tessa Beetge kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka nane gerezani mjini Sao Paulo.

Alikutwa na kilo 10 za coaccaine kwenye mkoba wake.

Akitoa hukumu hiyo, Jaji Piet Koen alielezea makosa yao kuwa mazito mno.

Alisema, " Familia nyingi zinaathiriwa na dawa za kulevya zinazoletwa hapa kinyume cha sheria. Huteseka kutokana na wafanyabiashara wanaosababisha kutawaliwa na usambazaji wa mara kwa mara na kujikuta wakiwa wanaendela kutumia dawa hizo.

Watu hao wawili, ambao walikana mashtaka, walisema watakata rufaa dhidi ya hatia yao ya kufanya biashara hiyo.

Wangeweza kuhukumiwa kifungo cha miaka 15 jela.

Upinzani umetoa wito wa kumtaka Bw Cwele ajiuzulu, ukisema kama hajui shughuli za mkewe zilizo kinyume cha sheria, basi hana haja ya kuendelea kuongoza kitengo cha kijasusi nchini humo









TRA 'wambana' Dk Slaa









MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), 'imemkaba kooni' Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) Dk. Willibrod Slaa, kufuatia tuhuma alizozitoa dhidi ya ofisa wa mamlaka hiyo kuisababishia serikali hasara ya mabilioni ya fedha.

Hivi karibu, gazeti moja lilimkariri Dk. Slaa akitaja majina ya watu mbalimbali wanaotuhumiwa kuwa ni mafisadi.Pia wakati akihutubia katika mkutano wake wa hadhara mkoani Tabora, alitaja orodha ya watuhumiwa hao akiwamo oafisa wa TRA, Placidus Luoga.Gazeti hilo lilimkariri Dk. Slaa akidai kuwa Luoga aliingizia serikali hasara ya Sh800 bilioni kwa kuzuia magari ya Kampuni ya Tango, Transport ya jijini Dar es Salaam kwa miaka 10 kwa kisingizio cha kutolipa kodi.

Alidai kuwa kitendo hicho, kiliilazimisha kampuni hiyo, kufungua kesi mahakamani ambako ilishinda na serikali kuamriwa kuilipa kiasi hicho cha fedha.Gazeti hilo lilimkariri kiongozi huyo wa Chadema akidai kuwa tayari serikali imeshailipa kampuni hiyo Sh500 milioni.

Hata hivyo jana TRA kupitia taarifa yake iliyotolewa na Idara ya Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi, imekanusha madai hayo na kuyaita kuwa uzushi tu wa Dk Slaa na kumtaka atoe uthibitisho wa madai yake hadharani.

"Huu ni uzushi unaopaswa kulaaniwa vikali kwa sababu unapotosha wananchi na hasa wasomaji wa magazeti. Dk. Slaa atoe nakala ya hukumu hiyo ili wananchi wamwamini. Bila kufanya hivyo kutaonyesha kuwa ametoa habari za uongo kwa kusingizia mahakama," ilisema taarifa.

Taarifa hiyo ilimtaka Dk. Slaa kutoa vielelezo vya maelezo yake hadharani na kwenye mkutano ili awathibitishie wananchi kuwa alichosema ni cha kweli.

TRA ilisema kama Dk. Slaa atashindwa kufanya hivyo, ni dhahiri kuwa yeye si mtu makini na ni mtu mwenye nia ya kupotosha umma wa Watanzania na kuchafua heshima ya Mamlaka ya Mapato Tanzania.

"Kudanganya watu kwa siri au hadharani ni aina mojawapo ya aina nyingi za kutokuwajibika. Kutokuwajibika kuna sura nyingi na uongo ni mojawapo. Dk. Slaa lazima ajisafishe na hili," ilisisitiza taarifa ya TRA. Taarifa hiyo ya TRA ilisema Luoga hajawahi kuzuia wala kukamata magari yanayodaiwa na Dk. Slaa.

