KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, January 6, 2011

Mkuu wa Wilaya Acharazwa Bakora


Ili asisahau ahadi alizozitoa wakati wa kampeni za uchaguzi, mkuu wa wilaya moja nchini Peru alimualika mtu amcharaze bakora mbele ya umati wa watu.
Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 23 wa nchini Peru ambaye alichaguliwa kuwa mkuu wa wilaya alitumia njia ya aina yake ya kujikumbusha ahadi alizozitoa wakati wa kampeni wa uchaguzi.

Abraham Carrasco baada ya kuchaguliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Chilca, aliamua kuwaita watu kushuhudia akicharazwa bakora kabla ya kula kiapo cha kuitumikia wilaya hiyo.

Mbele ya mamia ya watu waliokusanyika, mkuu huyo wa wilaya alicharazwa bakora tatu ili azikumbuke ahadi alizozitoa wakati wa uchaguzi.

Carrasco alimchagua mzee mmoja aliyekuwa akiheshimika katika wilaya hiyo ndio amcharaze bakora kabla ya kula kiapo.

"Usiwe mwizi", alicharazwa bakora ya kwanza, "Usiwe muongo", alicharazwa bakora ya pili "Usiwe mvivu", alicharazwa bakora ya tatu.

Baada ya kucharazwa bakora, Carrasco alimbusu mikono mzee aliyemchapa bakora na kisha kula kiapo cha kuitumikia vyema na kwa uadilifu wilaya hiyo.

Carrasco alisema kuwa ataihifadhi bakora iliyotumika ili iwe kumbukumbu yake kwa ahadi alizozitoa wakati wa kampeni za uchaguzi

No comments:

Post a Comment