KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Monday, February 28, 2011
Waokoaji New Zealand waishiwa matumaini
Kwa siku ya pili mfululizo makundi ya waokoaji huko Christchurch yameendelea na juhudi za kuwasaka watu waliokwama ndani ya vifusi kufuatia tetemeko la ardhi.
Hali ya afweni ilijitokeza kila manusura walipogunduliwa kutoka vifusi vya afisi katika majengo yaliyobomolewa vibaya.
Hata hivyo wahudumu wa makundi ya waokoajii wanakiri kuwa kwa sasa wamejitayarisha kuopoa maiti zaidi ikiashiria kuwa wameishiwa na matumaini.
Jamaa wa waliopotea wameonywa kuwa watakamatwa endapo watavuka vizuizi vilivyowekwa kuzuia raia wasiingie majengo yaliyo katika hali mbaya katikati mwa mji wa Christchurch.
Zaidi ya saa 36 baada ya tetemeko la ardhi kutokea maelezo zaidi ndiyo yameanza kujitokeza tangu Waziri Mkuu John Key ataje tetemeko hili kama unyama wa maumbile.
Mwanamke mmoja akiwa na mtoto wake mikononi alifariki papo hapo baada ya kugongwa na vifusi. Hata hivyo, Mtoto aliyembeba alinusurika.
Kundi la waokoaji kutoka Uingereza litajiunga na makundi kama hayo ya Australia na Marekani kuongezea juhudi za uokozi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment