KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, January 12, 2011

Shambulio la Gaza uchunguzi wafanywa



Ramani ya Israel

Uchunguzi uliofanywa na Israel juu ya jeshi lao kushambulia meli zilizokuwa zikienda kutoa msaada huko Gaza Mei mwaka jana, ambapo wanaharakati tisa Wakituruki waliuawa umesema kuwa hatua hiyo ilifanywa kulingana na sheria za kimataifa.

Uchunguzi huo nao umesema kuweka kizuizi huko Gaza ni halali.

Shambulio hilo lilisababisha nchi nyingi za kimataifa kulaani tendo hilo la Israel.

Awali katika ripoti iliyotolewa na umoja wa mataifa ilisema kuwa makomando wa Israel walifanya ukatili wa hali ya juu ambao haukubaliki.

Habari zaidi zinasema kuwa kuna taarifa itakayotolewa na kuna hisia kuwa italeta mgawanyiko na hata kutupuliwa mbali na wahakiki kutoka Israel.

Taarifa hiyo inasema ingawa kuna masikitiko kuwa raia wa Uturuki waliangamia, jeshi la wanamaji la israel liliendesha kazi yake kwa kufuata sheria.

Aidha, jeshi la wanamaji la Israel lilichokozwa na Waislamu wenye msimamo mkali wakiwa kwenye msafara wa meli.

Lakini, Wapalestina zaidi ya 600 waliokuwa wakisafiri kwenye msafara huo wanaipinga taarifa hiyo.

Shambulio hilo ni la aibu kwa Israel na kwa uhusuano wake wa umma.

Serikali ya Israel ina matumaini ya uchunguzi zaidi kurekebisha hali hii.

Ripoti itakayotolewa baada ya uchunguzi huo itawasilishwa kwa wachunguzi walioagizwa na Katibu Mkuu wa umoja wa Mataifa Ban Ki Moon.

Uchunguzi huo pia itazingatia ushuhuda uliokusanywa na serikali ya Uturuki.

Uchunguzi uliofanywa na shirika la kutetea haki za binadamu la Umoja wa Mataifa mwaka jana ulionesha jeshi la wanamaji la Israel lilfanya ukatili kupindukia

No comments:

Post a Comment