KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, February 19, 2011

Miaka 20 jela kwa Luteni Kanali Kibibi


Mahakama moja ya kijeshi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, na ambayo imekuwa ikiendesha kesi ya ubakaji, leo imemkabidhi Luteni Kanali Kibibi Mutware hukumu ya miaka 20 jela.

Alipatikana na kosa la uhalifu dhidi ya binadamu kwa kuwaacha wanajeshi chini ya mamlaka yake kubaka, kuwapiga na kuwaibia wakaazi wa Fizi mali yao, wakati wa siku kuu ya mwaka mpya.


Akiwa ni kati ya wanawake wengi ambao hupata usaidizi katika kliniki za kuwasaidia Goma
Wanawake 49 walitoa ushahidi katika mahakama hiyo katika mji wa Baraka.

Mwandishi wa BBC, Thomas Hubert anaelezea kwamba hii ni mara ya kwanza kwa kamanda katika jeshi la nchi hiyo kuhukumiwa kwa kosa la ubakaji ambao umekuwa ukifanyika mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Mashirika ya misaada yamekuwa mara kwa mara yakisema vikosi vya serikali vimekuwa vikitajwa sana katika kuhusika kwa uhalifu huo wa ubakaji katika eneo la Kivu.

Mahakimu katika mahakama hiyo ya kijeshi pia walitoa vifungo vya kati ya miaka 15 hadi 20 kwa wahusika wengine watatu waliohudumu chini ya Luteni Kanali Kibibi, na kati ya miaka 10 hadi 15 kwa wanajeshi wengine watano wa vyeo vya chini.

No comments:

Post a Comment