KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, January 29, 2011

Niger yaenda kwenye uchaguzi

Waziri Mkuu wa Niger, Mahamadou Danda


Watu
wa Niger watapiga kura kesho (31 Januari 2011) kuchagua wabunge na rais wakati ambapo wagombea wanautaka utawala wa kijeshi wa nchi hiyo uibadili tume ya uchaguzi. Je, uchaguzi huo utarejesha demokrasia nchini humo?

Mnamo mwezi wa Februari mwaka uiliopita, wanajeshi wa Niger walitwaa madaraka kwa kumpindua Rais Mamadou Tanja, kwa sababu alikuwa anakusudia kufanya njama za kuibadili katiba ili aongeze kipindi cha mamlaka yake ya urais.

Hali ilikuwa ya mvutano muda mfupi baada ya kumalizika kampeni za uchaguzi.Wagombea urais wanane kati ya 10 wametishia kuususia uchaguzi huo ikiwa serikali ya kijeshi haikuuakhirisha.

Wajumbe hao wamelalamika juu ya maandalizi mabaya ya uchaguzi wa majimbo. Hayo ameyasema pia aliyekuwa Waziri Mkuu Hama Amodou, mwenye matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika uchaguzi huo hapo kesho.

"Ikiwa uchaguzi wa bunge na wa rais utafanyika katika mazingira kama yale ya uchaguzi wa majimbo, basi tutakabiliwa na matatizo makubwa." Amesema Amodou.

Lilikuwa jambo la kuvutia kumwona Amadou ghafla akiwa pamoja na hasimu wake mkubwa wa kisiasa, chama cha MNSD kilichokuwa kinatawala nchini Niger.

Itakumbukwa kwamba chama hicho ndicho kilichomvua madaraka ya uwaziri mkuu, Amadou alipokuwa katika serikali ya Rais Tanja. Amadou alikabiliwa na tuhuma za rushwa na alitiwa jela ambako sasa rais wa hapo awali. Tanja anatajwa pia kwenye tuhuma za rushwa.

Shabaha ya uchaguzi huo hapo keshi nikurejesha demokrasia nchini Niger, baada ya jeshi kutwaa madaraka mwezi februari mwaka jana. Lakini pana utatanishi juu ya tume ya uchaguzi. Msemaji wa chama cha MDN ameutaka utawala wa kijeshi uibadili tume hiyo. Msemaji huyo Malam Sani Mahamanne ameeleza kuwa tume hiyo ina sifa mbaya.Ameeleza kuwa wagombea wa vyama vyote kumi wametaka kuahirishwa uchaguzi huo.

Lakini wananchi wa Niger hawataki kuona mivutano baina ya wanasiasa bali wanataka kuona matatizo ya nchi yao yanatatuliwa.

Niger inakabiliwa na vipindi vya ukame mara kwa mara vinavyosababisha njaa nchini. Hali ya elimu pia imo katika hali mbaya .Maalfu ya vijana hawana aira.

Wagombea wote wanatoa ahadi zinazofanana. Lakini suala la ugaidi halitiliwi maanani miongoni mwa wagombea- yaani harakati za makundi yanayoyakiribia alkaida ambayo mara kwa mara yamewateka nyara watu kutoka Ulaya.

Hivi karibuni tu vijana waliokuwa na silaha waliwateka nyara wafaransa wawili katika mji mkuu Niamey.Magaidi waliwaua wafaransa hao baadae. Hatahivyo baadhi ya wananchi wa Niger wanasema jambo muhimu zaidi ni mchakato wa kurudisha demokrasia nchini an hivyo kuweza kuepusha hatari ya kuimarika wanaitikadi kali wa kiislamu.

Watu karibu milioni saba wanastahiki kupiga kura hapo kesho. Wachunguzi wanatarajia kuona uchaguzi huo ukifanyika kwa utulivu. Katika changuzi za nyuma vyama vyote viliyakubali matokeo ya uchaguzi licha ya kasoro fulani zilizojitokeza.

No comments:

Post a Comment