KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, February 16, 2011

Maandamano Iran: Nini Kilichojiri

Baada ya maandamano mitaani nchini kote siku ya Jumatatu ,vyombo vya habari vya serikali na tovuti vimejaa maoni na mijadala kuhusu umuhimu wa matukio hayo.

Kwa viongozi wa upinzani wa vuguvugu la Green Movement, haya yalikuwa maandamano makubwa ya kuonyesha nguvu za wafuasi wao katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja.

Lakini maoni ya mhariri wa gazeti lenye msimamo mkali Kayhan yaliwakebehi waaandamanji hao kuwa ni "genge la takataka" ambazo zinaweza kutupiliwa mbali.


Maandamano Iran




Ni wazi kabisa kuwa maandamano ya Jumatatu nchini Iran yaliishangaza serikali na viongozi wa upinzani wa vuguvugu la Green Movement.

Kwa vile watu walikuwa tayari kujitokeza mitaani bila kujali vikosi vya usalama kunaonyesha jinsi baadhi ya wananchi walivyo na hasira dhidi ya serikali.

Halikadhalika inabainisha kuwa madai ya serikali kuwa vuguvugu la Kijani limeishiwa hayana msingi.

Tangu kuzimwa kwa nguvu maandamano yaliyofuatia uchaguzi mkuu wa 2009 serikali imesisitiza kwamba hakuna vuguvugu lenye nguvu nchini Iran.

Wakati maandamano yakianza nchini kote siku ya Jumatatu na tovuti za upinzani zikivuma na taarifa kutoka mitaani -vyombo vya habari vya serikali viliendelea kuripoti kwamba hali ni tulivu.

Lakini wabunge wa Iran walipoanza kujadili matukio hayo katika bunge siku ya Jumanne,ilikuwa wazi kutokana na hasira zilizojitokeza katika mjadala huo kwamba wana wasiwasi mkubwa na kile kilichotokea.

Kwa mara ya kwanza kikao cha Majlis(bunge) kilisikia wito wa sio tu kuwafungulia mashtaka viongozi wakuu wawili wa upinzani - Mir Hossein Mousavi na Mehdi Karroubi - bali hata wauwawe.


Ni vigumu kukisia watu wangapi walijiunga na maandamano mjini Tehran na miji mingine siku ya Jumatatu.

Sababu moja ni kwamba vikosi vya usalama vilifanya kila liliowezekana kuwazuia watu wasikusanyike katika eneo moja.

Wakiiga mfano wa maandamano katika uwanja wa Tahrir (Ukombozi) mjini Cairo, waandamanaji nchini Iran walielekea uwanja wa Azadi (Uhuru) mjini Tehran.

Lakini vikosi vya usalama vilizifunga barabara kuu zinazoelekea katika kitovu cha jiji ikimaanisha kuwa maandamano hayo yalitawanywa katika jiji zima.

Huu ndio mkakati uleule ambao watawala wamekuwa wakiutumia dhidi ya upinzani kwa jumla katika miaka miwili iliyopita.

Maandamano yasio na uongozi
Kwa kuwazuia viongozi wa vuguvugu la upinzani katika kifungo cha nyumbani na kuwatia mbaroni wengine wengi serikali imeweza kuwazuia wafuasi wa vuguvugu la Green, wengi wao wakiwa wa tabaka la katikati, kujaribu kuimarisha mtandao mkubwa zaidi unaowakilisha matabaka yote ya jamii za Iran.

Pia wamewaandama wanaharakati wa vyama vya wafanyakazi,wanafunzi na makundi ya kutetea haki za akina mama katika juhudi za kuhakikisha kwamba hawaungani na kuanza kugeuza mkondo wa kisiasa nchini


Karroubi na Mousavi


Kama wenzao katika miji ya Cairo naTunis, wengi wa wafuasi wa upinzani waliojitokeza katika mitaa ya Tehran wiki hi ni kutoka kizazi cha Facebook .

Lakini wakati waandamanaji katika Misri waliungwa mkono na jeshi la nchi yao na pia serikali ya Marekani, mambo ni tofaut Iran .

Jeshi lenye nguvu la Walinzi wa Mapinduzi ndilo linaloongoza mapambano ya upinzani wowote dhidi ya serikali.

Na matamshi ya hadharani ya Rais Obama huenda kukaipa kila sababu serikali kuwashtumu wapinzani kuwa ni" wasaliti wanaoungana na Israeli " na kuwakandamiza.

Misimamo inayobadilika

Maandamano m,apya ya wiki hii yamewapa wafuasi wa vuguvugu la Green Movement supporters matumai mapya lakini wazi kua bado vuguvugu hilo liko mbali sana kuweza kuleta mageuzi ya kimsingi yaliyoshuhudiwa katika Misri au Tunisia.

Hata hivyo baadhi ya wachunguzi ndani na nje ya Iran wanasema wanaona upinzani umeanza kubadilika.

Shutuma za waandamanaji siku ya Jumaatatu zililengwa dhidi ya kiongozi mkuu wa utawala wa Iran - Ayatollah Khamenei.

Baadhi yao walitia moto picha zake na hata kudai auwawe-jambo ambalo usingeweza kufikiria kabla ya uchaguzi wa 2009 .

Kwa kuwatenga viongozi wa vuguvugu la KIJANI kutoka kwa mashina yao ya vijana, serikali huenda umeusukuma upinzani katika mkondo wa msimamo mkali zaidi.


Mousavi na Karroubi wakiwa bado wanashikilia kuleta mageuzi ndani ya mfumo wa hivi sasa, hasira zinazozidi kupamba moto kama zilivyoshuhudiwa mitaani wiki hii zinaonyesha kuwa baadhi ya wafuasi wa upinzani huenda wasiridhike na mageuzi na sasa wanalenga kufanyike "mapinduzi.







Misri yazitaka nchi za Ulaya na Marekani kuzuia mali za Mubarak

Rais wa zamani wa Misri


Hosni MubarakMisri imeziomba nchi za Ulaya na Marekani kuzizuia akiba za benki za aliekuwa rais wa nchi hiyo Hosni Mubarak. Nchi kadhaa ikiwemo Ujerumani zimethibitisha zimelizipokea ombi hilo na zimeahidi kufanya uchunguzi.

Kwa mujibu wa taarifa ya shirika la habari la Ujerumani DPA, Misri imetoa ombi kwa nchi za Umoja wa Ulaya la kuzizuia akiba za benki za aliekuwa rais nchi hiyo Hosni Mubarak.Shirika hilo limezinukulu duru za kidiplomasia za Umoja wa Ulaya. Mawaziri wa Umoja huo leo watakutana kulijadili ombi hilo la Misri.

Ombi hilo limetolewa kwa Uingereza,Ujerumani na Ufaransa la kuzizuia fedha za viongozi wa ngazi za juu wa utawala wa Mubarak.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague amesema nchi yake italizangatia ombi hilo na kwamba itachukua hatua madhubuti na za haraka endapo patapatikana ushahidi juu ya wizi wa fedha za serikali ya Misri.


Akizungumza bungeni waziri Hague alisema kuwa serikali ya Uingereza imepokea ombi kutoka kwa serikali ya Misri la kuzikamata mali za viongozi kadhaa waliokuwamo katika utawala wa Rais Hosni Mubarak.

Bildunterschrift: Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Mawaziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle (Kulia), na William Hague wa UingerezaWaziri Hague aliliarifu bunge kuwa Uingereza tayari imeshakua hatua kama hiyo kuhusiana na Tunisia baada ya rais wa nchi hiyo Zine El Abidine Ben Ali kupinduliwa na watu wake. Amehakikisha kwamba Uingereza itashirikiana na nchi nyingine za Umoja wa Ulaya na washirika wake wa kimataifa katika kulitekeleza ombi la Misri.

Mawaziri wa Umoja wa Ulaya leo watakutana mjini Brussels kulijadili ombi la Misri, Na waziri Mkuu wa Luxemburg Jean-Claude Juncker amezitaka nchi za Umoja wa Ulaya ziige hatua iliyochukuliwa na Uswisi ya kuzizuia mali za Mubarak.

Ujerumani pia imesema kuwa imelipokea ombi la Misri la kuzitia kufuri akiba za benki za viongozi wa serikali na wabunge wa Misri waliokuwamo katika utawala wa Mubarak.

Lakini Uingereza ndiyo hasa ipo chini ya shinikizo la kuchukua hatua dhidi ya mali za Mubarak na familia yake kutokana namadai kwamba Mubarak na watu wake wameficha mamilioni ya fedha nchini Uingereza.

No comments:

Post a Comment