KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, February 28, 2011

Congo yapongezwa kuwaathibu wanajeshi

Msemaji wa Ikulu ya White House



Marekani imeipongeza serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kwa kuwatia hatiani wanajeshi 9, waliohusika katika ubakaji wanawake wengi katika eneo la Baraka, Mkoa wa Kivu mashariki mwa taifa hilo.

Msemaji wa serikali ya Marekani, PJ Crowley, amesema kifungo cha jela kwa wanajeshi hao kilichotolewa mapema wiki hii, ni hatua muhimu.

Wanajeshi waliohusika katika ubakaji

Zaidi ya wanawake 60 walibakwa katika shambulio lililotokea katika mji wa Fizi, mapema mwaka huu.

Miongoni mwa wale waliopatikana na hatia ni afisa wa ngazi ya juu katika jeshi, Kanali Kibibi Mutware Daniel, aliyehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela.

Hii ni mara ya kwanza kwa kesi ya ubakaji dhidi ya kamada wa jeshi kufanikiwa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo

No comments:

Post a Comment