KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, January 12, 2011

Vibaka Walipokwapua Brifkesi ya Mzungu


Za mwizi zilitimia arobaini wiki hii wakati kibaka mmoja katika eneo la Feri alipowaponza wenzake wote na kupelekea wote wapewe kisago cha nguvu na raia weneye hasira ale kibaka huyo alipoamua kukwapua brifkesi ya mzungu.
Sakata hilo la aina lake lilitokea eneo la feri upande wa Kigamboni ambapo vijana wanaojihusisha na wizi walimvamia mmoja wa wazungu watalii ambao uraia wao haukufahamika mara moja na kumpora brifkesi yake.

Baada ya kumpora na kutimua mbio, wasamaria wema walimfukuza kibaka huyo amabaye kama kawaida yao alikimbilia kwenye maskani yao yaliyopo kwenye ufukwe wa bahari ya Hindi.

Whenga walisema siku za mwizi ni arobaini kwani kitendo cha mwizi huyo kukimbilia kwenye maskani yao kiliwafanya wananchi wenye hasira waamue kuwashushia kichapo vibaka wote waliokutwa kwenye maskani hiyo.

Wezi hao waliokolewa na askari wa jeshi la maji Navy ambao walikuwa wamevalia kiraia ambapo hadi wanawasili eneo hilo walikuta wezi wengi wakiwa wamezimia kwa vipigo walivyopewa na wananchi wenye hasira.

Kijana mmoja anayejishughulisha na wizi kwenye eneo hilo ambaye alinusurika kichapo kwa kutokuwepo eneo la eneo la tukio wakati wizi huo ulipofanyika, aliwatetea wenzake kwa kuiambia Nifahamishe.com "Maisha yamekuwa magumu, vitu vyote vimepanda sana ikiwemo Sukari ,Mchele Unga , Umeme kila kitu hapa kimepanda, Kutokana na ugumu wa maisha tunalazimika kuiba kwani hata watoto wa vigogo na vigogo wenyewe wanaiba tena sana tu", alidai kibaka huyo amabaye hakutaka kutaja jina lake

No comments:

Post a Comment