"Hakuna ofisa wa TRA mwenye akili timamu anayeweza kukaa na mali ya mtu anayedaiwa kodi kwa miaka 10 huku akijua kuwa anatakiwa kukomboa kodi hiyo. Anatakiwa kuuza mali hiyo ili serikali ipate kodi; Kwa afisa yoyote aliye kwenda shule hawezi kufanya hivyo akishuhudia mlipa kodi anapeleka kesi Mahakamani ambako atapata fidia ya sh.800 bilioni," ilisema sehemu ya taarifa.


Ilisema hata kama ofisa huyu hajaenda shule, lakini hawezi kuhusika na mpango kama huo.
Ilisemwa mujibu wa maelezo ya Dk. Slaa,mahakama iliona kuwa Tango Trasport ya Dar es Salaam ilipata hasara ya wastani wa Sh80 bilioni kwa mwaka."Kwa biashara ya kawaida Tanzania, mahesabu kama haya hayawezi kuingia vyema kichwani kwa yeyote mwenye busara," imesisitiza TRA.

Hata hivyo TRA katika taarifa yake ilisisitiza kuwa Luoga haifahamu Kampuni ya Tango Transport ya jijini Dar es Salaam ambayo magari yake yamewahi kuzuiwa kwa muda wa miaka 10.

Imefafanua kuwa kumbukumbu zilizoko TRA zinaonyesha kuwa kampuni ya Tango Transport ni ya Arusha na kusisitiza kwamba hakuna taarifa zinazoeleza kuwa TRA imewahi kukamata magari ya kampuni hiyo kwa miaka 10.
Juhudi za gazeti hili kumpata Dk. Slaa kuzungumzia taarifa ya TRA hazikufanikiwa kwa kuwa simu yake ya mkononi haikuwa hewani






Libya: Waasi wajipanga baada ya Gaddafi






Chakula kimepungua maeneo ya waasi
Waasi wa Libya wametoa mwelekeo wa kisiasa kwa nchi hiyo iwapo Kanali Gaddafi ataondoka madarakani.

Mwelekeo huo unaonyesha kuanzishwa kwa serikali ya mpito wakati katiba mpya inaandikwa na uchaguzi kufanyika.

Mahmoud Jibril alitoa pendekezo la Libya baada ya Kanali Gaddafi katika mkutano wa kwa wajumbe wa nchi zinazounga mkono waasi uliofanyika Rome Italia.

Alifafanua kuwa serikali ya mpito itaanza kazi mara moja ili kutoa maekezo ya utendaji wa siku kwa siku na kuweka ulinzi, shirika la habari la AFP imeripoti.

Mahmoud Jibril,kiongozi wa Baraza la Kitaifa la Mpito (NTC) amekubaliana na mpango wa misaada uliopitishwa na nchi 22 zinazounga mkono waasi hao.

Katika habari nyingine, Ufaransa imewaamuru wanadiplomasia 14 wa Libya wanaomuunga mkono Kanali Gaddafi kuondoka nchini humo ndani ya siku mbili.

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa alisema maafisa hao wametajwa kuwa 'watu wasiotakiwa nchini humo.








JK aahidi ongezeko la mshahara kima cha chini







RAIS Jakaya Kikwete ameahidi kuongeza mshahara wa kima cha chini kwa wafanyakazi nchini katika bajeti ijayo.
Hayo yalisemwa na Rais Kikwete mjini Morogoro jana, katika viwanja vya Jamuhuri katika sherehe za Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani[May Day] yaliyofanyika mjini humo kitaifa.

Mchakato huo utaenda sambamba na maandalizi ya bajeti ya serikali kwa mwaka ujao wa fedha wa 2011/12.

Kipindi cha miaka mitano, serikali iliweza kupandisha kima cha chini cha mshahara kutoka shilingi. 48,000 hadi 180,000 ikiwa ni dhamira ya serikali ni kuimarisha na kuboresha maslahi ya watumishi kadri inavyowezekana.

