KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, January 12, 2011

Shahidi amkanyaga Jerry


SHAHIDI wa tatu katika kesi inayomkabili mtangazaji wa TBC1 Jerry Muro amedai mahakamani kuwa mshitakiwa huyo alifika ofisini kwake na kumtaka atoe rushwa ya shilingi Mil. 10 na kabla ya hapo alimtishia bastola ili aweze kutoa fedha hizo.
Shahidi huyo ambaye alikuwa mtunza Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani, Michael Wage alitoa ushihidi huo jana katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu ya jijini Dar es Salaam.

Wage alidai kuwa alipokea simu ya Murro Januari 28, mwaka jana akiwa Bagamoyo na alimueleza anamuhitaji kwa mahojiano mafupi.

Alidai kesho yake waliweza kukutana katika hoteli ya Califonia majira ya saa 5 asubuhi lakini Jeryy alimtaka shahidi huyo wakazungumze katika hoteli ya SeaCliff na baadae kumueleza kuwa ana tuhuma nzito za ubadhilifu wa fedha na ufisadi na kumueleza anamuandalia kipindi maalum cha tuhuma zake katika kipindi cha usiku wa habari kinachorushwa na TBC.

Aliongeza shahidi huyo kuwa, Jerry alimwambia kuwa yeye pia
ni afisa wa jeshi mwenye nyota tatu amesomea nchini Uingereza na Marekani, na alifungua dashboard ya gari na kutoa pingu, akamwambia akileta fujo atamfunga, pia alimtishia kwa kumuonyeshea na bastola

“ tulipofika pale Sea cliff walimkuta mtu mwingine aliyejitambulishwa kama Naibu Mkurugenzi wa Takukuru na akaingia mwingine Muro alinitambulisha kuwa huyu ni Kaimu Mkurugenzi wa Takukuru”.

“Walinitisha na kuniambia nitoe Shilingi milioni 10 ili wanisaidiwe wasiwe kumshitaki na alikubali na kuwaambia kwa muda huo alikuwa na kiasi cha shilingi milio moja na nyingine angewamalizia kesho yake.

Wage alidai mara baada ya kutoka pale alikwenda kuripoti tukio hilo kituo cha Polisi cha Kati, na Januari 31 waliweza kumpigia simu Jerry aweze kuja kummalizia pesa hizo akiwa na askari lakini Jerry alipofika mahali alipowaona askari alitaka kukimbia lakini aliweza kukamatwa na kupelekwa kituoni

No comments:

Post a Comment