KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, January 29, 2011

Wanawake waongoza kutumia dawa za kulevya -Dar


UTAFITI umebaini kuwa wanawake jijini Dar es Salaam wanaongoza kwa utumiaji wa dawa za kulevya.
Akitoa utafiti huo Dkt. Deo Mtasiwa, alisema utafiti walioufanya umebaini kuwa wanawake huongoza kutumia dawa hizo hususani zile za kujidunga.

Alisema kuwa asilimia 50 wanawake hutumia dawa hizo na wanaume umebainika kuwa sawa na asilimia 25 wanaotumia dawa hizo.

Mtasiwa amesema kuwa, wameandaa mpango maalum ya kuwatibia wagonjwa hao watakaojitokeza hospitalini.

Amesema wameandaa mpango huo katika hospitali ya Taifa Muhimbili na wagonjwa wote watakaofika hapo watafanyiwa uchunguzi na kupatiwa matibabu bure

No comments:

Post a Comment