Raisi Kikwete pia aliwataka na kuwaonya waajiri kote nchini kujali maslahi ya wafanyakazi wao ili kuboresha gharama za upandaji wa maisha na kutoa onyo kwa ambaye atakaidi ongezeko hilo









Bin Laden 'alipanga shambulizi jipya'




Usafiri wa reli Marekani



Nyaraka zilizopatikana katika nyumba ya Osama Bin Laden zinaonyesha kuwa alikuwa na mipango ya kuishambulia tena Marekani ikiwemo wakati wa maadhimisho ya miaka kumi ya Septemba 11, taarifa kutoka Marekani zimearifu.

Mpango mmoja ulilenga kushambulia usafiri wa reli Marekani, ripoti zinasema, ingawa hakukuwa na taarifa za tishio la moja kwa moja lililogunduliwa.

Maafisa wanachunguza kompyuta, DVDs na nyaraka nyingine zilizochukuliwa kutoka kwenye nyumba hiyo Abbottabad ambako wanaamini Bin Laden alijificha kwa miaka sita.

Rais Obama anatarajia kukutana na baadhi ya vikosi vilivyohusika katika operesheni hiyo.

Atakuwa na mkutano wa faragha Fort Campbell, Kentucky, na baadhi ya Wanamaji walioendesha operesheni hiyo.

Alhamis, Rais Obama alizuru eneo la Ground Zero lililokumbwa na shambulio la Septemba 11 2001 mjini New York , na kuweka shada la maua ikiwa ni kumbukumbu ya karibu watu 3,000 waliothiriwa na shambulio hilo.

Aliziambia familia za waliothiriwa kuwa haki sasa imetendeka lakini Marekani 'haitasahau.








Magari ya mitumba yaitikisa Chadema









CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimekiri kwamba suala la ununuzi wa magari yaliyotumika lilizua mjadala kwenye kikao chake cha Kamati Kuu kilichomalizika Jumatatu wiki hii.

Maelezo ya mvutano huo yalitolewa jana na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari baada ya gazeti hili toleo la Jumatatu kuandika juu ya suala hilo.

Hata hivyo, Dk Slaa alisisitiza kuwa mvutano huo ulikuwa wa kawaida hasa ikizingatiwa kuwa ni suala ambalo haliepukiki penye mjadala wa watu wengi akisisitiza kwamba demokrasia ndiyo iliyoamua.
Gazeti hili liliripoti kuwa mkutano huo ulitokana na baadhi ya wajumbe kupinga na wengine kuunga mkono suala la ununuzi wa magari yaliyotumika yenye thamani ya Sh480 milioni.

Baadhi ya waliokuwa wanapinga mkakati huo walisema kuwa ulikuwa unalenga kumnufaisha Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe ambaye alikuwa achukue nafasi hiyo kukiuzia chama magari ambayo tayari ameyatumia.

Miongoni mwa wajumbe wa Baraza hilo, Profesa Mwesiga Baregu na Dk Kitila Mkumbo walinukuliwa wakisema kwamba isingekuwa sahihi kwa chama hicho kinachopinga ufisadi kufanya ufisadi kwa kununua magari chakavu wakati wamekuwa wakiibana serikali.

Akitoa ufafanuzi huo jana, Dk Slaa alisema msuguano huo ulikuwa ni wa kawaida na ulikuwa sehemu ya kuwezesha demokrasia kuchukua mkondo wake. Alikiri kuwa kwenye mchakato huo, Mbowe ana magari matatu ambayo chama kinataka kuyanunua.

Alisema hoja hiyo ilimalizika kwa Baraza kuamua kuwa Mbowe aendelee kushawishiwa ili akubali kukiuzia chama magari hayo. Alielezea kuwa magari hayo aliyanunua na yakaanza kutumiwa na chama kwenye kampeni za uchaguzi uliopita.

