KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, February 16, 2011

Kampeni za uchaguzi kukamilika UgandaRais wa Uganda Yoweri museveni
Wagombea wa kiti cha Urais na Ubunge nchini Uganda, wanakamilisha kampeni zao tayari kwa uchaguzi mkuu utakaofanyika siku ya Ijumaa.

Rais Yoweri Museveni, ambaye anawania muhula wa nne wa Urais wa Uganda, kupitia chama tawala cha National Resistance Movement, NRM, anatarajiwa kufanya kikao na waandishi wa habari, kabla ya kukamilisha kampeni yake na mkutano wa hadhara mjini Kampala.

Mpinzani mkuu wa Rais Museveni, Kizza Besigye anayewania kiti hicho kupitia chama cha Forum for Democratic Change, FDC, naye atakuwa na mkutano katika chuo kikuu kimoja mjini Kampala.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Uganda, Badru Kiggundu, ametoa wito kwa viongozi wa vyama vyote vya siasa nchini humo, kuvunja makundi yote ya wapiganaji ambayo yaliundwa kwa dhamira ya kulinda masanduki ya kupigia kura

No comments:

Post a Comment