KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, January 12, 2011

Misri yalaumu 'jeshi la kiislamu'


Misri imesema ina ushahidi kuwa kundi la wapiganaji la Kipalestina huko Gaza ambalo lina uhusiano na al-Qaeda lilihusika katika shambulio la bomu kwenye kanisa mjini Alexandria, ambapo watu ishirini na mmoja waliuawa katika mkesha wa mwaka mpya.

Waziri wa mambo ya ndani wa Misri, Habib al-Adly, amesema kundi liitwalo 'jeshi la Kiislamu' lilipanga na kutekeleza shambulio hilo.

Shambulio hilo ni baya zaidi kutokea dhidi ya Wakristo nchini Misri katika kipindi cha karibu muongo mmoja.

Kundi hilo la Gaza limekanusha kuhusika na shambulio hilo na maafisa nchini Misri hawajatoa maelezo zaidi kuhusu shambulio hilo.

Kutokana na shambulio hilo kumekuwa na ghasia baina ya polisi na Wakristo wa madhehebu ya kicopti.

'tuna ushahidi wa kutosha kuwa 'jeshi lao la Kiislamu ' wamehusika katika kupanga na kutekeleza shambulio hili la kigaidi,' Bw Adli alisema katika maadhimisho siku ya Polisi nchini Misri.

Rais Hosni Mubarak aliwasifu polisi akisema kupatikana ushahidi huo kutasaidia kutuliza roho za raia wa Misri.

Shambulio la Alexandria lilisababisha Wakristo ambao ni wachache zaidi nchini humo kuandamana na kuilaumu serikali kwa kutowajali.

Msemaji wa kundi hilo la 'jeshi la Kiislamu' amesema kuwa kundi lao halikuhusika katika shambulio la Kanisa nchini Misri.

Lakini aliongezea kuwa : 'Tunawasifu wale waliotekeleza shambulio hilo'.

'Jeshi la Kiislamu' limelaumiwa kwa utekaji nyara na vurugu huko Gaza

No comments:

Post a Comment