"Magari hayo Mheshimiwa Mbowe aliyanunua kwa ajili ya biashara zake lakini kwa kuwa chama kilikuwa katika matatizo ya usafiri, akakubali kuyatoa yakisaidie ili baadaye tumrejeshee," alisema Dk Slaa na kuongeza kuwa magari mawili yanaendelea kutumiwa na chama hivyo ni vyema wayanunue.

Kuhusu chama hicho kununua vitu vilivyotumika wakati kimekuwa kikiipinga vikali serikali kutumia vitu vilivyotumika, Dk Slaa alisema njia inayotumiwa na Chadema iko wazi zaidi ukilinganisha na ile ya serikali.
Alidai kuwa kwenye michakato ya ununuzi serikalini kuna mazingira mengi yanayoruhusu ufisadi hasa katika kujadili bei lakini suala la kununua magari ya Mbowe, suala kama hilo haliwezi kupata nafasi.

Mshahara wa Dk Slaa
Katika hatua nyingine, Mbowe alisema kuwa chama hicho kimeamua kumlipa Dk Slaa mshahara na maslahi yanayolingana na anayopata mbunge.Alisema hiyo ni kwa sababu chama hicho ndicho kilichokuwa kimemshawishi aache kugombea ubunge katika Jimbo la Karatu, Arusha ambako alikuwa na nafasi kubwa ya kushinda na kumtaka agombee urais ambao mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete alitangazwa kuwa mshindi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mbowe alisema uamuzi huo ulifuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na vikao vikuu vya chama hicho, kama vile Kamati Kuu na kisha kuidhinisha malipo hayo.

"Itakumbukwa kuwa Mheshimiwa Dk Slaa hakuomba nafasi ya kugombea uraisi, aliombwa. Tunajua alikuwa mbunge na alikuwa na nafasi kubwa ya kushinda tena nafasi hiyo, lakini akakubali ombi la chama," alisema Mbowe na kuongeza: "Hii siyo mchezo! Uamuzi wa namna hiyo ni wa kujitoa. Ndiyo maana Kamati Kuu ikakubali apate mshahara na marupurupu sawa na yale ya mbunge."

Mbunge anakadiriwa kuwa anapata mshahara pamoja na marupurupu yanayokaribia kufikia Sh7 milioni kwa mwezi.

Chadema kilitumia Sh1.3 bilioni kusaka urais 2010
Akizungumzia Uchaguzi Mkuu uliopita, Mbowe aliwaambia waandishi wa habari kuwa chama chake kilitumia Sh1.3 bilioni katika kampeni za uras.

Alivitaja vyanzo vya fedha hizo kuwa ni Sh 338.9 milioni za ruzuku, Sh 235.9 milioni kutoka kwa marafiki, Sh32 milioni michango mbalimbali ya wanachama na mali mbalimbali za watu zenye thamani ya Sh719.7 milioni.









Jeshi la Polisi lawatahadharisha wanawake








JESHI la polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewatahadharisha wanawake nchini, kutodanganyika kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na wanaume papo kwa papo kwa kuwa kumekuwa na wimbi la mauaji wanawake baada ya kujitokeza mwanaume anayewarubuni
Akizungumza na wanahabari Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suileman Kova, amesema amejitokeza mwanaume anayetuhumiwa kuua wanawake waliofikia wanne jijini Dar es Salaam katika maeneo ya Tandika, Keko, Mtoni kwa Azizi Ally na Buguruni kwa Mnyamani katika kipindi cha miezi mitatu.

Amesema mwanaume huyo amekuwa akirubuni wanawake hao kimapenzi kwa kuwaahidi donge nono la fedha na kisha kwenda nao katika nyumba za kulala wageni na kuwalazimisha kufanya mapenzi kinyume na maumbile na anapomaliza haja zake kuwanyonga.

Kova amesema katika uchunguzi uliofanywa na jeshi la polisi limebaini kuwa katika nyumba zote za wageni walizouawa wanawake hao wamebaini ni mwanaume wa aina moja ambaye wahudumu wa nyumba hizo walipoeleza mazingira na maelezo yao yamefafana na kudai kuwa mwanaume huyo hupendelea kuvaa vazi la T-shirt na suruali aina ya jeans, mweupe, mtanashati na kukadiriwa kuwa na miaka 30 hadi 32.

Kova amesema mtuhumiwa huyo ambaye anasakwa ameonekana kuwalenga wanawake ambao wako ndoani [wake za watu] kwa kuwarubuni kuwaahidi fedha nzuri na kasha kuwanyonga na kutokome bila hata kuiba kitu chochote kutoka kwa marehemu.
.
Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi kumsaka mtuhumiwa huyo kumkamata na kumchukulia hatua zinazostahili na jamii wametakwi kutoa ushirikiano katika suala hilo








Obama azuru eneo la mashambulizi 9/11






Rais Obama akiweka shada la maua katika eneo la mashambulizi mjini New York.



Rais wa Marekani Barack Obama amezuru eneo ambalo mashambulizi ya 11 Septemba yalitokea mjini New York.

Ziara hiyo inafanyika siku nne baada ya kuuawa kwa kiongozi wa kundi la Al-Qaeda Osama Bin Laden, nchini Pakistan.

Inaaminika Bin Laden ndiye aliyepanga mashambulizi hayo ya 9/11 mwaka wa 2001.

Rais Obama aliweka shada la maua kuwakumbuka takriban watu 3000 waliofariki na pia kuzungumza na jamaa zao katika eneo hilo.

Awali Obama aliwaambia maafisa wa kikosi cha kuzima moto kuwa: ''Wakati tunaposema hatuwezi tukasahau, tunamaanisha vivyo hivyo''.

Ziara hiyo inakuja siku moja baada ya rais wa Marekani kusema hatachapisha picha ya mwili wa Osama Bin Laden.

Kiongozi huyo wa Al-Qaeda aliuwawa na vikosi maalum vya jeshi la Marekani kaskazini mwa Pakistan siku ya Jumatatu.

Baadaye mwili wake ulizikwa kwenye bahari kutoka kwa ndege ya Marekani iliyokuwa imembeba.

Majeshi ya Pakistan yalikiri kushindwa kugundua alikojificha Bin Laden na kusema wataanzisha uchunguzi.

Pakistan pia imedokeza kuwa itatizama upya ushirikiano kati yake na Marekani iwapo kutatokea uvamizi mwingine bila ya wao kufahamishwa kama ilivyofanyika na Osama bin Laden





Besigye kupelekwa ng'ambo kwa matibabu








Kiongozi wa Upinzani nchini Uganda Dkt Kizza Besigye atapelekwa ng'ambo kwa matibabu zaidi.

Mkewe kiongozi huyo Bi Winnie Byanyima aliambia BBC kuwa madaktari wanaomshughulikia mwanasiasa huo katika hospitali moja Mjini Nairobi wanahofia kuwa Besigye alipata madhara makubwa ya sumu kwenye ngozi na macho yake.

Kiongozi huyo wa upinzani alisafirishwa hadi Nairobi kwa matibabu zaidi baada ya kupigwa na polisi wa Uganda wakati wa kuzima maandamano aliyokuwa akiongoza ya kutembea kwa miguu hadi kazini kupinga kuongezeka kwa gharama ya maisha nchini Uganda.

Bi Byanyima amemuomba Rais Yoweri Museveni kufanya mashauriano na upinzani pamoja na viongozi wa Kidini ili kutafuta suluhu juu ya matatizo yanayoikumba Uganda badala ya kuwa timua nguvu kupita kiasi kutawanya maandamano

No comments:

Post a Comment